Elections 2010 Sheria kui kuu za uchaguzi mkuu 2010

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,711
2,226

Jenerali Ulimwengu
Oktoba 27, 2010

Jumapili, Oktoba 31, tunapokwenda kupiga kura kuwachagua rais, wabunge na madiwani tufanye hivyo kwa kuzingatia sheria kuu kumi zifuatazo:
1) Tambua kwamba kura ni silaha takatifu inayokuwezesha kumchagua Yule unayeamini kwamba unaweza kumkabidhi sehemu ya maisha yako na ukawa salama.
2) Tumia busara.
3) Jua kwamba ni usaliti kwako mwenyewe na kwa wananchi wengine iwapo utapiga kura kwa misingi ya rushwa. Anayekununua hakuthamini. Kwake wewe ni bidhaa tu, kama maharage.
4) Usiruhusu hisia za ubaguzi wa kabila, rangi, dini, jinsia, au ubaguzi wa aina yo yote nyingine ile utawale uamuzi wako katika kupiga kura.
5) Tenda haki kwa wengine, na pia dai haki yako kutoka kwa wengine.Usimwonee ye yote na wala usimruhusu ye yote akuonee.
6) Watetee na walinde wanyonge na wasiojiweza. Wasaidie ili waweze kutumia haki yao ya kupiga kura.
7) Imarisha uhuru wako na uhuru wa nchi yako kwa kuhakikisha kwamba uchaguzi unakuwa na maana, na kwamba kila kura inayopigwa ina maana.
8) Epuka vurugu, vitisho na ugomvi. Kura ni jambo la raha, si karaha.
9) Kumbuka kwamba amani ni mwana wa haki. Penye haki, aliyeshindwa akubali kushindwa, na aliyeshinda bado atende haki kwa aliyeshindwa.
10) Tambua kwamba uchaguzi unakuja na kwisha, viongozi huja na kuondoka, lakini Taifa na watu wake hudumu milele. Tuliza hamasa, epuka chuki, uwe na ustahamilivu.
Hii ni fursa adhimu; ifurahie.
MY TAKE
Nimezipenda namba kumi na nne ingawa kwa ujumla zote ni nzuri na zinafaa
 
Inaonekana kuedit title ni issue,any ni sheria kuu kumi za uchaguzi mkuu 2010
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom