Sheria ipitishwe kulazimisha backup

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
SHERIA IPITISHWE KULAZIMISHA BACKUP

Kwa mfano umetukanwa kwa njia ya mtandao , ukashitaki kwenye vyombo vya dola , vyombo vya dola katika kufuatilia sakata lako kwa njia ya mtandao wanakuta aliyekutukana alitumia mtandao wa MAISHABORA kwa ajili ya kutuma barua pepe hizo na aina zingine za matusi , vyombo hivi vinaenda kwenye Ofisi za MAISHABORA wanaambiwa huwa hawahifadhi taarifa za wateja wao wanaotumia vifaa vyao kwa ajili ya mawasiliano na watu wengine , kama wanahifadhi basi ni kwa muda mchache tu .

Kumekuwa na matukio ya kihalifu ambayo yanahusiana na mitandao kama ya simu , computer na vifaa vingine lakini kampuni zinazotoa huduma hizi nyingi huwa hazihifadhi taarifa za mawasiliano yao kiasi kwamba inakuwa tabu sana kudhibitisha baadhi ya vitu vyanzo vyake .

Nilikuwa naomba kampuni zote za mawasiliano yanayohusu ummah yatungiwe sheria ambayo itawalazimisha kuhifadhi mawasiliano ya wateja wao wote pamoja na taarifa sahihi za wateja wao wote endapo chochote kitatokea huko mbeleni iwe tahisi kutafuta ushahidi na taarifa zingine muhimu , pia kampuni hizi zilazimishwe kupitisha mawasiliano yao kwenye kituo chetu cha mawasiliano ambacho serikali ndio msimamizi mkuu wa kusimamia huduma zote za mawasiliano zinazopitishwa hapo .

Ingawa tumekuwa hatuna sheria za mtandao ambazo watu wengi wanazililia sasa hivi , ni vizuri pia serikali ifikirie suala hili kwa kina zaidi kwenye sheria hizo pia kunaweka kupatikana vipengele vya kubana kampuni hizi kwenye masuala ya kuhifadhi taarifa za watu .

Kuchuwa mfano huu , Kuna wakati nilikuwa nchi fulani kwa muda wa wiki 4 , nikapatiwa email ya muda kwa ajili ya mawasiliano yangu toka sehemu ambayo nilikwepo , wakati naondoka nikaomba hiyo email ifungwe wakaniambia haitafungwa sheria za nchi zao haziruhusu kufunga anuani hiyo mpaka baada ya miezi 10 , kuna masuala ya kodi , takwimu na mambo mengine mbali mbali tu yanahitajika kufanyika na kuhakikisha email hiyo haikutumika kwenye masuala ambayo ni kinyume na kazi za sehemu husika .

Hata unapokuwa na email mfano ya yahoo , unapoamua kuifunga , itakuwa pending kwa siku 90 mpaka wahakikishe email hiyo ilitumika kwenye shuguli ambazo sio za kuvunja sheria , haijawahi kushitakiwa popote na wala haina misukosuko mengine ambayo inahusiana na uhalifu wa mtandao , sijui kwa mitandao mengine ila gmail inakulazimisha kufungua account nyingine ndio iwe mbadala kwa hiyo ambayo unataka kuifunga .
 
Mkuu Shy,

Hapa sijaelewa unazungumzia kitu gani, je unaweza kupanga hoja hii tena?
 
Sidhani kama ni idea nzuri.
Kwanza anonymity ni kitu muhimu sana kwenye internet, anonymity ina madhara yake lakini benefits ni nyingi sana inabidi tulipe hiyo cost ya anonymity.

Pili hakuna njia ya kumtambua mtu aliyefungua account hata ukihifadhi data gani, naweza kufungua account na jina Bill Gates, na kila kitu feki. Nikitumia cafe au public wifi kuiaccess IP address nayo inakuwa useless.
 
Back
Top Bottom