Sheria inasemaje kuhusu kesi ya madai katika suala hili linalonikabili?

Ruhazwe JR

JF-Expert Member
Jan 31, 2011
3,403
920
Ndugu zangu wana JamiiForums,

Ninaomba kufahamishwa juu ya kesi za madai kuanzia procedure za kufungua kesi. Ninadaiwa milion 3 ambazo niliazimwa na rafiki yangu wa karibu, wakati tunakopeshana tulienda kuandikiana kwa wakili wa kujitegemea na tulipofka pale wakili alidai hata kama tunapeana kindugu lazima tuweke kiwango cha riba endapo siku itazidi kwa siku ya marejesho.

Baadaye mambo yakaeniendea vibaya ambapo hadi sasa sijaweza kurejesha mkopo na nipo namuuguza mke wangu ambaye ana mtoto wa miezi tisa.

Napigiwa simu na mtu ambaye simjui, anadai yeye ni ndugu wa anayenidai ananitafuta akiwa na RB ya kunikamata.

Naomba kujua haki zangu ni zipi ingawaje nadaiwa katika hili, nielimisheni sina ufahamu wowote juu ya Elimu ya Sheria na nifanye nini maana nipo mbali na natafutwa kwa RB ukizingatia itakua ni mara ya kwanza kwenda Polisi na Mahakamani.
 
Ukishashitakiwa kwa kuwa tayari unao mkataba wa kimaandishi na ambao umepitishwa na Mwanasheria hapo huna ujanja lazima utiwe hatiani na masharti utayopewa na mahakama utatakiwa udiclare pato lako ili uweze kulipa kwa awamu mpaka umalize deni la watu...
 
ukishashitakiwa kwa kuwa tayari unao mkataba wa kimaandishi na ambao umepitishwa na mwanasheria hapo huna ujanja lazima utiwe hatiani na masharti utayopewa na mahakama utatakiwa udiclare pato lako ili uweze kulipa kwa awamu mpaka umalize deni la watu.....
<br />
<br />
 
Nashukuru kaka,je watazingatia sana uwiano wa den na kipato?mfan naweza kupata lak2 kwa mwezi watanikadiliaje
 
The standard of proof is different. All you need is the preponderance of the evidence.
 
Ruhazwe, kwanza kudaiwa sio kosa la jinai bali la madai hivyo hiyo RB isikutishe wala huwezi kutiwa ndani.

Aliyekushitaki atakuwa amekusingizia kesi ya wizi wa kuaminiwa lakini kama ni kudaiwa tuu sio kosa la kufunguliwa RB as if wewe ni mhalifu.

Dawa ya deni ni kulipa tuu, nakushauri kuwa mkweli kwa mdai wako mwambie your situation ya sasa na mpe commitment kuwa una nia ya dhati ya kulipa deni lake.

Kwa vile deni ni la muda mrefu, hivyo riba itakuwa imeliongeza mara dufu, kwanza lipa ile principal halafu omba waiver kwenye riba ili aipunguze to a reasonable ammount ambayo unajua utamudu kulipa.

Inawezekana ni wewe ndio umemfikisha mdai wako hapo alipofika kwa kutokuwa mkweli na longo longo nyingi.

Just feel good wala usijisikie vibaya kudaiwa. Hata hao matajiri unaowajua wewe, wana madeni lukuki.
 
Kama alivyosema Pasco kesi ya madai haihusiani na RB ya polisi. Itakuwa huyi ndugu yako ametoa taarifa za wizi au utapeli. Kama unavyosikiaga msemo wa mtaani kwamba mdaiwa hafungwi...huu msemo unaukweli 80%. Kisheria kinachotakiwa kufanyika ni huyo mdai wako kukuandikia hati ya nia ya kukushtaki kwa kushindwa kulipa deni ndani ya muda mliokubaliana kimkataba na baada ya muda atakao ainisha kwenye hati tajwa. Mara nyingi huwa ni siku 14 au 30 au yaweza kuwa zaidi.

Ndani ya huo muda uliotajwa kwenye hati ya nia ya kukushtaki waweza ijibu kwa kumuomba akuongeze muda au waweza kupinga deni ama riba au waweza kukaa kimya. Muda ukiisha mdai wako atakupeleka mahakamani na utapata hati ya kuitwa mahakamani (summons) na nakala ya hati ya mashtaka (plaint), Hapo una siku 21 za kujibu kama wataka au waweza kaa kimya ukisubiri siku ya kusikiliza kesi kufika na kesi kuanza kusikilizwa.

Mkataba mlioandikishana kwa wakili utakuwa ushahidi kwamba kweli alikukopesha pesa ambazo ulitakiwa kulipa ndani ya muda fulani. Kesi ikiisha na ikaonekana umeshindwa kesi basi hukumu itakuwa ulipe deni na gharama za usumbufu (kama zipo). Baada ya muda kupita na ukishindwa kulipa deni ataomba kukaza hukumu na kukamata baadhi ya mali zako, au kuomba fungwe mieze sita.

Pole kwa matatizo ila ni ya kawaida na yasikutie hofu ni vitisho tu. NB Polisi wakija na RB waambie hakuna kosa la jinai ila ni madai na awana haki ya kukukamata. Cha muhimu uwe na nakala ya mkataba mlioingia ili kuwashawishi polisi
 
Do! Quinty unatisha mkubwa,nashukuru kwa maelezo yako ya kina.je endapo atakua ameripot tofauti kama vile wizi/utapeli nitatumia njia gani kukanusha?

Nashukuru sana na ntazidi kuwafahamisha zaidi
 
da, wadau mko juu. naomba msaada pia kuna jamaa nlifanya naye kazi, nikamkabidhi aendeshe Bajaji,ndani ya wiki akaondoka na 40000, na tairi sh 80000 na spanner 20000. yangu 2014 October, namdai kiheshma hanielewi.

sheria inasemaje?
 
Nimegundua jambo Watanzania ni waoga na tunadhuliwa haki zetu kwa kutojua SHERIA ...ndg mleta mada sijui mpaka leo mmefikia wapi manake uzi huu ni wamiaka mingi.....MTU anaekudai lakini anajifanya kujua kukupeleka Polis kwa utapeli manake hiyo ni Jinai banana nae Mahakamani...

utamtupa kesi ya utapeli then unampandisha yeye Mahakamani kukufungulia KESI ya Uongo ikibidi unamtajia Fidia kubwa Kumfilisi ili akili imkae sawa kitu ambacho watu wengi hawajui...Polis hawafungui KESI za madai ukienda pale sana sana wakikuona hujielewi wanakwambia wambakie kesi mdai wako wakiamini wee utawapoza Hela...ikiwa wanajua wee utashindwa Mahakamani lkn wameshakula kwako
 
Anachohitaji hapo ni procedure katika civil, nini kinaanza, nini kinafuata hadi mwisho ili kama hana wakili ajue kinachoendelea pale mahakamani. kama nimemwelewa nafikiri hivyo ndivyo anavyomaanisha.
 
DAWA YA DENI NI KULIPA si kutafuta msaada wa kutokulipa
USHAURI:Mwende anayekudai mweleze nia yako ya kulipa na jinsi utakavyolipa lakini unapomwendea nenda angalau na kiasi cha fedha kama robo ya fedha unazodaiwa au kama hazitoshi tafuta mtu atakayesimama na wewe kama mdhamini kumhakikishia mdaiwa jinsi utakavyolipa HIVYO HASIRA YA ANAYEDAI ITAPUNGUA au kutoweka kabisa kwani yote hayo yamesababishwa na wewe.

Kama tukianza kutafuta watu wa kututetea tusilipe madeni matokeo yake UAMINIFU UTATOWEKA na Tutashindwa KUSAIDIANA SISI KWA SISI au tukitaka kusaidiana tutawekeana masharti magumu KUMBUKA BADO SHIDA ZAKO HAZIJAISHA BADO UTAHITAJI TENA MSAADA ambao Hautaupata Tena. Mimi nimeshapeleka kesi zaidi ya ishirini za madai mahakamani na hakuna hata kesi moja mdaiwa alishinda Bali wote walihukumiwa kulipa na wengine walikuwa na mawakili lakini kinachomtia mtu hatiani ni ule mkataba alioingia na Ushaidi wa vielelezo vya kuonyesha mdaiwa amekiuka mkataba na kukataa kulipa deni.
 
Quinty, Huu uzi ni wa muda mrefu lakini nina imani sheria ni zilezile. Naomba kuelimishwa juu ya "Endapo mdaiwa hana mali inayokamatika katika kukazia hukumu na mdai akaamua kuiomba mahakama impe hicho kifungo cha miezi 6, akimaliza hicho kifungo deni linakuwa limeisha au bado lipo pale pale?"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom