Sheria gani inazuia pornography Tanzania?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Nimejaribu kutafuta kwa haraka sheria inayokataza pornography katika Tanzania. Najua ipo mahali fulani. Sijui kama ni ile ya utangazaji au ya magazeti au ya ndoa au SOSPA n.k Kama kuna mtu naomba anielekeze kwani kuna jambo muhimu sana nataka niliandikie makala..
 
Kuna sheria inayohusiana na mambo ya filamu (Film and Audio Visual), kitu kama hicho (Sina uhakika sana!), nadhani ndo inasimamia hayo masuala. Pia kwenye Penal code" kuna vipengele vinavyohusiana. Inahitaji kupekua sana sheria zetu ili kupata hasa ni sheria ipi inazuia pornography.
 
Pornography ni kama prostitution, hakuna sheria rasmi ya kuzuia bali filamu za porno zinazuiliwa na sheria ya Filamu Tanzania. Porn magazines zinazuiliwa na sheria ya magazeti ya mwaka 1976. Porn kwenye internet haizuiwi na sheria yoyote kwa sababu mpaka sasa Tanzania hatuna any cyber legistlation.

Sheria hizo zote hazizuii porno as porno bali zinazuia filamu ama picha zozote zinazolwenda kinyume cha maadili ya Mtanzania na zinahusu public. Kutumia porn video kama sex orientation kwa lengo la kudumisha penzi ama kunusuru ndoa zenye hatari ya kuparaganyika kwa unsatisfactory sexual life is justified reason,

Ndio maana wadada zetu wanaotumia miili yao kama kitega uchumihawavunji sheria yoyote, na wale wanaokamatwa hushitakiwa kwa kosa la uzururaji na sio prostitution. Kulitokea kesi dhidi ya uendeshaji madanguro, sikumbuki walitumia sheria gani.
Kama mpaka Monday utakuwa hujapata, I'll be in a better position kukupatia references.
 
Nimejaribu kutafuta kwa haraka sheria inayokataza pornography katika Tanzania. Najua ipo mahali fulani. Sijui kama ni ile ya utangazaji au ya magazeti au ya ndoa au SOSPA n.k Kama kuna mtu naomba anielekeze kwani kuna jambo muhimu sana nataka niliandikie makala..

Baadhi zimo humo humo ulipopitia. Utakuwa ulizikosa kama ulijielekeza katika neno “pornography.” Halipo, zimetumika lugha nyingine.

PORNO KWA WOTE:

THE PENAL CODE, 1980
Traffic in obscene publications
Section 175. ( 1 ),( 3 ),( 4 )

(1) Any person who:

(a) for the purpose of or by way of trade or for the purpose of distribution or public exhibition, makes, produces or has in his possession any one or more obscene writings, drawings, prints, paintings, printed matter, pictures» posters, emblems, photographs, cinematograph -films or any other objects or any other object tending to corrupt morals:

(b) for any of the purposes above mentioned imports, conveys or exports, or causes to be imported, conveyed or exported any such matters or things, or in any manner whatsoever puts any of them in circulation; or

(c) carries on or takes part in any business, whether public or private, concerned with any such matters or things, or deals in any such matters or things in any manner whatsoever, or distributes any of them, or exhibits any of them publicly, or makes a business of lending any of them; or

(d) advertises or makes known by any means whatsoever with a view to assisting the circulation of, or traffic in, any such matters or things, that a person is engaged in any of the acts referred to in this section, or advertises or makes known how, or from whom, any such matters or things can be procured either directly or indirectly; or

(e) publicly exhibits any indecent show or performance or any show or performance tending to corrupt morals,

is guilty of a misdemeanour, and is liable, to imprisonment for two years or to a fine of two thousand shillings.

PORNO KWA WATOTO

THE SEXUAL OFFENCES SPECIAL PROVISIONS ACT, 1998-4
Sexual Exploitation of Children
Sect. 12 Amendment of the Penal Code, adding Sect. 138 B ( 1 ),( 2 )

In this section "child" means a person of the age of less than eighteen years.

Any person who:

(a) knowingly permits any child to remain in any promises for the purposes of causing such child to participate in…any form of obscene or indecent, exhibition or show;

(b) acts as procurer of a child for the, purposes of…any form of indecent exhibition or show;

(c) induces a person to be a client of…any indecent exhibition or show, by means of print or other media, oral advertisements or Other similar means;

(d) takes advantage of his influence over, or his relation ship to, a child, to procure the child for …any form of sexual abuse or indecent exhibition or show-

(e) threatens, or uses violence towards, a child to procure the children…for any form of sexual abuse or indecent exhibition or show,

(f) gives monetary consideration, goods or other benefits to a child or his parents with intent to procure the child…for any form sexual abuse or indecent exhibition or show

committs the offence of sexual exploitation of children of not less than five years and not exceeding twenty years.
______________________

1. All typos, mangled syntax, spelling mistakes, and completely meaningless language are from the statutory provisions themselves, relevant sections were copied as they are.

2. Panaposema “misdemeanor” chukua tahadhari maana sheria zimebadilishwa na siku hizi hakuna tofauti kati misdemeanor na felony Tanzania.
 
Last edited:
Tanzania does have several laws which govern that issue of pronography:

SOSPA deals mainly with prostitution perse

News Paper Act (1976) deals mainly with publication of pornagraphic materials(which is about to be repealed) and Broadcasting Act which deals mainly with censorship.

SOSPA is the main source, if you read it carefully it has got all answers for your.

Marriage Act does not cover this area of pornography.

I don't know exactly which area or the main focus of your research( as you can see the laws are scattered all over)

Shadow.
 
Shadow,

Nisaidie, kwenye hizo Newspaper Act of 1997 na Broadcasting Act of 1976, ni wapi wanaongelea pornography? (Nimeweka attachment ya hizo Acts unionyeshe hizo sections.)

Halafu, nadhani si sahihi kusema SOSP Act "deals mainly with prostitution." Kuna kila aina na namna ya sex-related offenses mle, including child pornography, isipokuwa pornography in general.
 
Attachments

  • BROADCASTING ACT OF 1976.pdf
    88.6 KB · Views: 377
Kuna wakati niliingia Bongo na gazeti Playboy ambalo lilikuwa na mahojiano na Jimmy Carter. Sikujua wakati huo kuwa Playboy imepigwa marufuku. Airport wale Waswahili wakanisaili lakini kabla sijaondoka niliwaona wao wakiperuziperuzi kurasa za gazeti.
 
Shadow,

Nisaidie, kwenye hizo Newspaper Act of 1997 na Broadcasting Act of 1976, ni wapi wanaongelea pornography? (Nimeweka attachment ya hizo Acts unionyeshe hizo sections.)

Halafu, nadhani si sahihi kusema SOSP Act "deals mainly with prostitution." Kuna kila aina na namna ya sex-related offenses mle, including child pornography, isipokuwa pornography in general.

Kuhani heshima yako mzee,

Kama nilivyosema hapo juu sheri ya ya magazeti(1976) inampatia waziri husika mamlaka ya kutunga kanuni ambazo zitasimamia ethics na conduct ya wanahabari. Katika kufanya hivyo mamlaka mojawapo ya waziri ni "kucensor" ( kwa tafsiri isiyo sahihi: kulifungia gazeti lolote litakaloenda kinyume na maadili ya uandishi) likiwemo suala la kuchapisha picha za ngono.

Hivyo hivyo bodi ya utangazaji tanzania( soma kuhusu wajibu wa bodi ya utangazaji) utaona moja ya kazi zake ni kufanya censorship ya habari.

Kuhani ukisoma regulations zilizotungwa kusimamia hizo sheria mama ndo utaweza kuona ni namna gani 'censorship' inavyofanyika Tanzania katika jitihada za dola kulinda 'maadili" ya kitanzania.

Kwa hiyo kuna sheria zilizogawanyika katika maeneo mawili katika hili suala la pornography:

Mosi, sheria zinazosimamia na kulinda usambazaji wa habari na kuhakikisha mbali na mambo mengine picha za uchi hazisambazwi Tanzania ( rudia kusoma habari ya vijkarida vya ngono -ubungo)

Pili kuna sheria ya makosa ya jinai (Penal Code) Chapter XV. Offences against morality - kama sheria hii ilivyofanyiwa marekebisho na sheria ya makosa ya kujamiina ya mwaka 1998 (SOSPA).

Hakuna set ya sheria Tanzania ambayo inasimamia kusambaza , kununua au kumiliki pornographic materails.
 
Wapi hapo Mzee Shadow?

Sheria za magazeti hizo hapo juu, si utaje sehemu Mkuu! Wapi iliposemwa Waziri ana nguvu ya ku regulate ethics za waandishi wa habari (kitu ambacho wewe unaki equate na porno), wapi Mzee?

Pia kwenye Penal Law, under "Offenses Againts Morality," uliyoitaja, naomba mstari mmoja tu unaongelea porno! (Nime attach Penal Code hapo chini iwe rahisi kwako ku copy and paste mstari. Kama zimerekebishwa na SOSP Act, na hiyo nayo nimeiweka hapo chini tuweze kuona ni wapi SOSP Act ime amend chapter XV of Penal Code ikaongelea prohibition of Porno).

Mwisho, japo si mwisho wa yote, una maana gani "Hakuna set ya sheria Tanzania ambayo inasimamia kusambaza , kununua au kumiliki pornographic materails"? Ningependa kujua kama, na ni wapi, wamefuta sheria inayokataza "Traffic in Obscene Publication" iliyoandikwa Section 175 of the Penal Code.
 
Attachments

  • PENAL CODE of 1980.pdf
    549.2 KB · Views: 102
Sasa wakulu mkisha kubaliana ukweli uko wapi mmoja atoe summary ya makubaliano yenu wanasheria. Maana hoja zenu wote zinafanana na ukweli japo ukweli wenyewe ninyi ndio mnaoujua zaidi. Hapa mi ni mwanafunzi wenu.
 
Utamaduni wa Mtanzania hauruhusu mambo hayo. Utafungwa kwa kutumia kigezo hicho tu.
 
Wapi hapo Mzee Shadow?

Sheria za magazeti hizo hapo juu, si utaje sehemu Mkuu! Wapi iliposemwa Waziri ana nguvu ya ku regulate ethics za waandishi wa habari (kitu ambacho wewe unaki equate na porno), wapi Mzee?

Pia kwenye Penal Law, under "Offenses Againts Morality," uliyoitaja, naomba mstari mmoja tu unaongelea porno! (Nime attach Penal Code hapo chini iwe rahisi kwako ku copy and paste mstari. Kama zimerekebishwa na SOSP Act, na hiyo nayo nimeiweka hapo chini tuweze kuona ni wapi SOSP Act ime amend chapter XV of Penal Code ikaongelea prohibition of Porno).

Mwisho, japo si mwisho wa yote, una maana gani "Hakuna set ya sheria Tanzania ambayo inasimamia kusambaza , kununua au kumiliki pornographic materails"? Ningependa kujua kama, na ni wapi, wamefuta sheria inayokataza "Traffic in Obscene Publication" iliyoandikwa Section 175 of the Penal Code.

Mzee Kuhani, with due respect:

Kwa faida ya wasomaji, naomba nianzie chini kwanza kwa kuangalia nini maana ya neno “Pornography”. Nitatumia kamusi ya “Black Law Dictionary” toleo la mwaka 2008 pg. 1199 naomba kunukuu:

“Pornography, material (such as writings, photographs, or movies) depicting sexual activity or erotic behavior in a way that is designed to arouse sexual excitement * Pornography is a protected speech under First Amendment unless it is determined to be legally obscene. The last part shows the legal protection under the U.S. Constitution.

Deriving from the same which is echoed again on our SOSPA (1998):
Black Dictionary defines “child pornography” to mean: material depicting a person under the age of 18 engaged in a sexual in sexual activity. (Child Pornography is not protect by 1st Amendment) even if it fall falls short of the legal standard for obscenity – and those directly involved in its distribution can be criminally punished”

Having quoted from that legal authority, so that to simplify my argument as far criminating and sanctioning of pornographic materials is concerning under the Tanzanian Jurisdiction then lets now look at the particular laws:

As I expressly referred to chapter five of the Penal Code as amended by SOSPA (1998) and the section I referred are as follow as far as indecency act ( to which under our laws pornography is part of it) is section 38A of SOSPA

138A. Any person who, in public or private commits, or
is a party to the commission of, or procures or attempts to
procure the commission by any person of, any act of gross
Indecency with another person, is guilty of an offence
and
liable on conviction to imprisonment for a term not less than
one year and not exceeding five years or to a fine not less
than one hundred thousand and not exceeding three hundred
thousand shillings; save that where the offence is committed
by a person of eighteen years of age or more in respect of
any person under eighteen years of age, a pupil of a primary
school or a student of secondary school the offender shall be
liable On Conviction to imprisonment for a term not less than
ten years, with corporal punishment, and shall also be ordered
to pay compensation Of all amount determined by the court
to the person in respect of whom the offence was committed
for any injuries caused to that person,'

138B- (I) Any person who-

(a) knowingly permits any child to remain in any promises,
for the purposes of causing such child to be sexually
abused or to participate In any form of sexual activity
or in any obscene or indecent, exhibition or show
;
children
(b) acts as procurer of a child for the, purposes of sexual
intercourse or for any form of sexual abuse or indecent
exhibition or show;
(c) induces a person to be a client of a child for sexual
intercourse or for any form of sexual abuse, or inde-
cent exhibition or show, by means of print or other
media, oral advertisements or Other similar means;
(d) takes advantage of his influence over, or his relation.
ship to, a child, to procure the child for sexual, intor.
course or any form of sexual abuse or indecent exhib.
ition or show-

On the other limb of my argument was that minister under the newspaper act as been given a power to make regulations to control mass media. Under the two laws the work of the minister is to do the censorship of what ought to be published. He/she can sanction any media or publishing house for a certain period or indefinitely. The same power has been granted to the board ya utangazaji.

To drive the point home, my argument as far the issue of not having a set of law governing pornography was that there are several laws which regulate indecency acts (read pornography) and that there is no single law that does that in Tanzania.
There those laws that provides for the dissemination, conducts and ethics such as news paper Act 1976(soon to be repealed) and there those laws that criminalize such as Penal Code Chapter XV as amended by the SOSPA.

Recommendation:

Tanzania is no longer an oasis in this world of cyber space, I am urging the three arms of government to have a look and enact a new law that will specifically deal with Cyber crimes and child pornography.

Shadow.
 
Shadow, naona leo hauko direct.

Ni hivi:

Awali ya yote, hakukuwa na mjadala juu ya maana ya neno pornography katika mwamvuli wa sheria za Tanzania. Na hata kama ingekuwepo, nisingeshawishika na "authority" ya Black's Law Dictionary. Sio tu kwamba ni kamusi ya mfumo wa kigeni, bali hata huko ugenini kwenyewe hakimu wa Kimarekani anapokuwa na utata katika kutafsiri maana ya neno (kama maana ya kisheria au kitaalam haijulikani) kitu cha kwanza anafanya ni kutafuta "the ordinary meaning of the word," hivyo anavuta a Websters! Akitoka hapo mchezo wa dictionary umekwisha, anaenda kwenye step nyingine ya kutafsiri sheria, statutory construction, kama vile kutafuta nia ya wabunge, legislative intent. Kwa hiyo tafadhali tuweke pembeni uchambuzi wa kigeni hapa, hususan kutumia "authority" zisizo authority.

La pili, Waziri hawezi kupewa nguvu ya kuandika regulations zinazo kataza pornography kwa kigezo cha ku regulate ethics za uandishi kwa sababu ethics za profession huwa ni tenuous, debatable, principles even within the field itself, huwezi kumfungisha mtu jela kwazo. Bunge ndio linaandika, lina define vitendo au kutokutenda kunakotengeneza a criminal offense, linaweka mens rea, penalty, actus rea and all that good stuff. Vitu anavyoruhusiwa Waziri ku regulate sio pornography:
Section 53, Newspaper Act, 1976
The Minister may make regulations
for the better carrying into effect the purposes and provisions of this Act, and without prejudice to the generality of the foregoing, may make regulations:

(a) prescribing the forms of registers, returns, applications notices and bonds, and other forms to be used under this Act;

(b) prescribing the particulars and other matters to be entered in the registers:

(c) prescribing the place and manner of keeping copies of newspapers delivered to the Registrar under this Act, or the manner in which and the purposes for which any such copies shall, consistently with the purposes and provisions of this Act, be dealt with or disposed of;

(d) prescribing the information to be furnished to the Registrar by way of periodical return or otherwise;

(e) prescribing the particulars and matters to be published by the Registrar and the manner of such publication;

(f) prescribing the fees which may be levied under this Act,

(g) Prescribing anything which under this Act is to be or may be prescribed.

Tatu, unasema "hakuna set ya sheria Tanzania ambayo inasimamia kusambaza, kununua au kumiliki pornographic materails" lakini hukuonyesha ni lini wamefuta prohibition ya "Traffic in Obscene Publication" under the Penal Code:

Traffic in Obscene Publication
Penal Code, Sect. 175 (1 )

Any person who:

(a) for the purpose of or by way of trade or for the purpose of distribution or public exhibition, makes, produces or has in his possession any one or more obscene writings, drawings, prints, paintings, printed matter, pictures» posters, emblems, photographs, cinematograph -films or any other objects or any other object tending to corrupt morals:

(b) for any of the purposes above mentioned... in any manner whatsoever puts any of them in circulation; or

(c) carries on or takes part in any business, whether public or private, concerned with any such matters or things... or distributes ...or exhibits...in public

(d) advertises or makes known by any means whatsoever with a view to assisting the circulation of, or traffic in, any such matters or things…

(e) publicly exhibits any indecent show or performance or any show or performance tending to corrupt morals,

is guilty of a misdemeanour, and is liable, to imprisonment for two years or to a fine of two thousand shillings.

La nne, section 138 A of SOSP Act inayosema "Any person who, in public or private commits, or procures any act of gross Indecency is guilty of an offence" haiongelei pornography kwa sababu kinachokuwa criminilized hapa ni "gross indecency." Ukurasa wa mbele, wa mwanzo kabisa katika sheria hii ume define "gross indecency" means sexual act that is more than ordinary but falls short of actual intercourse and may include masturbation and indecent physical contact or indecent behaviour without any physical contact.

Kwa hiyo ukiuza gazeti la kikubwa, kwa mfano, hiyo provision haikuhusu, ila mkono wa sheria utakufikia kutumia Penal code, section 175 inayokataza biashara za usambazaji wa obscene material. Kwa upande wa child pornography ni SOSP Act sect. 138 B na sio "gross indecency" provisions za section 138 A. Hiyo 138 A inakataza kugusana, kujigusa, au kuwa na tabia freaky freaky!

Bm21, heshima mbele. Unasema mmoja aandike summary. Well, obviously hakuna makubaliano, lakini hata yangekuwepo nisingekubali falsafa yako ya kuwaachia "wanasheria...mnaojua zaidi" watoe hitimisho la wote. Isitoshe, mimi si mwanasheria wala mwana chochote. Lakini hata mahakamani kuna wazee wa baraza ambao wanachambua smokescreen na bullcrap za wanasheria. Tazama bullcrap za Andrew Chenge na smokescreen za Pinda, Masha, Sitta, Simba, na wanasheria wengine tuliowaamini kuendesha meli. Katika enzi hii ya mapinduzi ya habari atakaekuja akasema "mimi ndiye yule ajae kuwaletea habari njema na neno la kweli, kwa maana nalikufa mtini kwa ajili yenu" ataambiwa "onyesha mbavu."

I am done talking.
 
Last edited:
Naomba ni modify swali nzima ili lilenge kitu ambacho natafutia jibu; Ni sheria gani ina regulate pornography? Msisitizo wangu hasa ni kujaribu kuangalia issue kama hii:

a. Mke na Mume wakipiga picha za utupu au za mambo yao ya ndoa na wao wakapeana picha hizo, mmoja wao akikutwa nayo itakuwa ni porn kwa misingi ya sheria mlizonukuu?

b. Binti wa kike zaidi ya miaka 18 ambaye hafanyi kitendo chochote cha kingono na akapiga picha ya kuonesha maumbile yake kumtumia rafiki yake wa kiume, mchumba n.k na mtu mwingine akainasa picha ile atakuwa amevunja sheria yoyote ile?
 
Mmmhh...some people in here can relate to that...hehehehehe
 
Naomba ni modify swali nzima ili lilenge kitu ambacho natafutia jibu; Ni sheria gani ina regulate pornography? Msisitizo wangu hasa ni kujaribu kuangalia issue kama hii:

a. Mke na Mume wakipiga picha za utupu au za mambo yao ya ndoa na wao wakapeana picha hizo, mmoja wao akikutwa nayo itakuwa ni porn kwa misingi ya sheria mlizonukuu?

b. Binti wa kike zaidi ya miaka 18 ambaye hafanyi kitendo chochote cha kingono na akapiga picha ya kuonesha maumbile yake kumtumia rafiki yake wa kiume, mchumba n.k na mtu mwingine akainasa picha ile atakuwa amevunja sheria yoyote ile?

Mwanakijiji, Heshima yako,

Kifungu cha 175(a)(d) cha sheria ya jinai Kinaweza kutumika kuwatia matatani watuhumiwa kwani ni kazi kuweka kwa mtuhumiwa kuonyesha kwamba hakuwa na nia ya kusambaza picha hizo kwa mujibu wa vifungu hivyo viwili.

175.—(1) Any person who—

(a) for the purpose of or by way of trade or for the purpose of
distribution or public exhibition, makes, produces or has in his
possession any one or more obscene writings, drawings, prints,
paintings, printed matter, pictures» posters, emblems, photographs,
cinematograph -films or any other objects or
any other object tending to corrupt morals: or

....

d) advertises or makes known by any means whatsoever with a
view to assisting the circulation of, or traffic in, any such
matters or things, that a person is engaged in any of the acts
referred to in this section, or advertises or makes known
how, or from whom, any such matters or things can be
procured either directly or indirectly;
 
Nadhani nawapata vizuri sana. Vipi kuhusu Privacy ya mtu chumbani/nyumbani kwake? kama mtu yuko katika chumba chake na mkewe au wapenzi wawili na mtu (a pervert) au vinginevyo anarekodi hayo na kuyachapa kwenye kwenye vyombo vya habari. Najua sheria itakayomshtaki msambazaji, lakini wale watu wenyewe (mke na mume, wapenzi) wana legal recourse gani ya kutetea privacy yao na hata ikibidi kulishtaki gazeti au chombo kilichotangaza mambo yao ya chumbani?
 
Kwa dhana hiyo,

Then hilo suala litakuwa linaingia katika makosa ya madai (Tort Law) ambayo test yako ni kulingana na ushaidi ulio nao kuthibiisha dai au madai yako( Under the balance of probability au prepondorance of evidence). Mara nyingi unaweza kutoka kesi zilizokwisha amuliwa na mahakama za Tanzania au kutumia kesi za nje katika kujaribu kuishawishi mahaka kuamua kulingana na matakwa yako ( persuasive authority).

Pili, hapo mshitaki (Plaitiff) anaweza kuomba mahakama imuaru mshitakiwa alipe gharama za "kumuumiza" ( damage) ambazo zinaweza kuwa general au specific kulingana na mahakama itakavyoona.

Kwa sasa ni hayo tu.

Shadow.
 
Mhh JF..kwa kweli nimeikubali.
Yaani mtililiko wa jamaa hawa wanasheria ni mzuri...na unaenda kwa fact....
Keep it up wakuu.
 
Kulitokea kesi dhidi ya uendeshaji madanguro, sikumbuki walitumia sheria gani. Kama mpaka Monday utakuwa hujapata, I'll be in a better position kukupatia references.

Nahisi Tanzania ni moja ya nchi zilizoidhia azimio la UN. Azimio hilo ambalo linakataza biashara ya binadamu, pia linaharamisha mtu yeyote kufaidika kwa namna yoyote na ukahaba wa mtu mwingine. Article 3, ya Azimio la UN kuhusu ya biashara ya watu inatafsiliwa kama:

paragraph (a) "Trafficking in Persons defines Trafficking in Persons as the recruitment, transportation, transfer, harbouring or receipt of persons, by means of the threat or use of force or other forms of coercion, of abduction, of fraud, of deception, of the abuse of power or of a position of vulnerability or of the giving or receiving of payments or benefits to achieve the consent of a person having control over another person, for the purpose of exploitation. Exploitation shall include, at a minimum, the exploitation of the prostitution of others or other forms of sexual exploitation, forced labour or services, slavery or practices similar to slavery, servitude or the removal of organs."

Kwa hili hata kwa nchi zilizoruhusu ukahaba, anayetakiwa kufaidika nao ni yule tu anayeufanya na sio dalali au mwendeshaji wa danguro; unless, awe amewapangisha hawa makahaba kwenye hiyo nyumba inayodaiwa kuwa danguro; kama wapangaji wa kawaida na wenyewe wakafanya ukahaba kwa raha zao.
 
Last edited:
Back
Top Bottom