Sherehe za miaka 47 ya Muungano

EL lazima awepo, wanajidai kusema mafisadi waondoke ila kuwataja majina hawadhubutu kwa hiyo yupo kwenye chama kama kawa. Labda keshajivua gamba na kawa mpya ila sumu ni ile ile na amekuja kwa heshima ya chama chake kuuenzi muungano....
 
naona viongozi wa ccm wanachelewa kufika uwanjani maana hawana ha kuzungumza juu ya muungano-coz umejaaa matatizo
 
JK anaingia uwanjani.
Yuko kwenye gari la wazi pamoja na CDF mwamunyange, wanazunguka uwanja na kushangiliwa kwelikweli!
 
kama sherehe inaisha saa 6 kamili- muda huu JK ndo anafika -had halaiki na magwaride na utambulisho wa wagen uishe itakuwa ni sa 6 kasorobo-then yeye atasalimia tu na kufunga shehere pasipo kuzungumza jambo lolote
 
JK Anapokea heshima ya kijeshi, inapigwa mizinga sambamba na wimbo wa Taifa.
 
Uwanjani kukoje? Yaani wananchi wamejitokeza kwa wingi au waliopo ni kama mafungu ya manyasi ktk uwanja wa kwata?
 
Uwanjani kumejaa tisheti za rangi ya bendera, hiyo inamaanisha wengi waliopo huko uwanjani wamepata bahasha zao tayari
 
Hivi jamani haya mambo ya Muungano nafikiri iko haja kuyazungumza kwa undani na kwa umakini sana.Inapaswa tujiulize kama sababu zilizopelekea muunganiko huu mwaka 1964 bado ni valid lakini tuangalie faida zingine kama zipo kwasasa za muungano huu otherwise tufanye referendum tuone maoni ya wananchi wetu wa pande zote za muungano. isije ikawa huu ni muungano wa Kikwete tu na labda na wazee wengine wachache!
 
Uwanjani kumejaa tisheti za rangi ya bendera, hiyo inamaanisha wengi waliopo huko uwanjani wamepata bahasha zao tayari
kweli, Nakumbuka kuna watoto waliandamana baada ya kunyimwa bashasha siku ya kuzima mwengi kule Kigoma kama sikosei...
 
Hizo bendera 2 zilizoshikiliwa na kikosi cha bendera ni zipi? Mie sizijui. Nielewesheni.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom