Sherehe bila kadi wala MC mnaionaje?

charger

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
2,320
1,369
Habari mabibi na mabwana wa baraza,naamini mpaka unasoma uzi huu basi utakuwa umzima wa afya.Kama sivyo nikupe pole.
Leo ninataka niwaletee hii mada ambayo inaweza kuwa namitazamo tofauti kwa wana jamvi.
Jambo lenyewe ni kuhusu sherehe.Watu wengi kama sio wote wanapenda sherehe na kushereheka na watu wao maalum.Na sherehe inakuwa sherehe nzuri kama una mtu wako maalum wa kwenda nae huko shereheni.Ishu inaanzia hapa,utakuta mmepokea kadi kwamba Bi&Bw flani mnaalikwa kwenye sherehe Fulani,ukumbi utatajwa au eneo la tukio,muda,na mambo mengine kadhawakadha mfano watoto hawaruhusiwi.Na sherehe ikianza kunakuwa na ratiba maalumu kwamba kitaanza hichi na kumalizika na hichi.Kwa mfano kama ni harusi utasikia
1.Wageni kuingia ukumbini
2.Utambulisho
3.Kukata keki/ndafu
4.kutoa zawadi
5.Chakula ………………………………………….na mambo kibao tu
Kwa mtazamo wangu minadhani sherehe isiyokuwa na kadi,ukumbi maalum,au ratiba huwa inapendeza na kufana zaidi.Sherehe bila MC,Kwa mfano kama ni harusi basi sio kila siku bibi harusi abebe bwana siku nyingine mambo yanabadilika, zawadi inatolewa mlangoni na sio ukumbini, keki inaliwa kwenye gari,mziki unafunguliwa bafuni,maharusi wanapanda baiskeli sio gari,au maarusi wanatembea kwa miguu,au ukumbi bila viti,nataka kumaanisha yani mchanganyo tu hiyo inakuwa poa zaidi au wadau mnaonaje????au mnapenda mambo yampangilio na format ???????????
Nawasilisha kwa yeyote atakaye husika.
 
Mkuu charger...mawazo yako ni ya kizazi kijacho au ni hiki hiki cha masharobaro!!!

Mkuu Vince ni yale yale mambo yetu au topic imekua ngumu?:lol::lol::lol:
 
Mpiga picha anapiga kwa simu yake ya mchina, ila kadi muhimu mpangilie ndo usiwe ule tuliouzoea kila siku mc nae sio kila siku chumvichumvi
 
Halafu sherehe zingin formallity zilezile zinaboa sana ma mc wajaribu kuwa wabunifu sherehe ifane
 
Back
Top Bottom