Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SHENAZ amefariki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Sep 10, 2007.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2007
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 10,035
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  KWA HUZUNI ILIYONIJAA MOYONI NINGEPENDA KUTOA TAARIFA YA KIFO CHA DADA YETU na MTOTO WA ILALA BI SHENAZ. KWA NIABA YA WANA JAMBO FORUMS KULE KWENYE MAPENZI NA BURUDANI PAMOJA NA JAMBO FORUMS KWA UJUMLA NINGEPENDA KUTOA RAMBI RAMBI ZETU NA KWA SISI WENGINE TUNASEMA INNA LILLAHI WA INNA ILLAHI RAJUUN
  [​IMG]
  Malkia wa kunengua miondoko ya Taarab na Mduara nchini, Shenazi Salum pichani ni miongoni mwa watu 27, waliokufa kwenye ajali ya basi, iliyotokea juzi kwenye Kijiji cha Majenje, Mbarali, Mbeya.

  Kwa mujibu wa mdogo wa mwanamuziki huyo aitwaye Hanifa Salum, Shenazi alifariki dunia, muda mfupi baada ya kutokea ajali hiyo, iliyohusisha magari matatu....

  alisema, Shenazi alipata ajali hiyo, alipokuwa akirejea nyumbani kwake Dar es Salaam na alikuwa akitoka Tunduma, Mbeya kwenye shughuli zake za muziki "Alituaga kwamba anakwenda Mbeya kufanya ‘shoo', hatukujua kama ndiyo kifo kilikuwa kinamwita, lakini ndiyo hivyo Mungu kamchukua," alisema Hanifa huku akitokwa na machozi.
  Rafiki wa Shenazi ambaye naye ni mnenguaji maarufu, Mwajuma Thabit ‘Rose Jimama', anasema kuwa marehemu alikwenda Mbeya na mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la Tuki.

  Rose alisema: "Nilipata taarifa kama Shenazi amepata ajali, nikapiga namba yake, ikapokelewa na polisi mmoja huko Mbeya, nikamuomba nataka kuongea na Shenazi, akanijibu, unataka kuongea na maiti? "Nilichanganyikiwa, yule polisi aliniambia rafiki yangu Shenazi amekufa na Tuki hali yake ni mbaya, nidhani utani, lakini yote ni mipango ya Mungu."

  Habari zaidi zilisema kuwa rafiki huyo wa Shenazi, Tuki, amevunjika miguu yote na alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Chimala, Mbarali. Shenazi alikuwa kwenye basi la SABCO aina ya Scania, T443 APF ambalo liligongana na lori pamoja na magari mawili yanayomilikiwa na Halmashauri ya Mbarali.
  [​IMG]
  Ajali hiyo iliyoua watu 27, ilisababisha majeruhi 33. Shenazi alitarajiwa kuzikwa jana ambapo mwandishi wetu walifika nyumbani kwao, Ilala, Dar es Salaam na kukuta taratibu za mazishi zikiwa zimeshaanza kufanywa. Mbali na kunengua, malkia huyo atakumbukwa kama kungwi, aliyekuwa akiwafunda watu kabla ya ndoa, pia ni mwigizaji ambapo enzi za uhai wake aliwahi kucheza Filamu ya Kitchen Party ambayo ilipata umaarufu mkubwa.

  INNA LILAHI WA INAA LILAHI RAJWUUN


  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Sep 10, 2007
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 8,079
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 48
  Binafsi simfahamu huyu Shenaz, lakini ndiyo hivyo, kazi ya Mungu haina makosa. Nammwombea Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake pema peponi hadi tutakapokutana tena siku ya kiyama.
   
 3. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 4,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mungu amlaza mahala pema peponi, amina !
   
 4. t

  tz_devil JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2007
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 318
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 18
  Inna Lillahi Wainna Lillahi Rajuun.

  Wana JF, hili suala la ajali Bongo linatisha. Watu 27 wamepoteza maisha na wengine 33 wamejeruhiwa vibaya sana na sheria za usalama barabarani zipo. Haupiti mwezi tunasikia ajali za kutisha kama hizi; hivi serikali inampango gani? Mzee Mwapachu na wizara yake wako wapi? Inasikitisha.
   
 5. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2007
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 10,035
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  naweza kusema kuwa niliwahi kuwa very close na huyu dada wakati naishi Ilala flats..huyu dada alikuwa hana khiyana na alikuwa na roho nzuri sana na mimi kwa kweli private life yake ilikuwa hainipi tabu kabisa. Yaani I am still in shock!
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Sep 10, 2007
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 8,079
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 48
  Vipi picha zimefutwa? hazionekani tena.
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2007
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 10,035
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  naona zimefutwa
   
 8. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 3,048
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 38
  Ina Lilah wa Ina Ilaihi Rajiuun... Sijui kama leo Melody watapiga muziki pale LANGO LA JIJI, maana ni mwanachama wao.
   
 9. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2007
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 925
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 18
  RIP shenaz. InAfrica Band watamkumbuka sana.
   
 10. M

  Masatu JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2007
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,756
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mhhh!!!!!!!!!
   
 11. Ole

  Ole JF-Expert Member

  #11
  Sep 10, 2007
  Joined: Dec 16, 2006
  Messages: 1,168
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 38
  Hakuna aliyefuta picha zozote. Angalia source yako.

  Thanks.
   
 12. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #12
  Sep 10, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,750
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 38
  mungu amlaze pahali pema peponi ameen

  pia nnawapa pole ndugu, wanafamilia, majirani, mashabiki wake na vipenzi vyake pamoja na wote walioathirika na msiba huu kwa njia moja au nyengine
   
 13. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #13
  Sep 10, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 3,042
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 38
  Bwana alitoa, bwana ametwaa Jina lake na lihimidiwe!

  Tangulia tu nyuma yako sote tu wakuja!

  Familia Poleni sana mlio guswa na misiba hii, pia Naomba Mungu awaponye haraka majeruhi walioko hospitalini.
   
 14. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #14
  Sep 10, 2007
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 4,085
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  RIP Shenaz
   
 15. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #15
  Sep 10, 2007
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 1,656
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 48
  brazameni mbona unatuacha kwenye mafumbo?
   
 16. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #16
  Sep 10, 2007
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,279
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mungu amlaze mahali pema.


  Brazameni bana, wapeleke mapenzi na mapendo/pugu road ukawaelezee basi.
   
 17. comfort

  comfort Member

  #17
  Sep 10, 2007
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona waguna vp???:confused:
   
 18. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #18
  Sep 10, 2007
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,542
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 48
  Ingawa namsikiaga tu kwa mbali, lakini kwa kuwa ni bin adam mwenzangu na mtanzania ambaye anapoteza maisha bila hatiya walah namuombea fanaka huko aliko ingawa tutavuna tulichopanda hapa duniani....

  ...Wewe brazameni mboni kuweka habari nusunusu?? ina maana ulikuwa unaingilia private zake au una maana gani??? Tujue kama ulikuwa shemeji yetu au mzee wa private.... Lakini pile sana kaka
   
 19. Jembajemba

  Jembajemba JF-Expert Member

  #19
  Sep 10, 2007
  Joined: Feb 3, 2007
  Messages: 714
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  Mmmh !!! jamani taratibuni huyu keshakuwa marehemu tujaribu kumuheshimu, sio kuanza kumtolea aibu zake - haifai waungwana.

  Ninamuomba M/Mungu amsamehe madhambi yake, kwani sisi bin-adam sote ni wenye kufanya makosa.

  sisi tuliokuwa hai tujitayarishe na safari ya kwenda akhera kwa kuacha yale ambayo Muumba katukataza kwayo, hapa duniani ni mwenye kupita tu njia sio maskani yetu, kama sio leo basi kesho unaweza kurudisha namba.

  wafiwa nawaomba muwe na subira katika kipindi hiki kigumu. na wale ambao wamelazwa hospitali nawaombea kwa M/Mungu awajaalie wapone haraka na warudi katika shughuli zao za kujenga Taifa - amen.
   
 20. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #20
  Sep 10, 2007
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,542
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 48
  ..Sure sure and i am deeply sorry if i offended anyone especial wafiwa... I am afrikan and i must respect customs...
  Jamani niliteleza ila natumai mtaniweka ktk fungu la wastaarab tena...
   

Share This Page