Shemeji mbona unatuumiza?

Mwalufunamba

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
211
129
Huyu ni shemeji yangu kwa kaka yangu amabaye tulitengeneza undugu shuleni. Nilipokuwa naingia form I yeye alinipokea akiwa Form III. Alinipenda, nikampenda. Ndiye aliyenifanya nisionje manyanyaso yoyote ya Form II. Tukiwa shuleni alikuwa mshauri wangu mzuri pia ndiye aliyekuwa mweka vitu vyangu vya thamani. Wazazi wangu walimpenda na hata wake walinipenda; tunatokea wilaya na vijiji tofauti na tulikutana shuleni tu.

Katika shule alizopita (O and Alevels) na Chuo, ndiko nami nilikopita.

Katika harusi yake nilikuwa Mtunza fedha. Japo ukweli ni kuwa toka hatua za awali kaka yangu kumtafuta shemeji nilijulishwa na kaka mwenyewe, siku ya kutoa mahali nilikuwa katika msafara.

Nilipokuwa katika maandalizi ya kuoa, shemeji alikuwa ndiye wifi mshika bango la nguvu kuona kila kitu kipasacho kwa bibi harusi mtarajiwa kuwa nacho, anapata. Kwa sababu hiyo baada ya harusi jina la shemeji lilikufa na kuwa "Mama mdogo" Ambalo lilipelekea hata mumewe kuwa "Baba mdogo"

"Mama mdogo" toka mwaka jana mwishoni hadi sasa ni hili, anapenda kuvaa sketi ambazo pindo lake la chini liko juu kidogo na magoti ama exactly na magoti. Sasa tatizo ni pale anapopanda pikipiki, mapaja mpaka nguo za ndani nyakati fulani zinakuwa katika matangazo. Bahati mbaya ni kuwa hayo ninayaona kwa macho yangu kwa kuwa ofisi zetu zipo jengo moja japo ni makampuni mawili tofauti; na sisi tupo ground floor. Wao walihamia mwaka jana mwanzoni, baada ya sisi. Siku nyingine wafanyakazi wenzangu wananiambia "mwone mama yako"" paja za mama zinalipa" "kwanini usifumbe macho, umama wenyewe wa hiari; kwani kuna ubaya gani kuonja kwa shemeji" na kadha wa kadha.

Nilimwambia "mama mdogo", kuwa nguo hizo zinampunguzia heshima na watu wanaanza kumdharau, kwani wanamwona anapokuja au anapotoka ofisini. Anaitikia vizuri kuwa amesikia lakini utekelezaji sifuri.

Siku moja nikamwambia Baba mdogo, na nikamwambia asifiche aseme ni mimi nimesema. B' mdodgo alimwambia na siku moja nikaitwa. Tulikuwa na mjadala mzuri kabisa. Ma mdogo anakubaliana na ukweli huo lakini anang'ang'ania ni nguo anazozipenda. Siku hiyo, mumewe alimwambia heshima yangu inalindwa na wewe. Unapokuwa kituko huko nje, heshima yangu inapungua sana. Alisema mengi kwa kweli.

Nje ya mazungumzo Ba' mdogo aliniambia, alikwisha mkataza mara kadha kuvaa sketi hizo. alizishitukia siku walipokuwa wakwenda kazini na gari yao. Alipokaa kiti cha mbele, nguo ilijivuta na mapaja yakawa wazi. Alimwambia arudi akabadilishe nguo anamsubili hadi atakapokuwa tayari. Alirudi kubali nguo. Baadaye akawa anakaa kitu cha nyuma anapogundua "amevaa tatizo". Sasa siku hizi anamtindo, anapovaa nguo hizo anakwepa kupanda gari ya familia. Anasingizia kuwahi sana kazini, na kupanda daladala. Akishuka kituoni anapanda pikipiki hadi kwenye jengo letu. Kitendo cha kutokupanda gari la familia na mkewe kimekuwa kinamhuzinisha kiasi kwamba siku akisema hapandi gari, naye anaamua kuliacha anapanda daladala."Sitaki kuonekana ninamsimanga mke wangu kwasabababu ya gari.Yeye anapanda daladala, mimi niko kwenye gari ya famiilia. No" aliniambia. alisema pia kuna mtu alikwisha mbwatukia kuwa haoni aibu mkewe kuchapa lapa kwenye vumbi na kupanda daladala wakati yeye anakwenda kazini na gari ambalo anajaza watu wengine, waomba lift?

Shemeji anatuumiza, mimi, Baba mdogo na mke wangu (japo naamini wako wengine wengi wanaochukizwa na vaa yake). Naomba ushauri nini kifanyike ili asiendelee.

{Baba mdogo kaniruhusu niandike hili hapa, yeye hajajiunga na JF ila huwa anapita kusoma}
 
Huyo anahitaji kushughulikiwa.....
We mwache tu, Ulimwengu utamfunza.....
 
Huyo mama mdogo si mtoto mdogo, atakuwa anafahamua analolifanya na kwa nini anafanya hivyo. Wa kumuweka kiti moto na kumdadisi kwa undani zaidi kinachomsibu ni mume wake, na siyo mtu mwingine yeyote.
 
Mpaka huyo shemeji atakapoona ni tatizo, au mtakapomconvice kuwa ni tatizo kuhusu uvaaji wake; na kumpa sababu ambazo ataziona ni za msingi; mtakuwa mnatwanga maji kwenye kinu.

Mmeshamuweka kikao mara nyingi lakini yeye majibu yake ni kuwa ndizo nguo anazozipenda.

Tafuteni, au wadada au wamama wenye mtazamo kama wake halafu muongee nao ili labda wao watajaribu kumuonesha bado anaweza pendeza akivaa nguo zilizo ndefu kidogo.
Na pia mpaka pale ambapo utamaduni utabadilika, kwa muda huu tamaduni yetu inaelekeza aina fulani ya mavazi kwa mazingira fulani na kwa umri fulani.
 
Ningekuwa Mumewe, Ningekuanya hizo nguo zote na kuzichoma moto tuone atafanayeje, na ningepitisha sheria kuwa sitak kuziona ngu za aina hiyo Kwangu na nisingetaka majadiliano zaid ya utekelezaji, Mwambie Ba Mdogo aache ujinga na kuwa strong, Unless anatengeneza Mazingira ya Mamdogo kuja kumegwa one day
 
Akikua ataacha! lakini naona kuna tatizo hapo, kwanini huyo mama mdogo amsikilize mumewe? hamuheshimu? au mumewe ni mpole kiasi kila anachomwambia anadharau. Na je, vp kwa mambo mengine akimwambia/akikatazwa huwa anatekeleza? hizo nguo fupi ameanza kuvaa baaada au kabla ya ndoa?
 
Ningekuwa Mumewe, Ningekuanya hizo nguo zote na kuzichoma moto tuone atafanayeje, na ningepitisha sheria kuwa sitak kuziona ngu za aina hiyo Kwangu na nisingetaka majadiliano zaid ya utekelezaji, Mwambie Ba Mdogo aache ujinga na kuwa strong, Unless anatengeneza Mazingira ya Mamdogo kuja kumegwa one day

Wana Jf wanaogopa sana kumegewa...
 
Mwambie Mumewe amwambie msimamo wake kuhusu hizo nguo na aanze mtindo wa kumnunulia Mkewe nguo ndefu lakini zinazofanana na zile anazopendelea Mkewe
 
Aiseee babaangu mpeleke ubungo kwa mzee wa upako ikishindikana chukuwa kimini chake kimoja 2 nenda nacho kwa kakobe kikaombewe
 
nyie ndo mnaovunjaga ndoa za watu......

Na huyo kaka yako mnafiki, kipindi chote hakujua nguo anazopenda mwenza wake mpaka wakaja kuoana?

Akishavaa nguo chini ya goti mtamwambia nywele zinatamanisha.......

Mwisho mtamwambia chakula hakinogi aache kazi apike jamani...................

Hakuyaona haya kabla hajamuoa?
Kubadili mitindo ya mavazi wangeanzana wenyewe hukoooooo ila kwa sasa unajenga chuki tu hapo kati yako na shem wako......... Ipo siku utakuja na thread hapa
 
talk to her in a positive way huku mkimshauri mavazi mbadala takayoyapenda.

Kama habadiliki endeleen kumpenda na kumjali huku mkimshauri kwa upendo.

I believe with time atabdailika. hawezi vaa vimin maisha yake yote.

Binadamu tuna evolve go to pick, decline and then die.

If u cant win her, leave her or join her.
 
kwani mumewe hana sauti kwa mkewe, kama habadiliki hyo inaonesha dharau ya hali ya juu!!!!!
 
Mpaka huyo shemeji atakapoona ni tatizo, au mtakapomconvice kuwa ni tatizo kuhusu uvaaji wake; na kumpa sababu ambazo ataziona ni za msingi; mtakuwa mnatwanga maji kwenye kinu.

Mmeshamuweka kikao mara nyingi lakini yeye majibu yake ni kuwa ndizo nguo anazozipenda.

Tafuteni, au wadada au wamama wenye mtazamo kama wake halafu muongee nao ili labda wao watajaribu kumuonesha bado anaweza pendeza akivaa nguo zilizo ndefu kidogo.
Na pia mpaka pale ambapo utamaduni utabadilika, kwa muda huu tamaduni yetu inaelekeza aina fulani ya mavazi kwa mazingira fulani na kwa umri fulani.

Nashukuru. Nafikiri hapo kwenye bold ni utakelezaji tu.
 
nyie ndo mnaovunjaga ndoa za watu......

Na huyo kaka yako mnafiki, kipindi chote hakujua nguo anazopenda mwenza wake mpaka wakaja kuoana?

Akishavaa nguo chini ya goti mtamwambia nywele zinatamanisha.......

Mwisho mtamwambia chakula hakinogi aache kazi apike jamani...................

Hakuyaona haya kabla hajamuoa?
Kubadili mitindo ya mavazi wangeanzana wenyewe hukoooooo ila kwa sasa unajenga chuki tu hapo kati yako na shem wako......... Ipo siku utakuja na thread hapa

Na huo ndo ulikuwa mtazamo wangu!
Enzi za uchumba ilikuwaje? hakuwa akivaa hivyo? na wewe huyo shemeji yako umemzoea sana..ushamfanya dada aako ebu muheshimuni bana..wewe na kaka yako!!!!!!!!!!!! shabash....eti mkamuweka kikao..we ukiwa kama nani!??
 
Ningekuwa Mumewe, Ningekuanya hizo nguo zote na kuzichoma moto tuone atafanayeje, na ningepitisha sheria kuwa sitak kuziona ngu za aina hiyo Kwangu na nisingetaka majadiliano zaid ya utekelezaji, Mwambie Ba Mdogo aache ujinga na kuwa strong, Unless anatengeneza Mazingira ya Mamdogo kuja kumegwa one day

Nimependa hiyo kwa red
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom