'Shemeji kaniuzia kesi'

unajua rshps ziko za aina nyingi..kuna zingine unakuta jamaa hataki kabisa kusikia mwanamke wake yuko bar hata kama yuko na rafikie..kwa hiyo unaweza ukute jamaa kadanganywa kua bibie anaenda kwa ndg yake kumsalimia kumbe yuko bar au pengine hata hajamuambia chochote ila jamaa anajua bibie yuko tu nyumbani so inawezekana sana alikua pale hajafanya kosa lolote lakini kumbe jamaa wengine hawataki kabisa kusikia partners wao wako bar coz wengi hua wanaamini kua mwanamke mwenye heshima haruhusiwi kukaa bar tena mwenyewe bila ya jamaa yake

nilitaka kusema hivihivi, mtotowamjini kanisaidia.
 
Huo kwa kweli ni mtego! Hudhani pia kuwa inawezekana anataka kuona kiwango cha mapenzi (au loyalty) ulichonacho kwa huyo rafiki yako (mumewe)?

Kama ningekuwa ni mimi, ningem press huyo shemeji aniambie ukweli wote ni kwa nini anataka nimtunzie hiyo siri. Pengine Mungu anataka "kumwokoa" rafiki yako kupitia kwako...kuwa makini usimwache rafiki yako aangamie.
SMU Sijakusoma..
Una maana shemeji anaweza kuwa anapima 'loyaltness' yangu kwa broo??
Is this possible eeh!!!!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: SMU
Yep! Kama kweli wanampenda rafiki yako, na unaona kuna dalili za kuangamia, utaacha aangamie?
SMU ndio maana nimeshingwa kujudge in the first place..na nikaamua kuwashirikisha mzee!
Wazo hilo linaniijia.. but how do i connect dots to conclude a malicious act??
 
Last edited by a moderator:
Hapa nilipo sijaijibu meseji na sijampigia simu shemeji kumuuliza chochote!!..Nimepanga nimyamaze kama meseji inavyosema but naona kama sitamtendea haki rafiki yangu...
Licha ya kutomtendea haki rafiki yako, lakini ahadi ya Mwana Tanu inasema Nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko. Lakini pia vitabu vya dini (zote) vinorodhesha kusema uwongo kuwa ni dhambi. Jiepushe na dhambi hiyoi kwa kusema kwa rafiki yako kile kilichotokea. Ukinyamaza na wewe utakuwa ni accomplice wa uhalifu huo
 
Mkuu hapo umenena..ila inatakiwa busara pia ya hali ya juu katika kumwokoa huyo rafiki yake.
Maana akikurupuka tu na kwenda kumtonya jamaa pia itakuwa ni mambo mengine. Ni vyema kutafuta njia sahihi ya kumuokoa jamaa katika huo mtego Kama unahisi mke wake hajatulia.
 
SMU ndio maana nimeshingwa kujudge in the first place..na nikaamua kuwashirikisha mzee!
Wazo hilo linaniijia.. but how do i connect dots to conclude a malicious act??
SnowBall ,katika maisha yangu ya kila siku, ni nimejiwekea misingi fulani fulani ambayo mara nyingi inanirahisisha kufanya maamuzi. Inawezekana na wewe pia unayo ya kwako. Mmoja katika ya misingi hiyo ni kutendea wengine kile ambacho ungependa utendewe. Sasa katika kadhia hii umetuonesha kuwa huyo ni mke wa rafiki yako, hivyo pengine kuna uwezekano mkubwa ukataka kujiweka katika nafasi ya huyo rafiki yako. Sasa jiulize, kama ungalikuwa wewe ndiye mume wa huyo dada, ungependa kutendewa vipi na rafiki yako?

Nafahamu ipo misingi mingine unayoweza kuitumia kufanya maamuzi, kama vile kutenda kile ambacho hakileti madhara au hata kama kinaleta madhara basi ni kwa kiwango kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Wala usiseme lolote. Hata ukihojiwa, umeona nini hapo?
Huna ushahidi wowote kwamba alikua akifanya makosa.
She just did not want you to disclose that to her man.
Ukisema utakua mbea. maybe atamwambia mwenyewe.

Anasubiri the right moment, ndio amwambie, au maybe
ana sababu zake za kumficha mumewe kuhusu mtoko huo.
We chuna, kaa pembeni. Ukiulizwa na rafiki yako maybe...
ila usijaribu kukurupuka na kumwambia rafiki yako. DON'T!
Mwali umenisemea...
Mambo ya mapenzi haya, unaweza sema, lakini ukaonekana wewe ni mchonganishi....
Mkuu nakuomba uipotezee.
 
Last edited by a moderator:
Mwelezi kwa wazi shemejio kwamba mchezo anaoucheza ni hatari.
Mkanye na umpe nasaha awe mwaminifu kwenye mahusiano yake ya ndoa. Mwenendo wowote nje ya hapo utapelekea ndoa kuyumba.
Kama kweli umemaanisha kupata ushauri basi mweleze kuwa unaangalia nyendo zake kama atabadilika na ikishindikana mwambie utamshtaki kwa rafikiyo...

Just thinking fast
 
.... Mmoja katika ya misingi hiyo ni kutendea wengine kile ambacho ungependa utendewe. Sasa katika kadhia hii umetuonesha kuwa huyo ni mke wa rafiki yako, hivyo pengine kuna uwezekano mkubwa ukataka kujiweka katika nafasi ya huyo rafiki yako. Sasa jiulize, kama ungalikuwa wewe ndiye mume wa huyo dada, ungependa kutendewa vipi na rafiki yako?

Nimekusoma mkuu!!!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Mbona huyo semeji alikuwa na wasiwasi kama hakua anafanya jambo baya? Mbona ni kitu normal tu kumsindikiza rafiki yako mahali kama ni salama? Au pengine alishakatazwa kufika bar in any how na huyu mume au pia usikute alishampigia simu na akamdanganya yuko nyumbani? Kuna jamaa nilikuwa naye maeneo fulani siku moja (of course akiwa meza yake na mwanamke). huku nyumba naona wife alimpigia simu na pale nafikiri alimuuliza mahali alipo na akamjibu "niko maeneo ya Tegeta, subiri naongea na mtu nikimaliza nitakupigia...". Nilichoka na mibile phones!!!
 
...Kama kweli umemaanisha kupata ushauri basi mweleze kuwa unaangalia nyendo zake kama atabadilika na ikishindikana mwambie utamshtaki kwa rafikiyo...Just thinking fast
Paw ninamaanisha aisee..
Na kama una nondo zingine wewe zimwage tu mkuu!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Paw
Hapa inategemeana mn na aina ya urafiki
ulionao na rafiki yako
mimi nina rafiki ambae ishu kama hiyo ningemueleza so fast
ikiwezekana hapo hapo kwenye simu
but rafiki huyo ni mmoja tu......wengine siwezi
nanyamaza kimyaa......sio tu marafiki hata ndugu yangu
ningenyamaza.......

na huyo shemeji mimi ningemtoa nishai fasta
kwa kumwambia'hainuhusu na usinihusishe'
 
Mr Rocky kwa kweli sikuona chochote na kiukweli baada ya kuwasalimia niliconcentrate kusoma magazeti yangu niliyokuwa nayo mzee..Nimeshangaa kupigwa biti asubuhi yake...

Mkuu huo wasi wasi unatoka wapi sasa kama hakuna chochote kibaya kliliendelea baada ya hizo starehe za bar
Asiwe na wasi wasi kama hana lolote la kuficha maana wasi wasi wake unakupa mashaka na wewe kuchunguza ni nini kilitokea baada ya hapo
 
Take it easy, na kama utaamua kupiga kimya kwa rafiki yako ni nzuri ila ebu jiweke kwenye position ya rafiki yako pia then think it critically. yaani angekuwa mkeo kakufanyia hivyo afu rafikiyo alifahamu. Huyo mama alikuwa na dhambi ndo maana alikuwahi kukueleza kilichompeleka pale, so hata usijaribu kumjibu kwa msg yake kwa msg kwani inaweza kuja gundulika na ikawa ushahidi kuwa ulishiriki hujuma na pengine ulihongwa. Hivyo ukiamua kupiga kimya kwa jamaa pia piga kimya kwa shemiyo pia yaani usmjibu kwa msg.
 
Hapa inategemeana mn na aina ya urafiki
ulionao na rafiki yako..

The Boss nimekusoma..
Kiukweli mshikaji ni jamaa yangu sana but sio miongoni mwa the best three friends of mine..
Ingawa pia kama ataipata habari (tuseme his wife was cheating)kwamba i knew the story na sikumuambia anaweza kunimind kimtindo..
 
Last edited by a moderator:
The Boss nimekusoma..
Kiukweli mshikaji ni jamaa yangu sana but sio miongoni mwa the best three friends of mine..
Ingawa pia kama ataipata habari (tuseme his wife was cheating)kwamba i knew the story na sikumuambia anaweza kunimind kimtindo..

Basi hapo uchune tu
ikitokea kaambiwa,jifanye shemeji alikuambia kuwa ana taarifa za mtoko wake
na hukuwa na sababu za kuingilia vitu personal
 
Back
Top Bottom