Tayana-wog
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 23,144
- 26,646
Kwa kifupi, Beatrice Shellukindo kawaambia wabunge wa CCM kuwa wanachofanya wabunge wa upinzani ni sahihi kabisa, wako hapo kukosoa chama tawala na ndivyo wanatakiwa kufanya kama wabunge wa upinzani. Badala ya kukwashambulia wangechukuwa yale mazuri wanayoambiwa na upinzani.
Pia kasema wabunge wa upinzani wanapenda sana chama tawala na wanachofanya ni kukosoa ili chama tawala kijirekebishe na hivyo kuendelea kubaki madarakani.
Kwa maoni yangu Beatrice Shellukindo ameonesha uelewa mzuri sana wa siasa za vyama vingi ndani ya bunge. Ameonesha kuwa na ngozi mungu jambo ambalo ni muhimu kwenye ulingo wa siasa. Wabunge wa CCM wanaoshambulia wapinzani ni kutoelewa nini kazi za ya wapinzani. Kuna utoto wa hali ya juu CCM!
...amesoma alama za nyakati!