Shellukindo na Kamati Yako Mmepatwa na Nini?

Uliona hata Speaker Sitta alivyouongoza mjadala huu? Tuachane na mawazo finyu kwamba kuna badiliko lolote la maana linaweza kuletwa na Bunge letu hasa baada ya vikao vya NEC ya CCM kutoa angalizo kwa Sitta.

Ukimwondoa Dr. Slaa na Christopher ole Sendeka, wabunge waliobaki kwenye vita ya Ufisadi waliobaki ni wasanii.
 
Mimi huwa naota siku ambayo wananchi watapunguza ushindi wa CCM katika Bunge na Serikali za mitaa ANGALAU kwa robo tu ndipo nikubali kwamba sasa wa-Tanzania wanahitaji mabadiliko - wanatuma ujumbe maalumu kwa viongozi. Lakini kila uchaguzi ni ushindi wa kishindo! Hapo tena mbunge gani awe na ujasiri wa kupingana na Chama kikiamua kushikilia msimamo wake?

Nakuunga mkono mia kwa mia(hasa hapo kwenye red)!
 
Hukuna mpambanaji hapa ni wivu na makelele kwa waliokosa nafasi za ufisadi
Tanzania ya watanzania kama jana leo na siku zote amina

Tusubiri wazee wote mungu awachukue ndo tujenge nchi
 
Wapiganaji wa ufisadi CCM wanapigania nini? Sishangai unafiki ulioonyeshwa na shelukindo/mwakyembe/sitta/manyenye/sendeka/kilimba/mpendazoe katika kuhitimisha suala la RICHMOND..

Nasikitika sehemu kubwa ya jamii bado haijawaelewaa vemaa wanafiki hawa wa demokrasia nchini. kwa hili natumai adhabu yao INAKUJAAA...


ndiyo maana ilisemwa kuwa siasa ni mchezo mchafu
 
Watu pipoooooooo. CCM si wanafiki ila watu ndio wanafiki kwani unakumbuka ya Dr. H. Mwakyembe? ni CCM hiyo lakini unajua unafiki upo kwa hao Mafisadi si CCM. CCM safi Kikwete safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii spika safi?
Chama ni watu na hakuna kama hakuna watu. Hivyo kama watu ni wanafiki basi chama ndicho kinafiki. Huwezi kutenganisha kichwa na kiwiliwili bado ukawa na mtu kamili!!!!! Huwezi kutenganisha chama na wanachama wake halafu bado kikawa chama!!!!
 
Hofu ya uchaguzi imetanda....Hivi kuna mtu ameona 'Speed and standards" katika Bunge hili? Mie sijaona labda nyie wenzangu.....

Hujajibu swali! Mzee wetu Mwanakijiji ameuliza:

Dr. Mwakyembe na Selelii wamesema nini kwenye huo mjadala hapo jana?

Shelukindo si mwanasiasa per se alikuwa civil servant wa muda mrefu kabla ya kuingia kwenye ubunge. Wapo wengine kama yeye ambao wameingia siasa baada ya kuona hawana kitu cha kufanya kabla ama baada ya kustaafu, we shouldn't expect much from them. Isitoshe wengi wao ni wale waliokuwa kwenye mfumo wa Chama Kimoja na allegience wakati wote iliambatana na miongozo ya Chama na si mawazo na maamuzi binafsi yenye manufaa kwa umma.

Inabidi tufike mahali tupeleke macho na masikio yetu kwa 'vijana' walioingia kwenye siasa wakiwa bado wabichi ingawa wanao uwezo wa kufanya kazi kwenye greener pastures ndani na nje ya nchi lakini wamemua kuingia kwenye siasa wakiwa na uchungu wa dhati na nchi yao. Tatizo lililopo ni kwamba humo CCM wamejikuta wako katikati ya manyang'au wasiojali mustakabali wa wananchi na Taifa kwa ujumla bali wanajali matumbo yao na ya familia zao. Kuweza kushindana na kuwashinda manyang'au hao ni kazi inayohitaji mbinu na umakini wa hali ya juu.

 
Ukimwondoa Dr. Slaa na Christopher ole Sendeka, wabunge waliobaki kwenye vita ya Ufisadi waliobaki ni wasanii.

Nakubaliana na wewe kuwa wapamanaji wa kweli ni DR.Slaa na OLe Sendeka, hawa wengine ni wachumia tumboni ambao sasa naamini walitumiwa kuhijack mapambano dhidi ya ufisadi toka Upinzani na kuifanya agenda ya CCM ikiwa ni mbinu ya kuidhoofisha agenda hiyo; na kweli wamefanikiwa lakini kwa usaliti huo adhabu yao wataipata October huko majimboni kwao, wasije wakamlaumu mtu kwani wamejichimbia kisimani wenyewe na mafisadi watawacheka!!!
 
Ukimwondoa Dr. Slaa na Christopher ole Sendeka, wabunge waliobaki kwenye vita ya Ufisadi waliobaki ni wasanii.

I beg to differ! Ole Sendeka ni type ya wale watu wanaouma na kupuliza he is not fit to be called 'mpiganaji wa kweli'!
 
walitamba,wakajinadi,wakasema hiyo ni ajenda ya CCM wapinzani wanadandia wakaapa kwa viapo vya unafiki bora wakatwe shingo zao kwa maslahi ya taifa hili tambo hizo zimeisha jana mjengoni SHAME!! Mapokeo yanasema dalili za mnafiki akisema anasema uongo, akiahidi hatimizi hiyo ndio nafasi yao wanajali zaidi maslah yao na chama chao na ufisadi utaendelea KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
 
I beg to differ! Ole Sendeka ni type ya wale watu wanaouma na kupuliza he is not fit to be called 'mpiganaji wa kweli'!

Inawezekana kuwa yuko hivyo unavyosema kwa mambo mengine tusiyoyajua lakini kwa hili la RICHMONDULI kusema kweli Ole SEndeka hakuteteleka mpaka walipofunga mjadala!
 
Nilifurahishwa sana na mchango wa Dr Slaa na Sendeka. Hawa ndio wapiganaji wa kweli! Hakika wameonyesha jinsi walivyo na uchungu na nchi yetu.
 
hizi ndizo si hasa za watanzania bado haujawapata Wazalendo halisi wa kutuwakilishia matatizo yetu na kuupigania vilivyo dhidi ya serilkali hii dhalimu ilojaa rushwa na ufisadi
 
Mwakyembe na Selelii wote wamekalia makuti makavu majimboni watokako pamoja na Mpendazoe, kwahiyo ndio maana wamekubali yaishe pengine mafisadi watawaonea huruma warudi mjengoni!! Kulikuwa hakuna sababu ya kusalimu amri dakika za mwisho kama ni kuogopa kuenguliwa na ccm wakati wa uchaguzi, kuna falling back position ya kuwa Independent; hawana sababu ya msingi ya kuthrow in the towel!!
.
Waliokuwa Makamanda na Wapambanaji, nadhani wamethibitika kuwa wanamgambo mamluki wa matumbo yao. Heri waliokaa kimya kama Mama Kilango, Seleli na Mwakiembe, kuliko waliofunua vinywa na kutoa madudu kama Mpendazoe, Manyanya na Ole Sendeka.

Tumerudi kwenye party supremacy ndipo serikali inafuatia na bunge buruzwa kushika mkia.

Waliojinyamazia naamini wale genuine, wanaumia ndani kwa ndani hivyo wakaamua bora lawama kuliko fedheha ya kutupwa nje na CCM, they are playing safe than sorry.

Kamanda wa kweli aliyesimama mpaka mwisho ni one and only Dr. Slaa, na amesimama na atahesabiwa.
 
mi nshajiachia longtime mabo ya wanasiasa wetu, japo sio mwisho ipo siku watalipa kila walichotufanyia, Godbless Tanzania
 
Sure, huyu ni Kamanda mkweli na hafichi chochote! mean slaa Dr

naye atajapata thawabu yake hapa hapa, wapo duniani wengi waliachwa wakasimama alone but wamshinda, kama sio Slaa yataendelezwa na sisi wenye uchungu wa nchi hii!!
 
Ole Sendeka na Slaa wanatoka mkoa Arusha!tungekuwa na wabunge 2 wanamna hii kutoka kila mkoa ,tungefika mbali kujali maslahi ya taifa.Mikoa mikubwa kama Mwanza ,Shinyanga ,Tabora it is a big joke,maana wabunge wake wengi ni YES men.
Hata akina Cheyo ni mapesa tu,hakuna anachofanya kuleta upinzani kamili bungeni.

Na ukiangalia mikoa mingi yenye yes men,ni very poor na maendeleo ni duni sana pamoja na resources walizonazo

Ukiwa
 
Maelezo haya hapa chini yanayohusu Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imenisikitisha sana kwa jinsi Kamati hiyo ilivyotishiwa nyau na mambo ya "Posho Mbili kwa kazi moja!"
Source: Mwananchi

Mimi sioni, kwa kauli za Shellukindo kama tuna wapambanaji katika vita hii ya ufisadi! Mjadala wa Richmond ndio huo umezikwa rasmi jana, wapambanaji (ukimwondoa Dk Wilbrod Slaa na Christopher ole Sendeka) wanaonekana walinywea kama wamenyeshewa mvua maskini! Hata hivyo nimefurahishwa sana na jinsi Dk Wilbrod Slaa alivyopambana mpaka mwisho! Soma kauli yake hapa chini:

SOURCE: Mwananchi

Hongera sana Dk Wilbrod Slaa! Upambanaji wako utakumbukwa daima na Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu!
.
Tangu mwanzo tulisema wapiganaji ndani ya ccm,wanapigania matumbo yao na ya watoto wao,lakini baado wenye mawazo finyu wakasema wanapigania maslahi ya taifa.Hayo ndiyo masalahi ya taifa?
 
.
Tangu mwanzo tulisema wapiganaji ndani ya ccm,wanapigania matumbo yao na ya watoto wao,lakini baado wenye mawazo finyu wakasema wanapigania maslahi ya taifa.Hayo ndiyo masalahi ya taifa?

Hili la "posho mbili kwa kazi moja" Mh William Shellukindo wala asingelisema hadharani, angalau amekuwa mkweli, anyway!
 
Back
Top Bottom