Shein: Vigogo wanaosababisha ajali washtakiwe kama wengine

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
Shein1%2822%29.jpg

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein



Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, amesema serikali inapenda kuona sheria inachukua mkondo kwa kushughulikia uhalifu wa makosa ya barabarani bila ubaguzi hasa makosa hayo yanapofanywa na viongozi.


"Jeshi la Polisi lazima muwe karibu katika kusimamia sheria hata kama gari ya waziri limevunja sheria, hatua zichukuliwe,” alisema.


Aliyasema hayo juzi mjini hapa wakati akizindua mpango wa miaka 10 wa usalama barabarani visiwani Zanzibar.


Alisema ili kufanikisha kujenga Zanzibar isiyokuwa na ajali, Wizara ya Miundombinu na Jeshi la Polisi lazima wafanye kazi kwa karibu kusimamia sheria bila ya hofu au upendeleo.


Dk. Shein alisema katika kukabiliana na tatizo la ajali zinazosababisha maisha ya watu kupotea, lazima watu wote wanaovunja sheria kwa kuendesha ovyo magari wakamatwe na kufunguliwa mashtaka.


“Ni lazima tuachane na ile tabia lile ni gari la fulani haligusiki...Tusiwafumbie macho wenye lengo la kutaka waonewe imani kwa kufanya makosa kwa makusudi," alisema.


Kuhusu elimu ya usalama barabarani, Dk. Shein alisema shule zote za msingi na sekondari zitashirikishwa elimu ya usalama barabarani katika kipindi chote cha utekelezaji wa mpango wa miaka 10 unaolenga kupunguza ajali kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2020.





CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom