Shein, Pinda hamna kazi za kufanya?

Makaayamawe

JF-Expert Member
Feb 21, 2009
341
9
Hivi hawa wakuu hawana kazi ya kufanya mpaka wawe wasindikizaji wa Vasco Da Gama (JK) kila akitimua? Hata kwenda Zambia lazima wadamkie airport? Hivi hawana kazi za kufanya?

IMG_2256.JPG

Rais Jakaya Kikwete, akifurahia jambo pamoja na Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein (kushoto), na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere alipokuwa akisindikizwa kupanda ndege kwenda Zambia jana.​
 
Last edited:
Hivi angesindikizwa na mke wake na katibu wake mkuu asingefika huko Lusaka?
 
Jamani kweli viongozi wakuu wa nchi maskini kama hii wanatoa kicheko kikubwa kama hicho hadharani? Napata maswali mengi kuhusiana na kicheko chao?
 
Msatu hamna protocol inayomlazimisha PM au Makamu wa Rais lzm aende uwanja wa ndege kila siku kumuaga Rais anapokwenda nje ya nchi.

Protocol karibu za kila nchi zinafanana na hii ya Rais kuagwa na kila afisa mkuu wa serikali ni kielelezo kingine kuwa hawa akina Shein hawana kazi za kufanya.Tunaona kila siku wakuu wa nchi zingine wakiondoka airpot huwa hamna msururu kama huu wa JK na watu wake!

Namuunga mkono mtoa hoja,hawa hawana kazi za kufanya!
 
mambo ya protokali hayo

protokali inatuongezea makali wanyonge.
Sheion ana msafara wake na pia pinda ana msafara wake, jamani je haya si matumizi mabaya ya pesa za wanyonge??
Sisi walala hoi ndio walipa kodi, wahindi na mafisadi wengine wana misamaha ya kodi, na hata inapobidi walipe kodi wanajua namna wanavyokwepa kulipa kodi.
 
Msatu hamna protocol inayomlazimisha PM au Makamu wa Rais lzm aende uwanja wa ndege kila siku kumuaga Rais anapokwenda nje ya nchi.

Protocol karibu za kila nchi zinafanana na hii ya Rais kuagwa na kila afisa mkuu wa serikali ni kielelezo kingine kuwa hawa akina Shein hawana kazi za kufanya.Tunaona kila siku wakuu wa nchi zingine wakiondoka airpot huwa hamna msururu kama huu wa JK na watu wake!

Namuunga mkono mtoa hoja,hawa hawana kazi za kufanya!

Hii ni made ina Tanzania na wala haijaanza leo toka enzi za Mwalimu!
 
Sikumbuki kumuona Mwalimu akisindikizwa kwenye kila safari aendayo na baraza lote la mawaziri au hata na akina A.Jumbe, E.Sokoine, C.Msuya n.k. Huu ukosefu wa kazi umeonekana zaidi kwenye hii awamu ya wababaishaji.

Hata kama hii tabia ilikuwapo hapo awali, hivi ni vigumu kwa hawa mataahira kugundua kuwa wanachofanya sio kitendo cha kuwajibika?

Kwa msongamano wa magari ulivyo Dar, huku kusindikizana sio ajabu kukatumia nusu nzima ya siku ya kazi. Ama kweli hatutafika.
 
Msatu hamna protocol inayomlazimisha PM au Makamu wa Rais lzm aende uwanja wa ndege kila siku kumuaga Rais anapokwenda nje ya nchi.

Malafyale,
Umenena mkuu. Huu ni ubabaishaji wa wazi uliopachikwa jina la Protocol. Kama hawa, Vice na PM, hawajui kuwa wanachofanya sio kitendo cha uwajibikaji, basi wana haki ya kujiuzulu.

Wabunge wetu nao wako wapi, hawawaulizi hawa vilaza ni kwa nini wasiwe ofisini badala ya kuranda-randa DIA au kumsindikiza JK ni majukumu yao ya kazi?
 
Hivi hawa wakuu hawana kazi ya kufanya mpaka wawe wasindikizaji wa Vasco Da Gama (JK) kila akitimua? Hata kwenda Zambia lazima wadamkie airport? Hivi hawana kazi za kufanya?

Main.jpg

Rais Jakaya Kikwete, akifurahia jambo pamoja na Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein (kushoto), na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere alipokuwa akisindikizwa kupanda ndege kwenda Zambia jana.​

Mkuu waliendawote watatu Zambia kwa wakati mmoja? Maana hamna source so sina uhakika kama picha ina husiana na statement yako. ILa kama ni kweli wamechemsha. Viongozii watatu wakuu wa nchi wataendaje nje ya nchi kwa wakati mmoja? Tena kwenda destination hiyo hiyo.
 
MwanaFalsafa1,

..Kikwete peke yake ndiye aliyekwenda Zambia baada ya kutoka Libya alipokuwa kuhudhuria mkutano wa AU.

..kila Raisi anaposafiri basi Makamu na Waziri Mkuu lazima wawepo Airport kumuaga.

..hata anaporudi safari wanakuwepo airport kumpokea.

..viongozi wengine kama Mkuu wa Mkoa, makamanda wa Jeshi na Polisi, na watumishi kibao hushiriki ktk zoezi la kumuaga na kumpokea Raisi.

..Makaayamawe anashauri kwamba utaratibu huu umepitwa na wakati na unapaswa kusitishwa kwani hauna tija yoyote kwa taifa.
 
Hawa washaconclude kwamba.

1. Matatizo ya wabongo ni mengi na makubwa sana.
2.Ukijifanya kuyatatua huwezi, na vyovyote utakavyofanya utapewa lawama
3. Tumbua maisha tu, masikini watakuwepo, matatizo yatakuwepo na hayaishi, zamu yetu kula.

Unafikiri wanajali kitu zaidi ya kupalilia matumbo yao?
 
..sasa JK naye alirudi Bongo kufanya nini?

..angepitiliza tu toka Tripoli moja kwa moja mpaka Lusaka.

..yaani naona kama aliingia Dar kubadili masanduku tu!!
 
Last edited:
MwanaFalsafa1,

..Kikwete peke yake ndiye aliyekwenda Zambia baada ya kutoka Libya alipokuwa kuhudhuria mkutano wa AU.

..kila Raisi anaposafiri basi Makamu na Waziri Mkuu lazima wawepo Airport kumuaga.

..hata anaporudi safari wanakuwepo airport kumpokea.

..viongozi wengine kama Mkuu wa Mkoa, makamanda wa Jeshi na Polisi, na watumishi kibao hushiriki ktk zoezi la kumuaga na kumpokea Raisi.

..Makaayamawe anashauri kwamba utaratibu huu umepitwa na wakati na unapaswa kusitishwa kwani hauna tija yoyote kwa taifa.

Eh nae huyo Makaayamawe basi thread yake haileweki.
 
MwanaFalsafa1,

..Kikwete peke yake ndiye aliyekwenda Zambia baada ya kutoka Libya alipokuwa kuhudhuria mkutano wa AU.

..kila Raisi anaposafiri basi Makamu na Waziri Mkuu lazima wawepo Airport kumuaga.

..hata anaporudi safari wanakuwepo airport kumpokea.

..viongozi wengine kama Mkuu wa Mkoa, makamanda wa Jeshi na Polisi, na watumishi kibao hushiriki ktk zoezi la kumuaga na kumpokea Raisi.

..Makaayamawe anashauri kwamba utaratibu huu umepitwa na wakati na unapaswa kusitishwa kwani hauna tija yoyote kwa taifa.

Joka hapa umenena. Huu utaratibu umepitwa na wakati na unatuongezea tu umasikini.
 
Back
Top Bottom