Shein akataa uwaziri, asusia kikao

Ndio bye bye hiyo, yaani hata kama inajulikana wazi kuwa dalili za mvua kali ni upepo mkali ila wengine wanabaki kusema kuwa ni mawingu.

Woga wa ccm umeuponza Muungano ,CCM waliona CUF ikishinda Uraisi Zanzibar basi makamo wa Raisi wa Muungano atakuwa ni kutoka CUF ,ndio wakaona Raisi wa Zanzibar awe ni waziri asie na wizara maalum katika Muungano, utumbo huu mwenye akili haukubali na WAZANZIBARI hapa ndipo penye tundu kubwa la kuachana na Muungano ,ndio hapohapo watakapo pata upenyo ,hizo kero zingine ni akiba

Waliifuata akili ya baba wao wa Taifa Nyerere ,kumbe wakati ule hata akili yake ilikuwa imepata ugonjwa , matokeo yake ndiyo haya
 
kama kweli anakuwa waziri akiingia ktk baraza la mawaziri hiyo nayo ni kero nyingine ya muungano,tutaishughulikia wakati wa maoni ya katiba mpya
 
Tanganyika nchi? Zanzibar ni semi autonomous area, ingawa haina recognition UN lakini ni nchi. Lakini tanganyika je? Sio kitu maana mumejisaliti na kulikataa jina la tanganyika mkawa mnakumbatia utanzania

Frustrati0n must b erroding your hearts n brains severely u guys frm island..Loh nway lemme be kind by sayn poleni n simple advice to u is "dnt let external force drive u,juc ask th lybians 4 th experience" buh if u thnk ts internal drive n people's willing,i wish u ol th best"
 
Mkuu, huyo jamaa aliapishwa kama waziri. Sababu za kutohudhuria mwandishi hajaifafanua vizuri. Imekaa kiudaku udaku maana haielezi kama amenukuliwa au ameipataje habari. Ila kisheria ni waziri na alishaapishwa. Bado nashindwa kuamini kwamba kutohudhuria kwake ni kwasababu amesusa maana habari haijajieleza!

Umesema vyema. Habari hii imekaa kiudaku udaku! Si lazima kila kikao cha baraza la mawaziri kila waziri lazima ahudhurie. Kile ni kikao kama vikao vingine na vinaprotocal yake. Wapo wenye udhuru na walio kikazi nje ya nchi. Aliyeandika hii habari labda anataka tuamini kwamba ndo mwanzo wa kuuvunjika kwa muungano!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom