Elections 2010 Shein ajitoa kinyanganyiro cha Urais Zanzibar

Status
Not open for further replies.
Nina maswali kidogo kuhusu hiyo quote hapo juu na uchaguzi wa mwaka huu.

Mara ya mwisho kwenye reconciliation walisema kwamba Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), wajumbe wake pia watateuliwa kutoka CUF ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwenye chaguzi zitakazofuata. Na kumbukumbu yangu inasema kwamba Karume alimteua mjumbe mmoja akidai kwamba ni mwanachama wa CUF, lakini CUF walisema Karume hakutakiwa kuteua yeye moja kwa moja, alitakiwa awaambie CUF ili wampe jina maana wao CUF ndiyo wanawajua wanachama wao vizuri. Sikumbuki sakata hilo liliishia wapi. Maswali:

1. Je, kuna any developments kuhusu kuhakikisha kamba ZEC inajumuisha pia wana CUF ili kuondoa hisia za kuibiwa kura ama udanganyifu wa kura za maruhani?

2. CUF wamefanya maandalizi gani kuhakikisha kwamba mwaka huu wizi hauwezi kufanyika tena?

3. Kuna dalili zote za CCM kuanza njama za kuiba kura?

Najua unaweza usiwe na majibu ya kutosheleza, lakini hata hint tu zinatosha ili kupata feeling what is on the ground na tujue mapema kama mchezo mchafu utaendelea as usual ama mwaka CUF watashangilia badala kulia.

Ni hayo tu Mkuu, usiwe unapotea sana maana msimu wa news muhimu na za uhakika umewadia.
Mkuu Halisi, Keil
Wapo watu wanaweza kutusaidia kitaalamu zaidi. Ila ninachoweza kudadavua katika maswali hayo ni kama ifuatavyo:
Itakumbukwa katika muafaka wa mwanzo au wapili ilitakiwa pawepo mabadiliko ya tume kwa kuingiza wajumbe kutoka vyama vya siasa na hili lilifanyika kwa CUF kuingiza wajumbe wawili na CCM kadhalika. CUF iliwapeleka ndg. Nassor Khamis Mohammed(mwanasheria) na ndg.Ayoub Bakar na CCM ikawakilishwa na ndg. Khatib Mwinchande na Said Bakari Jecha ambaye amewahi kuwa kitengo cha usalama wa taifa na waziri katika wa SMZ kama sikosei na bado ni mjumbe wa tume.

Cha ajabu licha ya kuwa wajumbe wa CUF wamo humo lakini bado ZEC imekuwa ikiongozwa na makada wa chama cha Mapinduzi na usalama wa taifa. Tokea tume iundwe Wenyeviti wake wote wamekuwa ni makada wa CCM kuanzia jaji Zubeir Juma Mzee, Mzee Masauni (baba yake Masauni aliyefukuzwa ubosi UVCCM)...na huyu wa sasa Khatibu Mwinchande ambaye awali alikuwa mjumbe wa tume hiyo kwa tiketi ya CCM sasa ndo mwenyekiti wake. Uadilifu wa tume bado una mashaka na wajumbe wawili wa CUF humo hawawashi wala hawazimi.

Kuhusu maandalizi ya kuzuia wizi wa kura kwa CUF hali imekuwa ngumu, kwa sababu moja kubwa, CCM wana mbinu nyingi za kuiba kura, hawaibi kwa kuziongeza zao, wanaanza kuzipunguza za CUF...mfano kuwakataa kuandikisha wapiga kura wake ,ukizingatia tume ni yao wao na mchakato wa kupandikiza wapiga kura hewa huwa ni rahisi kwao, bila shaka haya yote tumeyashuhudia katika hatua ya ku up date daftari la wapiga kura.

Ilichofanya CUF,kama kawaida ya Maalim Seif, ambaye ni ukweli usiofichika kuwa hakuna mwanasiasa yeyote anaeziweza siasa za visiwani kama Maalim Seif, amecheza karata yake ambayo mimi naiita "confusion card" nyinyi iiteni "MARIDHIANO BAINA YAKE NA KARUME". Karata hii tayari inafanya kazi yake vizuri sasa hivi, kwakuwa imeshakigawa chama cha mapinduzi vipande vipande. Ni triki ambayo imeshakigawa chama cha mapinduzi Zanzibar na kumchanganya mwenyekiti wake Kikwete.

Hapa binafsi nayakumbuka maneno ya Maalim Seif aliyosema katika mkutano wa hadhara Kibandamaiti,baadha ya kutanganza kumtambua karume,alisema"wanaosema injini ya Maalim Seif imechemsha wanajidanganya....injini ya Maalim haijachemsha bado ipo fit na subirini mtaona..." nakweli sasa tunaona, kirusi cha MARIDHIANO kinaichachafya CCM yote.

Hapa CUF wanafaidika vipi?
Kama DR.Shein atalazimishwa kupita basi hivyo hivyo atalazimishwa kuwa rais Zanzibar na serikali ya mseto itaundwa hata kama kura ya maoni itasema HAPANA. Kwa hiyo maalim kurudi ikulu ni suala la kusubiri tu,ukizingatia CUF inaweza kum KNOCK OUT,Dr.sheni kwa kumuwekea pingamizi kugombea, ambayo ipo wazi kuwa hana sifa yakuwa mgombea baada ya kupoteza ile ya kuwa mwakilishi.

Kama Bilal atapitishwa itachukuwa mda kidogo CCM kupotea kwa kuwa migogoro ya siasa haita kwisha iwapo kura ya maoni italazimishwa kuwa HAPANA, nikimaanisha karata ya CUF itabaki kwa kura ya maoni tu na mkakati mweingine ambao ni siri ya chama.
Nafikiri kwa suala la tatu litakuw limejibika kwa lapili.
 
Mkuu Keil,
Kwenye post#39, nikweli nukuu za waandishi wakati mwengine zinatupa ziada ya kazi. Ila wacha tuzamie zaidi kupata uasahihi wa vifungu vyenyewe ila nakumbuka vizuri context ya kifungu cha katiba na sheria ya uchaguzi ya zanzibar ambazo zinambana Dr Sheni.
Kwanza, katiba imetowa masharti ya sifa za mtu kuwa rais kwa maana ya kuwa na sifa ya kugombea nafasi yenyewe. Katiba imeweka wazi kwa pamoja na mambo mengine mgombea nafasi ya urais anatakiwa pia awe na sifa ya kumuwezesha kuchaguliwa kuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi.

Sifa ya kuchaguliwa kuwa mwakilishi hana kwa kuwa hana sifa ya kuchagua wala kuchaguliwa kama ilivyowekwa katika sheria uchaguzi inayotaka awe amejiandikisha au sifa ya kujiandikisha kupiga kura, ambazo Dr.Sheni hana zote mbili.

Sifa ya kujiandikisha hana kwakuwa hakujiandikisha popote Zanzibar kama mpiga kura au sifa ya kuandikishwa hana kwa kuwa amepoteza sifa ya ukaazi katika jimbo lake la Makanyageni Pemba,ambako ili uweze kuandikishwa katika jimbo la uchaguzi kuchaguwa mwakilishi au mbunge lazima uwe mkaazi wa hapo kwa kipindi kisichopunguwa miaka mitatu, sheni hana sifa hiyo, amekuwa nje ya jimbo la Mkanyageni tokea alipoteuliwa kuwa makamo wa rais na Mkapa mpaka nusu muongo wa Kikwete.
 
Mkuu Junius,

Nimekupata vyema kuhusiana na hilo la kupoteza sifa ya ukaazi huko jimboni kwake Mkanyageni. Lakini ninaona kwamba hapo kuna kasoro kidogo.

Ninaomba nipate tafsiri ya neno mkaazi. Mawaziri wa SMZ wana ofisi na makazi (nyumba za kuishi) Unguja, je, ingetokea mjumbe wa Baraza kutoka Pemba ameteuliwa kuwa Waziri/Naibu Waziri na akajikuta anahamia Unguja kwa miaka mitano, ina maana atakuwa amepoteza sifa ya ukaazi?

Kwa uelewa wangu, mkaazi ni mtu ambaye anaishi na kufanya kazi katika eneo aliposema ana makazi yake. Hii ina maanisha kwamba familia yake (nucleus) na shughuli zake zote ziko hapo aliposema kwamba ni mkaazi.

Hicho kipengele cha mkaazi kinahitaji marekebisho kwa watu ambao ni wanasiasa na wanajikuta makazi yao yanahamishwa kulingana na responsibilities za kisiasa. Mfano, Maalim Seif sijui anaishi wapi maana almost kila siku ninamuona yuko Dar ama Unguja. Kwa mtu kama huyo unaweza kuta hata familia yake alishaihamishia Dar kwa kuwa ndiko ambako kuna ofisi yake na shughuli nyingi za kisiasa anazofanya.

Ndiyo maana ninasema hicho kipengele kina walakini na kinahitaji marekebisho ili kuweza kuwa-accommodate watu wanaokuwa relocated kwa sababu ya majukumu ya kisiasa.

Swala la Dr. Shein kutojiandikisha, hilo siwezi kuliongelea. Labda alijiandikisha Bara ambako ndiko makazi yake yalipo na ni rahisi kwenda kupiga kura. Pia inawezekana hakuwahi kufikiri kwamba angeweza kugombea hiyo nafasi ama Uwakilishi, maana huwezi kutoka kuwa Makamu wa Rais then urudi kwenda kugombea uwakilishi, achilia mbali Urais wa Zanzibar.
 
Nimepata taarifa hivi sasa kutoka kwa mmoja wa waandishi walioko Dodoma kuwa kuwa Dk. Shein ameondoa jina kwenye kinyanganyiro cha urais Zanzibar.

Mwenye data atupatie jamani

Urais Zanzibar rafu tupu: DK SHEIN ADAIWA KUJIONDOA

sheinhoye.jpg

Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein

UTATA ulikuwa umegubika harakati za kuwania urais wa Zanzibar jana wakati taarifa mbalimbali zilipokuwa zikivujishwa kutoka kwenye vikao vya siri, ikiwemo habari kwamba Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein kuwasilisha barua ya kujitoa kwenye kinyang'anyiro cha nafasi hiyo muhimu visiwani Zanzibar.

Hata hivyo, watu walio karibu na viongozi wa juu wa CCM zilieleza kuwa Dk Shein hajajitoa na kwamba huenda habari hizo zinatolewa na wapinzani wake kutaka kuchafulia harakati zake za kuingia Ikulu ya Zanzibar.

Wakati joto likizidi kupanda mkoni hapa, visiwani Zanzibar gumzo limeibuka baada ya rais wa zamani, Dk Salmin Amour kuibuka mjini Dodoma akiwa ameambatana na mgombea wa kiti hicho, Shamsi Vuai Nahodha, ambaye kwa sasa ni Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi.

Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31 utaipatia Zanzibar rais wa saba tangu mapinduzi ya mwaka 1964 kutokana na rais wa sasa, Amani Abeid Karume kumaliza vipindi viwili vilivyochukua miaka miaka 10 baada ya kushinda mara mbili kwenye uchaguzi wa mwaka 2000 na 2005.

Harakati za kupata mrithi wake kutoka ndani ya CCM zimekumbwa na matukio kadhaa na wakati siku ya mkutano mkuu uliopangwa kufanyika Jumamosi na Jumapili ikikaribia, kumekuwepo na taarifa nyingi ambazo zinaonekana kuvujishwa na watu walio kwenye makundi yanayopingana.

Harakati hizo pia zimegubikwa na suala la Upemba na Uunguja huku suala la muafaka uliofikiwa baina ya Karume na kiongozi wa CUF, Seif Sharrif Hamad likichukua nafasi kubwa kutokana na baadhi ya wagombea kuunga mkono hatua hiyo huku wengine wakipinga.

Mwananchi ilitaarifiwa kuwa Dk Shein alijitoa kwenye kinyang'anyiro cha urais baada ya kushauriwa na viongozi wenzake na kuwasilisha barua hiyo majira ya saa 5:00 asubuhi.

Vyanzo kadhaa vya habari vililieleza gazeti hili kuwa Dk Shein alifikia uamuzi huo kwa kuandika barua ya kujitoa baada ya kutathmini mazingira ya hali ya kisiasa kwa wajumbe wa mkutano wa halmashauri kuu.

Habari zilisambaa jana asubuhi kuwa Dk Shein alikuwa na mazungumzo ya faragha na mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na kwamba jambo hilo la kujitoa lilizungumzwa.

Kwa mujibu wa habari hizo, Dk Shein alielezwa mapungufu kadhaa ya kikatiba dhidi ya azma yake na kwamba mapungufu hayo yangemwengua kwenye kinyang'anyiro hicho hata kama chama kingempitisha.

"Aliambiwa kuwa katiba ya Zanzibar inamwengua kuwa mgombea na kwamba hata kama angegombea na kushinda, angeweza kuwekewa pingamizi la kisheria," kilieleza chanzo chetu cha habari.

"Wao hawakumlazimisha kujitoa bali walimtaka apime mwenyewe uzito wa suala hilo halafu afikie uamuzi wenye manufaa kwake na chama."

Kwa mujibu wa chanzo hicho, Rais Kikwete katika mkutano huo alimwahidi Dk Shein kuwa angemteua tena kuwa makamu wa rais kama ataamua kujitoa kwenye uchaguzi huo.

Ingawa chanzo hicho hakikufafanua jinsi katiba ya Zanzibar inavyombana Dk Shein katika kinyang'anyiro hicho, sifa za mgombea urais wa Zanzibar ni pamoja na kuwa na kitambulisho cha Uzanzibari Ukaazi na kuishi Zanzibar kwa muda usiopungua miaka mitatu.

Hata hivyo, Dk Shein, ambaye alikuwa akiishi Unguja kabla ya kuteuliwa kuwa makamu wa rais mwaka 2001 baada ya makamu wa rais wa wakati huo, Dk Omar Juma kufariki, asingeweza kuishi Zanzibar kwa muda wote huo kwa kuwa wadhifa wake wa Makamu wa Rais unamruhusu kuishi popote ndani ya Tanzania.

Dk Shein, aliyekuwa Waziri Kiongozi, Dk Mohamed Ghalib Bilal na Shamsi Vuai Nahodha, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inayomaliza miaka mitano ya awamu ya pili ya utawala wake visiwani humo wanatajwa kuwa ndio waliopata alama za juu katika mkutano wa kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar.

Visiwani Zanzibar kumeibuka hisia tofauti za kibaguzi baada ya Dk Salmin, ambaye amekuwa haonekani hadharani kwa muda mrefu, kuibuka mjini Dodoma, anaripoti Salma Said kutoka Zanzibar.

Viongozi wa vyama vya upinzani ni miongoni mwa waliotoa maoni kuhusu kujitokeza kwa ghafla kwa Dk Salmin mjini Dodoma, huku baadhi ya wanachama wa CCM Zanzibar hasa wenye msimamo wa maridhiano wakisema kuwa rais huyo wa zamani ana lengo la kurejesha nyuma juhudi zinazoendelea za kuwaunganisha.

Said Soud, mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP), alisema kuibuka kwa Dk Salmin ni dalili za kukataa maridhiano ambayo kwa kiasi kikubwa yamepiga hatua ya kuondoa chuki na ubaguzi kati ya Wapemba na Waunguja.

“Ni ishara ya kambi inayokataa maridhiano ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa," alisema Soud akizungumzia kuonekana Dodoma kwa Dk Salmin ambaye aliiongoza Zanzibar wakati hali ya kisiasa ikiwa tete.

"Ni jambo la kusikitisha sana na kuhuzunisha kwani siasa za chuki zinaendelezwa na ndio maana likaibuka suala la kuwa Shein sio Mzanzibari na kwamba ati amezaliwa Bagamoyo... pia kwamba Aboud hajasoma... hizi zote ni chuki dhidi ya Wapemba tu; wanataka kuturejesha nyuma.”

Kauli ya Soud iliungwa mkono na katibu mkuu wa TADEA, Juma Ali Khatib ambaye alisema Salimin anataka kuwarejesha Wazanzibari pale alipowaacha yeye ambapo chuki zilitawala hadi baadhi ya wafanyakazi kufukuzwa kutokana na fitna za kisiasa.

“Anajua kuwa hakuna chuki za kisiasa za Upemba na Uunguja hivi sasa kutoka kuazishwa kwa maridhiano mwaka jana. Tunawaomba CCM wawe makini sana kumuangalia mtu huyu... siasa zake ni za kizamani na hazipaswi kuendelezwa,” alisema Khatib.

Naye Ali Omar wa NCCR- Mageuzi alisema: “Tunapozungumzia hili, hatuingilii utaratibu wa CCM, lakini tunajali sana utaifa na kuendelea kwa amani na utulivu nchini na watu kama Salmin wenye mawazo ya mgando wasiotaka mabadiliko hawatufai kwa sasa ni vyema wakatupisha.”

Baadhi ya wana-CCM wa visiwani hapa nao walikuwa mstari wa mbele kupinga Dk Salmin kutia mkono wake kwenye urais wa Zanzibar.

“Tumefurahi zaidi Dk Salmin kwenda Dodoma tukijua kuwa kuwepo kwake kutatuletea mgombea anayekubalika Unguja na Pemba, lakini kama ana ajenda ya kumuunga mkono mgombea Shamsi Nahodha, hilo litakuwa ni kurejesha nyuma katika maridhiano,” alisema kiongozi mmoja wa CCM ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.

Hata hivyo, Kada maarufu wa CCM, Baraka Mohammed Shamte alisema kuwepo kwa Dk Salmin Dodoma ni jambo la kawaida kwa kuwa ana haki ya kushiriki vikao vya chama chake hasa wakati wa maamuzi mazito kama ya kumteua mgombea wa urais wa nchi yake.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa wameelezea kuwa kama Dk Shein atajitoa kwenye kinyang'anyiro, Dk Gharib Bilal atakuwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda kwa kuwa ana uhakika wa kupata karibu kura zote za mikoa ya Kanda ya Ziwa kutokana na ushawishi mkubwa wa kada wa siku nyingi wa CCM anayetokea kwenye moja ya mikoa hiyo.

"Awali kundi hilo liliandaliwa kumpigia kura Abood, lakini baada ya kuondolewa lote limehamia kwa Bilal," chanzo kingine cha habari kilisema.

Chanzo hicho cha habari kilitaja mikoa hiyo na idadi ya kura ambazo Bilal anaweza kuzichukua kwenye mabano kuwa ni Tabora (2), Shinyanga (3), Mwanza (4), Mara (5), Kigoma (3), Kagera (3) na Singida (2).

Mikoa mingine ni Ruvuma (3), Mbeya (3), Arusha (4), Manyara (2), Iringa (1), Dare es Salaam (3), Morogoro (3), Kilimanjaro (1) na Lindi (3).

Habari nyingine zimeeleza kuwa Nahodha ana nafasi kubwa kumshinda Dk Bilal kwani anakubalika kwa zaidi ya nusu ya wapiga kura wa visiwani Zanzibar na baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara.

"Kura 45 za makundi maalum hazitabiriki. Bilal ana hakika ya kupata kura tano kati ya kura 15 za vijana, kura 10 za UWT. Kura 7 za wazazi zitategemea mwelekeo wa mwenyekiti (JK) na kura nyingine zilizobaki zinahitaji nguvu ya kampeni za mgombea," alisema.

Katika hatua nyingine, zaidi ya wanachama 200 kutoka Zanzibar wako mjini Dodoma kumpigia kampeni Dk Bilal na wanahoji sababu za Dk Bilal kujiamini kupita kiasi kwenye kinyang'anyiro hicho, wakihisi kuwa huenda aliahidiwa kitu na serikali ya awamu ya tatu.

Mussa Juma anaripoti kutoka Dodoma kuwa wafuasi wa Dk Bilal sasa wanamtaka rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kushawishi wajumbe wa kamati kuu na halmashauri kuu ya CCM kutimiza ahadi yake wanayodai alimpa mgombea huyo mwaka 2000.

Dk Bilal alichukua fomu ya kugombea urais wa Zanzibar mwaka 2000 na akapeleka tena jina mwaka 2005 katika kipindi ambacho wana-CCM walitarajia kuwa Karume angeachiwa awe mgombea pekee wa chama hicho ili amalizie kipindi cha pili cha utawala wake.

Hata hivyo, Dk Bilal aliondolewa na Karume kupitishwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM.

Wakizungumza nje ya ukumbi wa CCM Makao makuu jana, wafuasi hao wa Dk. Bilal walisema muda wa Dk Bilal kuingia Ikulu ya Zanzibar umefika sasa kwani aliombwa kusubiri mwaka 2000 ili kumpisha Rais Karume na alitii.

"Tangu mwaka 2000, sisi Wazanzibari tulikuwa tukimtaka Bilal, lakini akaambiwa na Mkapa asubiri na huu ndio muda wake," alisema mwanachama wa CCM, Juma Haji toka maskani ya Kisonge.

Naye kada wa CCM Zanzibar, Baraka Shamte alisema tangu mwaka 2000 chaguo la Wazanzibari ni Bilal na hawajabadili nia yao.

"Sisi tumekuja huku kuleta ujumbe wa Wazanzibari kuwa tunamtaka Bilal... kama watatuletea mtu mwingine, basi litakalotokea Zanzibar, CCM itajuta," alisema Shamte.

Mwananchi ilishuhudia na kuwasikia baadhi yao wakieleza mbele ya wanaCCM wenzao kutoka Tanzania Bara kuomba msaada wa kutafutiwa wajumbe wa mkutano huo ili kuwaweka sawa kabla ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika leo.

Habari hii imeandaliwa na Kizitto Noya Dar, Exuper Kachenje na Habel Chidawali, Dodoma

Urais Zanzibar rafu tupu:DK SHEIN ADAIWA KUJIONDOA
 
Tatizo, sera za CUF ni za chuki, ubaguzi, udini, nk.

There is no right to speak if you dont have fact and figures, and to get it you have to conduct a research, sasa mzee uyasemayo unauhakika nayo ua ni ushabiki tu kama kawaida yeyu watz kwanini tusiwaachie watz wafanye uamuzi or otherwise if you have five facts and figure which shows CUF ni wabaguzi, wadini, wachuki ambao ni vyema ukaunufaisha uma, it is your call Buchanan!
 
Shein hajajitoa...tena umeshaandaliwa mkakati wa kumpitisha kwa mchezo wa rafu kama kawaida...wa Zenj mlie tu Bara tutaendelea kuwachagulia rais indirectly for ever.
 
Tatizo lako ni kwamba akili na macho yako yanadanganyika na ujanja wa CCM!! Hakuna Rais aliyepata kutawala Tanzania anaeendekeza UDINI na ukabila kama Kikwete; sina haja ya kudhihilisha hilo, mifano iko wazi ila nikuambia tu tabia yake ya kupeleka miradi ya kiwanja cha ndege , bandali na Viwanda ili mradi Bagamoyo ndiko anakotoka ni ashara tosha ya mtu anayejipendelea kwa maamuzi yake bila kuangalia faida kwa nchi nzima.

Unapochangia tafadhali kama haujui kitu kaa kimya au tafuta taarifa kamili. Unadhani utakuwa unawaambia nini watanzania wasiojua jambo hili? Huu mpango wa SEZ/EPZ ulianza wakati wa uongozi wa rais Mkapa na ndipo ikaundwa EPZA kama mamlaka ya kuratibu shughuli hizi. Mipango hii iko mikoa mingi sana ya nchi hii angalia www.epza.co.tz utapata taarifa kamili. Inamaana EPZ ya pale mabibo pia kajenga Kikwete? Acha uzushi na uzandiki toa taarifa zenye kuelimisha jamii
 
Once again Dodoma is HOT HOT HOT pamoja na kuwa kuna kijibaridi flani nyakati hizi lakini Dodoma.......................ah is just HOT; Yaani huu mji we acha tu......................inabidi tuwatafute Wajerumani watuaambie ilikuwa nini hasa siri yaWao kuuufanya Mji na hatimaje Baba wa taifa kuamua yawe MAKAO MAKUU ya SERIKALI!
 
Leo nimesikia hadi Mama Karume katia timu mjini hapa du! "Mama wa Taifa la Zanzibar", Naam Dodoma kumekucha once again Watanzania wote wanaelekeza masiko yake hapa!
 
Shein hajajitoa...tena umeshaandaliwa mkakati wa kumpitisha kwa mchezo wa rafu kama kawaida...wa Zenj mlie tu Bara tutaendelea kuwachagulia rais indirectly for ever.

Source..Mwanainchi

poll.png
Nani atakuwa Rais wa awamu ya sita Zanzibar? Dk Ali Mohamed Shein 1114 55.5%
Mohamed Gharib Bilal 495 24.7%
Shamsi Vuai Nahodha 159 7.9%
Mohamed Aboud Mohamed 68 3.4%
Ali Abeid Amani Karume 50 2.5%
Maalim Haroun Ali Suleiman 38 1.9%
Omar Sheha Mussa 27 1.3%
Ali Juma Shamhuna 20 1%
Hamad Bakari Mshindo 19 0.9%
Mohammed Yussuf Mshamba 18 0.9%
 
Kuna tetesi nimezipata kuwa Dr Shein anaweza kushinda amini usiamini. Kuna wazawa yaani wanzilishi wa CCM wametia mguu kudai kuwa CCM Kusini ambalo linaongozwa na Dk Salmin limekuwa likishutumiwa halitetei maslahi ya wazanzibar bali maslahi ya matumbo yao na jamaa zao kusini. Inasemekana, wanadai wao ni wanamapinduzi but ukweli wanatamaa ya madaraka. Hawa wazee wamesema kuwa watampigia kampeni Dr Shein na wamesema akishindwa watampa Shamsi Vuai Nahodha but hawampi Dr Bilal. Stay tuned!!!!
 
Tatizo lako ni kwamba akili na macho yako yanadanganyika na ujanja wa CCM!! Hakuna Rais aliyepata kutawala Tanzania anaeendekeza UDINI na ukabila kama Kikwete; sina haja ya kudhihilisha hilo, mifano iko wazi ila nikuambia tu tabia yake ya kupeleka miradi ya kiwanja cha ndege , bandali na Viwanda ili mradi Bagamoyo ndiko anakotoka ni ashara tosha ya mtu anayejipendelea kwa maamuzi yake bila kuangalia faida kwa nchi nzima.
Muwamba ngozi always anavutia kwake.
 
There is no right to speak if you dont have fact and figures, and to get it you have to conduct a research, sasa mzee uyasemayo unauhakika nayo ua ni ushabiki tu kama kawaida yeyu watz kwanini tusiwaachie watz wafanye uamuzi or otherwise if you have five facts and figure which shows CUF ni wabaguzi, wadini, wachuki ambao ni vyema ukaunufaisha uma, it is your call Buchanan!

Kwani mimi nimewashikilia watz wasifanye maamuzi? Kama nisemayo ni uwongo, si watz wataona kwamba ni uwongo na watakichagua chama hicho (CUF)? Sasa wasiwasi wako ni nini hapa? Au kuna ka ukweli ambako kanaonekana kukuuma kwenye hili?
 
Mkuu Halisi, Keil
Wapo watu wanaweza kutusaidia kitaalamu zaidi. Ila ninachoweza kudadavua katika maswali hayo ni kama ifuatavyo:
Itakumbukwa katika muafaka wa mwanzo au wapili ilitakiwa pawepo mabadiliko ya tume kwa kuingiza wajumbe kutoka vyama vya siasa na hili lilifanyika kwa CUF kuingiza wajumbe wawili na CCM kadhalika. CUF iliwapeleka ndg. Nassor Khamis Mohammed(mwanasheria) na ndg.Ayoub Bakar na CCM ikawakilishwa na ndg. Khatib Mwinchande na Said Bakari Jecha ambaye amewahi kuwa kitengo cha usalama wa taifa na waziri katika wa SMZ kama sikosei na bado ni mjumbe wa tume.

Cha ajabu licha ya kuwa wajumbe wa CUF wamo humo lakini bado ZEC imekuwa ikiongozwa na makada wa chama cha Mapinduzi na usalama wa taifa. Tokea tume iundwe Wenyeviti wake wote wamekuwa ni makada wa CCM kuanzia jaji Zubeir Juma Mzee, Mzee Masauni (baba yake Masauni aliyefukuzwa ubosi UVCCM)...na huyu wa sasa Khatibu Mwinchande ambaye awali alikuwa mjumbe wa tume hiyo kwa tiketi ya CCM sasa ndo mwenyekiti wake. Uadilifu wa tume bado una mashaka na wajumbe wawili wa CUF humo hawawashi wala hawazimi.

Kuhusu maandalizi ya kuzuia wizi wa kura kwa CUF hali imekuwa ngumu, kwa sababu moja kubwa, CCM wana mbinu nyingi za kuiba kura, hawaibi kwa kuziongeza zao, wanaanza kuzipunguza za CUF...mfano kuwakataa kuandikisha wapiga kura wake ,ukizingatia tume ni yao wao na mchakato wa kupandikiza wapiga kura hewa huwa ni rahisi kwao, bila shaka haya yote tumeyashuhudia katika hatua ya ku up date daftari la wapiga kura.

Ilichofanya CUF,kama kawaida ya Maalim Seif, ambaye ni ukweli usiofichika kuwa hakuna mwanasiasa yeyote anaeziweza siasa za visiwani kama Maalim Seif, amecheza karata yake ambayo mimi naiita "confusion card" nyinyi iiteni "MARIDHIANO BAINA YAKE NA KARUME". Karata hii tayari inafanya kazi yake vizuri sasa hivi, kwakuwa imeshakigawa chama cha mapinduzi vipande vipande. Ni triki ambayo imeshakigawa chama cha mapinduzi Zanzibar na kumchanganya mwenyekiti wake Kikwete.

Hapa binafsi nayakumbuka maneno ya Maalim Seif aliyosema katika mkutano wa hadhara Kibandamaiti,baadha ya kutanganza kumtambua karume,alisema"wanaosema injini ya Maalim Seif imechemsha wanajidanganya....injini ya Maalim haijachemsha bado ipo fit na subirini mtaona..." nakweli sasa tunaona, kirusi cha MARIDHIANO kinaichachafya CCM yote.

Hapa CUF wanafaidika vipi?
Kama DR.Shein atalazimishwa kupita basi hivyo hivyo atalazimishwa kuwa rais Zanzibar na serikali ya mseto itaundwa hata kama kura ya maoni itasema HAPANA. Kwa hiyo maalim kurudi ikulu ni suala la kusubiri tu,ukizingatia CUF inaweza kum KNOCK OUT,Dr.sheni kwa kumuwekea pingamizi kugombea, ambayo ipo wazi kuwa hana sifa yakuwa mgombea baada ya kupoteza ile ya kuwa mwakilishi.

Kama Bilal atapitishwa itachukuwa mda kidogo CCM kupotea kwa kuwa migogoro ya siasa haita kwisha iwapo kura ya maoni italazimishwa kuwa HAPANA, nikimaanisha karata ya CUF itabaki kwa kura ya maoni tu na mkakati mweingine ambao ni siri ya chama.
Nafikiri kwa suala la tatu litakuw limejibika kwa lapili.

Kaka Junius umejibu majibu ambayo naamini hata wataalamu wetu wasingeweza kujibu kwa kuwa wengi wameathirika na U-CCM.. shukran sana na hii usijeshangaa siku moja ikachotwa na kutumika katika vyombo vyetu siku sijazo maana ndio ukweli mkubwa
 
Habari kutoka chanzo muhimu kinasema jina la Dr Shein limeshapitishwa. Kinachofanyika sasa ni kuona namna ya kuhalalisha hili jambo ili lisiwagawe wazanzibar. Yaani CCM ni kiboko; kama ni hesabu wanaanzia kwenye jibu kwanza ndo wanakuja kwenye workings ku-justify jibu waliloliweka.
 
ukweli ni kwamba majority ya wazanzibar wanamtaka bilal hata maskani zote uko zenji uyu bilal has strong appeal ila inasemekana si wa kupelekeshwa ni dizaini ya salmin amour anapenda siasa za chuki na ubabe, kwa cuf huyu jamaa ni bad news wasiombee apite, watashughulikiwa kisawasawa!
 
Kuna tetesi nimezipata kuwa Dr Shein anaweza kushinda amini usiamini. Kuna wazawa yaani wanzilishi wa CCM wametia mguu kudai kuwa CCM Kusini ambalo linaongozwa na Dk Salmin limekuwa likishutumiwa halitetei maslahi ya wazanzibar bali maslahi ya matumbo yao na jamaa zao kusini. Inasemekana, wanadai wao ni wanamapinduzi but ukweli wanatamaa ya madaraka. Hawa wazee wamesema kuwa watampigia kampeni Dr Shein na wamesema akishindwa watampa Shamsi Vuai Nahodha but hawampi Dr Bilal. Stay tuned!!!!

duhh Hii sasas ni kiboko full,

Any News???

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom