Sheikh Yahya awatabiria mikosi wanasiasa

warea

JF-Expert Member
Jan 22, 2010
244
65
Hata kama anayotabiri yanawafaa wateja wake, hii ni hatari kwa usalam wa raia.

Is this what free speach means?
Huku si ndio kuwaambia majambazi wawaandame wanasiasa? Halafu watu wakidhurika, watu waseme yeye alitabiri?

Habari kamili hii hapa:

MTABIRI maarufu Afrika Mashariki na Kati, Shekhe Yahya Hussein, amesema baadhi ya viongozi na wafanyabiashara maarufu nchini kuwa wengi wao watatekwa na kuporwa mali zao na kwamba matukio hayo yatafanyika kati ya mwezi huu na Julai mwaka huu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Shekhe Hussein aliwataka viongozi na wafanyabiashara hao, kuchukua tahadhari katika shughuli zao na hasa katika kipindi hicho.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi hao wanapaswa kujichunga ili wasitekwe, wasiibiwe mali zao na kufanywa bidhaa."Kuanzia April 19 na kuendelea hadi Julai viongozi wa vyama vya siasa na wafanyabiashara maarufu, wajichunge ili kuepuka kutekwa nyara na kuibiwa na hata wao wenyewe kufanywa kama bidhaa," alisema Shehe Yahaya.

Alisema kwa kipindi hicho viongozi hao wanapaswa kuchukua* tahadhari kubwa hasa katika matembezi yao ya kila siku.Alisema utekaji nyara huo dhidi ya watu waliotajwa, utafanyika* wakiwa safarini au kwenye mikutano na kwamba ni vizuri wasiwe peke yao.

---------
ref: Shekhe Yahya awatabiria mikosi wanasiasa
 
Hata kama anayotabiri yanawafaa wateja wake, hii ni hatari kwa usalam wa raia.
Is this what free speach means?
Huku si ndio kuwaambia majambazi wawaandame wanasiasa? Halafu watu wakidhurika, watu waseme yeye alitabiri?

ref: Shekhe Yahya awatabiria mikosi wanasiasa

Wewe na hao wanaomuamini pengine mnaweza kuona kuwa ni jambo la kujadili lakini kwa kweli hili ni kati ya tulioyazoweya na hakuna haja ya kupoteza wakati!
 
Huyo sheikh mtabiri amezidi kwa uongo. Kabla ya uchaguz mkuu alitabiri kuwa mmoja kati ya Slaa na kikwete angekufa,mpaka sasa bado wanapeta.sheikh atalisemeaje hili?
'A lier should have a good memory' aliyosema sheikh anafikiri tumesahau? KATU hatutaongoza na fikra za huyo mbabu.
Basi ukimtegemea mwanadamu umepotea,matumain yako weka ktk Mungu wa kweli.
 
Hizi assignment mimi sipendi kweli,so niondoke JF kwenda kutafuta kasema nini?
kama huwezi kuweka hata chembe ya kile alichosema hamna haja kutupeleka kwenye magazeti
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom