Sheikh Ponda Issa Ponda SIYO Mtanzania....

JAPUONY

JF-Expert Member
Jul 16, 2010
383
186
Ndugu Wanabodi,

Napenda kuwaambia Watanzania wapenda AMANI na UTULIVU kuwa Sheikh Ponda Issa Ponda SIYO Mtanzania na kuwa ni Mtu wa Burundi aliyeingilia Kigoma na kuzamia Dar es salaam. Bw. Ponda analipwa na baadhi ya Watanzania walioko nje ya nchi kuratibu shughuli zote za vurugu kupitia mgongo wa dini ya Kiislmu ambayo hata siku mmoja mafundisho yake hayaelekezi watu kufanya vurugu na mauaji bali AMANI.

Bw. Ponda, anafadhiliwa na watu hao walioko USA, UK na nchi za Uarabuni. Nawathibitishia hili manake hata wakati wa sensa Bw. Ponda kupitia pesa hizo hizo aliweza kutoa machapisho tena za gharama akazisambaza nchi nzima kwa kutumia vijana ambao anawalipa yeye na yeye mwenyewe akiwa anazunguka katika baadhi ya mikoa kama ya Kigoma na Tanga. Wafadhili wake wengine tunawafahamu hadi kwa majina, akibisha tutamwaga hapa...!

Nimeona niwaambie hili ili mjue kuwa Ponda siyo kuwa natetea maslahi ya Waislamu bali TUMBO lake, pili, hana uchungu na vurugu ambazo anaziendesha hapa nchini. Tumekuwa tukirudi nyuma kwa uchumi siyo tu kwa sababu ya Rais wetu lakini pia kutokana na watu wachache kama hawa wakina Ponda.

Nina imani kuwa vyombo vya USALAMA vinafahamu hili lakini wameshindwa kuchukua hatua.

NOTE:
Ponda amelelewa toka Serikali ya Mwinyi, kuanzia vurugu za Mwembe Chai, Kiongozi Mkubwa wakati huo aliingilia kati kukamatwa Bw. Ponda na kumficha, unajua ni kwa nini?
Ameendelea kutoa AMRI kwa Serikali ya KIKWETE na serikali hiyo KUTII amri za Bw. Ponda! Wajua ni kwa nini?

==============
Agosti 18, 2013
Makachero waigusa familia ya Sheikh Ponda

*Wadai damu, mate na nywele

WAKATI Katibu wa Jumuiyana Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, akiendelea kuuguza jeraha linalodaiwa kutokana na risasi katika mahabusu ya Segerea, jijini Dar es Salaam, wingu jingine la mashaka limeizunguka familia yake. Mashaka hayoyanatokana na kitendo chamakachero wa vyombo vya ulinzi na usalama, wakiwemo wale wa Uhamiaji kudaiwa kuvamianyumbani kwa wazazi wake, Ujiji mkoani Kigoma,kwa nia ya kuilazimisha familia yake wachukuliwe damu kwa ajili ya vipimo vya vinasaba (DNA).

MTANZANIA Jumapili limedokezwa kuwa kabla na baada ya tukio la sasa la Sheikh Ponda kupigwa risasi, makachero hao wamejaribu kuifikia familiahiyo ya Ponda kwa takribani mara tano bila mafanikio yoyote.

Mmoja wa wanafamilia hao ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini akihofia usalama wake, amelidokeza MTANZANIA Jumapili kwamba makachero hao baada ya kushindwa kuwashawishi kutoa damu, wakataka wapatiwe mate au nywele kwa ajili ya kufanyia kipimo hicho iwa ajili ya kufanyia kipimo hicho ili kutambua kama Ponda ni ndugu yao na pia ni raia wa Tanzania.

"Tulikwisha shawishiwa sana, wakati fulani walitukatia hadi tiketi za ndege ili tuje Dar es Salaam kwa ajili ya kipimo hicho pamoja na kufanya mahojiano maalumu, lakinitulikataa, kwa sababu hawa jamaa wanaogopesha," alisema mwanafamilia huyo.

Alisema baada ya kukataa kutoa damu, ndipo walipofika kwa mara nyingine tena wakitaka kuchukua nywele za mamayake mzazi Ponda pamoja na za baadhi ya ndugu zake, lakini hilo nalo likashindikana baada ya wao kugoma.

"Tangu Sheikh Ponda aumizwe mama yake mzazi amekuwa mgonjwa,baada ya kupokea taarifa hizo kwa mshituko, hata hivyo familia kwa ujumla haina uhuru tena kwa sababu imekuwa ikifuatwafuatwana makachero hao pamoja na watu wa Uhamiaji.

"Kwa kweli hofu imetanda katika familia yetu na hatujui nini kinafuata kutokana na kuendelea kufuatiliwa na makachero, kwa mfano ile hatua ya kupewa tiketi ili kwenda Dar es Salaam ilitufanya tushituke kwa hofu ya kwamba labda kuna mpango wa kudhuru maisha yetu, wamekwisha kuja mara nyingi, wameomba mpaka kitabu wamekitoa mpaka nakala, alichoandika Sheikh Ponda,kinaitwa ‘Tanu mkoani Kigoma mwaka 1954'," alisema mwanafamilia huyo.

Wakati taarifa hizo zikiibuka sasa, kwa muda mrefu sasa kumekuwapo na habari za kukanganya juu ya asili ya Sheikh Ponda Issa Ponda, wengine wakidai kuwa ni raia wa nchini Burundi, taifa ambalo linapakana namkoa wa Kigoma, sehemu inayoelezwa ndiko alikozaliwa. Hata hivyo ndugu zake wanadai kuwawao ni raia halali wa Tanzania.

Wakati huo huo, chanzo kingine cha habari kimelidokezea gazeti hili jinsi Sheikh Ponda alivyofanikiwa kuwakwepa polisi Zanzibar, baada ya kudaiwa kutoa kauli za uchochezi katika mhadhara wa Kiislamu wakati wakiwa visiwani humo.

Inadaiwa kwamba Sheikh Ponda kabla ya kuhutubia mhadhara huo alipita gerezani kumuona kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed.

Kwamba baada ya kumaliza kuhutubia mhadhara huo, alianza safari ya kuelekea katika msikiti wa Mbuyuni.

Chanzo: Mtanzania.
 
Napenda kuwaambia Watanzania wapenda AMANI na UTULIVU kuwa Sheikh Ponda Issa Ponda SIYO Mtanzania na kuwa ni Mtu wa Burundi aliyeingilia Kigoma na kuzamia Dar es salaam.

Bw. Ponda analipwa na baadhi ya Watanzania walioko nje ya nchi kuratibu shughuli zote za vurugu
kupitia mgongo wa dini ya Kiislmu ambayo hata siku mmoja mafundisho yake hayaelekezi watu kufanya vurugu na mauaji bali AMANI. Bw. Ponda, anafadhiliwa na watu hao walioko USA, UK na nchi za Uarabuni. ........................................ Wafadhili wake wengine tunawafahamu hadi kwa majina, akibisha tutamwaga hapa...!

Kwenye red text. Wataje hapa laiv.
 
Ukweli husemwa:

Kama madai uliyoyatoa ni ya kweli, basi utakuwa ana mizizi imara ndani ya serikali ya Tanzania inayomfanya kuendesha shughuli za kidini na kijamii bila wasiwasi nchini huku akifahamu kama ni mhamiaji haramu.

Only in Tanzania.
 
Yaani nyie ndo matango kweli wewe ndo sio mtanzania na kardinal pengo wako.Hata huyu mlie mzika mara kumi kumi nae tumepata habari zake ni mrwanda mbavu kabisa.Go ponda will always behind you.
 
Yaani nyie ndo matango kweli wewe ndo sio mtanzania na kardinal pengo wako.Hata huyu mlie mzika mara kumi kumi nae tumepata habari zake ni mrwanda mbavu kabisa.Go ponda will always behind you.

Kwa taarifa yako, mimi SIAMINI katika DINI yoyote ile na hivyo SIEGEMEI upande wowote ule ki-imani.Toa comments zako ukijua hilo.
 
Kama unachosema una uhakika nacho sioni sababu kwa nini usimwage majina hapa wakiweza waje wakanushe hapa!

Nakumbuka vyombo vya habari vilimkariri Mufti siku za karibuni akidai pia kwamba huyu bwana hata shule iko "KIDUCHU". Kwa maneno mengine taarifa zake kwa kiasi zinaeleweka hata na viongozi wa BAKWATA.

Ongeza ufahamu wa Watanzania, ITATUTAFANYA TUAMINI KUWA WANAOMLINDA NDANI YA NCHI WANAMASILAHI NA VITENDO VYAKE!
 
hata wewe uliyeanzisha hii post ukizingua utaambiwa cyo mtanzania,nchi hii inajulikana watu wake ni waoga hata kupigania haki zao ukiwa jasiri unaambiwa siyo raia kwani wanajua kuhoji ukweli cyo tabia ya mtz ndo maana hata gen.ulimwengu aliambiwa cyo raia hata dr.salim ahmed salim pia aliambiwa cyo raia kwahyo ickutishe ni mbinu tu ya kunyamazisha watu.
 
Yaani nyie ndo matango kweli wewe ndo sio mtanzania na kardinal pengo wako.Hata huyu mlie mzika mara kumi kumi nae tumepata habari zake ni mrwanda mbavu kabisa.Go ponda will always behind you.

Hiyo haihalalishi uraia wa ponda. Ninachojua kwa kauli hii wewe pia uko kwenye payrol ya ponda! Kumbuka mkiendelea kumlinda Mkono wenye nguvu utamshughulikia yeye, wewe, na wote wanaomuunga mkono!
 
Mbona hapa nchini wapo watu wengi tu wa namna yake. Hawa ni watu tuliowakaribisha kwa mgongo wa kuwahifadhi kutokana na kadhia kwenye nchi zao.
 
Usalama wa taifa wanatakiwa kuwa na file lake loote na shughuli zake zoote kama anapata pesa nje wanatakiwa kujua wapi na kwa nani na kwa nini, ndio kazi yao sio kumteka Ulimboka!

Walishamkamata na kumfukuza nchini miaka ile ya mwembechai,sijui iliishiaje wakamuacha tena, sasa ameshakuwa sugu maana ni mzoefu kwa sasa.
 
Kama si mtanzania ,kama mnakumbuka dar es salaam wizara ya uhamiaji ilitoa details za kutosha kuthibitisha kua ni mtz??

Cheti cha kuzaliwa,shule ya msingi,sekondari(o level+a level) na vitambulisho vingine kama kura na vya kidini

Sasa we mtoa mada haya umeyapata wapi?
Kati ya wewe na wizara ya uhamiaji tumwamini nani??
Acha kujikoroga mkuu!!

'' Nan-sens on yua brein''
Try to put forward your effort on true stories
Badilika mkuu,,SHEIKH PONDA ni mtanzania halisi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom