Sheikh Msopa awapongeza Mbowe na Dr Slaa kuhusu kufichua ufisadi

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
Katika pita pita yangu nimekutana na habari hii toka kwa Sheikh Msopa ambaye hivi karibuni alitoa tamko la kuwashutumu Mbowe na CHADEMA. Mtu huyu huyu aliwahi kufanya press conference maelezo na kutoa tamko alilosaini yeye mwenyewe la kuwasifu watu hao hao ambao sasa anawakashifu.

Waislamu wajipanga kufichua mafisadi

2008-05-08 10:21:23
Na Godfrey Monyo


Baraza la Habari la Kiislamu Tanzania (BAHAKITA) limesema litazunguka jimbo kwa jimbo nchi nzima kuwafichua mafisadi. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa BAHAKITA, Sheikh Chifu Msopa, alipozugumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa katika kufichua ufisadi huo watahakikisha kuwa wanashirikiana pia na waumini madhehebu ya Kikristo.

Sheikh Msopa aliwataka maaskofu na viongozi wengine wa dini kukemea ufisadi kwa kutoa matamko badala yake wafanye kwa vitendo.

``Nawashuri viongozi wenzangu na hasa maaskofu tulitazame tatizo la ufisadi kwa jicho la mbali zaidi na sio kutoa matamko pekee yake,``alisema kiongozi huyo.

Alisema kuwa tayari wameanza kufanya mazungumzo na viongozi hao wa dini ili kwa pamoja wajitokeze hadharani kuelezea namna ya kutekeleza kazi hiyo ya kupinga ufisadi.

``Ni kwa vile bado tupo kwenye hatua za awali katika mazungumzo hayo la sivyo tungeweza kuja wote hapa na kusema kwa pamoja, japo wengine tayari tumeshakubaliana,`` alisema.

Sheikh Msopa alisema kwa upande wao wameanza kufanya kampeni hiyo kwa kupitia mikutano ya hadhara.

``Sisi tumeshaanza kufanya mihadhara hiyo na hivyo tunawataka watu kujitokeza kwa wingi kila wanapopata taarifa za kuwepo kwa mhadhara sehemu,`` alisema kiongozi huyo.

Aidha,BAHAKITA iliwapongeza viongozi na wanasiasa waliojitolea kufichua ufisadi, akiwemo Mbunge wa Karatu Dk. Willbord Slaa wa CHADEMA.

Katika hatua nyingine waliitupia lawama CCM na kudai kuwa ndiyo wanaotetea ufisadi nchini.

SOURCE: Nipashe
 
Fundi,
Ni kweli, njaa ni kitu kibaya sana, lakini wakubwa wanafanya uhaini wanapokaa tu huku taifa likiangamizwa na wachache kwa ulafi na njaa zao!
 
BHAKITA waliwahinkumpngeza Dr Slaa kwa kupambana na ufisadi, ccm ndo wakaingiza udini kwa tamaa ya madaraka.
 
Back
Top Bottom