Elections 2010 Sheikh Mkuu, Mufti Atoa Uhuru kwa Waislamu .....

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,551
...... Kumchagua Mgombea wa Dini yoyote!.

Zikiwa zimebakia siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban Bin Simba, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura, na kuitumia haki yao ya kidemokrasia kuwachagua viongozi wanaowataka, bila kujali misingi ya dini zao.

Mufti Simba, ameyasema hayo, leo jijini Dar es Salaam, katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi, yaliyofanyikia ofisini kwake, Bakwata Makao Makuu , Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Huku akinukuu vifungu vya Quoran Tukufu, Sheikh Mkuu, amewasisitiza Waislamu kuwa Uislamu unaitambua haki ya kupiga kura ni miongoni mwa haki za msingi za kiraia ambazo hazina haramu yoyote kwa Waislamu kupiga kura na kuwachagua viongozi wanao wapenda kwa kufuata vigezo vya sifa za viongozi hao, na sio kufuata dini wanazoziamini

Mufti Simba, amesisitiza kuwa ushindani wa kisiasa ni jambo la kheri katika kupata viongozi bora, hakuna sababu ya kuwekeana ugomvi, uhasama ama kutumia lugha zisizofaa ambazo zinaweza kutishia amani, utulivu, umoja na mshikamano wa Watanzania, kwani uchaguzi utapita, na Tanzania itaendelea.

Sheikh Mkuu, Mufti Simba, pia ameungana na viongozi mbalimbali wa kidini, kukemea siasa za udini katika kwa kutoa wito kwa Waislamu wote na Watanzania kwa ujumla, wawe huru kuchagua viongozi wanaowataka kwa mujibu wa uwezo, uadilifu, uchapakazi wao.

Mufti Simba alitolea mfano Marais wastaafu, Mwinyi na Mkapa, walichaguliwa na Watanzania kwa vigezo vya sifa za uongozi walizokuwa nazo bila kuangalia imani zao za dini, hivyo Tanzania kuendellea kusifika kama kisiwa cha amani.

Sheikh Mkuu, alimalizia kwa kuiombea dua Tanzania, uchaguzi mkuu upite kwa amani na salama, na kutoa mwito maalum kwa Waislamu wote Tanzania katika misikiti yoote ya Ijumaa, kuitumia swala ya Ijumaa ya kesho, kuswali kwa swala ‘Kunuti’, Ambayo ni dua maalum ya kuombea amani.
 
Back
Top Bottom