Sheikh Gologosi afariki katika ajali mbaya

GT,
Mkuu inabidi ukatoe ashahadu upyaaa! wewe nani wa kujua nani ataenda peponi?..

sababu kubwa ya kufanya hivyo ni ipi?

maana ningekuwa nimeabudu kinyago au nimemshirikisha Mungu sawa lakini kumsema mtu ambayewakati wa uhai wake alikuwa irrelevant kwa waislam

I'm sorry to dissapoint you, shekhe inabidi upitie tena reference zako
 
Sheikh Suleiman Gorogosi afariki dunia katika ajali ya gari

Na Said Hauni, Lindi
KAIMU Mufti wa Tanzania, Sheikh Suleiman Gorogosi amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea kwenye Kijiji cha Mnolela Wilaya ya Lindi Vijijini baada ya tairi ya mbele ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Mtwara kupasuka na kupinduka.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, Sifuel Shirima zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea jana saa 8:09 katika barabara ya Mtwara-Lindi wakati akitokea Uwanja wa Ndege Mtwara baada ya kushuka kwenye ndege akitoa jijini Dar es Salaam.

Kamanda Shirima alisema katika gari hilo kulikuwa na watu watatu, akiwamo Bakari Maguo, mfanyabiashara wa Lindi ambaye ni mmiliki wa gari hilo na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Lindi mjini, Bakari Fundi ambao wamejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Ligula mkoani Mtwara.

Gorogosi alikuwa amekwenda Lindi kufungisha ndoa ya mtoto wa Maguo ambaye ni mfanyakazi mstaafu wa Shirika la Taifa la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambayo ilikuwa ifungwe leo.

Ndugu wa marehemu Abilahi Mohammed aliiambia Mwananchi Jumapili jana kuwa mazishi wa Gorogosi ambaye alikuwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Lindi yatafanyika saa 10:00 jioni leo jioni mjini humo.

Pia Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata), lilitoa taarifa jana jioni likieleza kuwa Gorogosi lilithibitisha kifo cha Gologosi na kueleza kuwa atazikwa leo.

Marehemu ameacha wake wawili. Kabla ya kifo chake alikuwa pia mjumbe wa baraza la Ulamaa la Bakwata.

Siku za hivi karibuni, Sheikh Gorogosi alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari ambao ulimfanya kulazwa katika hospitali binafsi ya Fire jijini Dar es Salaam kwa wiki mbili, na juzi aliruhusiwa kurudi nyumbani kabla ya kwenda Lindi.

Mufti Sheikh Issa Bin Shaaban Simba alivunja baraza la maulamaa na kamati ya hija ya baraza hilo na kuviunda tena vyombo hivyo, huku akimkabidhi kukaimu nafasi yake Sheikh Gorogosi.

Mufti Simba, ambaye awali alikuwa Sheikh wa Bakwata Mkoa wa Shinyanga, alichaguliwa na Mkutano Mkuu wa Bakwata kushika wadhifa wa Umufti Oktoba 13, mwaka 2002, mkoani Dodoma katika uchaguzi ambao, masheikh tisa walijitokeza kuwania wadhifa huo. 

Masheikh hao, ni pamoja na marehemu Sheikh Gorogosi, Sheikh Suleiman Kilemile, Mbunge wa zamani wa Kibiti, Profesa Juma Mikidadi, Imamu Mkuu wa Msikiti wa Ma`amur, jijini Dar es Salaam, Sheikh Ahmed Twalib, Imamu Mkuu wa Msikiti wa Manyema, Kariakoo, Hamid Jongo.

Wengine, ni aliyekuwa Naibu Mufti, Sheikh Abubakar Zubeir, aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Ulamaa la Bakwata, Sheikh Ahmed Zubeir, Sheikh wa Bakwata Mkoa wa Kigoma, Tawfiq Malilo na aliyekuwa Msaidizi wa Mkurugenzi wa Idara ya Dini (Kitengo cha Usuluhishi) ya Bakwata, Sheikh Twaha Majaliwa.
source: Mwananchi Read News
 
Poleni Wafiwa...Sisi ni wa Allah(SW) na kwake tutarejeshwa!!

GT ...please maoni yako yanabore!!! ni Sawa umefika msibani ukaanza kumtukana marehemu mbele ya wafiwa au kadamnasi...!!! Waislam wengi hatuitaki bakwata, lkn hapa si mahala pake...lkn pia Haifai kuombeana KIFO....

Kanuni ya Msingi aliotufundisha Mtume(SAW)...inasema.Jiepusheni kutaja Mabaya ya Maiti zenu, na Jikumbusheni kwa Mema yake....!!
Umenikumbusha kitu cha msingi unapotokea msiba.
 
GT,

..kama una matatizo na Bakwata washambulie viongozi wake walio hai.

..sidhani kama ni uungwana kumshambulia marehemu kiasi unavyofanya hapa.
 
RIP . . . Sheikh Gologosi,

May the almigthy God rest his soul in eternal peace, Amen.
 
hebu tupumzishe mjomba...mambo hayo tuulize sisi, hakuna cha brain wala nini Sheikh mkuu anaogopwa na kila mtu maanawanasema majini alonayo hayawezekaniki na ukiingia kwenye anga zake basi ukae mkao wa kula

hakuna brains zozote ..kungekuwa na brains basi wasingekubali lile dula liuze pombe pale nje ya ofisi za BAKWATA shule ya Kindondoni Muslim..mpaka waislam wakaja kuliondoa kinguvu

sasa kama angekuwa na hizo brains mbona hawakuzitumia wakati wa kusign contract na tenants?

GT'
Kwahiyo ninyi waislamu mnafuga majini/mapepo/mashetani na kufanya uchawi? Huoni kuwa wote mwisho wenu ni jehanamu ya moto?

Tubuni dhambi zenu na kumpokea YESU nanyi mtaurithi uzima wa milele
 
Wanabodi,

Mbona siku hizi tumekuwa na roho mbaya kiasi hiki ? Kweli tunashindwa hata kumtakia Marehemu pumziko la milele ? Regardless ya tofauti zetu , mwenzetu ameshatangulia mbele ya haki , sasa sisi ni nani mpaka tumhukumu . Jamani Marehemu ameacha pengo kwa familia, jamii kubwa ya waislam na wapenda amani huko Tanzania , tujaribu kujiweka kwenye nafasi zao kwa dakika moja ...then tell me how would you feel kama watu wangekuwa wanamhukumu ndugu/baba yako . Honestly , this is plainly pathetic AND FOR THE FIRST TIME I AM EMBARRASSED TO BE A JF MEMBER. Mind you kila mtu ataonja u- mauti !

sababu kubwa ya kufanya hivyo ni ipi?

maana ningekuwa nimeabudu kinyago au nimemshirikisha Mungu sawa lakini kumsema mtu ambayewakati wa uhai wake alikuwa irrelevant kwa waislam

I'm sorry to dissapoint you, shekhe inabidi upitie tena reference zako
Matatizo yako na BAKWATA yapeleke huko huko BAKWATA na si hapa JF.Hivi una Roho gani wewe,yaani badala ya kuomboleza unaanza kutuletea lawama zako hapa.Hebu muache Sheikh Gorogosi apumzike kwa Amani bwana..Hata kama we dare to talk openly si kihivyo bwana...R.I.P Sheikh Gorogosi,Mungu akurehemu
 
Wakuu, mnakumbuka ripoti ya ajali ya Mwakyembe wakubwa walishauri watu wasitumie tubeless tires? Mnakumbuka? Walipotosha taifa.

Yale matairi traditional ( yenye mipira ndani ) ndio noma zaidi, hatari, na ndo maana tire makers waka do away with them. Tube huwa lina msuguano na tairi halafu litapata joto, matokeo yake linaweza burst. Pia, tubeless tire likipata puncture litatoa hewa taratibu, halitapasuka, wakati tube likipata katobo linaweza kupasuka kwa mlipuko kama vile unavyochoma chelewa kwenye puto halafu linapusuka PUUUUF! Hatari. (Chanzo)

Sasa wakuu, iweje polisi wetu watoe rai kwa umma kwamba watu waendelee kutumia matairi yenye mipira? Sijui matairi ya Marehemu Gorogosi yalikuwa ni aina gani, lakini inawezekana ndio hayo hayo maana Polisi wetu ndio wanayo ya recommend hayo. Can you imagine that?

Hili ni pigo kwa Taifa. Mungu karuhusu mja wake afe kifo cha violence namna hii na tunasema "Mungu amrehemu"? Angekuwa wa kurehemu angeshindwa kuepusha ka tairi kamoja kasipasuke? Mungu hata sikuelewi!
 
Calm down mkuu. Mbona kuna watu wengi sana wanakufa kwa ajali au vifo vibaya zaidi? Hao wanastahili? Ni watumishi tu wa Mungu wanaostahili kuondoka huko wamelala? Au labda utuambia kifo gani ni kizuri. Sote twazaliwa kwa njia moja lakini tunakufa kwa njia tofauti. Sheikh Gorogosi kaongoka kwa ajili lakini siyo wa kwanza wala hata kuwa wamwisho. Cha kuomba ni Mungu atupokee siku tutakayo ondoka lakini hatuna jinsi ya kupanga tutaondokaje. R.I.P. Sheikh Suleiman Gorogosi.
 
Hukunielewa, na tatizo ni Kiswahili, nadhani.

Sikusema chochote kuhusu "watumishi" wa Mungu. Nimetumia maneno "mja wake." Nimesema Mungu karuhusu "mja" wake afe kifo balaa namna hii. Hata wewe MwanaFalsafa unaweza kuwa mja wake. Na wewe ungekumbwa na zahma hili ningeweza sema hivyo hivyo, kwamba tunasema "Mungu amheremu," well, angekuwa wa kurehemu angemrehemu kumwepushia baa hili la kifo cha violence mbaya hii kwa kuzui katairi kasipasuke.

Na kama ni Mungu ndio anapanga kila kitu ikiwemo tutakavyokufa, basi hakuna haja ya kuimba hapa "Mungu amheremu... Mungu amrehemu...Inna Illa Illahi..." Si Mungu keshapanga? Usali usisali, kama si wa kurehemiwa hatarehemiwa, huwezi kumpigia Mungu gitaa.

Au kama maombi yetu yanaweza kumu influence Mungu, basi atuambie ni vigezo gani anatumia kusikikiza ombi lile, na kudharau ombi hili. Manake hata maombi ya kazi unajulishwa qualifications, na ukikosa unaweza jua ulichopungukiwa, ukaenda ongeza ujuzi, ukaja omba tena. Mungu asiyeeleweka hafai kutawala viumbe vyenye fikra, kitu ukikipa fikra utazua maswali. Sasa waja wa Mungu, mjibieni mueleweke, msimuangushe. Au kacheni.
 
Nimepokea kwa huzuni kubwa sana taarifa za kifo cha Sheikh Suleiman Gorogosi.
P.K.A. Sheikh Suleiman Gorogosi
 
GT,
Umenifadhaisha na kunisikitisha sana kwa maoni na posts zako katika thread hii. Hatuwezi kukuhukumu kwa unayoyafanya ila Mwenyezi Mungu ndiye muweza wa kila kitu. Ameamua kumuita Sheikh Suleiman ni kwa sababu anajua fika kuwa wakati wake wa kuifariki Dunia umefika.
Tafadhali, ya dunia tuyaache kama yalivyo na tumuombee Sheikh alale mahala pema peponi, Amen.
 
well, i am sorry to dissapoint you mimi sitoingia kwenye hii orgy ya kutaka kumfanya Gorogosi kuwa ni mtakatifu and i will stand by my opinion kuwa alikuwa ni useless kwenye interfaith dialogue in Tanzania.

Zaidi ya hayo huyu bwana aliendorse bila kuuliza maswali ile PREVENTION OF TERRORISM ACT YA 2002 amabayo kama alivyosema ISSA SHIVJI kuwa tulichokifanya ni kucopy and paste ile PATRIOT ACT,ya 2001 ya USA ...maana hatukukosea hata spelling!

Anyway Gorogosi kama kiongozi wa kidini alipoulizwa kuhusus hii issue jibu lake ni kuwa "ahh ntaweza wapi mie mambo yenu hayo bwana wee ahhh" sasa kwa waislam ambao waliathirika na PREVENTION DETENTION ACT ya 1964 surely mtu mwenye calibre ya Gorogosi should have known better what to say..lakini how can we forget maneno ya kejeli aliyoyatoa Gorogosi kuhusus Independent inquest wakati wa vurugu za MWEMBECHAI?

Labda ungepitia kitabu cha GOOD MUSLIM,BAD MUSLIM kilichoandikwa na Maamdani utaelewa ninachokiongelea hapa

Narudia tena huyu marehemu Gorogori hakucommand respect among the majority muslims bali alikuwa ana command respect ya hawa waliookuwa tayari kupata vijisenti ili wasiulize maswali. Sana sana Legacy yake itakuwa kuwa ni kujenga maduka ya pale kinondoni Muslim na Mwinyi kupigwa kibao mbele yake

INSHAALAH MWENYEZI MUNGU AMFIKISHE MAHALA ANAPOSTAHILI
 
Wakuu, mnakumbuka ripoti ya ajali ya Mwakyembe wakubwa walishauri watu wasitumie tubeless tires? Mnakumbuka? Walipotosha taifa.

Yale matairi traditional ( yenye mipira ndani ) ndio noma zaidi, hatari, na ndo maana tire makers waka do away with them. Tube huwa lina msuguano na tairi halafu litapata joto, matokeo yake linaweza burst. Pia, tubeless tire likipata puncture litatoa hewa taratibu, halitapasuka, wakati tube likipata katobo linaweza kupasuka kwa mlipuko kama vile unavyochoma chelewa kwenye puto halafu linapusuka PUUUUF! Hatari. (Chanzo)

Sasa wakuu, iweje polisi wetu watoe rai kwa umma kwamba watu waendelee kutumia matairi yenye mipira?
Sijui matairi ya Marehemu Gorogosi yalikuwa ni aina gani, lakini inawezekana ndio hayo hayo maana Polisi wetu ndio wanayo ya recommend hayo. Can you imagine that?

Hili ni pigo kwa Taifa. Mungu karuhusu mja wake afe kifo cha violence namna hii na tunasema "Mungu amrehemu"? Angekuwa wa kurehemu angeshindwa kuepusha ka tairi kamoja kasipasuke? Mungu hata sikuelewi!

2cnbc6c.jpg
 
GT,

..kama una matatizo na Bakwata washambulie viongozi wake walio hai.

..sidhani kama ni uungwana kumshambulia marehemu kiasi unavyofanya hapa.

Hebu nipumzsihe na risala zako bwana mbona mnataka kuleta unafiki? Nyerer kafa miaka mingapi leo na watu kama kawaida wanaendelea kumkosoa na kuelezea mabaya aliyoyafanya

so please spare me haya mambo ya kutkutaka kumromanticise Gorogosi as if alifanya kikubwa cha watu kujivunia

whats the point ya kuthink independently huku unaogopa ku express your mind freely ?
 
GT,

..kama una matatizo na Bakwata washambulie viongozi wake walio hai.

..sidhani kama ni uungwana kumshambulia marehemu kiasi unavyofanya hapa.

one minute mnataka watu waseme ukweli next minute mnataka stara..

whats the point?

halafu mnataka mpewe nchi
 
Wanabodi,

Mbona siku hizi tumekuwa na roho mbaya kiasi hiki ? Kweli tunashindwa hata kumtakia Marehemu pumziko la milele ? Regardless ya tofauti zetu , mwenzetu ameshatangulia mbele ya haki , sasa sisi ni nani mpaka tumhukumu . Jamani Marehemu ameacha pengo kwa familia, jamii kubwa ya waislam na wapenda amani huko Tanzania , tujaribu kujiweka kwenye nafasi zao kwa dakika moja ...then tell me how would you feel kama watu wangekuwa wanamhukumu ndugu/baba yako . Honestly , this is plainly pathetic AND FOR THE FIRST TIME I AM EMBARRASSED TO BE A JF MEMBER. Mind you kila mtu ataonja u- mauti !

Hebu tufafanulie Pengo lipi aliloliacha Marehemu labda ungeweza kutufahamisha jambo ambalo labda wengine hatulijui

Maana angekuwa accomplished scholar then tungesema kuwa ohh jamaa kaacha walth of academic works lakini ukweli ni kuwa HAKUNA sasa mbona mnataka kumfanya Gorogosi kitu ambacho hakuwa?
 
Back
Top Bottom