Sheikh Farid na wenzake wanyimwa dhamana

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Yule kiongozi wa kikundi cha UAMSHO Z'bar na wenzake leo wamepandishwa kizimbani wakituhumiwa kutoa maneno ya uchochezi na kusababisha vurugu ambapo hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo amewanyima dhamana mpaka Alhamisi kwani kuna vipengele ambavyo mawakili wao walivipinga kikiwepo cha kila mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili ambapo mmoja wao ni lazima awe mtumishi wa serikali.

Wao wanapinga kwamba serikali ndio iliyowashitaki sasa iweje waambiwe walete mdhamini ambaye ni mtumishi wa Serikali.

Hakimu atatoa maamuzi ya hoja hizo Alhamis hivyo viongozi wa UAMSHO wamekwenda rumande.

Kesi imefikishwa leo Mahakama kuu ya Zanzibar na Imeahirishwa hadi Alhamisi.

Mashtaka yanayomkabili Sheikh Farid na wenzake;
KUTOA MANENO YA UCHOCHEZI
KUSABABISHA VURUGU ZILIZOTOKEA MIEZI MIWILI NYUMA.

Mawakili wake walilamika kuwa upande wa serikali umeshindwa kuwapatia order paper ya washtakiwa.

Vile vile walilalamikia Jinsi Jeshi la polisi wanavovunja sheria kwa Kuwazuwia Mawakili hao kuonana na wateja wao ambao jambo ambali=o ni kinyume cha sheria.

Ugumu wa Dhamana:

Mawakili imetaka mahakama kuondoa baadhi ya vipengele vya DHAMANA ikiwemo kuwepo kwa barua ya sheha kwani masheha wakifatwa hujifanya wana vikao na hawataki kutoa.

Vile vile kuondoa kipengele cha kuwepo mdhamini mmoja ambae ni mfanyakazi wa serikali. Wanasheria hao wamesema haiwezekani ikawa serikali ndio inawashataki halafu lazima awepo mdhamini ambae anafanya kazi serikalini.

Baada ya makubaliano hayo Jaji ambae aliepangiwa kesi hiyo amesema kutokana na ugumu wa kesi hiyo ameiahirisha mpaka siku ya ALHAMISI wiki hii.
 
Hao lengo lao ilikuwa wajifiche ili wafuas wao wadai wametekwa na serikal na wapate sababu ya kuanzisha fujo, wakiigiza kuwa Viongoz wao waachiwe ili hali wamewaficha, bahat mbaya mipango imebuma
 
Kesi imefikishwa leo Mahakama kuu ya Zanzibar na Imeahirishwa hadi Alhamisi.

Mashtaka yanayomkabili Sheikh Farid na wenzake;


  • KUTOA MANENO YA UCHOCHEZI
  • KUSABABISHA VURUGU ZILIZOTOKEA MIEZI MIWILI NYUMA.

Mawakili wake walilamika kuwa upande wa serikali umeshindwa kuwapatia order paper ya washtakiwa.
Vile vile walilalamikia Jinsi Jeshi la polisi wanavovunja sheria kwa Kuwazuwia Mawakili hao kuonana na wateja wao ambao jambo ambali=o ni kinyume cha sheria.

Ugumu wa Dhamana;


  • Mawakili imetaka mahakama kuondoa baadhi ya vipengele vya DHAMANA ikiwemo kuwepo kwa barua ya sheha kwani masheha wakifatwa hujifanya wana vikao na hawataki kutoa.
  • vile vile kuondoa kipengele cha kuwepo mdhamini mmoja ambae ni mfanyakazi wa serikali. wanasheria hao wamesema haiwezekani ikawa serikali ndio inawashataki halafu lazima awepo mdhamini ambae anafanya kazi serikalini.
Baada ya makubaliano hayo Jaji ambae aliepangiwa kesi hiyo amesema kutokana na ugumu wa kesi hiyo ameiahirisha mpaka siku ya ALHAMISI wiki hii.
 
Kama kweli shehe farida alijificha hakutekwa na kikatokea kile kilichotokea zanziba anastahili kuchukuliwa hatua kali za kisheria manake mtu kama huyu anahatarisha amani ya nchi
 
kwa hivyo walimteka au alijeiteka? Kama alijiteka mbona hakufunguliwa kesi?

hapa kuna maswali mengi kuliko majibu. Polisi walishasema hakutekwa, so alijiteka nyara huyu mtu.
swala ni kwamba sasa aseme alikuwa wapi? labda ndio sababu anafunguliwa kesi ya uchochezi maana ile kujiteka nyara pia ni sehemu ya kuchochea watu wafanye vurugu
 
Serikali imekosea.Pamoja na makosa hayo Wangewashtaki kwa mauaji ya askari
 
hao ilibidi wapelekwe tu jela miaka wataambiwaga hukohuko.
mimi sidhani kama watawafunga. maana mwanzo UAMSHO walisema kama kiongozi wao hataonekana nao maaskofu hawataonekana tena ndio maana baadhi yao wakakimbia. sasa wakiwafunga utasikia UAMSHO wanasema na wao watawafunga maaskofu mpaka wenzao watoke. sijui kama serekali itapenda Askofu apate tabu yoyote hapa tz
 
Kwa vile mnaongozwa na akili taahira inawezekana! Lakini dawa ni kuwashushia kichapo tu tuone kama hiyo Idd italika!

marais wtu wa sasa wanahekima kubwa . Marais wote ni waislam. na kawaida ya muislam anaamini akitawala vibaya kwa kufuata matakwa ya wacahche huko aendako atakutana na Muumba wake ambae ananguvu kuliko yeye. tofauti na tawala za Mkapa
 
Amiri Sheikh Faridi kwa usalama wake asijetekwa au kujiteka basi ni jambo la busara anyimwe dhamana na mahakama hadi kesi itakapo katiwa hukumu maana tumeona madhara kwake mwenyewe Amiri na raia akipotea vurugu mtaani.

Bora umma wote wa Zanzibar na Tanganyika tujue Amiri yupo rumande salama salimin hadi mwisho wa kesi na wanaompenda Amiri wampelekee chakula na mahitaji mengine rumande ili akishinda kesi atokee mtaani akiwa ni mzima wa afya tele kuendelea na harakati zake.

Ile wenziwe wengine ruksa dhamana maana wao si hatari kwa usalama wa raia na mali zao.
 
Back
Top Bottom