Sheikh aandaa kongamano la kitaifa

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
WATANZANIA wametakiwa kujitokeza na kushiriki katika Kongamano la kitaifa linalotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu, ili kujadili mustakabari wa rasilimali zilizopo nchini.Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Sheikh Rashid Kayumbo, alisema ameazimia kuandaa kongamano hilo, ili kuona ni namna gani rasilimali zilizopo zinamnufaisha mwananchi tofauti na ilivyo sasa.Alisema kongamano hilo litashirikisha watu wa kada mbalimbali wakiwemo wabunge, vyama vya siasa, viongozi wa dini pamoja na asasi za kiraia.Sheikh Kayumbo alisema anakerwa na baadhi ya viongozi ambao wanawapa fursa kubwa wageni kutoka nje na kushindwa kuwasaidia Watanzania kupitia rasilimali zilizopo.“Ukipitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ndiyo utaamini kuwa serikali haina dhamira ya kweli katika kuwasaidia Watanzania,” alisema.Alisema kripoti hiyo inaonesha jinsi baadhi ya wawekezaji nchini walivyoweza kusaidiwa katika mitaji yao huku wakiwepo Watanzania waliokosa mitaji na serikali kushindwa kuwasaidia.Alibainisha kuwa kabla ya kufikia uamuzi wa kuandaa kongamano hilo, alijaribu kuwasilisha taarifa zake Ofisi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, lakini baadhi ya barua zake hazikujibiwa.

source: tanzania Daima
 
namuunga mkono 100% kabisa ni wapi hiyo niende na mie ,du nimekumbuka sina hijab!!!!sio kuandamana eti mtu kakojolea msaafu,KWA HILI WAKRISTO JITOKEZENI NA SIE PAGANISM WAABUDU CHINI YA MITI NJIA PANDA MAPANGO YA AMBONI HEBU TOKENI JAMANI!!!!!!!!! cacico kimenuka njoo huku
 
Last edited by a moderator:
Kiukweli nimefurahi kwa koment zote kuhusu hii thread, kwenye masuala ya msingi tusimame pamoja regardless nani kasema tutafika pema.
 
Ningekushukia wewe sema misemo imesaidia Funika kombe shetani apite.
namuunga mkono 100% kabisa ni wapi hiyo niende na mie ,du nimekumbuka sina hijab!!!!sio kuandamana eti mtu kakojolea msaafu,KWA HILI WAKRISTO JITOKEZENI NA SIE PAGANISM WAABUDU CHINI YA MITI NJIA PANDA MAPANGO YA AMBONI HEBU TOKENI JAMANI!!!!!!!!! cacico kimenuka njoo huku
 
Last edited by a moderator:
Nia ya mkutano siku zote huwa njema ila ngoja wakutane ni MAJUNGU,KULALAMIKA,KUENEZA CHUKI DHIDI YA UKRISTU N.K nasema hivyo kwa sababu nilishawahi kuingia kwenye kikao chenye jina zuri lakin yaliyozungumzwa humo yanatisha.
 
Shehe atapata wapi akili? amawarubuni Wakristo tu mjae mlipuliwe, jihadharini sana na magaidi.
 
Nadhani katika watu wadini hapa JF wewe unabeba bendera maana kila post ya dini lazima upost utumbo tu'au unafurahia sana watu wanapokwanguana kwa masuala ya dini?kuwa na hekma japo kidogo sio lazima kila post ushushe coment
 
Safari hii Sheikh kapata wapi akili nzuri ya namna hii??? Iwapo kweli atakihubiri hicho anachoitia watu, basi hii ni ishara nzuri. Ninampongeza sana!!! Lakini ngoja kwanza tusubili tuone!!!
 
Nadhani katika watu wadini hapa JF wewe unabeba bendera maana kila post ya dini lazima upost utumbo tu'au unafurahia sana watu wanapokwanguana kwa masuala ya dini?kuwa na hekma japo kidogo sio lazima kila post ushushe coment

Mkuu ukijibizana na mwehu wewe utaonekana ni mwehu zaidi! Hakuna jibu zuri kwa mwehu kama kumkalia kimya na kumdharau!
 
WATANZANIA wametakiwa kujitokeza na kushiriki katika Kongamano la kitaifa linalotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu, ili kujadili mustakabari wa rasilimali zilizopo nchini.Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Sheikh Rashid Kayumbo, alisema ameazimia kuandaa kongamano hilo, ili kuona ni namna gani rasilimali zilizopo zinamnufaisha mwananchi tofauti na ilivyo sasa.Alisema kongamano hilo litashirikisha watu wa kada mbalimbali wakiwemo wabunge, vyama vya siasa, viongozi wa dini pamoja na asasi za kiraia.Sheikh Kayumbo alisema anakerwa na baadhi ya viongozi ambao wanawapa fursa kubwa wageni kutoka nje na kushindwa kuwasaidia Watanzania kupitia rasilimali zilizopo.“Ukipitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ndiyo utaamini kuwa serikali haina dhamira ya kweli katika kuwasaidia Watanzania,” alisema.Alisema kripoti hiyo inaonesha jinsi baadhi ya wawekezaji nchini walivyoweza kusaidiwa katika mitaji yao huku wakiwepo Watanzania waliokosa mitaji na serikali kushindwa kuwasaidia.Alibainisha kuwa kabla ya kufikia uamuzi wa kuandaa kongamano hilo, alijaribu kuwasilisha taarifa zake Ofisi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, lakini baadhi ya barua zake hazikujibiwa.

source: tanzania Daima

vema pia ungetujuza huyu shehe ni wa taasis gani?, BAKWATA au Ponda?, maaana isijekuwa ni shehe wa madrasa ya kizuiani anajifanya kuitisha kongamano la kitaifa, asijjekuwa anataka watu wakusanyike aanze kumwaga pumba!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom