Shehe Mkuu wa Tanzania awakataza Waislamu kushiriki maandamano ya kisiasa

Huyu hana kitu kabisa...di mdo wa ku[pachikwa tu huyu hata Waislamu wote hawamtambui? Chadema wanafanya siasa, Uislamu umeingiaje hapo? Haya ngoja tuone kuelekea 2015, itakavyokuwa

Mwangalie tu mtu, kwanza yeye mwenyewe ndiye aliyekaa Kisharishari, amekata tamaa anaomba fadhila kwa C c m, huu ni mtaji wa ccm, hakuna cha ccm kilicho salama karne hii.
 
Tatizo waisilamu wana vikundi vingi, na kila kikundi kina wasemaji kadhaa. Kuna kipindi kiliwahi kurushwa katika ile FM Radio yao kikiwataka waisilamu wasiende Loliondo kwa Babu. Baada ya siku chache, hapa juzi nimesikia shekhe mmoja Dodoma akisema waisilamu wanaweza kwenda tu Loliondo kupata kikombe! Sasa inakuwa confusion nani ni nani katika waisilamu. Heri huku upande mwingine inajulikana Kakobe au Mwingira kawaambia waumini wake (sio wakristu wote) kuwa wasiende, lakini kwa waisilamu unakuta tamko linasea "Waisilamu msifanye/mfanye kitu fulani" Sielewi nani ana~manage uisilamu hapa.
 
Tatizo waisilamu wana vikundi vingi, na kila kikundi kina wasemaji kadhaa. Kuna kipindi kiliwahi kurushwa katika ile FM Radio yao kikiwataka waisilamu wasiende Loliondo kwa Babu. Baada ya siku chache, hapa juzi nimesikia shekhe mmoja Dodoma akisema waisilamu wanaweza kwenda tu Loliondo kupata kikombe! Sasa inakuwa confusion nani ni nani katika waisilamu. Heri huku upande mwingine inajulikana Kakobe au Mwingira kawaambia waumini wake (sio wakristu wote) kuwa wasiende, lakini kwa waisilamu unakuta tamko linasea "Waisilamu msifanye/mfanye kitu fulani" Sielewi nani ana~manage uisilamu hapa.

Mwenyezi Mungu ndio ana-manage uislamu, hao ni viongozi wakitoa agizo ambalo alipingani na dini tunalifuata kama linapingana na dini tunalipotezea. Leo nimeamini kuwa wapenzi na wanachama wengi wa CHADEMA ni waikristu.
 
Mkuu sana Mufti Issa bin Shaban Simba....Chadema ni Chama cha siasa,sio taasisi ya dini,imesajiliwa kwa kufuata taratibu na kanuni zote zilizowekwa na ofisi ya Msajili na ndio maana inakidhi vigezo vya tume ya taifa ya uchaguzi! U mtu mkuu sana na mwenye hekima 'ya juu' na ndiyo maana ukachaguliwa na jopo la viongozi wa juu kushika wadhifa ulionao! Kwa kua katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hairuhusu ushabiki wa dini kwenye mambo ya siasa yafaa sasa nawe kuingia kwenye siasa ukiweka kofia ya dini pembeni! Baada ya kufanikisha hili nitakuelewa! Kinyume na hapo niseme unatumia nafasi yako vibaya! Salaam!
 
http://www.mwananchi.co.tz/news/4-h...i-simba-chadema-wanavuruga-amani-nchini.html#http://www.mwananchi.co.tz/news/4-h...i-simba-chadema-wanavuruga-amani-nchini.html#-1 #4 Mdanganyika 2011-03-23 05:28 nadhani vyeo vingine vinatakiwa kuwa na hekima na uelewa na kama viongozi wa dini ndio hawa bora nikawa mpagani....hivi kama hauelewi jambo hususan la mambo ya kimataifa ukinyamaza utapungukiwa na nini? ...ati mufti....ngojea niishie hapa kwani wapambe wake wakisoma hii na jinsi mawazo yao yalivyo finyu wataishia kunisomea dua...waswahili bwana....
Quote










http://www.mwananchi.co.tz/news/4-h...i-simba-chadema-wanavuruga-amani-nchini.html#http://www.mwananchi.co.tz/news/4-h...i-simba-chadema-wanavuruga-amani-nchini.html#+1 #3 mwamba 2011-03-23 05:25 Quoting Mhifadhi:
Mh!​
NI KEWLI SHEKHE MKUU HAPO UMEPOTOKA..NI NINI KINACHOKUSU[NEN O BAYA] KUSEMA KWAMBA CHADEMA INAVURUGA AMANI YA NCHI KAMA SI YALE MAWAZO KWAMBA CHADEMA NI CHAMA CHA WAKRISTO? KUAMINI HIVYO NIKUTOWATENDEA WATANZANIA NA KUTAKA KULETA MGOGORO WA KIDINI.PIA KUSEMA MAREKANI INAPIGA VITA UISLAMU SI SAHIHI MBONA WANANCHI WA LIBYA HAWAMTAKI WEWE UNA UCHUNGU KULIKO WA LIBYA? KAMA MTU NI MBAYA HATA KAMA ANATOA MISAADA KWENYE DINI HAIFUTI UBAYA WAKE.GADAFI NI DIKTETA,WALA SIYO MWISLAMU SAFI,UISLAMU NI DINI YA KULETA AMANI LAKINI GADAFI ANAUWA WATU KILA HUO NDIO UISLAMU?
Quote










http://www.mwananchi.co.tz/news/4-h...i-simba-chadema-wanavuruga-amani-nchini.html#http://www.mwananchi.co.tz/news/4-h...i-simba-chadema-wanavuruga-amani-nchini.html#0 #2 Mhifadhi 2011-03-23 04:59 Mh!
Quote










http://www.mwananchi.co.tz/news/4-h...i-simba-chadema-wanavuruga-amani-nchini.html#http://www.mwananchi.co.tz/news/4-h...i-simba-chadema-wanavuruga-amani-nchini.html#+1 #1 mbiligi 2011-03-23 04:58 Hilo tamko ni kwa niaba yako Mh Mufti na wanachama wenzako wa CCM pamoja na Makamba anayeeneza siasa za Udini.
Ghaddaf ameua laia wake ambao ni waislamu, mbona hamkutoa tamko? Uongozi wa Gaddaff sawa na uongozi wa serikali ya CCM ambayo haujali raia wake. Nyie bakwata mbona hamkutoa Tamko mauaji ya Gongo la Mboto?
Nyie Bakwata piganieni mahakama ya kadhi na mali za waislamu zilizotaifishwa n

Mahakama ya kadhi yenyewe wakipewa hawana pesa ya kuendesha hadi watumie hadi za dini nyingine, mali za waislam si amechukua Yusuf Manji? Kwani yeye msikitini hafiki wamkamate? Mbona wanalalamika na mtu wako naye?: na Wakristo warudishiwe Mahospitali yao yote na Mashule tuone kama Serikali watakuwa na Hospitali hata moja ya Rufaa
 
Kiwete ni kweli inabidi apinge huu upuuzi vinginevyo atakuwa anauunga mkono ujinga wa huyu Mufti, hivi wakristu wakiwa na akili mbaya kama hizi nao wawaambie wakristo waandamane hii nchi itakalika? Rais kikwete kama kweli si mdini kemea huu upuuzi, hawa watu wanataka kutupeleka kubaya sasa, huyu Mufti nilijua ana busara kumbe nae kama wenzake tu. Hivi yeye hajui kama wakristo wakiamua kuweka rais wao hii nchi haitakaa itawaliwe na muislamu? Yaani nimesoma hii habari nikitetemeka, tunakokwenda sio kuzuri, viongozi mmelianzisha, hasa kikwete, naomba mlimalize wenyewe, mlifikiri ni dogo.

jk amesahau kwamba amechaguliwa na watu wa dini zote! Sasa hivi amejificha nyuma ya masheikh ndio wamekuwa wasemaji wake! Ama kweli akili ni nywele....!
 
Gazeti la Mwananchi nao ni wachochezi, Mufti hakutaja jina la chama chochote, japo kuwa unaweza kuhisi alikuwa analenga chama gani.
Walitakiwa kumnukuu kama alivyosema, yeye hakutaja chama chenu.
 
Mahakama ya kadhi yenyewe wakipewa hawana pesa ya kuendesha hadi watumie hadi za dini nyingine, mali za waislam si amechukua Yusuf Manji? Kwani yeye msikitini hafiki wamkamate? Mbona wanalalamika na mtu wako naye?: na Wakristo warudishiwe Mahospitali yao yote na Mashule tuone kama Serikali watakuwa na Hospitali hata moja ya Rufaa
Muhimbili ni ya kanisa?
 
Yani nae kaingia kwenye mtego wa JK nae,namuonea huruma huyu baba kwani anaonesha kiwango chake cha ujuha...........Amani hailindwi na maneno wala silaha ya aina yeyote bali ni kwa kutenda haki kwa watu na kutekeleza kwa majukumu kwa serikali.....huyu anataka kupotosha waislamu tu,ili sera yao ya udini ifanikiwe
 
jk amesahau kwamba amechaguliwa na watu wa dini zote! Sasa hivi amejificha nyuma ya masheikh ndio wamekuwa wasemaji wake! Ama kweli akili ni nywele....!

Kikwete kachaguliwa na waislamu asilimia kubwa, hao wadini nyingine waliomchagua hawafiki hata 20% ya kura alizopata.
 
Mnamshitukia leo hii? Mbona kitambo ni kiongozi wa CCM na mtetezi damdam piga garagaza ua? Bahati mbaya kitendo cha Dr Slaa kuwa Mkatoliki tena Padre, ndugu zangu waislam wanakitafsiri kama CDM ni adui wa kidini, wakidhani CDM ni tawi la Katoliki. Wana bahati mbaya sana kwa sababu hata viongozi wa kiislam wanashabikia sana hilo na kuwafanya wafuasi wengi kuitikia bila kufikiri. Wanasahau kwamba kwa waislam wengi kuwapo CCM haina maana kuwa ccm ni tawi la kiislam. Chadema kuna waislam pia na kuingia chadema haina maana wameokoka. Kadhalika wakristo wapo ccm wengi sana na kuingia huko haina maana wameslim. Kwa yeyote anayefaidika na ufisadi wa ccm na serikali yake ni lazima atakuwa kinyume na mtu yeyote anayewasema waziwazi, maana mkate wao unaingia mchanga.

Sasa watanzania tusipoamka na kuelewa umuhimu wa Taifa mbele tutabaki na ushabiki wa kipuuzi daima na kutopea zaidi katika umaskini wakati wengine mafisadi wanaishi peponi hapahapa nchini. Lazima hali hiyo tuikomeshe. Wapinzani wa chadema wanakoroma sana lakini wanaelewa ukweli uko wapi. Mimi sina chama tangia mfumo wa vyama vingi uanze, lakini Tanzania ndio chama pekee, na utanzania ndio hasa kipaumbele changu. Sanasana naona chadema wanaongea juu ya kuimarisha utanzania wangu ingawa nao wanayo madhaifu yao, lakini ccm madhaifu yao nimingi zaidi na ya miaka mingi iliyojaa kiburi cha kukataa kutakasika. Namshauri Mzee wetu Simba azeeke vizuri na kwa heshima, asiingie kwenye mkumbo wa kina Kakobe.
 
... hao ni viongozi wakitoa agizo ambalo alipingani na dini tunalifuata kama linapingana na dini tunalipotezea....
Navyojua mimi kiongozi wa kiroho anatoa mwongozo, sasa kama kila akitoa tamko inabidi mtu individually alifikirie kivyake, maana yake wapo watakaolipotezea na wapo watakaolifuata, na kunakuwa hakuna maana ya kiongozi
 
Who is shehe simba, Ataingizaje udini kwenye siasa? Ingekaaje kama Pengo angesema wakatoliki wasishiriki mambo ya CCM? Na je, ndani ya chadema wapo wakristu pekee au na waislamu wapo? Huyu nae kaanza pumba.Ushehe wa elimu dunia ni taabu uelewa finyu
 
AMECHELEWA SANA KUSEMA BINAFSI NILILITEGEMEA HILO, Ametoa kauli isiyo na hoja yoyote ndani yake. Wadau kumbukeni huyu mzee anakiwango cha chin kielimu so kunauwezekano kuchangia kwa uelewa mdogo alionao!

Kumbe elimu yake ya Madrasa, nawashauri viongozi wote we dini kabla ya kusoma elimu yeyote ya Mungu wasome kwanza vizuri elimu ya Dunia hii maana Mungu mwenyewe hataki wajinga: Mshike sana elimu usiache aende zake, Maana itawasaidia kuweza kuwaongoza aina tofauti tofauti za za watu, wakijua ndani ya wafuasi wao kuna Wasomi sana, wasiosoma kabisa, matjiri,maskini sana, wenye akili sana na mbumbumbu pia wapo Vijana wenye damu changa na Wazee waliochoka kufikiri, hapo panahitaji Elimu ya kutosha kuwaunganisha watu wote hao waweze kukaa pamoja maskini amwone tajiri hamdharau,na tajiri amwone anamhitaji maskini, msomi aone umuhimu wa kumshauri asiyesoma ili naye aone ana thamani, Mzee aone kijana anatakiwa ushauri mzuri wa hekima pia akijua wakati wa kumwachia majukumu umefika atamkabidhije: sasa viongozi wa dini wasiposoma ndo maana wanatushauri kujilipua tukaione pepo tunajilipua bila kumhoji anayetuahidi hiyo kama yeye hataki kwenda? Si aanze yeye kujilipua kama peponi ni kuzuri tuone mfano kwake? Tumeliwa! Halafu tunapokea tu misaada toka libya kumbe nyuma yake ni kutugawanya: inafikia hatua sasa hata sadaka za Mafisadi zikataliwe Makanisani na misikitini! Japo sadaka haiondoi dhambi ya mtu /sadaka ya fisadi au muuaji haiondoi dhambi yake hata siku moja, tuseme kweli kama Kardinali Pengo amesoma akaelimika.
 
SHEHE Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban bin Simba, amewataka Waislamu wote nchini kutoshiriki katika maandamano ya wanasiasa yanaoendelea nchini kwa vile yanalenga kuleta uvunjifu wa amani.

Mufti Simba ametoa agizo hilo alipozungumza na Baraza la Maulamaa lililowashirikisha mashehe na maimamu mbalimbali wa Tanzania katika Msikiti wa Farouk uliopo katika Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Amewataka waumini hao wa Kiislamu kuvunja ukimya katika mambo mbalimbali yanayojitokeza nchini hususani yanayohusu mustakabali wa Taifa, na kuwataka mashehe na maimamu wa misikiti yote nchini kuwaasa waumini wa dini hiyo kuyapinga maandamano hayo kwa njia ya kistaabu ili amani idumishwe.

Bila kutaja chama au wanasiasa wanaoendesha maandamano hayo, Mufti Simba amesema , kimantiki maandamano hayo si halali kwa kuwa yanaonesha waziwazi kudhoofisha nguvu za Rais aliyepo madarakani katika utekelezaji wa majukumu yake.

“Sisemi ni wanasiasa wa wapi wanaochochea maandamano hayo kwa kuwa kila mmoja anajionea mwenyewe, wao badala ya kutetea amani wanageuka na kuwa wavurugaji wakubwa wa amani,” amesema Mufti Simba leo.

Aidha, amesema, hivi sasa Rais Jakaya Kikwete anaandamwa kutokana na imani ya dini yake huku waumini na viongozi wa Kiislamu wakibaki kimya bila ya kuyazungumzia masuala yanayojitokeza likiwemo hilo.

Amesema, tofauti na uongozi wa marais wanaokuwa na imani ya Kiislamu, marais wanaokuwa na imani ya Kikristo huwa hawaandamwi kiasi hicho na hivyo kuleta tafsiri kuwa imani ya dini ndiyo chanzo cha yote yanayofanywa rais aandamwe.

“Misikiti iungurume na wala isikae kimya, ukimya ufe na yalaani mabaya yote hayo pamoja na dini ya Kiislamu kufanywa tabaka la chini, tuamke na tushikamane kwa pamoja” alisema Mufti Simba.

Amelaani mashambulizi ya baadhi ya Magharibi dhidi Libya, akisema kinaonesha ile ni vita dhidi ya Uislamu na siyo vinginevyo kwa kuwa ni kawaida ya nchi ya Marekani kuziandama nchi zenye Waislamu.

Kuhusu Mahakama ya Kadhi, ameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa uanzishwaji wake kwa kuwa ni moja ya nguzo muhimu ndani ya dini hiyo huku pia akiwataka maaskofu kuacha kuingilia kati suala hilo.

Ameshangazwa kuona Waislamu wanapotaka kufanyiwa jambo lolote kunajitokeza ugumu kulitekeleza tofauti na dini nyingine, jambo alilosema halipaswi kufanywa hivyo kwa kuwa ‘wote ni watoto wa baba mmoja.’

Source: Habari Leo

Kama haya ndiyo maneno ya kiongozi wao, hao wa chini yake sijui watakuwaje.
 
Elungata unataka kauli gani nawe umesema huo ndo ukweli wako? We lala tu, tumekusoma kabla hujaandika.

Elungata mwenyewe inaonekana pia hajipendi, huwezachukia Chadema ukawa unajipenda, na sbabu zipo tukianzia elimu na ugumu wa maisha jumlisha ufisadi.
 
Siku yaja, Pale waumini wake, yaani waislamu kwa ujumla watakapogundua kuwa Mnatumia Udini kuficha maovu mtaondolewa kwa Nguvu kama inavyotokea sasa kwatika nchi za Kiarabu.

Tunisia, Misri, Yemen, Saudi Arabia, Bahrain, Jordan kote huko ni vijana wa Kiislam walio elimika na kutambua uovu wa viongozi wao ndio wameamua kuleta mabadiliko ya maisha yao. Kuwa muislam haina maana kuwa mjinga, bali kuwa mwerevu na kutetea haki zako. Dini ni staili ya maisha tu lakini ukweli unabaki pale pale kama hakuna chakula au matibabu dini haiwezi kukupatia hivyo vitu, au kama maisha ni magumu dini haiwezi kukupatia hilo. Je Kama huyu Sheikh anasema USA inaonea uislamu kwa nini waislamu wanakimbilia kuishi USA?
Hii inaonyesha kuna wengi tu wameanza kugunduo janja yenu nyie mnaojiita Mufti..... sasa wewe endelea na utaona wafuasi wako watakavyokugeuka wakishaujua ukweli.
 
Back
Top Bottom