She is attracted to a co-worker.. mgogoro na jamaa

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Ni kisa cha weekend kwa kweli; jamaa yangu mmoja kaja juu dhidi ya mke wake kwa sababu mkewe ka-admit kwake kuwa ni kweli yuko attracted to a co-worker japo huyo co-coworker hajajua kabisa kinachoendelea. Mke kaadmit akiaini kuwa ni bora kusema mapema kabla mambo hayajaenda pabaya. Sasa kumwambia jamaa jamaa kaja juu na maswali lukuki akijihoji kuwa labda yeye ndiye sababu au kuna vitu hafanyi japo mwanamke anasema kabisa wala haihusiani na yeye (mume) ni kitu ambacho hata mwanamke hakielewi kwanini yuko attracted na huyo mtu mwingine - tumuite John.

Sasa, shemeji yetu hamwelezi mshikaji kwa sababu anasema kama angekuwa na nia mbaya asingemwambia (jamaa anasema labda amesema ili kuhalalisha). Lakini she swears hajafanya lolote lakini alikuwa anajihisi kama amecheat maana yuko comfortable sana na huyo John na ana enjoy sana company yake. Hajui kama anampenda au anamtamani

Mshikaji anaamini yuko sahihi kukasirika na sasa hivi amekuwa more than insecure kwani shemeji yetu kwa kweli wamo. Imeanza kuleta mgogoro usio wa lazima...

Kweli kuwa attracted bila kufanyia kazi ni kucheat na je kuna hekima kumwambia mwenzio majaribu unayoyapata huko kazini na usipomwambia yakafikia pabaya nani wa kulaumiwa?
 
jf is never boring....lol

hii ni classic case aiseee...
wadada wachache wanaoweza kukwambia hivyo...

mimi nimewahi kuwa na msichana akawa 'yuko in love' na mtu mwingine
na huyo mtu hajui na wala huyo msichana hakuniambia....nilikuwa natazama 'picha' kimya kimya..
baadae ikapotea,jamaa alisafiri...(msiseme nilimsafirisha lol)...
 
mhh labda tu uishie na ...ehhh jaman tom yan pale kazin mscheshi uyooo...ukikaa nae yan uborek ana stor uyo jaman yan nikimwona tu naanza kucheka..mhh asipokuja kazin yan naboreka...akuna wa kutuchekesha yaan..nisipomwona tu lazima nimpigie manake dah yan yule....

KIUTU UZIMA APO ...atakokotoa mwenyewe...km ni ni UCHESHI TU...AU NI UCHESHI BINI KUPENAD KWA MBALI....


sasa ole wako uisimamishe hoja ahh mi john nampenda jaman..ukikaa nae unakuwa na amani...secure....anajali uyo..JAMAA APO LAZIMA AKURUKIE NA KWENZI!!!!!!!!!!!!!
 
Sio vizuri kumueleza mwenzio sababu siku akijakukueleza wewe sidhani kama utapenda sasa naona ili muheshimiane zaidi bora usimwambie na wala usipoteza mda wako kumfikiria huyo mtu...
 
Mmh Omba MUNGU yasikukute, utajitathmini mara mia mia hutaelewa kitu, lakini na nyie akina dada (baadhi yenu, sio wote msijenifungulia mashtaka bure) mbona mna mambo hivyo? Baadhi yetu sisi akina baba hua ikitokea na wewe ukamfolia (fall in) huwa tunamaliza chini kwa chini then maisha yanaendelea, sasa wewe hadi utangaze kwa mwenzio, na kesho akitoka nje utasemaje? maana atajaribu kwenda ku-test kisu nje ya kambi iliaone tatizo liko wapi, na hapo ndio hatarudi tena.....
 
Haikuwa busara kwa huyo mdada kumwambia mmewe hivyo hata km hakuna kinachoendelea na huyo john,kuna mambo ya kumwambia ila si hivyo,nashawishika kusema huyo dada anaonyesha dalili za kumchoka huyo jamaa au mapenzi yameisha coz hata uhic kumpenda mtu mwingine thamani ya upendo huo hauwezi kufanana au kulingana na ule wa uliempenda na ukaolewa naye may be km aliolewa kwa bahati mbaya na hukuwa na uhakika na maamuzi yake,
Yani kabla ya kusema au kufanya jambo ni lzm angejiuliza je ingekuwa yeye ndie aambiwe hayo na mumewe angejisikiaje!
 
Nafikiri huu ni mfano mzuri wa ndoa zile za kukubali kuoa/kuolewa kwa sababu fulani na si mapenzi ya dhati kwa yule mwana ndoa. Kuoa/kuolewa kwa sababu ya umri kufika, fedha, shinikizo, nk mwisho wake ndiyo huu.

Kwa mimi nahisi kama huyo mdada aliolewa na huyo mkaka kwa sababu fulani na si kwa mapenzi ya dhati, so ni kuwa huyo mkaka hajamkosea chochote mkewe ila mke sasa amempata yule ampendaye .....

Am trying to figure out ....
 
Inauma sana mtu ulie nae kwenye mahusiano kumpenda mwingine....inaleta maswali mengi na majibu sifuri....
 
Amefanya vibaya sana maana jamaa atakuwa amefedheheka sanaa, hata kukata tamaa, maana mkeo akikutamkia maneno kama hayo inaumiza na kujiona hufai kwake na huna mvuto na pengine inaweza pelekea mpaka jamaa akashindwa kutimiza wajibu wake wa ndoa kama hapo awali maana ule ujasiri hupotea kila wazapo hayo maneno, na hili si jambo dogo maana linaweza pelekea hata ndoa kuvunjika.
 
Hapo lazma nijiulize maswali mengi.
1. Kwanini ameamua kunieleza?
2. Je ikitokea huyo kijana amtongoze ataweza kweli kumkatalia?.
N.k
Uaminifu utapungua sana juu yake.
 
Mmh Omba MUNGU yasikukute, utajitathmini mara mia mia hutaelewa kitu, lakini na nyie akina dada (baadhi yenu, sio wote msijenifungulia mashtaka bure) mbona mna mambo hivyo? Baadhi yetu sisi akina baba hua ikitokea na wewe ukamfolia (fall in) huwa tunamaliza chini kwa chini then maisha yanaendelea, sasa wewe hadi utangaze kwa mwenzio, na kesho akitoka nje utasemaje? maana atajaribu kwenda ku-test kisu nje ya kambi iliaone tatizo liko wapi, na hapo ndio hatarudi tena.....

Kama unanisoma kichwani vile...............mimi kama mume ndo jamboa la kwanza kulitekeleza
 
Mshikaji anaamini yuko sahihi kukasirika na sasa hivi amekuwa more than insecure kwani shemeji yetu kwa kweli wamo. Imeanza kuleta mgogoro usio wa lazima...

Kweli kuwa attracted bila kufanyia kazi ni kucheat na je kuna hekima kumwambia mwenzio majaribu unayoyapata huko kazini na usipomwambia yakafikia pabaya nani wa kulaumiwa?


Tokana na human nature jamaa asingekasirika ingekua kama vile boya fulani.... IMO ana kila sababu ya kukasirika.

Nimeshindwa muelewa mdada.. genuinely. Ingekua kacheat ningeelewa, lakini hapo kumuweka mpenzi wake katika wakati mgumu saana, jamaa kiwango cha trust juu ya mwanamke imeharibika moja kwa moja,Kiwango cha mapenzi hamu itashuka kama sio kuisha. Katika mahusiano "Trust" ni kitu muhimu saana, however wapenzi ni muhimu saana kujua kua once in a while lying in muhimu ili kumlinda mwenzio kama kweli wampenda... kwa kumlinda kwa kumdanganya, alimradi huo uongo isiwe ni siri ambayo ni muhimu kutolewa na ambayo madhara yake ya kufichwa ni makubwa kuliko kua exposed.
 
but sometimes ni phase tu...mbona wapo watu wanajua wake zao wako 'in love' na mtangazaji wa tv
au muigizaji wa filam au mwanamuziki......kama hakuna uwezekano wa kukutana..
unadharau tu....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom