Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Sharobaro mmoja alitembelea kijiji kimoja mkoani sumbawanga.Alipokuwa huko aliamua kuvinjari mitaa mbali mbali kijijini hapo.Cha ajabu kila mwanakijiji aliyekutana naye,alimwangalia kwa mshangao huku akisikitika na kisha kuendelea na safari yake.Sharobaro akaamua kumuuliza bibi mmoja;Hey grandma,inakuwaje mi nakatiza mitaa,nimepiga jeans,t-shirt,raba kali na madini yangu shingoni lakini watu wananiangalia halafu wanasikitika,au ndo wananionea wivu? (Bibi akajibu);Mjukuu wangu,hiki kijiji kila mtu ni mchawi,watu wote wanavaa hirizi kujizuia wasionekane uchi,wewe badala ya kuvaa hirizi umevaa cheni na ndo maana kila mtu anakuona uko uchi wa mnyama mpaka wanakusikitikia!