Share Container - Mtandao Mpya Kwa Waagizaji wa Vitu Kutoka Nje

GenX

Member
Mar 16, 2012
12
0
Kwa wale wote wanaoagiza bidhaa kutoka nje kwa kutumia njia ya meli, sasa unaweza ku-share container kwa kutumia mtandao mpya nilioufungua February.

Kama kawaida, njia nzuri ya kujikwamua katika matatizo tunayoyakabili kila siku ni kutafuta solution yake. Nikiwa mmoja wa wapenzi wa JF has business forum, kuna thread moja nilisoma iliyokuwa inahusu ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na jinsi ilivyokuwa ngumu kupata aina tofauti ya ng'ombe. Kuna mchangiaji mmoja alisema kwamba kuna mfugaji Australia anaweza kusafirisha ng'ombe hao lakini MINIMUM lazima iwe X. Nafikiri hiyo condition peke yake inaweza ikawa kikwazo kwa watu wengi wenye lengo la kufuga.

Katika kuchambua tatizo hilo, nikafikiria kuwa kuna watu wengi wanakwama kusafirisha bidhaa nyingine kutoka nje kwasababu ya gharama ya usafirishaji au uwezo wa kujaza container zima.

Hapo ndipo nilipoamua kuanzisha huu mtandao ambao unaweza kumsaidia mtu yeyote ku-share shipping container ili kupunguza gharama za usafirishaji. Pia unaweza kupanga mapema zaidi na kujua ni watu wangapi watakuwa tayari hata kabla muda wenyewe kufika.

Huduma ni ya bure na mtu wa nchi yeyote anaweza kuitumia. Website ni Share Shipping Container and Save! - Sharenship.

Kama una swali lolote usiogope kuuliza. Nitakupatia majibu muda unavyokwenda.
 
@ C.T.U

Kwa mfano unataka ku-ship bidhaa zako kutoka nchi X kuja Tanzania lakini hizo bidhaa zako haziwezi kujaza container la futi 20 au 40. Kama ukiamua ku-ship kwa reja reja utalipia hela nyingi zaidi kuliko ku-ship container zima mwenyewe.

Kwa kutumia huu mtandao, unaweza kukaribisha watu wengine ambao wana mpango wa ku-ship bidhaa zao kutoka nchi hiyo hiyo X, mkachukua container zima na ku-share space. Mtu ambaye yuko tayari ku-share anaweza kukutumia "Private Message" ili muweze kupanga zaidi nini cha kufanya.

Tembelea ujionee mwenyewe.
 
@LAT

Yes, but this way is more power to consumer.

@C.T.U

Fafanua swali lako zaidi ila dhumuni kubwa ni ku-break the old tradition.

No need to check with them.
 
@LAT

Yes, but this way is more power to consumer.

@C.T.U

Fafanua swali lako zaidi ila dhumuni kubwa ni ku-break the old tradition.

No need to check with them.

great ..... nimekusoma vizuri sana!
 
Unaposema vitu kutoka nje what do you mean??? Nje ya wapi? Kuna waishio bara ya Asia, Ulaya, Amerika na hata Afrika kwa wale waishio ndani ya Afrika lakini nje ya Tz......tueleweshe zaidi pls. kwani mtu anaishi Ulaya hawezi kushare container na mtu anayeishi Amerika au Asia etc.
 
Unaposema vitu kutoka nje what do you mean??? Nje ya wapi? Kuna waishio bara ya Asia, Ulaya, Amerika na hata Afrika kwa wale waishio ndani ya Afrika lakini nje ya Tz......tueleweshe zaidi pls. kwani mtu anaishi Ulaya hawezi kushare container na mtu anayeishi Amerika au Asia etc.
jaribu kutembelea site aliyoweka link..... na hasa hasa soma FAQ nadhani utapata mengi...
 
@Pakawa

Swali zuri.

Huu mtandao ni mahususi kwa bidhaa zinazosafirishwa kwa meli na dhumuni hasa ni ku-share container space ili kuepuka gharama kubwa za kusafirisha hizo bidhaa kwa reja reja.

Sio lazima waagizaji wote wawe sehemu moja. Mfano wewe upo Marekani unataka kusafirisha bidhaa zako kuja Tanzania. Kama umekaribisha mtu mwingine ku-share space na huyo mtu yuko nchi X lakini mizigo yake iko Marekani na inaenda Tanzania, ni kiasi cha yeye kuwasiliana na wewe ili aone anaweza vipi ku-share space uliyonayo.

Kutumia huu mtandao, atakutumia private message kwa mawasiliano zaidi. Natumaini umenielewa ila kama una maswali zaidi usisite kuuliza.

@macho_mdiliko

Point yako ni nzuri.

Kama ulivyosema, inabidi utembelee website ili uweze kuelewa zaidi.
 
Wazo zuri sana na nakutakia mafanikio mema, haya ndio tunayataka kwa vijana wetu, sio kukaa kulalamika na kutaka serikali ikufanyie kila siku, kitu kama hichi hiyo serikali itakufanyia?
 
@Ribosome

Nashukuru sana. Kama ulivyosema, matatizo mengi tunaweza kutatua sisi wenyewe wananchi. Kwa upande wa serikali, wanatakiwa kuweka "Mazingira" ambayo yanamuwezesha mwananchi kutimiza malengo yake ya kujiendeleza. Wajasiriamali wanakwama kutokana na mazingira ambayo hayatoi uhuru katika biashara.
 
Hongera Gen X ....ufanikiwe. Unanipa changamoto kwa sisi tuliolalia idea zetu!:A S crown-2: Ila nafikiri pia ingepatikana ya East Africa kwa cargo nayo ingeweza kufanikiwa. Ila sina uhakika kama wasafirishaji wetu wana access sana mtandao.
 
@tankibovu

Asante sana. Ili ujue idea is a "Go" or "No-Go" lazima uifanyie kazi (action). Usijali sana ku-fail kwani during that process utajifunza mambo mengi sana. Kwa hiyo changamoto yangu kwako ni "take action now."

Kuhusu suala la East Africa, ni idea nzuri sana na unaweza kutumia both mtandao na wakala ambao wana physical address.
 
Suala la usalama wa mzigo wa mteja limekaaje? au nyie kazi yenu ni kuniunganisha na mwenye container, nikaambia container linaenda dar baadae likaenda Nairobi mtu akapigwa changa la macho!
 
je? kila mtu mwenye mzigo atakuwa na Bill of Lading yake au mta-share BL ?
 
@Amoeba

Swali zuri. Kama umenisoma vizuri, huu mtandao ni kwa ajili ya kuwaunganisha watu wanaotaka ku-share container space ili watume bidhaa zao. Suala la kampuni gani itasafirisha, insurance, lini litasafirishwa, nani atalikomboa mara litakapofika hivyo vyote ni kazi ya mtumaji/watumaji.

Kwa maana hiyo, once wewe kama mtumaji ukishapata mtumaji mwingine waku-share naye space, kazi inabakia kwenu kukamilisha details nyingine zote. Wajibu wa huu mtandao utakuwa umekamilika na kutimiza lengo lake la kuunganisha watu na pia kukusaidia wewe kutuma bidhaa zako kwa bei nafuu kuliko kutuma reja reja.

I hope you get the whole idea behind. If you have more questions do not hesitate to ask.
 
Very good idea GenX.

Actually the network can be very useful for small business people who ship their good out of Tanzania and other African countries. Well thought and well executed.
 
@Tatu

You bring up a very good point. My title might be misleading but for those who wants to share shipping container from Tanzania or other third world country to western and Asian countries, they can use the site as well without any problem.
 
Back
Top Bottom