Shangazi kaja na mchumba kutoka kijijini...Mwenzenu nipo dillema!

Wasukuma wanapenda sana wanawake weupe sana! Km ujuavyo, mila ya kisukuma humfanya mtu subjective kwa wakubwa wake hapa ndipo utata ujapo!


Gaguroto sio kweli, mie ni msukuma lkn nilipotaka kuoa na wazazi wangu sorry ni Baba tu aliniuliza swali moja tu....Unampenda? Nikamwambia eeehhh....Basi endelea unavyotaka bwana....Na baba angu sio msomi eti....Hulka tu ya mtu ndo inasumbua......
 
Mkuu moja kwa moja hapa kuna kitu unaficha, hivi kwenye red ulipoandika unamaanisha nini? Jamaa yako na ndugu zake ni wakabila, sema na wewe hapa unajaribu kuficha watu wasikushambulie tu...Hapo hakuna cha kufikiria wala nini moja kwa moja kama jamaa ako kweli ni mtu mzima I mean Over 18 swala la kuoa liko juu yake na sio juu ya wazazi wako maana huyo ni mke sio rafiki wala room mate au mfanyakazi mwenzio kuwa unachaguliwa...Mwambie aoe mapema, anaweza Oa hata yuko chuo...siku ya siku wazazi hawatakuwepo kukiwa nyumbani hakuivi ni yeye na mke wake.....
Ofcoz kuna element fulan za ukabila hapo! Jamaa ni msukuma, bint ni mchaga. Kifupi sioni logic ya hao ndugu zake kumletea binti toka kijijini (msukuma mwenzie), nadhani hawataki mchaga aolewe ktk ukoo wao! Hapa ndipo ugumu wa mambo ujapo!
 
Gaguroto sio kweli, mie ni msukuma lkn nilipotaka kuoa na wazazi wangu sorry ni Baba tu aliniuliza swali moja tu....Unampenda? Nikamwambia eeehhh....Basi endelea unavyotaka bwana....Na baba angu sio msomi eti....Hulka tu ya mtu ndo inasumbua......
So unataka kataa/unapinga kuwa wasukuma wanaelement za ukabila?
 
Aoe huyu aliyeletewa, mapenzi na kuzoeana kutaanza hukohuko kwenye ndoa.

Ilikuwa hivyo, tulipoanza kuhama makwetu na kwenda sehemu nyingine kutafuta maisha ndipo tukaanza na sisi 'kutafuta' wa kuoa. Achukue mke tu, simpo!

Mke ni yule ambaye muoaji amemchagua yeye mwenyewe. Mila na desturi za kuchaguliwa wachumba karne hii zimepitwa na wakati. Ndoa za aina hiyo huwa ni vigumu sana kudumu kwa muda mrefu kwani wahusika wanakuwa wameoana kwa kushinikizwa tu. Kwa ushauri wangu jamaa amsepe huyo mchumba aliyeletewa and let him go ahead with the one he has selected willingly.
 
Mke ni yule ambaye muoaji amemchagua yeye mwenyewe. Mila na desturi za kuchaguliwa wachumba karne hii zimepitwa na wakati. Ndoa za aina hiyo huwa ni vigumu sana kudumu kwa muda mrefu kwani wahusika wanakuwa wameoana kwa kushinikizwa tu. Kwa ushauri wangu jamaa amsepe huyo mchumba aliyeletewa and let him go ahead with the one he has selected willingly.
Unataka kusema mila zimepitwa na wakati? So kuletewa mke toka sikimbi ni kupitwa na wakati? Nimekusoma mkubwa, nitamshauri vizuri, nasaha zako nimezipenda!
 
Hao ndugu wa jamaa inaonyesha ni maprimitive sana, mhh! Bado kuna mtindo wa kuchaguliana wake/waume? Akomae na mchaga wake

1. Kwanza anajua kuzisaka

2. Wanajua kuzibana

nb, kama na Mmachame mi simshauri chochote, aamue mwenyewe. Aonyeshe uanaume wake
 
Hao ndugu wa jamaa inaonyesha ni maprimitive sana, mhh! Bado kuna mtindo wa kuchaguliana wake/waume? Akomae na mchaga wake1. Kwanza anajua kuzisaka2. Wanajua kuzibananb, kama na Mmachame mi simshauri chochote, aamue mwenyewe. Aonyeshe uanaume wake
Hahahahahahahaaaa! Sio mpalestina yule teh! Ni mchaga wa Rombo... Mekuuuu! teh! teh!
 
Huyu jamaa inaonekana ni mpori pori sitoshanga abado anashindwa kufanya maamuzi ,inaonekana ni kakulia kijijini maisha yake yote shule tuu ndio imempeleka kuona gari la kanza maishani, Iweje dunia ya sasa uchaguliwe mchumba wa kijijini , shule hana , halafu umfanye mkeo?.

Kuna kisa kama hiki, toka kwa jamii ya wa Kurya, jamaa mmoja kakaa nyumbani ,ana shangaa sijui shangazi au nani kaingia Kitunda na demu toka kijijini tena kakeketwa na kuambiwa ndio kachaguliwa mke, lakini hakukua na ajabu yeyote sababu huyu jamaa naye ni alitokea huko huko kijijini .
 
Huyu jamaa inaonekana ni mpori pori sitoshanga abado anashindwa kufanya maamuzi ,inaonekana ni kakulia kijijini maisha yake yote shule tuu ndio imempeleka kuona gari la kanza maishani, Iweje dunia ya sasa uchaguliwe mchumba wa kijijini , shule hana , halafu umfanye mkeo?. Kuna kisa kama hiki, toka kwa jamii ya wa Kurya, jamaa mmoja kakaa nyumbani ,ana shangaa sijui shangazi au nani kaingia Kitunda na demu toka kijijini tena kakeketwa na kuambiwa ndio kachaguliwa mke, lakini hakukua na ajabu yeyote sababu huyu jamaa naye ni alitokea huko huko kijijini .
Teh! KITUNDA NDIO MASKANI YA WAKURYA DAR ES SALAAM! Kwa mila za kikurya si ajabu!
 
Huyo mchumba wake nampa pole maana hata jamaa akimuoa ajue fika kuwa wakwe hawamtaki! Ndoa ataianza vibaya. Ni kweli ndoa ni makubaliano ya watu wawili lakini kwa waafrika usiombe ndugu wa mumeo wakuchukie kuna ambao wanafikia kuroga ili uachike. Nina mfano hai though siwezi ku prove mambo ya kishirikina ila mdada vimbwanga aliviona mpaka mwenyewe kabwaga manyanga.

Kwa ufupi ushauri ni mgumu yeye mwenyewe ndio anawajua wazazi wake and what they are capable of. Wangekuwa ni wazazi waelewa wasinge decide yote hayo bila kumshirikisha. Kwa ufupi ajiandae kutengana na familia endapo ataamua kuoa huyo mchumba mchaga.
 
Huyo mchumba wake nampa pole maana hata jamaa akimuoa ajue fika kuwa wakwe hawamtaki! Ndoa ataianza vibaya. Ni kweli ndoa ni makubaliano ya watu wawili lakini kwa waafrika usiombe ndugu wa mumeo wakuchukie kuna ambao wanafikia kuroga ili uachike. Nina mfano hai though siwezi ku prove mambo ya kishirikina ila mdada vimbwanga aliviona mpaka mwenyewe kabwaga manyanga.Kwa ufupi ushauri ni mgumu yeye mwenyewe ndio anawajua wazazi wake and what they are capable of. Wangekuwa ni wazazi waelewa wasinge decide yote hayo bila kumshirikisha. Kwa ufupi ajiandae kutengana na familia endapo ataamua kuoa huyo mchumba mchaga.
Mimi naungana na wale wote wanaolaani kitendo cha mila kutawala ktk mambo yahusuyo maisha ya watu hususani mahusiano. Mshikaji wangu inabid afanye maamuzi yatakayokuwa ni sahihi kwake!
 
Wanandugu kwa kuingilia mambo ya mapenzi duh! Usiombe ikutokee!
 
Back
Top Bottom