Shamsha uongo huu haufai kabisa, si lazima wazungu waseme!

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Date::10/2/2009Kamati kumhoji waziri kuhusu operesheni Loliondo
broken-heart.jpg

Exuper Kachenje

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, atalazimika kutoa ufafanuzi mbele ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, kuhusu operesheni ya kuhamisha wananchi huko Loliondo, wilayani Ngorongoro.

Hatua hiyo inafuatia taarifa zinazohusu mkanganyiko kuhusu operesheni hiyo ya kuwahamisha wananchi kutoka katika pori tengefu ambalo linadaiwa kuwa sasa amepewa mwekezaji wa kigeni.

Pia kuna madai kuwa mwekezaji huyo amekuwa akiendesha vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wananchi wa eneo hilo, vikiwemo vinavyokiuka haki za binadamu, bila kuchukuliwa hatua.

Ratiba ya vikao vya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyotolewa na ofisi ya Bunge Ijuma lililopita, inaonyesha waziri amepangiwa kutoa ufafanuzi wa opersheni hiyo.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Mwangunga amepangiwa kufanya hivyo Oktoba 10 mwaka huu wakati kamati hiyo itakapokutana katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam.

"Ijumaa 09/10/09, Waziri kutoa ufafanuzi kuhusu operesheni inayoendelea Loliondo," inaonyesha ratiba hiyo ambayo Mwananchi ina nakala yake.

Hivi karibuni waziri Mwangunga alikaririwa akisema kuwa waliohamishwa katika pori hilo si Watanzania na kwamba jamii ya Wamasai kutoka Kenya.

Kwa mujibu wa waziri huyo, watu hao walifuata malisho, kufuatia ukame uliikumba nchi yao na kusababisha mifugo kukosa malisho.

Waziri wa Maliasili na Utalii, pia alisemahakuna ukiukwaji wa haki za ubinadamu uliofanyika katika operesheni hiyo.

Alisema wizara yake kwa kushirikiana na Tume ya Upangaji wa Matumizi ya Ardhi, imeazimia kutenga maeneo ya pori tengefu, ardhi ya vijiji kwa njia shirikishi.


Katika eneo hilo kuna zaidi ya taasisi 30 zinazofanya kazi huku baadhi zikitajwa kuhusika na mvutano uliopo.

Mwangunga amezielezea tatsisi hizo kuwa zinashindana kibiashara. Alisema wafugaji wana haki ya kuendelea kuishi katika maeneo mengine ya pori la Loliondo, ambayo si tishio kwa usalama wao.
Tuma maoni kwa Mhariri
Facebook
 
Hivi huyu waziri anafahaamu ayasemayo? Yaani anadiriki kuwakana watanzania ambao ni sehemu ya waliomeka Jk madarakani kwa kukumbatia Mwarabu?

Anaposema hakuna hukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika katika operesheni hiyo, sijui pia ana maanagani.

Watu kupigwa, kuchomewa nyumba na maboma, wanawake kubakwa na mengine mengi yanayofanyika, yeye hayo kwake si ukiukwaji wa haiki za binadamu? Mbaya zaidi anawakana watanzania wenzake kuwa si watanzania bali ni wafugaji wa nchi jirani ya Kenya.

Huu ni unyanywasaji wa kikabila.
 
Hv nyie mmesahau kwamba hii ni serikali ya uwajibikasji wa pamoja?
Mwangunga atasema lipi ambalo linawakwaza weupe?
Au kuna mliyemwona huko sirikalini anafanya hivyo!
 
Mimi naona pamoja na mateso wanayopata hawa ndugu zetu wa maasi, wasikubali kabisa kuirudisha/kukipigia kura chama cha mapinduzi kwani hakiwadhamini kabisaaaaaaaaaaaaa!!!! Wachague chama kingine.
 
Hivi ni nini kauli ya JK katika jambo hili?, au ndo hivyo tena----- ni wamasia wa kenya.
 
Bunge la wa dutch limechukulia tukio hilo so serious na hata baadhi ya Nchi za EU . Wamehoji serikali juu ya makubaliano ya msaada kwa ajili ya utawala bora na sasa wanaona pesa yap inanunua bunduki wamasai wanalazwa nje . Soon huko Uholanzi mdutch mmoja anasema Mbunge wa eneo lake alikuwa anaongelea hali ya Tanzania na unyanyasaji kwa jila la Mwarabu , bunge litalipuka msishangae misaada ikakatwa zaidi . Tayari wamesha zuia baadhi ya pesa baada ya Serikali yetu kukosa majibu kwa maswali yao . Leo Shamsa anaongelea haya ? Ndiyo maana utalii TZ hauta endelea kwa watu kama huyu waziri .
 
mimi naona pamoja na mateso wanayopata hawa ndugu zetu wa maasi, wasikubali kabisa kuirudisha/kukipigia kura chama cha mapinduzi kwani hakiwadhamini kabisaaaaaaaaaaaaa!!!! Wachague chama kingine.


hivi mkuu mbona umechangia vizuri alafu unaonekana kusahau, kwani sisiemu hata usipoipigia kura unadhani ndo itashindwa kuwa madarakani, tafuta jinsi ya kuwa "advise" hawa jamaa kama watafute ngao na mikuki, kwani simba wanawaua vipi si kwa kunyatia na kwa kutumia mishale na upinde, basi hata huyo mwarabu siku akiingia wa "assume" kuwa ni simba na wa mwendee na mikuki na mishale.
 
Hivi ni nini kauli ya JK katika jambo hili?, au ndo hivyo tena----- ni wamasia wa kenya.

Mkuu huyu njemba anasema kitu? siku zote yuko kimya tu kwenye issue ya Rada, issue ya Richmond alipofunua mdomo wake kwa mara ya kwanza ni pale alipotaka mjadala huo umalizwe. Ni kiongozi ambaye anashangaza sana na ndiyo maana hastahili kabisa kugombea 2010 maana ataipeleka nchi pabaya zaidi kuliko hapa tulipo sasa.
 
Mods,
Hebu zichanganyeni hizi POST ukianzia na ile aliweka Invisible na video kutoka YOUTUBE. Nafikiri zitaleta mtiririko mzuri ili kila asomaye afahamu kwa kina zaidi ni UNYAMA gani umefanyika LOLIONDO. Ningelikuwa namfahamu mbunge wa bunge la Ulaya, ningelimpigia magoti ili akaliseme hili ndani ya EU.

Kuna haja ya huyu Mwaarabu na hao watumwa wake wawajibishwe. Hatuwezi kuwa watumwa wao milele na milele.... I wish ningelikuwa .....
 
Back
Top Bottom