nani tena huyo alionyshwa kwente tv, maana hapa tumeshatajiwa wagombea wengi
Kumbe!!!! nimeanza kupata mwanga juzi juzi Mwangunga alikuwa mgeni rasmi kwenye Kanisa letu Mavurunza, Ubungo kumbe ameamua kuanzia huko!!! nikashangaa hivi huyu Muislam, samahani siyo udini, wamemuwaza wapi mpaka aje huku kumbeee !!!!! lisemwalo lipo na alichangamsha mnada kweli CCM siwawezi.
Omutwale,waitu Shumalamu! La Nnape kugombea Ubungo hilo ni wazi siku nyingi linajulikana,Shamsa naona jimbo la Kongwa kaliona maji marefu maana Ndugai balaa na siasa bila shaka kanogewa nazo hivyo anahitaji jimbo,Mnyika ni wazi kwa umri wake atakuwa na ambitions kibao na ninasikia bongo yake inachemka(nasikia o-level alipata A kumi) na kwenye siasa ukiwa na bongo kali ni advantage because you think fast,diwani wa ubungo aitwaye Mringo naye anataka kujitosa kilingeni and indeed watch this guy kwa sababu amekuwa kwenye siasa za wilaya ya kinondoni muda mrefu na anamjua kila mtu,literally.Tusubiri si ajabu na wengine wakaja maana kabla Asha Migiro hajaenda UN ilisemekana naye alikuwa anajiandaa kupandisha bendera Ubungo,kunani Ubungo??????
Kwa hali ilivyo sasa ubungo, hakuna atakayemchagua mbunge toka CCM,Mnyika
Sidhani kama ni sahihi kusema kuwa Shamsa anavaana na Mnyika kwasababu hajateuliwa bado na CCM kuwa ndo mgombea wao! Na bado wapo wengi wanaotajwa kuwania nafasi hiyo tena nadhani katika ranking Shamsa yuko mbali mno kupata nafasi hiyo!
Nadhani anataka kutengeneza njia tu akumbukwe uteuzi wa bwana mkubwa.
Nadhani pia kaanza vibaya sana kwa hoja mbili DINI ..kaanza kwa kujivisha utetezi wa waisilami......JINSIA.....analia apewe nafasi kuwakilisha jinsia wakati wamepewa nafaisi kibao za wanawake.
Majina mengine yanayotajwa ambayo nadhani yanaushindani mkubwa ni pamoja na,
1. Hawa Ng'umbi
2. Nape Nnauye
3.Mringo....diwani wa kimara
4. Na kwa mbali Benno Malisa!
Kwani Mzee Keenja amefulia tayari? Hatagombea?
Ndiyo, Umepatia
Kama unakumbuka vizuri hata 2005 ni miongoni mwa Wabunge ambao JK alikuwa amegoma kuwavusha kitanzi shingoni. Na hata alipokubali kuwanadi walizomewa jukwaani mbele ya JK.
Hahahaha, wakati mwingine nadhani utani unazidi busara. Keenja alishinda Ubungo kwa asilimia 54 ya kura zote zilizopigwa. Wagombea waliokuwepo walikuwa 13 (hapo ndipo walipojikaanga - siri yako). Ina maana hata kama wagombea wote wa upinzani wangeunganisha kura zao, bado wangekuwa wameshindwa.Keenja ni miongoni mwa wabunge wengi wa CCM walioshindwa vibaya 2005 katika majimbo ya Dar, Msimamizi wa uchaguzi "mkurenzi wa municipal ya Kinondoni" Edgar Berege sijui kama bado anashikilia nafasi hii, ilibidi atumie mbinu zao za kupika matokeo ya kura, kumtangaza mshindi.
Sahihi kabisa. Tume huru ya uchaguzi inahitajika ili kuwa na haki zaidi katika uchaguzi. Tume iliyopo imeundwa ikiwa na upendeleo wa wazi kwa mwajiri wake ambae nae pia ni mgombea.Sisi hapa tupige kelele tu, lakini bila kuwa na Tume huru ya uchaguzi CCM itaendelea kupanga matokeo ya kura kwa kadiri wanavyoona inafaa. Hutu tuviti wanatowaachia wapinzani ni janja ya kuwaonesha wahisani kuwa Tanzania kuna demokrasia.
Kilichomwangusha zaidi John Mnyika ni kutegemea mawakala kutoka UDSM. Kwa bahati mbaya kura zilipingwa baadhi ya Faculty wakiwa kwenye mitihani na hivyo Mawakala toka UDSM wengi hawakwenda vituoni na hivyo kutoa mwanya wa wazi kwa CCM na Keenja kuchezea matokeo watakavyo. Hii haimaanishi kuwa napunguza ukweli katika hoja yako ya Tume Huru bali naonyesha mwanya wa ziada.
- Keenja ameamua kutogombea tena baada ya kufulia na kukamulia jimbo, kwa hiyo hapo Ubungo kwa dataz nilizonazo tutegemee wana-JF wawili kujitosa, Mnyika anataka kuendelea na shule lakini kuna wanaomshinikiza kujitosa, atakumbana na another JF,
- Mwagunga, angetafuta pengine, hapa ni moto wa kuotea mbali, maana nimekuwa nikishiriki mwenyewe kwenye kampeni za one on one na prominent wa jimbo hili, katika kujaribu kumsaidia a JF member unajua hili jimbo ni exceptional maana lina wasomi wengi sana, huenda hata kuliko majimbo yote nchini.
Hata mimi nilimuona channel 10 akisema haya mambo. Nilishangaa kwamba kama kampeni zikiamia nyumba za ibada uchaguzi utakuwa mgumu sana sana.yaani ukeli ni kwamba hata wakisema uchaguzi ni kesho japokuwa huyu mama ni waziri aliyepo madarakani hivi sasa,means bado ana nguvu kubwa ya serikali, lakini hawezi kufurukuta kwa mwanyika,na hilo liko wazi.Juzi nilimuona ktk runinga akipiga magoti kwa waislam, namnukuu, ''waislam wenzangu mungu akipenda ninategemea kugombea ubunge ktk jimbo la ubungo, sasa nikiwa kama muislamu mwenzenu naombeni msaada wenu'' mwisho wa kunukuu. mimi nikamshangaa sana huyu mama nilifikiri ni mtu makini kumbe bogas,kama nyerere angekuwa hai asingejaribu kuomba msaada kwa kutumia udini huyu mama,its true hata mimi ni muislam lakini stail aliyotumia huyu mama ni ya hovyo kabisa
Kuna wengine wanaotajwa kuwania kiti hicho vile vile. Wapo akina Prof. Wangwe, .......
Kwa muji bu wa Omutwale (gonga hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...zi-mkuu-ufanyike-mwezi-wa-kumi-mwaka-huu.html )
Prof. Wangwe atapambana na Dr. Zainabu Gama kwenye jimbo la KIBAHA