Shamba la Miti ukanda wa Pwani

Wandugu (Malila, LAT, etc), hiyo project ya Mianzi inaendeleaje? Je, inachukua muda gani kupanda hadi kuvuna? Na soko lake je? Nimevutiwa sana na huo mradi.

Mimi nilifanikiwa kuotesha michache, baada ya mafanikio nikaamua nipande mingi sana hasa kwa ajili ya ujenzi wa mabanda ya mifugo. Mbegu zilimea vizuri sana, dogo kapeleka mbuzi bila kujua, mianzi yote ililiwa na kuharibiwa vibaya, nakuja kushituka hakuna kitu, lakini nimeanza upya. Nataka mianzi shambani kwangu kwa ajili ya ujenzi.
 
Pole sana kwa hasara uliyopata. Ila pamoja na changamoto zote haujakata tamaa. Hakika wewe ni mpambanaji. Natamani siku moja nikuone "live" najua nitajifunza mengi sana kutoka kwako. Ubarikiwe.
 
Wandugu (Malila, LAT, etc), hiyo project ya Mianzi inaendeleaje? Je, inachukua muda gani kupanda hadi kuvuna? Na soko lake je? Nimevutiwa sana na huo mradi.

Nenda SIDO Dsm pale Nyerere Road, kawaulize aina ya mianzi yenye soko, mimi waliniambia aina hiyo yenye soko sana inapatikana Mby na Bulongwa Makete, na kuna baadhi ya fito za kusukia vikapu zinapatikana Kigoma.

Pamoja na kuwepo hiyo aina bora kabisa ya mianzi/fito hawa jamaa hawana mpango wa kuanzisha mashamba ya mianzi. Bado sijaweza kuwa na data kamili kuhusu muda wa uvunaji. Zamani kule Iringa ilikuwepo project ya Mianzi miti sijui ilifia wapi. Ngoja Wachina watuamshe.
 
Mimi nilifanikiwa kuotesha michache, baada ya mafanikio nikaamua nipande mingi sana hasa kwa ajili ya ujenzi wa mabanda ya mifugo. Mbegu zilimea vizuri sana, dogo kapeleka mbuzi bila kujua, mianzi yote ililiwa na kuharibiwa vibaya, nakuja kushituka hakuna kitu, lakini nimeanza upya. Nataka mianzi shambani kwangu kwa ajili ya ujenzi.

kiongozi nahitaji mianzi iliyokomaa unayo?
 
kiongozi nahitaji mianzi iliyokomaa unayo?

Mimi sina, ndio kwanza naotesha Mkuranga, sasa kama unataka mianzi iliyokomaa, nitakuunganisha na dogo mmoja pale Dundani na Mfuru Mwambao, ipo mianzi ya njano mikubwa na mirefu, pia imekomaa vizuri. Ndiko ninakochukua mbegu za kuotesha kwangu.
 
nimepata ardhi kubwa,ninahitaji kujua shamba la Miti ukanda wa pwani linawezekana?if yes miti gani inahimili mazingira ya ukanda wa pwani [rufiji,kilwa].
nawaza miti ya under 10 years.
mambo vipi, nimenunua shamba kama ekali 10 maeneo ya Kibiti wazo langu lilikuwa ni kupanda zao la miti kama wewe ulishaanza naomba uni PM tuwasiliane nije kupata elimu kutoka kwako.
 
Sasa ardhi ambayo mvua sio nyingi sana ( Bwawani) Morogoro no miti aina gani naweza kupanda?
 
hivi sasa bamboo haiitaji maji au hata sehemu kavu kama kiwangwa na Fukayosi huko bagamoyo inaweza kukubali?

nakubaliana na mtoa hoja aliyetangulia kuwa mitiki hainenepi sana ukanda wa pwani (e.g. bagamoyo bagamoyo).. mimi nimejaribu kupanda kama ekari 5 za Gmelina arborea,(white teak) huko Fukayosi. naona inakubali, ila sijajua sana kama inanenepa sana au la. ukitaka habari yake unaweza kwenda Gmelina arborea - Wikipedia, the free encyclopedia ila naona LAT anafahamu suala la species za miti unaweza kutusaidia taarifa zaidi
Mkuu white teak ilikubali??
 
mambo vipi, nimenunua shamba kama ekali 10 maeneo ya Kibiti wazo langu lilikuwa ni kupanda zao la miti kama wewe ulishaanza naomba uni PM tuwasiliane nije kupata elimu kutoka kwako.
Panda miti ya matunda
 
Back
Top Bottom