Shajala: Kipindi cha TBC1 kinachofunua watu wenye matatizo katika Jamii.

Masaki

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,463
752
Wadau,

Jana nilikuwa naagalia TBC1 na niliguswa sana na kipindi cha Shajala. Kipindi hiki kinaendeshwa na dada mmoja ambaye anaonekana ni mwanaharakati mahiri mweye nia njema ya kusaidi Watanzania waooshi katika mazingira magumu.

Kinawalenga zaidi watoto yatima, na wale wanaoishi katika mazingira magumu, waathirika wa virusi vya UKIMWI na kadhalika.

Kipindi cha jana kiliwahusu watoto wawili wa kike wanaoishi katika mazingira magumu sana huko Arusha baada ya kufiwa na wazazi wao wote wawili. Kilichonivutia zaidi ni uwezo mkubwa wa kujieleza wa mtoto mkubwa (kati ya hao wawili) kitu kinachoashiria uwezo mkubwa wa kiakili ambao atakuwa nao darasani.

Watoto hawa wanahitaji msaada wa hali na mali ili waweze kupata elimu katika mazingira bora zaidi.

Ningeshauri waendeshaji wa kipindi kile wawe na website, au wakishindwa basi wawe na hata blog ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi walioko duniani kote. Ninaamini watu wenye moyo wa kuchangia watoto wenye shida kama zile wapo wengi ila hawana taarifa au jinsi ya kufikisha michango yao.

Baada ya kipindi kuna nambari za simu zilionyweshwa kwa anayeta kuchangia, nilifanikiwa kunakiri namba mojawapo +255 754 005 657.
 
Back
Top Bottom