Shairi la wacheza bao la kete

Jan 4, 2012
61
23
Waungwana nauliza kama kuna mtu nakumbuka beti zote za shairi la WACHEZA BAO LA KETE WAONGO NA WAZANDIKI lililotungwa na Saidi Nyoka( Udogo si Hoja)? Natafuta Malumbano yao na Andanenga kuhusu kisa hicho tafadhali.
 
Ukilipata unipe nakala tafadhali. Nakumbuka kulisikia likiimbwa RTD linachekesha kweli kweli!
 
Nazikumbuka beti chache zifuatazo:

SAIDI NYOKA:

Watu wajidanganyao, mbali msiwatafute,
Ni hawa wacheza bao, mikononi wana kete,
Kutwa mlo wao hao, ni kumeza meza mate,
Wacheza bao la kete, waongo na wazandiki.

Waongo na wazandiki, wacheza bao la kete,
kitako hawabanduki, utadhani ni viwete,
Hawalijui riziki, japo nusu ya mkate,
Wacheza bao la kete, waongo na wazandiki.

Nina mtaji husema, kumbe lofa kiokote,
Kwenye bao kainama, hatoki lisimpite,
Huku njaa yamuuma, awaza wapi nipate,
Wacheza bao la kete, waongo na wazandiki.

zingine sikumbuki.........

ANDANENGA:

Saidi usituvunge, kwamba dhambi kubadili,
Michezo tusiipange, kwa majina mbalimbali,
Wewe Nyoka au Kenge, kwako jina la asili?

Zingine sikumbuki.............
 
Hivi vitu vitakuwepo makumbusho ya taifa. Kama havipo basi mkurungezi wa makumbusho ya taifa afutwe kazi mara moja.
 
Hiki kisa kilivuta watu wengi, hata mimi nilikisikia ila beti zake sina, tunashukuru kwa hizo beti chache ulizojaaliwa kukumbuka, ukijaaliwa kupata / kukumbuka beti nyingine twaomba uzilete jamvini
 
Nazikumbuka beti chache zifuatazo:

SAIDI NYOKA:

Watu wajidanganyao, mbali msiwatafute,
Ni hawa wacheza bao, mikononi wana kete,
Kutwa mlo wao hao, ni kumeza meza mate,
Wacheza bao la kete, waongo na wazandiki.

Waongo na wazandiki, wacheza bao la kete,
kitako hawabanduki, utadhani ni viwete,
Hawalijui riziki, japo nusu ya mkate,
Wacheza bao la kete, waongo na wazandiki.

Nina mtaji husema, kumbe lofa kiokote,
Kwenye bao kainama, hatoki lisimpite,
Huku njaa yamuuma, awaza wapi nipate,
Wacheza bao la kete, waongo na wazandiki.

zingine sikumbuki.........

ANDANENGA:

Saidi usituvunge, kwamba dhambi kubadili,
Michezo tusiipange, kwa majina mbalimbali,
Wewe Nyoka au Kenge, kwako jina la asili?

Zingine sikumbuki.............

Asante sana kwa Kumbukumbu hii maridhawa.
 
Back
Top Bottom