Shahidi: Mahanga alitangazwa mshindi bila kutatua matatizo

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

[h=2]
[/h]Imeandikwa na Kulwa Mzee, Dar es Salaam: Thursday, April 05, 2012 09:37
MSIMAMIZI Msaidizi wa Jimbo la Segerea, Samweli Bubegwa ameieleza mahakama kwamba majumuisho ya kura za ubunge katika jimbo hilo yalifanyika na Dk. Makongoro Mahanga, alitangazwa mshindi bila kutatua kura za migogoro zilizotoka katika vituo vya kupigia kura.

Alidai hayo jana Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mbele ya Jaji profesa Ibrahimu Juma, alipokuwa akihojiwa na Wakili wa mlalamikaji, Peter Kibatala.

Alidai walihakiki fomu za matokeo ya ubunge kwa vituo 749 na kufanya majumuisho pamoja na mgombea wa CCM, Dk. Mahanga bila kuwapo wagombea wa vyama vingine na walipomaliza walimtangaza mshindi.

“Katika majumuisho tulikuwa na Mahanga, wakala wake na wakala wa CUF, wengine wagombea na mawakala wao hawakuwapo katika majumuisho,”alidai.

Alidai hawakuweza kutatua kura zenye mgogoro katika jimbo hilo, kwa sababu hazikuwafikia kutoka vituoni japo katika fomu za matokeo zilizopo mahakamani kama kielelezo zinaonyesha kura zenye migogoro zilikuwepo vituoni.

“Hakukuwa na kura za migogoro Jimbo la Segerea, hazikutufikia sijui zilienda wapi, wasimamizi wa kata walipaswa kutufikishia ili tuzitolee uamuzi,”alidai.

Alidai hata vurugu zilizodaiwa kutokea Tabata, hawakupata taarifa kwa sababu waliopaswa kuwafikishia hawakuitoa ripoti.

Shahidi mwingine wa 13, ambaye pia ni Msimamizi Msaidizi ngazi ya Jimbo, Erick Foya alidai mahakamani kwamba hakumbuki fomu namba ngapi, ilikuwa ikihusu kura za wagombea gani kwa sababu ni muda mrefu umepita.

Aliungana na shahidi mwenzake kwamba katika majumuisho, alikuwepo Dk. Mahanga, wakala wake na wakala wa CUF, lakini wagombea wengine hawakuwapo.

“Nilikuwapo kuanzia saa mbili wakati majumuisho yanaanza hadi saa nane alipotangazwa mshindi, lakini sikumuona mgombea yoyote Arnatoglo,”alidai.

Alidai pamoja na wakala wa CUF kuingia katika majumuisho, lakini alikataa kusaini matokeo yalimtangaza Dk. Mahanga kuwa mshindi katika jimbo hilo.

“Wakati wa kusoma matokeo tulipokezana , kila mmoja alipochoka mwingine alikuwa akipokea, tulikuwa watano katika kufanya majumuisho,”alidai,

Alipotakiwa na Kibatala kutaja idadi ya wagombea udiwani katika Kata ya Segera walikuwa wangapi, alisema hakumbuki alisoma matokeo ya kata gani, hakumbuki kama fomu namba 24 B, ilikuwa ya matokeo ya udiwani na hajasikia matatizo yoyote yalitokea Vingunguti na Kiwalani.

Aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Segera, Fred Mpendazoe alifungua kesi akipinga ushindi wa Dk. Mahanga, akidai ni batili hivyo ubatilishwe na uchaguzi urudiwe. Kesi inaendelea leo.
 
Hawa majaji wa Tanzania utashangaa kuwa wakati nyinyi mnapeleka mashahidi, yeye anakuwa bize kuandika hukumu kwa vile ameshajua hukumu itakuwaje. Mkimaliza kutoa ushahidi tu na kama wewe ni mlalamikaji wa upinzani basi anatupilia mbali kesi yako kwa "kukosa ushahidi" ambao haukusikiliza, na kama mlalamikaji ni wa CCM basi malamaiko yake yanakubaliwa hata kwa kutumia ushahidi ambao haukutolewa mahakamani na sheria ambayo ilikuwa haina uhusiano na malalamiko hayo.
 
Back
Top Bottom