Sex addiction

mwanamasala

JF-Expert Member
Jun 20, 2009
248
12
Tumeona Tiger Woods na vimada wake.Jee hii ni Sex Addiction?Ni ugonjwa?Maana najaribu kufikiria mtu wa hadhi yake kwa nini afanye mambo haya?Hakujua kuwa kwamba atagundulika?Angekuwa bachelor isingekuwa tatizo,lakini ana mke na watoto 2!!!!!!!!!!!!!!!!hakuogopa ukimwi na magonjwa ya zinaa?

Mpaka sasa sijapata jibu!Au pesa nyingi ni mkosi?Anafuatia kama African americans wengine waliofall from grace!Michael Jordan,Mike Tyson,Mr Vick(anayechezea mbwa) na Michael Jackson?
 
asilimia kubwa ya wanaume wenye uwezo na maarufu au wenye uwezo wanawanawake nje ya ndoa na hii inatokana na vishawishi na majaribu wanayo kumbana nayo kutoka kwa wakina mama, hawa si wakulaumiwa maana ni vigumu kukwepa unaweza ila kwa asilimia ndogo sana, siyo wenye pesa tu hata mashehe mapadri wachungaji kwakweli wanazungukwa mno na majaribu, hivi unajua kuna wanawake wanawakonyeza wachungaji wakiwa wanahubiri?
 
Kwa baadhi yetu wengine, tukiwa na pesa mfukoni, basi tunakuwa unstoppable!

Kuna feeling ya kwamba .."naweza kufanya chochote nitakacho" .
Lkn pia, factor ya kutamaniwa na wanawake/wasichana inakuwa kubwa na ya juu sana, maana wanajua watapata msaada wa kulipiwa bili za DSTV!

Ishu hapa ni commitment ya mtu husika, kama anaweza kuresist majaribu haya!
Kama huwezi kuya'turn down basi matokeo yanakuwa kama ya huyu bwanamdogo!
 
Kwa baadhi yetu wengine, tukiwa na pesa mfukoni, basi tunakuwa unstoppable!

Kuna feeling ya kwamba .."naweza kufanya chochote nitakacho" .
Lkn pia, factor ya kutamaniwa na wanawake/wasichana inakuwa kubwa na ya juu sana, maana wanajua watapata msaada wa kulipiwa bili za DSTV!

Ishu hapa ni commitment ya mtu husika, kama anaweza kuresist majaribu haya!
Kama huwezi kuya'turn down basi matokeo yanakuwa kama ya huyu bwanamdogo!

PJ, mke pia anachangia..kama hakuridhishi..u r bound to find external help!!
 
Kuna vishawishi vingi vinavyoambatana na pesa na umaarufu. Kama hauna uwezo wa kujenga nidhamu ya kujikatalia ni lazima utaangukia mitego ya aina hiyo.Hao wanawake wote walikuwa wanajua wanachofanya maana the guy is a married man.namuonea huruma mkewe.
Tujifunze kujikatalia siku moja moja maana ni rahisi sana ku ruin hata career kwa utaratibu huo wa kuwa na vimada kumi na moja mtu mmoja. Ingekuwa huku kwetu TZ haina shida tungemuingiza kwenye kundi la wale wanaojiita madume ya mbegu.
 
tumeona tiger woods na vimada wake.jee hii ni sex addiction?ni ugonjwa?maana najaribu kufikiria mtu wa hadhi yake kwa nini afanye mambo haya?hakujua kuwa kwamba atagundulika?angekuwa bachelor isingekuwa tatizo,lakini ana mke na watoto 2!!!!!!!!!!!!!!!!hakuogopa ukimwi na magonjwa ya zinaa?

Mpaka sasa sijapata jibu!au pesa nyingi ni mkosi?anafuatia kama african americans wengine waliofall from grace!michael jordan,mike tyson,mr vick(anayechezea mbwa) na michael jackson?

mpinge shetani naye atakukimbia..
Jamaa alimkumbatia shetani.
Mshahara wa dhambi ni mauti
 
Tamaa zinaweza kukuharibia sana,yatupasa kuwa waangalifu sana ,wewe unakipato kidogo unaona hata hakitoshi,kumbuka hiyo ni ridhiki uliyopewa na mola wako.
wewe una mke wako lkn unaona hatoshi unaamua kwenda nje.
mimi naamini malipo siku zote ni hapa hapa duniani,Mungu ana kuonyesha na kutukukumbusha namna gani ya kuishi hapa duniani,
Kijana u staa ulimzidi sana mpaka hatua ya kukataa u afrika wake yote hiyo ndio tunasema tamaa
 
Back
Top Bottom