Serkali iwasaidie wananchi wake maskini

Mapinduzi

JF-Expert Member
Aug 23, 2008
2,422
94
Naamini serikali yetu inawajali sana wananchi wake na inawataka wote wawe na maisha bora. Ningeomba lau iwe inawapa wananchi maskini hasa wa vijijini walau elfu hamsini kila baada ya miezi mitatu.

Wananchi wa mikoa ya Dodoma, Singida, Shinyanga, Morogoro etc ni baadhi ya sehemu za nchi hii ambapo watu waishi kwenye lindi kubwa la umaskini. Ukosefu wa maji na miundombinu mingine ni katika mambo yanayowatesa wananchi hawa. Ningependekeza serikali ipange miaka mitano ya majaribio ya zoezi.

Nchi za wenzetu, tena nyingine hazina rasilimali yeyote kuizidi TZ wanaweza, kwani wao waweze wana nini na sisi tusindwe tuna nini?

Nategemea bajeti ya mwaka ujao itapunguza matumizi kwenye wizara na kuwafikia wananchi kwa kuwasubsidize wasiojiweza.

Wakatabahu!
 
This will never happen ndugu yangu!
Wewe kama una kidogodogo, chagua walengwa wako uwasaidie kivyakovyako.
 
This will never happen ndugu yangu!
Wewe kama una kidogodogo, chagua walengwa wako uwasaidie kivyakovyako.

Kwa nini unadhani inashindikana ilihali naona bajeti za mawizara ni kubwa mno?

Matumizi yanazidi mapato, kama ndivyo kwa nini wananchi waliowengi wasifaidike pia? Let say wazee na watoto yatima wahudumiwe na serikali.
 
Mkubwa,
umeshachungulia kasma za mawizara?
Kama ndiyo utaelewa na kama bado ni kuwa hakuna vifungu kwa shughuli ya kusaidia maskini.Pia humo humo kwenye mawizara utakuta kuna ngazi ya waofaidi na ngazi ya wanaoangalia tu na kusubiri mishahara yao kijungu jiko mwisho wa mwezi.
Iko wizara maalumu kuhudumia wasio na uwezo, lakini fungu wanalopewa halitoshi kitu.
 
Asante sana WoS kwa maelezo haya.

Ni kweli hakuna vifungu vya kusaidia maskini, labda huwa wanapitiwa tu au hawajui kama kuna watu maskini wanaohitaji msaada. Can't this be a wake up call to the govt?

Kama kuna ngazi za wanaofaidi na wasiofaidi huko wizarani, hao wasiofaidi kwa nini wanakaa kimya? kwa nini wameamua kufa kiofisi?
 
Mimi nadhani kuwapa pesa tu haiwezi kuwasaidia kujikwamua kiuchumi au kuwapa nafuu ya kudumu kwa matatizo yao. Kinachotakiwa ni kuweka mikakati ya kusaidia juhudi zao za uzalishaji ili ziweze kutoa tija kwa manufaa yao na ya Taifa kwa ujumla.

Kwa mfano, serikali inatakiwa kujenga miundombinu bora zaidi kwa kuhakikisha;

1. Barabara nzuri zinafika sehemu kubwa vijijini, ili kuwezesha huduma mbalimbali kuwafikia walengwa kwa urahisi badala ya kujenga miundombinu hiyo mijini peke yake.
2. Serikali inatakiwa kutafuta masoko ya mazao yoyote yanayozalishwa vijijini ili kuwapatia kipato wananchi huko
3. Serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa mazao ya wanavijiji kote nchini yanapata soko lililo fair na si kuruhusu kudhulumiwa na wafanya biashara kama ilivyo sasa
4. Serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa, wananchi wa vijijini wanapata pembejeo na malighafi nyinginezo kwa urahisi na kwa bei nafuu ili kuwawezesha kuzalisha kwa kiasi kikubwa na kwa tija zaidi.

Kama wananchi wa vijijini wakipatiwa pesa tu, mathalan shilingi 50 elfu uliyoipendekeza, baada ya muda mfupi pesa hiyo haitatosha na watahitaji pesa zaidi. Lakini vilevile, kama wakiona wanapewa pesa bila kufanya jitihada yoyote, wataamua kuacha kujitahidi kuzalisha na hivyo kuwafanya wawe masikini zaidi.

Inatakiwa serikali kuwa makini sana kwa kuboresha maisha ya vijijini ili watu wengi zaidi wavutiwe kuishi huko na kuzalisha zaidi. Hii inawezekana kabisa.
 
Asante sana WoS kwa maelezo haya.

Ni kweli hakuna vifungu vya kusaidia maskini, labda huwa wanapitiwa tu au hawajui kama kuna watu maskini wanaohitaji msaada. Can't this be a wake up call to the govt?

Kama kuna ngazi za wanaofaidi na wasiofaidi huko wizarani, hao wasiofaidi kwa nini wanakaa kimya? kwa nini wameamua kufa kiofisi?

Hebu tuwasubiri wenyewe waje wajibu..nisiwasemee bureee!
 
Back
Top Bottom