Seriously, "Wa-Tank men" mko wapi?

BongoTz

JF-Expert Member
Nov 3, 2006
272
3
Baada ya wengine wote (waandamanaji) kuwa wamenyamazishwa tuli na zaidi ya watu mia saba wakiwa wameripotiwa kuuawa, picha ya shujaa mwenye shati jeupe na suruali nyeusi akiwa amesimama peke yake mbele ya sanjari ya vifaru vya kijeshi vilivyokuwa vikiviringika kuelekea kwenye viwanja vya Tiananmen kuwatawanya wanafunzi-wandamanaji wa ki-china, itabaki kuwa na sehemu ya pekee kila mara siku ya kistroria ya jumatatu June 4, 1989 itakapokumbukwa. Wang Weilin ni jina bandia alilopewa Rais mstaafu Jiang-Zemin (kipindi hicho katibu mkuu wa CCP) alipotaka kujua zaidi kuhusu mwandamanaji huyo. Lakini ukweli ni kwamba hadi leo hii hakuna anayefahamu jina lake halisi kiasi cha kupelekea abatizwe jina bandia--"The Tank Man".

Ingawa baadhi ya wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanadai kuwa umri wake ulikuwa umepita kwa yeye kuwa mwanafunzi, kilichomsukuma kusimama peke yake mbele ya sanjari ya vifaru vilivyokuwa vikielekea Tiananmen square huenda pia ndicho kilichomsukuma Gandhi kuandamana kwa mfungo wa siku 21 bila kula wakati akipigania uhuru wa India.

Kitu hicho ambacho mwanafalsafa wa kale Lau Tzu hukiita "The Tao" (virtue), yumkini ndicho pia kilichowasukuma wanaharakati wa miaka ya sitini (1960s) kama vile Martin Luther King Jr, Ho Chi Minh, Patrice Lumumba, na wengine wengi kusimama kidete na kupinga vitendo vya udhalimu na uonevu vilivyokuwa vikiendeshwa na kundi la watu wachache waliodhani kuwa wanahaki ya kufanya kila walichojisikia kufanya pasipo kuulizwa na mtu yeyote yule.

"The Tank man" anatukumbusha kuwa mchakato wa mabadiliko yoyote yale yawe ya kisiasa, kijamii ama kiuchumi hayataletwa na viongozi wenye majina makubwa yaliyozoeleka masikioni mwetu (Malecela, Kingunge, Malima, Mwinyi, Chambiri, Msuya, Sitta, Chenge, ); bali mabadiliko halisi yataletwa na raia wa kawaida watakaohiyari kujitoa mhanga kutetea maslahi ya taifa bila kujali madhara yanayoweza kuwakumba hapo baadaye.

Kama Rais Kennedy alivyowahi kusema, utu wa kweli umekamilika ndani ya yule anayediriki kufanya kila awezacho kutetea haki na uhuru wake pasipokujali madhara yanayoweza kumkumba hapo baadaye.

Enough is enough.

Wakati umefika sasa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, shule za sekondari, wakulima vijijini, pamoja na tasisi mbalimbali nchini kuiga ujasiri wa "The Tank Man" na kuanza rasmi kutetea maslahi ya taifa letu pasipokujali madhara (personal consequences) yanayoweza kuwakumba hapo baadaye.

Kama ilivyo kwa nchi za Magharibi, tunapaswa sasa kuanzisha vikundi vidogovidogo ( grassroots movement ) vitakavyo hakikisha kuwa viongozi tuliowachangua wanawajibika na kutumika kwa ajiri ya wananchi na si vinginevyo.

Grassroots movement hizo zipange na ku-organize mambo mbalimbali yanayowabana viongozi waliowachaguliwa ili kuhakikisha kuwa maslahi ya taifa zima, na sio ya watu wachache (mafisadi), daima yanawekwa mbele.

Mambo kama:

>Ku-organize mikutano mikubwa ya hadhara na kuwakemea viongozi manafiki >wanaoweka mbele maslahi yao binafsi.
>Kutundika mabango makubwa ya Billboard yenye ujumbe wa kushinikiza.
>Kukusanya sahihi ku-petition jambo linalowakera.
>Kuchangisha hela za kurusha matangazo ya kampeni kwenye Tv, Radio , na magazetini.
>Ku-organize maandamano makubwa nchi nzima pale wananchi wanapoona nchi inaelekea kusipo.
>Wananchi wawaandikie wabunge wao kuwaeleza kile kinachowakera.
>Ku-organize " get out the vote", kwa kuwahamasisha watu kupiga kura, ikiwezekana kuwasafirisha kwenda kwenye vituo vya kura.

Kwamba, Dr. Harrison Mwakyembe ataporudi kuomba kula Kyela, movement imuulize, "...mwaka huu unaahidi kuongeza vitanda vingapi katika hospitali ya wilaya?" Kadhalika wananchi wa Mbulu nao wamuulize Philipo Sangka Marmo, "...nini mikakati yako katika kutatua tatizo lililopo la upungufu wa wauguzi katika hospitali yetu ya wilaya?" Endapo kama wataahidi kutatua matatizo hayo na kutoa maelezo ya kueleweka, basi wapewe nafasi ya kurudi Dodoma; lau wasipotoa maelezo ya kueleweka, basi movement itafute mbadala (alternative).

Kando na hayo, movement pia itoe kipaumbele kwenye suala la marekebisho ya katiba. Katiba ya sasa inampa Rais madaraka makubwa sana ya kiutendaji. Imefikia muda sasa kumpunguzia Rais madaraka hayo na badala yake Bunge na Mahakama ziwe na mamlaka makubwa zaidi ya kuidhibiti serikali.

Sambamba na hilo, wakati umefika pia kwa Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali kuchaguliwa kutoka nje ya Bunge kama ilivyo kwa nchi nyingi za Magharibi, mfano, Marekani. Haina maana kuwa na Bunge ambalo nusu ya wabunge ni viongozi wa serikali pia.

Katiba mpya iweke bayana kwamba mawaziri wote watoke nje ya Bunge ili iwe rahisi kwao kuwajibika kwa wananchi kuliko ilivyo hivi sasa.

Ikiwezekana pia, wakuu wote wa wilaya/mikoa wapigiwe kura na wananchi ili wawajibike moja kwa moja kwa wananchi kuliko ilivyo sasa ambapo hutelewa na Rais. Chamsingi hapa ni kupunguza madaraka toka kwa central government kwenda kwenye local government.

Swali linalobaki wazi ni hili: Je, " Wa-Tank Men" mko wapi?

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania!
 
Bongotz,

Asante kwa post nzuri
 
Kulikuwa hakuna haya ya kukoti bandiko lote na kuishia kusema Ahsante... ilhali ungeweza kusema Ahsante kwa kubonyeza tu...
 
Kibunango unachokisema nimeki note kutokea sana, ahsante kwa kukidhihirisha.

Wa Tank hatuna bongo.Sadly. Watu wame solicit walioko Marekani kuandamana ubalozi wa Tanzania DC. with the exception of jmushi KILA MTU KIMYA.
 
...

...wapo bwana, lakini kwakuwa 'ndivyo tulivyo' hufanywa 'laughing stock' upepo unapowageukia!
 
In other words wanaogopa kufanywa laughing stock?

Sasa wana tofauti gani na hao wapuuzi wanaowafanya laughing stock?
 
Pundit,
Wa-Tank man Bongo wapo, tatizo ni ukosefu wa kiongozi (leader) wa kuwaunganisha na ku-articulate vision kisha wafuate (wakiwemo raia wa kawaida).
 
Baada ya wengine wote (waandamanaji) kuwa wamenyamazishwa tuli na zaidi ya watu mia saba wakiwa wameripotiwa kuuawa, picha ya shujaa mwenye shati jeupe na suruali nyeusi akiwa amesimama peke yake mbele ya sanjari ya vifaru vya kijeshi vilivyokuwa vikiviringika kuelekea kwenye viwanja vya Tiananmen kuwatawanya wanafunzi-wandamanaji wa ki-china, itabaki kuwa na sehemu ya pekee kila mara siku ya kistroria ya jumatatu June 4, 1989 itakapokumbukwa. Wang Weilin ni jina bandia alilopewa Rais mstaafu Jiang-Zemin (kipindi hicho katibu mkuu wa CCP) alipotaka kujua zaidi kuhusu mwandamanaji huyo. Lakini ukweli ni kwamba hadi leo hii hakuna anayefahamu jina lake halisi kiasi cha kupelekea abatizwe jina bandia--"The Tank Man".

Ingawa baadhi ya wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanadai kuwa umri wake ulikuwa umepita kwa yeye kuwa mwanafunzi, kilichomsukuma kusimama peke yake mbele ya sanjari ya vifaru vilivyokuwa vikielekea Tiananmen square huenda pia ndicho kilichomsukuma Gandhi kuandamana kwa mfungo wa siku 21 bila kula wakati akipigania uhuru wa India.

Kitu hicho ambacho mwanafalsafa wa kale Lau Tzu hukiita "The Tao" (virtue), yumkini ndicho pia kilichowasukuma wanaharakati wa miaka ya sitini (1960s) kama vile Martin Luther King Jr, Ho Chi Minh, Patrice Lumumba, na wengine wengi kusimama kidete na kupinga vitendo vya udhalimu na uonevu vilivyokuwa vikiendeshwa na kundi la watu wachache waliodhani kuwa wanahaki ya kufanya kila walichojisikia kufanya pasipo kuulizwa na mtu yeyote yule.

"The Tank man" anatukumbusha kuwa mchakato wa mabadiliko yoyote yale yawe ya kisiasa, kijamii ama kiuchumi hayataletwa na viongozi wenye majina makubwa yaliyozoeleka masikioni mwetu (Malecela, Kingunge, Malima, Mwinyi, Chambiri, Msuya, Sitta, Chenge, ); bali mabadiliko halisi yataletwa na raia wa kawaida watakaohiyari kujitoa mhanga kutetea maslahi ya taifa bila kujali madhara yanayoweza kuwakumba hapo baadaye.

Kama Rais Kennedy alivyowahi kusema, utu wa kweli umekamilika ndani ya yule anayediriki kufanya kila awezacho kutetea haki na uhuru wake pasipokujali madhara yanayoweza kumkumba hapo baadaye.

Enough is enough.

Wakati umefika sasa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, shule za sekondari, wakulima vijijini, pamoja na tasisi mbalimbali nchini kuiga ujasiri wa "The Tank Man" na kuanza rasmi kutetea maslahi ya taifa letu pasipokujali madhara (personal consequences) yanayoweza kuwakumba hapo baadaye.

Kama ilivyo kwa nchi za Magharibi, tunapaswa sasa kuanzisha vikundi vidogovidogo ( grassroots movement ) vitakavyo hakikisha kuwa viongozi tuliowachangua wanawajibika na kutumika kwa ajiri ya wananchi na si vinginevyo.

Grassroots movement hizo zipange na ku-organize mambo mbalimbali yanayowabana viongozi waliowachaguliwa ili kuhakikisha kuwa maslahi ya taifa zima, na sio ya watu wachache (mafisadi), daima yanawekwa mbele.

Mambo kama:

>Ku-organize mikutano mikubwa ya hadhara na kuwakemea viongozi manafiki >wanaoweka mbele maslahi yao binafsi.
>Kutundika mabango makubwa ya Billboard yenye ujumbe wa kushinikiza.
>Kukusanya sahihi ku-petition jambo linalowakera.
>Kuchangisha hela za kurusha matangazo ya kampeni kwenye Tv, Radio , na magazetini.
>Ku-organize maandamano makubwa nchi nzima pale wananchi wanapoona nchi inaelekea kusipo.
>Wananchi wawaandikie wabunge wao kuwaeleza kile kinachowakera.
>Ku-organize " get out the vote", kwa kuwahamasisha watu kupiga kura, ikiwezekana kuwasafirisha kwenda kwenye vituo vya kura.

Kwamba, Dr. Harrison Mwakyembe ataporudi kuomba kula Kyela, movement imuulize, "...mwaka huu unaahidi kuongeza vitanda vingapi katika hospitali ya wilaya?" Kadhalika wananchi wa Mbulu nao wamuulize Philipo Sangka Marmo, "...nini mikakati yako katika kutatua tatizo lililopo la upungufu wa wauguzi katika hospitali yetu ya wilaya?" Endapo kama wataahidi kutatua matatizo hayo na kutoa maelezo ya kueleweka, basi wapewe nafasi ya kurudi Dodoma; lau wasipotoa maelezo ya kueleweka, basi movement itafute mbadala (alternative).

Kando na hayo, movement pia itoe kipaumbele kwenye suala la marekebisho ya katiba. Katiba ya sasa inampa Rais madaraka makubwa sana ya kiutendaji. Imefikia muda sasa kumpunguzia Rais madaraka hayo na badala yake Bunge na Mahakama ziwe na mamlaka makubwa zaidi ya kuidhibiti serikali.

Sambamba na hilo, wakati umefika pia kwa Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali kuchaguliwa kutoka nje ya Bunge kama ilivyo kwa nchi nyingi za Magharibi, mfano, Marekani. Haina maana kuwa na Bunge ambalo nusu ya wabunge ni viongozi wa serikali pia.

Katiba mpya iweke bayana kwamba mawaziri wote watoke nje ya Bunge ili iwe rahisi kwao kuwajibika kwa wananchi kuliko ilivyo hivi sasa.

Ikiwezekana pia, wakuu wote wa wilaya/mikoa wapigiwe kura na wananchi ili wawajibike moja kwa moja kwa wananchi kuliko ilivyo sasa ambapo hutelewa na Rais. Chamsingi hapa ni kupunguza madaraka toka kwa central government kwenda kwenye local government.

Swali linalobaki wazi ni hili: Je, " Wa-Tank Men" mko wapi?

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania!
Bango
 
Back
Top Bottom