Serious: Nifanyeje?

Mkuu unahitaji upumzishe ubongo kidogo.Kwa sababu wewe ni binadamu siyo mashine na hata mashine hufanyiwa ukarabati ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi. Ila la kuachana na JF sikubaliani nalo kwani hilo naliona liko kwenye damu yako.
 
Mzee Invisible,Pole sana
1.Umezungumzia watoto yatima. Lakini hukuzungumzia kama una watoto na kama una mke UNAYEKAA NAE-kama una mke basi hilo linaweza kuwa tatizo kubwa kuliko yote uliyoelezwa na ma Dr. na wana JF.Kama unaye/Unakaa nae,muombe aende yeye likizo na watoto hata kama ni kuwapumzisha kijijini kwenu kama huna uwezo wa kuwapeleka Hawaiiiiiiiiiii.Ubaki peke yako-utakuja kutueleza baada ya mwezi
2.Kinyume na hivyo-Kifo kinakukaribia,pesa utaziacha,hao wanaokufanyisha kazi ndio watakaokuzika,hawa wana JF sana sana watakutumia salaam za rambirambi(za mdomo bila hata senti). Kama hutaki kwenda likizo au kufuata ushauri wangu,basi andika urithi na endelea na kuwatumikia hao ma bepari. Mimi sioni shida JF kuwa static kwa week 2 zako za kupumzika kama inabidi kuliko kupeleka maiti vijijini.
Pole na Mungu atakujalia,kama hu sali/swali,sisi tutakuombea.
 
Nakubaliana kabisa na Katabazi. Ni aheri ukubali ushauri wa kumpumzika leo kuliko tukakusahau kabisa.
Mara nyingine watu tunajiweka mahali pa kuamini kama si sisi basi hakuna litakaloendelea. Yawezekana ni kweli, lakini kwa uzoefu wangu si kweli. Kuwepo kwako japo muhimu lakini si kweli ukikosekana kwa mwezi au week mbili itakuwa ndio basi. Jaribu kuimagine unmelazwa Intensive Care Unit kwa miezi miwili. Hujitambui, hujielewi. Bado si watu wanaokuhusu wataendelea na shughuli ikiwa ni pamoja kusikitika na kuugua kwako na pengine kukuuguza. Sikuombei hilo na Mungu apishe mbali, lakini tafadhali, Mkuu kapumzike. Kuwepo kwako ni kwa thamani zaidi kuliko hayo yote unayofanya na unayowafanyia watu ikiwa ni pamoja na hao watoto yatima uliowazungumzia.
What you are suffering from is FATIGUE na hamna dawa nzuri kama kupumzika. Si vizuri na sitakushauri uanze kufikiria Valium na jamii yake.
Bado tunakuhitaji sana, kama mzazi, mlezi, mshauri, kiongozi, and above all a considerate and well thought Human being.
 
I see, ni mara ya kwanza naleta tatizo langu kwenu wakuu.

Nina matatizo ambayo nahitaji ushauri wa haraka au wa kina ikiwezekana,.

Najisikia uchovu wa hali ya juu... Najisikia kucha kila aina ya kazi... Natamani kupumzika japo siku tatu tu niweze kurejea katika hali yangu ya kawaida.

Ugumu:

Nahitaji kuzima simu, kuwa mbali na pc kuwa mbali na familia yangu kabisa na kukaa alone kwa muda huo.

Si rahisi kuwambia familia kuwa nawaacha kwa muda huo, nahisi watajisikia vibaya.

Si rahisi kukaa mbali na JF, nikifanya hivyo nafsi inakuwa inanisuta all the times.

Si rahisi kuwaacha kwenye mataa makampuni manne ambao wameniajiri na kazi zao kulala siku moja kwao wanaona kama ndo mwisho wa makampuni yao (ilhali kuna wataalam wengi lakini wananikomalia).

Sina hamu na pesa zao hata kama wanasema wanavunja mkataba nami kwani mwili hauwezi kuvumilia hali niliyo nayo kwa sasa... Yani niko tayari kuacha na kupumzika liwalo na liwe.

Mbaya zaidi:

Nikiwa naendesha gari natamani kutokanyaga hata mafuta wala breki kwani nahisi vinanichosha mwili tu, nikiwa mbele kwenye foleni ya magari najikuta nimekuwa mwingi wa mawazo hata taa zikiruhusu nisipopigiwa kelele na wenzangu kushtukia inakuwa tatizo.

Je, wakuu nifanye nini???
unafanya kazi ya kulima au kubeba vitu vizitoooo.

jaribu kupata ED ya siku tatu uone hali itakuwajeee.

polee kaka, mchakamchaka wa third world na mambo yake!!!
 
Oh,

Asante mkuu BelindaJacob,

Nalilia kupumzika... Nahisi ndo suluhisho. Tatizo ni vipi nifanye? Baadae nahisi tatizo jingine labda ni la kisaikolojia na wala si uchovu.

Laba niseme zaidi:

Nina watoto 8 mpaka sasa (Nyumbani Tanzania) ambao hawana wazazi (yatima) na wengine wana wazazi lakini uwezo uko chini ninaowasomesha na sidhani kama inawezekana kupita dakika bila kuwawazia, hawa sidhani kama unaweza kunishauri kuwa niwabwage! Sintokusikiliza...

Hii hali inanitatiza SANA mpaka nafikia hatua ya kusema mbele zenu wakuu, kama kuna ambaye anaweza kunishauri kama kuna cha kunywa ama kula kunifanya nirejee kwenye form basi naomba sana anipe ushauri...

Hizo kampuni ninazozifanyia kazi ni kuwa nafanya kazi ya aina moja kwa wote isipokuwa kampuni tatu zimeridhia kuniacha nibaki kwa mwajiri wa mwanzo zenyewe zinatuma kazi zake kwa njia tofauti na wakti mwingine kuleta ofisini kwangu physically.

Kazi kwelikweli, Pole sana mkuu!

Kama wengi walivyokushauri, na kama kweli umepima pressure na sukari vyote viko sawa basi dawa ni kupumzika tu, no alternatives labda madaktari bingwa watuambie humu ndani kama kuna njia mbadala.

Binafsi hiyo hali ilishanitokea kilichonitibu ilikuwa ni kupata muda wa kutosha wa kupumzika katika sehemu isyokuwa na bughudha, pili kupunguza kama sio kuacha kuwaza kabisa, tatu nilizima simu yangu ya mkononi kwa muda wa siku tatu, ilinisaidia kwakweli.
 
Mkuu nakupa pole sn

Nakupa Offer ya 1 week uje upumzike paleeee Prisons Island, pana full Internet. Kuhusu JF usiwe na wacwac, set remote management ktk server yetu ya JF km mambo yakikorofisha mwenyewe uanelewa nini cha kufanya.....au sio Mkuu???

Uzima wakoni muhimu kuliko mambo yote uliyoyaorodhesha kuwa ndio kikwazo!!!!
 
Pole kwa hali unayojisikia. Hizo ni dalili za burnout syndrome Invisible. Ni mkusanyiko wa dalili mbalimbali zinazojitokeza ma matokeo ya uchovu wa muda mrefu wa kisaikolojia.Hali hii inaweza kuletwa na sababu mbalimbali ikiwemo busy managerial lifestyle au matumizi ya dawa fulani (je kuna dawa unazokunywa mara kwa mara?)
Unachopaswa kufanya ni kuwa na vipindi vya mapumziko changamfu-active rest periods.Hit the gym, go jogging, swim, play footbal just get you body move without much thoughts. Unajitaji kuwa na alternative activities kustimulate ubongo kwa sababu repetition ya matukio imechosha the most used pathways.
Ninakushauri uanze jogging mara tatu kwa wiki. Iwapo utachagua gym, basi iwe na hewa ya kutosha sio zile gym zilizojaa hewa ya ''vikwapa'' kwa sababu itakuchosha zaidi.
Pia ninakushauri unywe maji ya kutosha, at least 2 litres a day. Kuwa na chombo ambacho unaweza kumonitor unywaji wako wa maji. Unakijaza asubuhi na unajitahidi umemaliza kabla hujaenda kulala.
Katika hatua hii jitahidi usitumie vidonge au dawa yoyote kwanza, ili kuavoid dependance on them, Ila iwapo umeshauriwa kutumia dawa hiyo na daktari basi endelea nayo.
Fanya mazoezi kwa miezi miwili halafu tafadhali njoo JF kutueleza maendeleo.
 
pole sana invisible.
wengi wametoa ushauri :kupumzika,mazoezi maji kwa wingi nk.upande wangu pamoja na yote hapo juu ACHA kwa muda matumizi ya KAHAWA tafuta kahawa mbadala mfano maji ya moto na tangawizi mbichi,usiache kula chakula cha mchana hata kama uko kazini beba matunda.
hatuna mazoea ya kutumia vitamins,lakini jaribu kutumia multivitamins haswa zenye ginseng huwa zinasaidia sana kwa wenye uchovu wa mda mrefu.
 
Mimi nakushauri uanze kufanya mazoezi. Tafuta gym ujiunge na uanze kupiga nondo kwa sana. Sukuma uzito mara tatu au nne kwa wiki. Kama hakuna gym au kama huwezi kujiunga sasa hivi tengeneza vyma vyako mwenyewe. Pia anza kuwa unakimbia (cardio workout) kwenye treadmill. Kama huna vifaa unaweza kuvitengeneza mwenyewe na kukimbia wala huhitaji treadmill.

Kwa kifupi, jaribu ku diversify mambo uyafanyayo kwenye muda wako wa ziada.
 
kaka Invisible,

mimi nina mawazo tofauti kabisa na wengine, na wala sikushauri upumzike kabisa kabisa, wewe chapa kazi.

kwa wanaoamini Mungu huamini kwamba hapa duniani sisi ni wa kupita njia tu, na makao yetu ya milele ni mbinguni, huko ndio tutapumzika, tukiimba na malaika, na ndio pepo na raha mustarehe ilipo, ndio maana kwa sisi wakristu wakatoliki mtu anapokufa huwa tunasema: "Roho ya marehemu ( taja jina)" halafu tunajibu tunasema: "Apumzike kwa amani, Amina"

So kwa ushauri wangu, wewe chapa kazi, utapumzika siku tuakayozidiwa na hizo kazi zako, ukapata stroke ukiwa kazini kwako (ofisini) ukadondoka na ukafa hapo hapo, hapo ndio utaenda kupumzikia huko mbinguni tena kwa nafasi kabisa, huko hamna waajiri wanne, hamna jamii forum, hamna foleni ya magari, ni upepo mwanana na kula kuku tu...! So for now weee piga kazi ukisubiria STROKE
 
Invisible, how are you doing rafiki?
I am worried man, usije fikia kuweka lotion kwenye msosi kama Yo Yo.
Umefanikiwa ku-delegate baadhi ya majukumu yako?
Can you now go on holiday for two or three weeks? (You should be able)

Farida ana maoni gani kuhusu hili swala?
 
Pole sana...najaribu kuvuta picha ya hali unayojisikia..its very bad condition, umeshawahi kuwaona wataalamu wa afya kuhusu unavyojisikia? kabla hujatoa maamuzi yoyote?
Ila likizo kwa maana ya mapumziko ya akili na mwili ni muhimu sana. Uende mahali mbali na hujawahi kufika (labda mji mwingine), upate huduma hujawahi kupata (labda body massage na Yoga) na kuona vitu tofauti na mazingira uliozoea.

Pole sana.
 
I see, ni mara ya kwanza naleta tatizo langu kwenu wakuu.

Nina matatizo ambayo nahitaji ushauri wa haraka au wa kina ikiwezekana,.

Najisikia uchovu wa hali ya juu... Najisikia kucha kila aina ya kazi... Natamani kupumzika japo siku tatu tu niweze kurejea katika hali yangu ya kawaida.

Ugumu:

Nahitaji kuzima simu, kuwa mbali na pc kuwa mbali na familia yangu kabisa na kukaa alone kwa muda huo.

Si rahisi kuwambia familia kuwa nawaacha kwa muda huo, nahisi watajisikia vibaya.

Si rahisi kukaa mbali na JF, nikifanya hivyo nafsi inakuwa inanisuta all the times.

Si rahisi kuwaacha kwenye mataa makampuni manne ambao wameniajiri na kazi zao kulala siku moja kwao wanaona kama ndo mwisho wa makampuni yao (ilhali kuna wataalam wengi lakini wananikomalia).

Sina hamu na pesa zao hata kama wanasema wanavunja mkataba nami kwani mwili hauwezi kuvumilia hali niliyo nayo kwa sasa... Yani niko tayari kuacha na kupumzika liwalo na liwe.

Mbaya zaidi:

Nikiwa naendesha gari natamani kutokanyaga hata mafuta wala breki kwani nahisi vinanichosha mwili tu, nikiwa mbele kwenye foleni ya magari najikuta nimekuwa mwingi wa mawazo hata taa zikiruhusu nisipopigiwa kelele na wenzangu kushtukia inakuwa tatizo.

Je, wakuu nifanye nini???
Mkuu vipi tatizo limeisha????
mie ndo nimefanikiwa leo kujua kuwa sometimes Robot anaishiwa chaji.

Na dulilitatuaje maana wengi tutakumbwa na hili tifu halafu tukakosa suluhisho.
 
mkuu hapo utaalam wa kidaktari sina ila wa kikwetu nahitaji furaha. yani inabidi ucheke sana. tafuta ama mtu ama hadithi ikuchekeshe sio utabasamu ucheke mpaka unajisikia uadondoka kwenye kiti n amacho yanatoa machozi, basi utakuwa sawa. wataalam msiniulize kwa nini sina jibula kitaalam.
 
Pole Mkuu,
Ukiona hivyo ujue mother nature anakukumbusha tu kwamba mwili siyo machine isiyopumzika hata kwa maintenance.Unahitaji kuupumzisha mwili wako uweze kujikarabati wenyewe hata kama hauumwi kiasi cha kwenda kumshtakia daktari.

Jitahidi mara moja moja kujipa off hata ya siku moja kwa mwezi, miezi miwili kadri utakavyoona; chukua likizo ya angalau wiki mbili kwa mwezi - ukae mbali na shughuli zako za kila siku na ufanye vitu tofauti na ulivyozoea kila siku.

Njia nzuri sana za kujikarabati kimawazo na hata kimwili ni pamoja na - shughuli za bustani za maua au mbogamboga kama hauishi maghorofani - apartments.Pia unaweza kuogelea,kucheza golf,kuimba,kucheza muziki,kukimbia, kujisomea kitabu kizuri, kusafiri kwenda mbuga za wanyama n.k.Usimsahau my wife wako kwenye safari hizo kama utapanga LOL.
 
Mawazo mazuri WOS!

Kupumzisha mwili peke yake haitoshi. Liubongo nalo lahitaji hiyo treatment ya mapumzisho. Tatizo ni kwamba, mwili unaweza kuwa uko ufukweni unapunga upepo mwanana, lakini ubongo unang'ang'ana kusolve "unsolved" puzzles. Si umeona sasa tatizo hapo!

Kufanyike nini?
 
Pole sana Mkuu,hapo inabidi uchukue hatua kadha,kama hufanyi mazoezi anza kufanya, jaribu kupata usingizi wa kutosha,ikiwezekana jaribu kulala zaidi mwisho wa wiki,pata muda wa 'ku-switch off' pia mwishoni mwa wiki,anzaa na masaa kadhaa mpaka upate at least masaa 6,toka na familia muende beach au muende kuangalia sinema.Ni muhimu kuwahusisha familia katita kupunguza stress na tension kwakuwa ukiwakimbia na kuwa pekee kuna ile 'guilty feeling' itasumbua mapumziko yako.Anza na 'baby steps' utafika mahala utajisikia vizuri.Uko katika hatari ya kupata ajali na utendaji wako kushuka.Kila la heri.
 
I see, ni mara ya kwanza naleta tatizo langu kwenu wakuu.

Nina matatizo ambayo nahitaji ushauri wa haraka au wa kina ikiwezekana,.

Najisikia uchovu wa hali ya juu... Najisikia kucha kila aina ya kazi... Natamani kupumzika japo siku tatu tu niweze kurejea katika hali yangu ya kawaida.

Ugumu:

Nahitaji kuzima simu, kuwa mbali na pc kuwa mbali na familia yangu kabisa na kukaa alone kwa muda huo.

Si rahisi kuwambia familia kuwa nawaacha kwa muda huo, nahisi watajisikia vibaya.

Si rahisi kukaa mbali na JF, nikifanya hivyo nafsi inakuwa inanisuta all the times.

Si rahisi kuwaacha kwenye mataa makampuni manne ambao wameniajiri na kazi zao kulala siku moja kwao wanaona kama ndo mwisho wa makampuni yao (ilhali kuna wataalam wengi lakini wananikomalia).

Sina hamu na pesa zao hata kama wanasema wanavunja mkataba nami kwani mwili hauwezi kuvumilia hali niliyo nayo kwa sasa... Yani niko tayari kuacha na kupumzika liwalo na liwe.

Mbaya zaidi:

Nikiwa naendesha gari natamani kutokanyaga hata mafuta wala breki kwani nahisi vinanichosha mwili tu, nikiwa mbele kwenye foleni ya magari najikuta nimekuwa mwingi wa mawazo hata taa zikiruhusu nisipopigiwa kelele na wenzangu kushtukia inakuwa tatizo.

Je, wakuu nifanye nini???

Mkuu, hili linaweza kuwa ni tatizo kubwa sana kuliko unavyolidhania na ambalo halitamalizika kwa siku tatu tu. Jaribu kuwaona wataalamu wakuangalie zaidi kabla hali haijawa mbaya zaidi. Inawezekana kabisa kwamba huu si uchovu wa kawaida. Kila la heri.
 
Back
Top Bottom