Serious Fraud Office (SFO) yatoa tamko juu ya kesi ya Rada na Chenge

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Ofisi ya Uchunguzi wa makosa makubwa ya kifisadi(SFO) imesema imeshindwa kumhusisha Mhe Chenge na tuhuma za rushwa katika ununuzi wa rada.

Majibu hayo yamekuja miezi michache baada ya TAKUKURU kusema kwamba nayo imeshindwa kumhusisha Chenge na tuhuma hizo. Kitendawili kimeteguliwa. Kumbe mzee wa vijisenti hakuhusika na rushwa katika mradi huo.

Ukweli umedhihiri, je Uongo utajitenga?
 
Taja chanzo cha habari yako. Nakala ya hukumu ya kesi hiyo ilikuwekwa humu, kama uliisoma vizuri jaji alisema wazi kuwa rushwa ilitumika kuwalainisha maafisa wa Tanzania kuridhia ununuzi huo. Najua hivi leo Chege alikutana na wahandishi wa habari na kudai alisafishwa jambo ambalo siyo kweli.
 
Ofisi ya Uchunguzi wa makosa makubwa ya kifisadi(SFO) imesema imeshindwa kumhusisha Mhe Chenge na tuhuma za rushwa katika ununuzi wa rada.

Majibu hayo yamekuja miezi michache baada ya TAKUKURU kusema kwamba nayo imeshindwa kumhusisha Chenge na tuhuma hizo. Kitendawili kimeteguliwa. Kumbe mzee wa vijisenti hakuhusika na rushwa katika mradi huo.

Ukweli umedhihiri, je Uongo utajitenga?

Source wapi chumbani kwako?
 
Taja chanzo cha habari yako. Nakala ya hukumu ya kesi hiyo ilikuwekwa humu, kama uliisoma vizuri jaji alisema wazi kuwa rushwa ilitumika kuwalainisha maafisa wa Tanzania kuridhia ununuzi huo. Najua hivi leo Chege alikutana na wahandishi wa habari na kudai alisafishwa jambo ambalo siyo kweli.

I'm sorry jamani. Chanzo ni habari ya TBC1 saa mbili usiku huu
 
Na star TV wameelezea kwa kirefu kidogo!

Sijui watu wanasemaje katika hili.
 
Naona hawa sfo nao wanatuzuga kuna kitu wanakificha hapo....maana Tonny Blair na BWM wanahusika wanawafichia siri....ukweli unajulikana tunmaomba chenji yetu basi
 
Naona hawa sfo nao wanatuzuga kuna kitu wanakificha hapo....maana Tonny Blair na BWM wanahusika wanawafichia siri....ukweli unajulikana tunmaomba chenji yetu basi

SFO waliingia makubaliano na BAE kwamba wasingewashitaki BAE kwa kosa la kutoa Rushwa (ingawa wangeweza kufanya na kutoa ushahidi wa kutosha); sababu kubwa ni kwamba kama BAE ingepatikana na hatia basi isengeruhusiwa kufanya biashara (ku bid tenders), bara la Ulaya, marekani na sehemu nyengine duniani kwa muda fulani, na hii ingeidhoofisha kampuni na uchumi wa Uingereza kwa kiasi!!! Kwa hivyo basi mimi naona imekua bahati tu kwa kina Chenge etc ...lakini hata hivyo TAKUKURU ilikuwa na ushahidi na uhuru wa kufungua kesi zidi ya Chenge...huku Tanzania but obviously...not in the interest of the mighty and powerful!!!!!
 
Bajeti ya Serikali yapigwa panga Send to a friend Sunday, 13 February 2011 09:21 digg

NI KWA AJILI YA KUFIDIA NAKSI YA BILIONI 640
Mwandishi Wetu
HALI mbaya ya uchumi imeilazimisha Serikali kufumua bajeti yake ya mwaka wa fedha 2010/11 kwa kupunguza matumizi ya Wizara ili kufidia upungufu wa Sh670.4 bilioni zilizotegemewa kupatikana kutokana na makusanyo ya kodi katika mwaka huu wa fedha.

Uamuzi huu ambao umetokana na kupungua mapato ya ndani ya mwaka huu wa fedha, umesababisha Serikali kupiga panga fedha za miradi ya maendeleo na za matumizi ya wizara zote.

Taarifa za kuaminika ambazo Mwananchi Jumapili imezipata, zinaeleza kuwa fedha hizo zinapunguzwa kutoka katika kila wizara kwa viwango tofauti kulingana na bajeti ya wizara husika, ili kufidia makusanyo ya kodi yaliyokusudiwa na kulipia mahitaji ya fedha za mishahara na kuwalipa makandarasi wa Barabara.

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustaffa Mkullo, alipoulizwa kuihusina na hali hiyo alisema taarifa ya hali ya uchumi wa nchi alishaitoa hivi karibuni kwenye chombo kimoja nchini, hivyo hahitaji kuitoa tena.

"Nilitoa taarifa kwa wenzenu wa gazeti (sio Mwananchi) sasa siwezi tena kuirudia," alisema.

Habari hii inakuja wakati Serikali imeelezwa kuwa imetuma barua kwa nchi wafadhili kuziomba ziweze kuchangia miradi ya maendeleo katika bajeti yake.


Kwa mujibu wa taarifa hizo, Wizara ya Fedha na Uchumi (Hazina), imekuwa ikifanya vikao mbalimbali vya kujadili tathmini ya hali ya uchumi na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti tangu Desemba mwaka jana.

Katika vikao hivyo vilivyofanyika Januari11 hadi 24 mwaka huu ilibainika kuwa kuwepo kwa upungufu wa mapato kwa mwaka huu wa fedha unafikia Sh670.4 bilioni.

Kutokana na hali hiyo, Serikali imelazimika kupunguza fedha za matumizi kwa wizara zake, kiasi cha Sh480.51 bilioni ili kufidia upungufu huo.

Vile vile, itapunguza fedha za matumizi, kiasi cha Sh153 bilioni ili kuziba pengo la gharama za mishahara.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, Serikali inahitaji kiasi cha Sh258 bilioni kulipa madai ya wakandarasi wa barabara na mkandarasi aliyekarabati Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, huku fedha hizo zikielezwa kuwa mikataba yake ilifanyika nje ya bajeti ya mwaka 2010/11.

Kwa mujibu wa chanzochetu cha habari, katika mkutano wa makatibu wakuu wa wizara, uliofanyika hivi karibuni kuliibuka mjadala juu ya kwanini malipo ya kandarasi ya barabara yaonekane kuwa ni ya dharura wakati kuna wizara ambazo pia zinadaiwa na wakandarasi.

Mvutano mwingine ulihusu kiwango cha fedha za matumizi ya wizara zilizopendekezwa kupunguzwa, kuwa ni kikubwa na kuwa hali hiyo itazifanya wizara kushindwa kuendesha shughuli zake kwa kipindi kilichobaki cha mwaka wa fedha.

"Kulitolewa mapendekezo kuwa badala ya serikali kupunguza kiwango hicho cha fedha kutoka katika kila wizara, inatakiwa iibane Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuziba mianya inayosababisha kushindwa kufikia malengo ya makusanyo ya mapato," kilisema chanzo hicho.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Beno Ndulu akizungumza na waandishi wa habari mwanzoni mwa mwezi huu alisema hali ya uchumi wa nchi ni nzuri na kwamba Serikali ina hazina ya kutosha ya fedha.

Hata hivyo, pamoja na mjadala huo mkali, Mwananchi Jumapili imebaini kuwa Wizara ya Fedha imesema Serikali haina budi kulipa deni hilo la kandarasi ya barabara linalofikia Sh250 bilioni ili kuendelea na kazi ya ujenzi wa barabara kabla ya kuanza kwa msimu wa mvua.

Pia wizara hiyo imesema hali ya uchumi imeathiriwa na mgao wa umeme unaoendelea, na hivyo kuathiri mwelekeo wa kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato.

Wachambuzi wa uchumi, Serikali kulazimika kupunguza bajeti yake kunatokana na kuwepo kwa matumizi mabaya na utoaji holela wa misamaha ya kodi iliyosababisha kushuka kwa kiwango cha ukusanyaji wa mapato.

Habari zilizopatikana kutoka mkutano wa wahisani na watendaji wa Serikali kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2010/2011, ulifanyika hivi karibuni zinaeleza kuwa Serikali ina upungufu wa Sh600 bilioni kutoka kwenye bajeti ya Sh11 trilioni, iliyopitishwa na Bunge mwaka jana.

Kati ya Sh11trilioni, Sh6 trilioni zilitarajiwa kukusanywa kutoka vyanzo vya ndani vya mapato na kiasi kilichobaki kingetokana na fedha za wafadhili.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, John Haule, hivi karibuni alinukuliwa na vyombo vya habari akiwatoa hofu wananchi kwamba Serikali haina mpango wa kuwa na bajeti ndogo kukabiliana na hali hiyo.


Alisema Serikali inatarajia kuwa na mkutano wa kutathmini utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2010/11 ambao utatoa picha ya hali halisi ya uchumi wa taifa nchini.
 
Moja ya vitu ambavyo huwa sijielewi siwaelewi wenzangu wa-TZ ni sababu zinazotolewa kila kesi inapenda kinyume na matarajio! sababu hazikosekani. kuna kipindi SFO walitofautiana na Takukuru, kuna mengi yalisemwa yaliyoashiria kuwa SFO will do best of their job! leo kuna watu wanatoa sababu za kiu-chumi, sijui what what what!!! no one ever said they dont trust SFO, today majority will say they they dont trsut SFO simply because Chenge if 'free'!!

Kuna tatizo sehemu, what I believe the conducive place for criminals and all law breakers is jail!! if we have failed to address the issues that we have a problem in judiciary system, kuanzia mwendesha mashtaka wa serikali na majaji, we have a problem on who will initiate someone to be investigated whenever issues of immorals arises. Tunabaki tu EL, RA, Chenge, n.k!!! Ndiyo watu waliweka matumaini kuwa SFO will do better than our systems! we did confessed by our actions that our systems is nothing! yet we have received the very common games of laws world wide!
 
wakubwa naona mambo yanaanza kua magumu ila mwenye akili timamu lazima atajua jinsi ya kuchambua pumba na mchele, hapo kuna mchezo mchafu umefanywa na wazungu wakishirikiana na baadhi ya viongozi kupotosha ukweli, wao wanajua fika BA solution na akina Chenge walikua na dili fake na pia wanatambua hata akaunti ambazo pesa hizo zilifichwa lakini chaajabu leo mtu anakuja na kutoa facts kua habari hizo si za kweli, hapo wamepima faida na hasara ya kufuatilia na kuuweka wazi ukweli huo then wakagundua faida ni chache kuliko hasara.

Kwa mfano kama waki reveal ukweli na BA solution ikifungiwa lessen ya kufanya biashara watakao athirika si watanzania bali ni wao huko ulaya kuanzia mapato ya kodi pamoja na ajira kwa wananchi wao, pia SFO wameisha ona watanzania bado wapo kwenye giza nene na hawapo tayari kwa mabadiliko hivyo basi kama wakiendelea kufuatilia inshu hiyo watazidi kuharibu mahusiano mazuri kati ya makampuni yao na viongozi wa afrika ambao karibu woote ni mafisadi na wanafanya biashara haram ya silaha na madini kwa hao wazungu ambao ndio wanaofaidika zaidi.

mimi ukweli naujua na wala sidanganyiki najua chenge, mkapa, kikwete, somaiya, vithlan na wengineo walihusika kuanzia rada, ndege ya rais hadi vifaa vya kijeshi, inauma sana lakini sina jinsi ila naiombea nchi yangu mapinduzi ya kweli kama wanavyofanya wengine.
 
Kama hakukuwa na rushwa wasirudishe zile bilioni 21! wanazirudisha kwanini?

Lakini ruling ipi ifuatwe -- ya mahakama ya Uingereza iliyosema rushwa ilitembea au SFO ambao wamepata pressure ya serikali yao kutochukulia hili suala inavyotakiwa ili kulinda masilahi ya BAE yao? Chenge mwenyewe analielewa sana hili, anataka kutuizuga tu, anadhani siye ni mafala.

Na kwa nini mamlaka zetu zikubaliane na SFO katika kulindia masilahi ya BAE tukipuuza kulinda masilahi yetu ya kutokomeza ufisadi? Lakini kikubwa cha yote ni kwamba Wikileaks imetufumbua macho -- pale ilipomnukuu Hosea akisema kuna baadhi ya vigogo ambao serikali ya JK haitaki wakashitakiwa na mmoja wao ni Chenge. Hivi vijisababu vya sasa vya SFO -- imeona hivi au imeona vile ni ujinga mtupu.

Kwanza hivi serikali ilitoa tamko lolote kuhusu waliyosema Wikileaks kuhusu Hosea? Au iliuchuna tu, kama kawaida yake?
 
inawezekanaje mtu ambaye anatuhumiwa kwa ufisidi aitishe mkutano na waandishi wa habari aseme hahusiki . inashangaza sana mtuhumiwa kuwasemea shirika linalomchunguza hii ni kama issue ya ngeleja kuwasemea dowans kwamba lazima walipe kwa sababu wanashare kwenye hiyo kampuni. Hata watumie nguvu nyingi kujisafisha hawatabadilisha image yao kwa jamii-they are corrupt and i dont think if Tanzania needs them
 
wakubwa naona mambo yanaanza kua magumu ila mwenye akili timamu lazima atajua jinsi ya kuchambua pumba na mchele, hapo kuna mchezo mchafu umefanywa na wazungu wakishirikiana na baadhi ya viongozi kupotosha ukweli, wao wanajua fika BA solution na akina Chenge walikua na dili fake na pia wanatambua hata akaunti ambazo pesa hizo zilifichwa lakini chaajabu leo mtu anakuja na kutoa facts kua habari hizo si za kweli, hapo wamepima faida na hasara ya kufuatilia na kuuweka wazi ukweli huo then wakagundua faida ni chache kuliko hasara,
kwa mfano kama waki reveal ukweli na BA solution ikifungiwa lessen ya kufanya biashara watakao athirika si watanzania bali ni wao huko ulaya kuanzia mapato ya kodi pamoja na ajira kwa wananchi wao, pia SFO wameisha ona watanzania bado wapo kwenye giza nene na hawapo tayari kwa mabadiliko hivyo basi kama wakiendelea kufuatilia inshu hiyo watazidi kuharibu mahusiano mazuri kati ya makampuni yao na viongozi wa afrika ambao karibu woote ni mafisadi na wanafanya biashara haram ya silaha na madini kwa hao wazungu ambao ndio wanaofaidika zaidi.
mimi ukweli naujua na wala sidanganyiki najua chenge, mkapa, kikwete, somaiya, vithlan na wengineo walihusika kuanzia rada, ndege ya rais hadi vifaa vya kijeshi, inauma sana lakini sina jinsi ila naiombea nchi yangu mapinduzi ya kweli kama wanavyofanya wengine.
ndugu yangu aikuumi kama navyi umia mimi roho inaniuma sana juu ya hili tumuombe mungu
 
Chenge mwenyewe ndio ametangaza leo kupitia vyombo vya habari kwamba SFO wameona hakuna ushahidi wa Rushwa!! ajabu mtuhumiwa wa mkuu anasema hakuna ushahidi wa kumtia hatiani!! je kama ni hivyo hela zinarudishwa kwa ajili ya nini?!! ujinga huu.

Chenge siku zenu zinakuja na hakika mafisadi mtalia na kusaga meno huku mkijiuliza pakutokea wapi na hamtapaona!!
 
Mafisadi wa Tanzania mjiulize mubarak yuko wapi?!! je alivyoiba anavila sasa ama anaona vichungu?!! siku yenu yaja
 
Huu ni upuuzi wa hali ya juu sana. Kwanza anatakiwa awape watanzania jibu la swali la msingi kwamba akiwa Mwanasheria Mkuu kwanini alishindwa kuzuia ununuzi huo wa rada mbovu kwa bei isiyokua halali pamoja na mikataba mingine mingi feki iliyopitia ofisi yake wakati huo.

Kabla ya kujibu maswali hayo asijaribu kujisafisha na waandishi wahakikishe hayo ndiyo maswali ya kumtaka alieleze taifa. Kwanza anatakiwa pia ajibu kwamba kwanini anadhani serikali ya Tanzania haimchukulii hatua kwanini serikali yetu haioni umuhimu wa kulifanyia uchunguzi jambo hili ingoje SFO kutoa hukumu ni kwa manufaa ya nani? Au ya nchi gani?
 
Hello ALL, new here. But this post caught my attention. I am not fluent in swahili so may have not understood correctly what is stated in this post. However, I'd like to ask few questions in regards to Mr. Chenge:

1) Isn't he the one who appeared in a local newspaper and according to him a million dollars was vijisenti" (when he was asked about a million dollars being in his possession in an offshore account). If this is true then in a country where ppl are starving for the basic of human needs:food, clothing, housing, education, jobs etc..&in a country which hosted the freedom movements of Africa and gave Africa a humble, intelligent leader like Mwalmu Nyerere, this is a total shame for a government servant to say in public that a million dollars is just vijisenti to him). There is no justification for his words!!

2) Also, most of the TZ govt. contract scandals that have been making news for the past five years in the media, was it not the AG's role as legal govt. adviser to advice the govt? (am I missing something here?)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom