Serikiali na Mradi wa AIbino, JF Kazini...

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,232
8,429
Ni habari mbaya na kusikitisha kusikitisha kusiskia na kuona Ma albino wanaenedelea kuuawa ndani ya nchi yao wakati serikali inayopaswa kuwahakikishia ulinziikiwa haichukua hatua za ziada na makusudi kuwalinda.

Vitendo vya kikatili dhidi ya Ma albino vimekuwa vikiongezeka kila kukicha. Hapo tarehe 03/05/08 Mwananchi liliripoti kisa cha Vumilia Makoye mkazi wa kijiji cha Ilunga wilayani Magu kukatwa panga kisogoni na kisha kukatwa Mguu sehemu ya paja na wauaji hao kutokomea na mguu kusikojulikana.

Sidhani kama ikiwa wana jamii hawawatambua watu wanaotekeleza unyama huu, siamini kabisa ikiwa nguvu iliyotumia kumng'oa kanali Bacar visiwa vya Commoro inashindwa kutumika kuwang'oa makafiri hawa, haingii akilini kuona mfano wa mauji ya kimbali kama ya Rwanda yanatokea kwa kundi fulani la watu katika nchi ya Tanzania huku serikali ikishindwa kuchukua hatua kali na madhubuti ili kudhibiti.

Nashawishika kuamini kuwa, kuendelea kwa mauaji ya kundi hili la Ma albino serikali imeshindwa!!!!!!!! Kwani haitoshi tu kusema IMANI ZA KISHIRIKINA. Hawa wanaotekeleza mauaji haya tunawafahamu.

Hebu jaribu kusimama katika nafasi ya Vumilia Makoye ghafla watu wanakupiga Panga na kuondoka na Mguu wako. Hakika inauma sana. Hebu fikiria Ma alibino wengine wanaishi maisha gani kutokana na wimbi hili la kuwasaka na kuwa geuza deal.

Ikiwa serikali imeweza kukomesha ujambazi, kwa hili inatania.

Kutokana na hali hii nawaomba wana JF tujitokeze kuweza kuwasaidia ndugu zetu hawa Ma albino. Tuwataje kwa majina wapangaji, watekelezaji, mawakala, na wanunuaji wa viungo vya Ma albino. Naamini hapa JF hakuna linaloshindikana.

Kwa pamoja tutashinda.
 
Inawezekana ndugu kuna viongozi wetu ambao nao ni washirikina na ndio njia hiyo wanayoitumia pia
hili jambo ni jepesi sana kuweza kulimaliza, lakini hao viongozi wanaona kama kawaida tu na kujifanya wakiendelea kufumbia mambo huku wakidanganya kufuatilia kwa undani.

Inakuwaje serikali inashindwa na kijimtandao cha watu wachache kabisa??
Au wanataka kutuambia pia kuwa hili kundi nalo ukilimaliza linaweza kuitikisa serikali kama la Mafisadi??

Hii ndio Serikali yetu bwana chini ya Msanii mkuu, na ndio maana hata nyuki nao wameanza kukasilika na kumvamia!!!!!!

Mkuu,

Kila kitu ni viongozi tu, je na sisi wananchi tuna majukumu gani katika nchi yetu?

Huu ni uhalifu ambao lazima wananchi tuwajibike na kuwa tayari kuufichua.

Serikali peke yake haiwezi kukomesha ujinga huu mkubwa.

Nina jiuliza hivi miaka 44 ya uhuru, Watanzania imetusaidia nini? Ni kama sasa tunarudi kule kule ambako mwalimu alitutoa miaka ya 60.

Hivi kweli kuna watu wanafikiri kuua Watanzania wenzao kutawasaidia kwenye mambo yao?
 
mtanzania kama raia wa kawaida,hana sauti ktk tanzania ya leo,zaidi ya viongozi na mafisadi
 
Mkuu,

Kila kitu ni viongozi tu, je na sisi wananchi tuna majukumu gani katika nchi yetu?

Huu ni uhalifu ambao lazima wananchi tuwajibike na kuwa tayari kuufichua.

Serikali peke yake haiwezi kukomesha ujinga huu mkubwa.

Nina jiuliza hivi miaka 44 ya uhuru, Watanzania imetusaidia nini? Ni kama sasa tunarudi kule kule ambako mwalimu alitutoa miaka ya 60.

Hivi kweli kuna watu wanafikiri kuua Watanzania wenzao kutawasaidia kwenye mambo yao?

Ukiwa wewe ni kiongozi unatakiwa uwe kiongozi wa kila jambo. Ukikaa nyuma unaongoza nini, na tunapoongelea viongozi wa nchi tunamaanisha ni serikali. Kwa hiyo tunataka serikali tuone inafanya nini katika. Kukaa kimya na kufumbia macho ni kushindwa.

Serikali inapewa taarifa muhimu haitoi ushirikiano na wanawanchi ikiwa ni pamoja na kutowapa mshindo nyuma (Feedback. Wananchi wanavunjika moyo matokeo yake vitu vinaendelea kwenda kombo kama haya mauaji ya albino.

Kwa hiyo JF tuje ni mikakati ya kusaidia kumaliza tatizo hili. Napendekeza wananchi wapige kura za maoni kwa siri katika maeneo yote ambayo matukio haya yametokea kuwabaini mawakala na watekelezaji kwani haiwezekani watu watoke mbali kwenda kutekeleza unyama huu.

Hili likiachwa litakuja kuwa kama suala la wachawi kukatawa mapanga. Halina ufumbuzi hadi sasa. Bibi zetu wananendelea kuteseka.
 
............Kwa hiyo JF tuje ni mikakati ya kusaidia kumaliza tatizo hili. Napendekeza wananchi wapige kura za maoni kwa siri katika maeneo yote ambayo matukio haya yametokea kuwabaini mawakala na watekelezaji kwani haiwezekani watu watoke mbali kwenda kutekeleza unyama huu.

Hili likiachwa litakuja kuwa kama suala la wachawi kukatawa mapanga. Halina ufumbuzi hadi sasa. Bibi zetu wananendelea kuteseka.............

.......naunga mkono hoja
 
hapo kwa albino kuuwawa halafu juhudi zinazochukuliwa na serikali ndo hizo tena, kwasababu wao eti sio albino na wanalala nyumba salama, Kilio cha albino kitafika huko vingine vinakofikaga, na itakuwa tamu kwao pia.
Hapo sipo kabisa, ikiwa ufisadi unaadhibiwa hapahapa duniani, ole wao..!
 
Ni habari mbaya na kusikitisha kusikitisha kusiskia na kuona Ma albino wanaenedelea kuuawa ndani ya nchi yao wakati serikali inayopaswa kuwahakikishia ulinziikiwa haichukua hatua za ziada na makusudi kuwalinda.

Vitendo vya kikatili dhidi ya Ma albino vimekuwa vikiongezeka kila kukicha. Hapo tarehe 03/05/08 Mwananchi liliripoti kisa cha Vumilia Makoye mkazi wa kijiji cha Ilunga wilayani Magu kukatwa panga kisogoni na kisha kukatwa Mguu sehemu ya paja na wauaji hao kutokomea na mguu kusikojulikana.

Sidhani kama ikiwa wana jamii hawawatambua watu wanaotekeleza unyama huu, siamini kabisa ikiwa nguvu iliyotumia kumng'oa kanali Bacar visiwa vya Commoro inashindwa kutumika kuwang'oa makafiri hawa, haingii akilini kuona mfano wa mauji ya kimbali kama ya Rwanda yanatokea kwa kundi fulani la watu katika nchi ya Tanzania huku serikali ikishindwa kuchukua hatua kali na madhubuti ili kudhibiti.

Nashawishika kuamini kuwa, kuendelea kwa mauaji ya kundi hili la Ma albino serikali imeshindwa!!!!!!!! Kwani haitoshi tu kusema IMANI ZA KISHIRIKINA. Hawa wanaotekeleza mauaji haya tunawafahamu.

Hebu jaribu kusimama katika nafasi ya Vumilia Makoye ghafla watu wanakupiga Panga na kuondoka na Mguu wako. Hakika inauma sana. Hebu fikiria Ma alibino wengine wanaishi maisha gani kutokana na wimbi hili la kuwasaka na kuwa geuza deal.

Ikiwa serikali imeweza kukomesha ujambazi, kwa hili inatania.

Kutokana na hali hii nawaomba wana JF tujitokeze kuweza kuwasaidia ndugu zetu hawa Ma albino. Tuwataje kwa majina wapangaji, watekelezaji, mawakala, na wanunuaji wa viungo vya Ma albino. Naamini hapa JF hakuna linaloshindikana.

Kwa pamoja tutashinda.

Japo inauma ngoja tujikumbushe
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom