Serikalini viongozi wachokana - Mtendaji Kata amtunishia msuli DC - Dodoma

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
KATIKA hali isiyo ya kawaida Mtendaji wa Kata ya Nondwa katika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma,amemtunishia msuli Mkuu wa Wilaya hiyo, Betty Mkwasa. Hali ilitokea baada ya Mkwasa kuhoji ni kwa nini kata hiyo ya Nondwa haijachangia ujenzi wa shule ya sekondari na kusababisha watoto waliofaulu katika kata hiyo kupelekwa kusoma kata nyingine.

Mtendaji huyo, Yoram Ndahani baada ya kuhojiwa aliinuka na kujibu kwamba yuko tayari kuchukuliwa hatua yoyote kwani hakuwa na maelekezo ya michango ya namna hiyo. Hali hiyo ilifanya Mkuu wa Wilaya kuinuka na kumhoji kiongozi kwa nini anajibu jeuri kwani alikuwa na haki ya kuulizwa juu ya utendaji wake.

"Usipende kudharau wanawake, sizungumzi kama mwanamke nazumgumza kama kiongozi tena ni Mkuu wa Wilaya, lakini najua angekuja Mkurugenzi hapa usingemjibu hivi kwa vile anakulipa mshahara,” alisema Mkwasa na kuongeza: “Utambue kuwa hata huyo Mkurugenzi anaripoti kwangu na angekuwa kiongozi mwingine hapa wewe usingebaki hapa angeenda kukutupa mahabusu ujifunze namna ya kuzungumza na kumjibu kiongozi wako" .

Kutokana na hali hiyo, Ofisa Tarafa wa Kata ya Mpalanga Michael Mkunya aliomba radhi kutokana na kauli hiyo huku viongozi wa kata waliokuwepo hapo wakiomba radhi kutokana na kitendo hicho ambacho walikiita kisichopendeza.

"Kazi ya kiongozi ni kuelekeza, suala la msimamo linatupa shida kidogo kama ni suala la msimamo wa kisiasa ijulikane wakati mwingine anapofika kiongozi mkuu kubali kuelekezwa na
si kubishana," alisema Katibu Tarafa.
 
KATIKA hali isiyo ya kawaida Mtendaji wa Kata ya Nondwa katika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma,amemtunishia msuli Mkuu wa Wilaya hiyo, Betty Mkwasa. Hali ilitokea baada ya Mkwasa kuhoji ni kwa nini kata hiyo ya Nondwa haijachangia ujenzi wa shule ya sekondari na kusababisha watoto waliofaulu katika kata hiyo kupelekwa kusoma kata nyingine.

Mtendaji huyo, Yoram Ndahani baada ya kuhojiwa aliinuka na kujibu kwamba yuko tayari kuchukuliwa hatua yoyote kwani hakuwa na maelekezo ya michango ya namna hiyo. Hali hiyo ilifanya Mkuu wa Wilaya kuinuka na kumhoji kiongozi kwa nini anajibu jeuri kwani alikuwa na haki ya kuulizwa juu ya utendaji wake.

"Usipende kudharau wanawake, sizungumzi kama mwanamke nazumgumza kama kiongozi tena ni Mkuu wa Wilaya, lakini najua angekuja Mkurugenzi hapa usingemjibu hivi kwa vile anakulipa mshahara, alisema Mkwasa na kuongeza: Utambue kuwa hata huyo Mkurugenzi anaripoti kwangu na angekuwa kiongozi mwingine hapa wewe usingebaki hapa angeenda kukutupa mahabusu ujifunze namna ya kuzungumza na kumjibu kiongozi wako" .

Kauli ya Betty inaonesha hajiamini kabisa.
 
PHP:
"Utambue  kuwa hata huyo Mkurugenzi anaripoti kwangu na angekuwa kiongozi  mwingine hapa wewe usingebaki hapa angeenda kukutupa mahabusu ujifunze  namna ya kuzungumza na kumjibu kiongozi wako" .
Kauli mbofu mbofu hizi!...!
Ukiona raia wanakujibu hovyohovyo uanze kuhoji aina ya uongozi wako...Aidha hujiamini, au huna uhakika na unachoagiza na kufuatilia.
 
Wee mgogo, umeambiwa jina ni sawa na ng'ombe ili liwe la kwako peke yako? Kalisajili basi uwe na hati miliki nalo.


Hati miliki kwenye jina hailipi kwetu ugogoni. Kuna mambo mengine yenye kutuongezea vipato na heshima zaidi ya hati miliki kwenye majina. Ask tinga tinga
 
hivi vyeo vya makada wa ccm havina msingi wowote zaidi ya siasa za kupotezeana mda.
Naamini ni muda muafaka kufutiliambali cheo hichi cha ukuu wa wilaya kupitia rasimu ya katiba mpya.
 
hivi vyeo vya makada wa ccm havina msingi wowote zaidi ya siasa za kupotezeana mda.
Naamini ni muda muafaka kufutiliambali cheo hichi cha ukuu wa wilaya kupitia rasimu ya katiba mpya.

How many people would be job less? Wengine wanaishi kwa kuuza maneno sasa watayauzia wapi?
 
Mtendaji huyo, Yoram
Ndahani baada ya
kuhojiwa aliinuka na
kujibu kwamba yuko
tayari kuchukuliwa hatua yoyote kwani hakuwa na maelekezo ya michango ya namna hiyo.

Mbona sioni tatizo kwenye majibu ya huyu mtendaji, kama hakuwa na maelekezo walitaka afanyaje?
 
huyu betty hata udom mgomo wa 2010 tulimkataa mpaka msekela na yy pia.hajiamin anatoa majbu mepec kwa hoja nzto zenye mashkoa.yan majbu ya zaman kwa maswal mapya
 
How many people would be job less? Wengine wanaishi kwa kuuza maneno sasa watayauzia wapi?

Solution ya jobless iko mikononi mwa jobless;
Mkemia asiye na ajira atafungua kiwanda cha gongo,
Mwanasheria asiye na ajira atashiriki organized crime officialy kama ajira per se,
mkunga asiye na ajira atafungua ofisi ya kutoa mimba near by secondary schools,
mwanasiasa asiye na ajira atafungua kanisa lake,
Kwa mfano wa karibu tazama documentary hii ya MUNGIKI jirani zetu kenya na wasomi wasio na ajira.[video]www.youtube.com/watch?v=P-51vhFC1eM[/video]
 
Kwani huyu mtendaji wa kati alisema anamjibu hivyo kwasababu ni mwanamke au kwasababu alikuwa ana taarifa au maelekezo ya hiyo michango...nadhani tuache uoga wa kijinga na kutojiamini.Jibu la mtendaji lilikuwa sahihi kabisa,kuwa sina taarifa.
 
[/COLOR]Hati miliki kwenye jina hailipi kwetu ugogoni. Kuna mambo mengine yenye kutuongezea vipato na heshima zaidi ya hati miliki kwenye majina. Ask tinga tinga

Mbukwenyu! Usilalamike basi Ndahani zikiwa nyingi.
 
Kashazoea kudanganywa...... mkuu bado tunaendelea na mchakato.....mkuu upembuzi yakinifu haujakamilika......mkuu tutatoa taarifa rasmi..... mkuu mi sio msemaji.....

Ndo majibu yanayowapendeza wakuu wetu haya......hata kama ni invalid ones

Keep going Ndahani na kwa sababu umemwambia uko tayari kwa lile tishio kuu ndo mana akakuacha hureeeeeeee
 


"Usipende kudharau wanawake, sizungumzi kama mwanamke nazumgumza kama kiongozi tena ni Mkuu wa Wilaya, lakini najua angekuja Mkurugenzi hapa usingemjibu hivi kwa vile anakulipa mshahara," alisema Mkwasa na kuongeza: "Utambue kuwa hata huyo Mkurugenzi anaripoti kwangu na
angekuwa kiongozi mwingine hapa wewe usingebaki hapa angeenda kukutupa mahabusu ujifunze namna ya kuzungumza na kumjibu kiongozi wako" .


Kutupwa mahabusu kwa kujibu swali? Camon Betty, are you referring North Korea or Tz?
 
“Utambue kuwa hata huyo Mkurugenzi anaripoti kwangu na angekuwa kiongozi mwingine hapa wewe usingebaki hapa angeenda kukutupa mahabusu ujifunze namna ya kuzungumza na kumjibu kiongozi wako" .

Tangu lini DED akaripoti kwa DC? DED anaripoti Ofisini kwa Waziri Mkuu.
 
Back
Top Bottom