Serikali yetu na majumba ya kifahari!

babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
5,221
3,166
P1030775.JPG


P1030784.JPG

Spika akiwa anakagua ujenzi wa makazi yake mapya ambayo yanajengwa kwa kodi zetu.


wodi.jpg

Hii ni hali katika hospitali zetu.Baadhi ya walipa kodi wakiwa wamelala au kukaa chini kutoka na uhaba wa vitanda na viti,sehemu ya pesa zao ndio zinatumika kujenga majengo ya kifahari.

Mwanzoni mwaka huu kama sio mwishoni mwa mwaka jana watu wengi walipiga kelele kuhusu kiasi cha pesa kilichotumika kujenga makazi ya gavana wa benki kuu.Baadhi yetu tuliamini serikali itaanza kujirekebisha kutoka na kosa hilo hasa baada ya kuwa waziri mkuu anayejulikana kama “mtoto wa mkulima” ambaye mara nyingi amekuwa akituashiria hapendi makuu.Sasa jumba la kifahari kama hili linajengwa on his watch, tutaanza kuona hata hiyo ya kukataa magari ya kifahari ni kujitafutia umaarufu wa kisiasa.
 
Inatia hasira kweli hapa sijui tataambiwa bilioni ngapi jmn,
kwa mtindo huuu wacha tubebe mabox tuu
 
6362196.jpg

Hii ni nyumba ya Gavana wa benki kuu kati ya nyumba mbili zilizo gharimu bilioni 5.7,ilizuwa manunguniko mengi kutoka kwa wananchi kutoka na gharama kubwa kupita kiasi.
 
6362196.jpg

Hii ni nyumba ya Gavana wa benki kuu kati ya nyumba mbili zilizo gharimu bilioni 5.7,ilizuwa manunguniko mengi kutoka kwa wananchi kutoka na gharama kubwa kupita kiasi.


WHAAAAAAATTTTTTTTTT!!! 5.7 BILLIONS!!!! this is crazyyyyyyyy
 
Do you think kwa nini huwa tunatukanwa kuwa ni MONKEYS?
Ni matendo kama haya!
Hasa viongozi wetu ,hawana aibu kabisa.

Huyo Spika mwanamke,labda atembelee pale Temeke hospital ,kama Naomi Campbell alivyfanya,may be umonkey utamtoka
 
Inatia hasira kweli hapa sijui tataambiwa bilioni ngapi jmn,
kwa mtindo huuu wacha tubebe mabox tuu
Ni kweli kabisa.Ubaya sio tu pesa zinazo chakachuliwa, pia inakatisha watu tamaa ya kufanya kazi kwa bidii kwa kuamini bila ufisadi hauwezi kufanikiwa.
 
Hivi Sita alikuwa anaishi hotelini au???
Kama sijakosea aliishi hoteli kwa muda halafu wakamkodishi nyumba ya bei mbaya,Hii yote kwa sababu kuanzia juu mpaka chini kumeoza.Unajua kuna baadhi ya wizara kama mkuu akibadilishwa, huyo mpya ana nunua gari jipya hata kama lililokuwa linatumika alikununuliwa muda sio mrefu?
 
Inatia hasira kweli hapa sijui tataambiwa bilioni ngapi jmn,
kwa mtindo huuu wacha tubebe mabox tuu
e bana nambie basi unabebea box lako wapi nije nikusaidie huko uliko,jua la bongo na politiko +ufisadi vimenichosha:A S crown-1:
 
Hivi Sita alikuwa anaishi hotelini au???
mshasahau kwamba ni juzi tu hapa tulikua tunajadili juu ya mabilioni yaliyotumika kujenga jumba jipya lenye hadi ya spika sitta.?leo hii huyu mama nae anajengewa la kwake.mweeeeh
 
Nyumba zote wameuziana bado pale magogoni... siku CDM wakiingia wataambiwa wajenge yao maana itakuwa ishauzwa!!
 
Then wanatuambia Vijana taifa la kesho.......Huu ni upuuzi mkuu, I dont no why wanaowalinda bado wanaendelea kuwalinda. Ukiangalia Polisi, magereza Mishahara yao ni Mibovu kupita kiasi ila hao Polisi wakisikia kuna maandamano bado wanaenda kuwapiga watu ambao hata wao watawakomboa....Sijui wamelishwa sumu gani??? sijui wameridhika na nini??? When is turning point Day??? Kila kitu kimeshauzwa nchi hii... I guess hata sisi wananchi tumeshauzwa ila hawajaanounce officially.
 
Msekwa na Sitta walikuwa wanaishi wapi?
Msekwa anaishi nyumba zilizouzwa za serikali, Makinda hawezi kum replace humo.

Sitta alikuwa akiishi hotelini kwa muda akiwa spika wakati nyumba ya spika inajengwa, sasa imekwisha. (Yeye hakuwahi kununua nyumba za serikali, alikuwa ashatoka serikalini wakati zinauzwa).

Kwa kuwa Waziri anapewa nyumba, Serikali imeshindwa kumtoa Sitta ili Makinda aingie kwenye nyumba ya spika, ambayo ilitakiwa iwe ya spika tu, kwa hiyo inajengwa nyingine ya Makinda!

all this boneheaded bullshit by our government is done in our name
 
Msekwa aliuziwa nyumba ambayo ilibidi kila spika awe anakaa (kama ikulu ya bunge),alipokuja sitta akawa hana nyumba ya kukaa akapangishiwa nyumba masaki akawa analipiwa $7,000 (kama 12M) kwa kwa mwezi kukaa humo,naona saiv ndo wameamua kujenge nyumba nyingine ya spika ambayo itakua permanent. Me loving Tanzanian politics jmn watu wanaiba mpk takataka
 
Back
Top Bottom