Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Heshima mbele wazee,

Na hasa Mzee Lunyungu, tuliza boli tunalifuatilia kwa makini hili suala na hivi karibuni nitatoa taarifa yangu rasmi, on this ishu!

tunajaribu kuepuke kupayuka payuka, bila facts, ili ku-keep up na heshima ya hii forum!

Ahsante!
 
...kama anamtetea balozi,labda. ila,we subiri uwe balozi halafu utayaona[mi sijawahi kuwa]....balozi si mungu kazi'utu! kuna anayoweza na mengine huwa mazito kwake.

si kazi tukasikia wamepelekwa moscow naye ndiye aliyeomba au fanikisha iwe hivyo.

Kama ni mimi ndiyo Balozi nisingeweza kuona Wananchi wezangu wanapata tabu kwa kisingizio cha Hakuna Fedha ningeweza kutafuta njia yoyote Kuhakisha wanapata Mahitaji muhimu kama chakula na malazi (wangekula kile ninachokula mimi na wangelala pale ninapolala mimi)na kutafuta uwezekano wa kuwarudisha nyumbani kwa njia yeyote ile wakapambane na Bodi ya mikopo huko.Ningewachukulia kama raia wenzangu waliopata shida nchi ya watu na mimi kama Balozi hilo ni moja ya jukumu langu kuhakikisha raia mwenzagu hawapati shida kwenye Nchi za watu.
 
Mzee Mwanakijiji,
Vipi ikiwa kuna simu toka kwa wabinafsi wa Tanzania imeshawatangulia Kiev?..
 
Mkandara, hiyo simu haitaathiri wao kwenda ubalozini, kwani wamenunua tiketi ya kwenda tu.. hawarudi tena shuleni hadi serikali aidha itoe guarantee ya wao kuendelea na masomo, au kuwarudisha nyumbani waendelee na masomo (vyuo gani???). Mtamsikia wenyewe Prof. Msolla akiwaruka wanafunzi hawa na kusema kwa ujasiri kuwa walienda huko kivyao vyao wakati ushahidi wa barua n.k sasa hivi uko mikononi mwangu... barua za tangu kwenda kuomba visa, barua toka vyuo hivyo kuahirisha msimu wa masomo n.k... Muda wa kuburuzwa na serikali yetu wenyewe umepita!! I'm doing my part (exposing this) natumaini na wengine watafanya kazi zao (call for Msolla's, Mama Katunzi's, Nyatega's etc resignations). Vingenevyo itakuwa ni sikio la kufa....
 
Matukio ya aina hii yanasikitisha, yanaudhi, yanakatisha tamaa, yanaaibisha.......

Ni matukio ya aina hii ndio yanayopelekea wakati mwingine mtu kuanza kujiuliza maana ya uTanzania ni nini. Lakini tunaelewa kuwa ubovu katika uongozi wa nchi sio ubovu wa utaifa wenyewe.

Hakuna sababu yoyote ile inayoweza kuwa justification ya tendo hili la aibu kubwa sana katika historia ya taifa la Tanzania. Hivi kweli rais wetu baada ya aibu hii anaweza tena kutembea kifua mbele kati ya viongozi wenzie wa kimataifa?

Hata kama serikali haikuwa na uwezo wa kifedha kuwasaidia vijana hawa, angalau hata hiyo ya kuwarudisha nyumbani tu, lilikuwa ni jukumu la serikali yenyewe kufanya mipango ya kutatua tatizo hili kwa njia yoyote ile, hata kama ni kuomba msaada wa huo ubalozi wa Uingereza uwasaidie kuwarudisha vijana nyumbani, kuliko kuwatelekeza hivi hivi tu kana kwamba hawana taifa. Kwa njia hii sasa aibu ya taifa na serikali itatapakaa dunia nzima.


Hata kama kosa ni la vijana
 
Kalamu kama wangetaka kuwarudisha wangewarudisha... vijana wametoa malalamiko yao hadi Ikulu (nakala za barua zipo)...
 
I hope JK ataliona hili na kulifanyia kazi!.. nakumbuka wakati akiapisha hawa mawaziri aliwaambia kuwa - Hana Ubia na mtu!.. sasa ni wakati wa kuwaonyesha wananchi kweli hana ubia na mtu.
 
Mkandara... matamanio ni kitu kibaya sana kwani yasipotimizwa mioyo ya watu huvunjwa. Watu wametumaini mengi kweli kuhusu serikali yetu na matamanio hayo yamebakia kama mtu mkinga maji ya mvua huko jangwa la sahara!! Hata hivyo mvua hunyesha kila baada ya miongo kadhaa...
 
mwanakijiji

Hongera,

Pili, swala hili limekuja wakati muafaka na tukio la chuo kikuu, kwani hata hao wa UKraine wako kwenye bodi ya mikopo.

Kunajitihada zozote za kulifanya hili swala lionyeshe picha kubwa zaidi? Kuunganisha na wale wanafunzi wa dar? Kama inawezekana wanafunzi wa dar walitolee tamko hili!!
 
Mwanakijiji, natumaini umefanya ila natoe angalizo tu. ili kupata lengo ulilolisema, natumaini ulishaongea na watu wachache nyumbani kutandaza uozo huu na muhimu kabisa wewe na nguvu ya kumwambia ama kumshauri muungwana a way forward....
 
Ninamfahamu Professor Msola personally tangu akiwa Dean wa Faculty of Veterinary Medicine pale SUA. Sikujua kuwa anaweza kuwa mtu arrogant namna hiyo. Kitendo cha yeye kukata simu makusudi kutoendelea na swala hilo la wanafunzi inaonyesha jinsi alivyolidharau na kulipuuza. Nadhani ni afadhali arudi kwenye kazi ya chaki tu, anaiweza sana. Lakini hii ya kuongoza wizara nadhani haiwezi kabisa.
 
Je na hawa ni wajinga na wazembe kama mlivyo waita wa UD? Maana watu wengine humu walijifanya kukandia UDSM sasa hapa waje watuambie je na hawa nao ni wazembe na wajinga? Serikali inakwepa wajibu wake kama kweli iliwapeleka huko inawajibu wa kuwasomesha na kugharamia kila kitu. Tumeona wanafuzi 56 mlimani wamesimamishwa masomo watu wako kimya na hii ni hihi Body ya mipoko noo sorry I mean ya mikopo. Wanatutia aibu sana sasa vijana wetu wa UDS walikuwa ombaomba na kuuza miili yao kwasababu ya Body ya mikopo. Sasa hivi tunashuhudia wengine wanakuwa wakimbizi ugenini kwa sababu ya hii hii body. Something is wrong with this body watu wawajibishwe hatuwezi kwenda hivi. Ila ili hili liwe na sauti na nguvu inatakiwa iunganishwe na UDSM na hilii linamaanisha wale wanafunzi wa UDSM walionea nii ni ishara wazi kabisa.
 
kama wameomba ukimbizi nawaunga mkono.na hiyo ni basic human right yao afterall serikali yetu imeshindwa kuwatimizia kama katiba yetu inavyosema
 
I hope JK ataliona hili na kulifanyia kazi!.. nakumbuka wakati akiapisha hawa mawaziri aliwaambia kuwa - Hana Ubia na mtu!.. sasa ni wakati wa kuwaonyesha wananchi kweli hana ubia na mtu.
Mkandara!
Huyu JK naye ni Mhusika hivi hata kama wasaidizi wake ikulu waliofikishiwa hizo barua hawakuwajibu vijana au kutatua tatizo lao yeye kama Rais wa Nchi amelipokeaje hili?Hivi Mkandara wewe upo nje Lakini unaelewa nini kinaendelea inakuwaje Rais wa Nchi ashindwe kuelewa nini kinaendelea,kwani kuwa Rais Hakukufanyi ushindwe kutafuta habari mbali mbali kupitia vyanzo vyako visivyo rasmi ikiwemo kupitia magazeti,TV na Redio ,Kwani kuna mengine kupitia vyombo hivi yana ukweli na hawa vijana walishapeleka malalamiko hata kupitia vyombo vya Habari hivi tuseme JK hakuyasoma hayo au Ndiyo yale yale ya Kudharau wananchi wao.
 
Hiyo ndio falsafa ya ANGUKA Ari Nguvu na Kasi. kuna barua inasambazwa inasemekana ietoka kwa mwl. ni vyema mkafanya jitihada mkaipata walau ninaweza kuwafanya nyuso zenu zitabasamu kwani kila kukucha huwa tunajadili matatizo yanayosababishw na hawa watawala wetu wasiotujali sisi wana wa nchi hii na badala yake wanawajali wageni na kuwakumbatia siku hadi siku.
 
siku zote habari ambazo haziwafurahishi wasaidizi wake,maranyingi huwa hawapendi bosi wao hazipate.jaribuni tu kufikiri kwente ngazi ya familia tu.kuna vitu huwa vinafanywa na watoto,mke,au mume lakini vikawa gunzo mtaani lakini katika familia likawa siri yaani baadhi yao kutojua kabisa nini kinaendelea kati yao.
 
Back
Top Bottom