Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Wanafunzi hao walikwenda Ukraine kwa udhamini wa serikali au ki vyao?

....ndio wakaomba mikopo kama wengine. sasa,nadhani hoja hapa ni kutelekezwa.

kuhusu huyo balozi kama niliyaelewa vizuri maelezo...ni kuwa kashasaidia sana,kikomo kikafika!

mengine sijui!
 
Poleni waungwana wa Kiev. Ile hebu tupambanue issue kwanza, hawa wanafunzi wana documentary evidence to back up their claims? au wanataka wasaidiwe kwa hisani na huruma?. Maana inawezekana serikali ikasema haiwatambui ikiwa kweli na vigezo. Je walisign mikataba ya kupewa pesa za mkopo?, Mbona serikali ilisema jamaa walinyimwa mkopo wakaamua kwenda kwa kung`ang`aniza? wakuu tuwe makini sana!!! I have been a student I know how life is and indeed I was in Kiev last time..bila pesa hapafai...I agree. But MKJJ kama unawezo jaribu kutafuta nyeti za ndani ujue uhalali wa haya madai ya waungwana huko Ukraine na tuanze kujenga hoja huku tukijua kwamba we are supported by facts and laws and not rhetorics. Mi siamini kama Msollwa anaweza kuwa na hii jeuri kama kweli wanafunzi walisign mikopo na wana madai halali-possibility ni kwamba wanafunzi walitumia shortcut kwa kuambiwa nendeni pesa zitakuja bila maandishi yoyote! Na hapo ndo issue inaanzia, huwezi kuwa na argument kama in the first place huna vigezo. It may sound absurd, but knowing my country, ni vema tuwe tunaangalia haya mambo kwa upeo mpana saaaaana. Tusipenda kugeneralize mambo

Kwa hiyo MKKJ mi ningekushauri utafute wandani wa bodi pale Dar ujue the other side of the story from rank and file officers ambao sio KATUNZI NA KABAKA. Maana niliona tangazo la scholarship za kwenda Eastern Europe recently zikitangazwa na serikali..nilishtuka..kama masharti niliyoyaona ndo yalitumika kwa hawa jamaa basi wameliwa na sisi humu tutakuwa tunapiga kelele za nje ya mlango ambazo hazitamzuia Chitalilo kuuchapa usingizi.
 
Tangu nizaliwe na kuifahamu dunia hii sijawahi kusikia jambo linalotia aibu kama hili. Kwa maana nyingine, watoto wetu huko Ukraine sasa ni "wakimbizi" wa ubalozi wa UK. Hivi ni balozi gani anayewakilisha serikali ya Tanzania huko Ukraine.

Maswali mengi sana yanaibuka kichwani mwangu.

(a) Je serikali ya UK kupitia ubalozi wake imeahidi kuwasaidia lolote?

(b) Watoto wale walipolia sana kuhusu shida yao miezi kadhaa iliyopita, je serikali yetu ilichukua hatua gani?

(c) Kwa mlolongo huu wa serikali kuwanyanyasa wanafunzi wa kitanzania walioko Tanzania pale pale na walioko nchi za nje, je serikali hii kweli ina mkakati wowote wa kuwaendeleza watanzania kielimu?

(d) Nini sera ya elimu kwa Tanzania?

(e) Hivi kweli watoto wa viongozi wakubwa wa Tanzania wanasomea kwenye manyanyaso ya aina hii hii? Najua mimi niliwahi kusoma na mtoto mmoja wa Nyerere na watoto wawili wa (Aboud) Jumbe pale Tabora Boys', ambapo mtoto wa Kawawa naye alikuwa pale Tabora Girls'; je, kweli leo bado kuna watoto wa viongozi wanasoma katika mazingira haya wanayosomea watoto wengine?
 
kanda2, walienda kwa udhamini wa serikali wakiahidiwa kuwa fedha za malipo ya masomo zinawafuata nyuma. Walipofika Ukraine, serikali ikabidili utaratibu mzima wa mikopo na hivyo hao vijana wakajikuta kama watu walioachwa uwanja wa ndege na kujikuta nchi waliyotoka imepinduliwa na kupewa jina jingine na wao wenyewe wakajikuta hawana nchi (Tom Hanks ring a bell?).

Sasa serikali ikawa inaendelea kuwaahidi kuwa inashughulikia matatizo yao na mwishowe wameamua kuwakana waziwazi. Leo ni mara ya kwanza on record Waziri amesema hawawatambui wanafunzi hao.
 
Mzee Kichuguu unanikumbusha mbali,wakati huo Shule zile zilikuwa zinaitwa Warsar na Berlin, sina shaka ni wakati wa Msaki (RIP) na Ndeki (RIP).Nilikuwa nataka kukutaarifu tu kuwa Balozi wetu huko ni Patrick Chokala!Heshima mbele Mzee.
 
Alirudi Tanzania Kuomba Kura na Yeye ya Kutuongoza!
 
Balozi Chokala amefanya kila awezalo na wiki iliyopita amebakia kusema "mwombeni Mungu". Mikuki, wanafunzi 29 wote waondoke nyumbani kwa ahadi ya mdomo tu...? ingekuwa mmoja ningesema inawezekana. Vipi kuhusu wanafunzi wa Cuba ambao nako kwenye situation kama hiyo? Vipi wale wa Urusi ambao wanaishi kwa kubangaiza wakipewa dola 200 kwa mwezi (ikilipia chakula, mavazi, dawa n.k). Malipo ambayo ya mwisho yamepokewa mwezi uliopita na sasa wameletewa barua kuwa hakuna malipo mengine hadi mwezi wa tisa? miezi hii minne wataishi vipi?
 
Mwawado, kweli, nilikuwa pale TS enzi za Warsaw na Berlin wakati wa Msaki (RIP), Kusila, na Ndeki (RIP). Elimu ilikuwa inatolewa kwa watoto wote bila kujali uwezo wa wazazi wao.

Mwanakijiji, unasema balozi Chokala kawasaidia watoto wale hadi yeye mwenyewe kashindwa. Je aliposhindwa anafanya nini? na je ataweka wapi uso wake kuona kuwa watoto wa kitanzania ni ombaomba kwenye ubalozi wa UK huku waliahidiwa na serikali kuwalipia huko. Najua mimi miaka miwili iliyopita kuna ndugu yangu mmoja alipata mojawapo ya skolaship hizo, nikamzuia na kumtafutia shule nyingine kwingineko; nilikuwa na wasiwasi huu huu.
 
Cha ajabu nini hasa hadi tunafikia kutafuta kuitetea serikali!....
Je, sio serikali hii pia iliyowaahidi wnafunzi wa vyuo vyetu vikuu kuhusu gharama za ada hapa nyumbani?. Na leo hii kuna baadhi yetu wanasema mgomo wao haukuwa halali...Yaani kiini cha yote kinatupwa pembeni hali
Budget ya mwaka imetumiwa vibaya kuzidi makadirio kwa kiwango kikubwa sana na ajabu moja wapo ya matumizi sio ELIMU.
hawa viongozi wafanye nini hadi kuwaonyesha wananchi kuwa tuna viongozi bomu? nashangaa hata ofisi ya rais wanakuwa na maswali kama haya na kudai ushahidi wakati ushahidi upo mikononi mwao....
Je, inapotekea mauaji, ni jukumu la mfiwa kutafuta ushahidi at the crime scene ama ni kazi ya crime investigator!
 
kichuguu... Chokala hadi alienda hadi kwenye hivyo vyuo ndio wakawaacha waendelee kusoma hapo.. na akatoa dola 50 kwa kila mwanafunzi toka mfukoni mwake???. Serikali ikaahidi itatuma ujumbe ufike kule kabla ya Mei Mosi mwaka huu kupitia Urusi na baadaye Ukraine, taarifa ya ziara hiyo imefutwa na sasa serikali wanasema hawawatambui.. period.
 
kama vile nimeona mtu ameongelea namna watoto wa baba wa TAIFA walivyosoma tabora boys..na wa kawawa pale tabora girls...

sikuhizi hiyo ngumu ...hembu mliopo hapo UK tuambieni maisha anayoishi RIZ...nasikia hiyo apartment anayokaa ipo kiwango si mchezo..rent ya mwezi ingeweza kuwalipia pesa ya kujikimu hao walalahoi vijana wetu 28 hapo kiev...

kuhusu vijana kwenda ubalozi wa uk wako right ..angalia passport yako utaona wameandika kama mtanzania utakuwa mahali ambako ubalozi wetu haupo[ukraine upo lakini hauna msaada]...ukipata tatizo unaweza kuripoti ubalozi wa united kingdom[someni passport zenu.....
hawa watoto walipelekwa na serikali...uhakika huo pia ninao..wako wanaosomeshwa na wazsee wao na hao inawezekana sio miongoni mwao...kwani idani ya wanafunzi wetu pale pamoja na wanaojilipia ni wengi zaidi.....aibu..aibu,,..aibu!!!!!!
hao kama hawatalipiwa bora waombe ukimbizi..you know what ,kale kauhuru kanapotea sasa..kama hawa hapa wamegoma wanaambiwa wakaape kwa WAKILI hawa ambao jk atasema wamemuaibisha atasema wakaape kwa nani...au wakaape kwenye KABURI LA BABA WA TAIFA ,BUTIAMA!!!!!

Nashauri next time watoto ...wawe wanaenda at least once Kuandamana kutembelea kaburi la baba wa TAIFA kumlilia na kumuimbia ule wimbo maarufu...
"kama sio juhudi zako nyerere ,kama sio juhudi zako nyerere ,kama sio juhudi zako nyerere ...na kikwete angesoma wapiiiiiiii""""" nafikiri kama sio shule jk angekuwa mvuvi mmoja tu kati ya wavuvu au wakwevi..au mgemaji wa tembo .,pale bagamoyo ...au msaidizi pale mlingotini...
sio kwamba natania kama sio nyerere wengi wetu tungekuwa pia wachunga ndama au mbuzi au kwa bahati ngombe.....tumesahau????!!
 
Balozi Chokala amefanya kila awezalo na wiki iliyopita amebakia kusema "mwombeni Mungu". Mikuki, wanafunzi 29 wote waondoke nyumbani kwa ahadi ya mdomo tu...? ingekuwa mmoja ningesema inawezekana. Vipi kuhusu wanafunzi wa Cuba ambao nako kwenye situation kama hiyo? Vipi wale wa Urusi ambao wanaishi kwa kubangaiza wakipewa dola 200 kwa mwezi (ikilipia chakula, mavazi, dawa n.k). Malipo ambayo ya mwisho yamepokewa mwezi uliopita na sasa wameletewa barua kuwa hakuna malipo mengine hadi mwezi wa tisa? miezi hii minne wataishi vipi?
mwanakijiji!
Usimtetee Balozi Chokala,Kwanini yeye ameshindwa kuwasaidia raia wake ugenini hata kwa chakula hata kuwapa malazi pale ubalozini moscow ktk hali ya kishida hivyo hivyo na kibinadamu,wanafunzi hao wa kitanzania na hatimaye wakasaidiwe kwenye Ubalozi wa kigeni.Jibu la Kwamba waombe mungu si Jibu makini kwa mtendaji kwani yeye ni sehemu ya kutoa msaada kwa jamii anayoingoza,Mungu tunamuomba kwa wale tunaoamini hivyo Lakini yeye kama mwakilishi wa Nchi amesaidia vipi kuhakikisha wananchi wake wanapata angalau huduma ya Mlo na Malazi.Hivi wangekuwa wanae wa Kuzaa angewajibu jibu la namna hiyo na kumwaga manyanga?Nini faida ya nchi kuwa na Balozi Nchi Nyingine ikiwa haiwezi hata kusaidia Raia wake wanapofikwa na shida na kuhitaji msaada?
 
...kama anamtetea balozi,labda. ila,we subiri uwe balozi halafu utayaona[mi sijawahi kuwa]....balozi si mungu kazi'utu! kuna anayoweza na mengine huwa mazito kwake.

si kazi tukasikia wamepelekwa moscow naye ndiye aliyeomba au fanikisha iwe hivyo.
 
sasa hivi nazungumza na kiongozi wa msafara wakiwa ndani ya treni kuelekea Kiev... safari ya karibu masaa 10 hivi.... stay tuned...
 
kama vile nimeona mtu ameongelea namna watoto wa baba wa TAIFA walivyosoma tabora boys..na wa kawawa pale tabora girls...

sikuhizi hiyo ngumu ...hembu mliopo hapo UK tuambieni maisha anayoishi RIZ...nasikia hiyo apartment anayokaa ipo kiwango si mchezo..rent ya mwezi ingeweza kuwalipia pesa ya kujikimu hao walalahoi vijana wetu 28 hapo kiev...

kuhusu vijana kwenda ubalozi wa uk wako right ..angalia passport yako utaona wameandika kama mtanzania utakuwa mahali ambako ubalozi wetu haupo[ukraine upo lakini hauna msaada]...ukipata tatizo unaweza kuripoti ubalozi wa united kingdom[someni passport zenu.....
hawa watoto walipelekwa na serikali...uhakika huo pia ninao..wako wanaosomeshwa na wazsee wao na hao inawezekana sio miongoni mwao...kwani idani ya wanafunzi wetu pale pamoja na wanaojilipia ni wengi zaidi.....aibu..aibu,,..aibu!!!!!!
hao kama hawatalipiwa bora waombe ukimbizi..you know what ,kale kauhuru kanapotea sasa..kama hawa hapa wamegoma wanaambiwa wakaape kwa WAKILI hawa ambao jk atasema wamemuaibisha atasema wakaape kwa nani...au wakaape kwenye KABURI LA BABA WA TAIFA ,BUTIAMA!!!!!

Nashauri next time watoto ...wawe wanaenda at least once Kuandamana kutembelea kaburi la baba wa TAIFA kumlilia na kumuimbia ule wimbo maarufu...
"kama sio juhudi zako nyerere ,kama sio juhudi zako nyerere ,kama sio juhudi zako nyerere ...na kikwete angesoma wapiiiiiiii""""" nafikiri kama sio shule jk angekuwa mvuvi mmoja tu kati ya wavuvu au wakwevi..au mgemaji wa tembo .,pale bagamoyo ...au msaidizi pale mlingotini...
sio kwamba natania kama sio nyerere wengi wetu tungekuwa pia wachunga ndama au mbuzi au kwa bahati ngombe.....tumesahau????!!

Hizo pasi zimeandikwa hivyo lakini huo mkataba ulishakufa siku nyingi Labda kama wameweka makubaliano tena.nakumbuka kuna mwaka kuna jamaa wakitanzania walikwama Lebanon kwaajili pasi zao zilikuwa zikikaribia kumalizika muda walienda ubalozi wa uingereza kama pasi zilivyoandikwa walielezwa kwamba huo mkataba ulikuwa wa muda tu baada TZ kupata Uhuru Lakini kwasasa ulikwisha muda.Cha Ajabu TZ waliendelea kutoa kila pasi mpya na zilizofuatia na maelezo hayo.Na Hata kwenye hizo pasi wameelezea kujiandikisha au kujiorodhesha kwenye hizo Balozi za UK kama kutakuwa hakuna Ubalozi wa TZ.Lakini vijana wamenda pale si kwasababu hiyo wameenda kwasababu ya kuomba msaada wa kijamii kutokana na shida wanazozipata kutokana na serikali kutowajibika ipasavyo.
 
sasa hivi nazungumza na kiongozi wa msafara wakiwa ndani ya treni kuelekea Kiev... safari ya karibu masaa 10 hivi.... stay tuned...
Waambie wafanye kweli sio wafike pale wakipewa mlo na kupangashiwa hotel au hosteli na visenti kidogo waone wamefika Lazima wawatumie hawa wazee kuwafundisha uongozi wetu nini wanatakiwa kufanya kwa wananchi wao.
 
Aisee machozi yananitoka kabisa nikijiaribu kujenga taswira ya adha walizopata watoto hawa huko waliko; Mungu awasidie huko waliko.
 
Aisee machozi yananitoka kabisa nikijiaribu kujenga taswira ya adha walizopata watoto hawa huko waliko; Mungu awasidie huko waliko.
Amesikia vilio vyao.............................Huoni Balozi wa Uingereza Hakuweka Ngumu! Kwani siku zote hamtupi mja wake ni sisi waja huwa kuna wakati hasa wa raha tunamtumikia shetani..............tunajisahau!
 
Aisee machozi yananitoka kabisa nikijiaribu kujenga taswira ya adha walizopata watoto hawa huko waliko; Mungu awasidie huko waliko.

Nadhani ushauri-nasaha kama huo pia alitoa Balozi Chokala........
Ain't you suprised how things are solved kwa kufuata ushauri huo. Sometimes I wonder tunahitaji serikali ya nini??????
 
Back
Top Bottom