Serikali Yawapoza Wafanyakazi!

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,701
IKIWA imesalia takriban miezi miwili na nusu kabla ya uchaguzi mkuu, serikali inaonekana kuwaangukia wafanyakazi kwa kuongeza mishahara, huku kima cha chini "kikikaribia mapendekezo ya pili ya Tucta ya Sh260,000" ambayo awali yalikataliwa na serikali.

Ongezeko hilo limefanyika katika kipindi ambacho kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu kura za wafanyakazi ikianza kutumiwa kama mtaji wa kisiasa na wanasiasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31.

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) ilieleza kukerwa na kauli ya Kikwete kuwa serikali yake haitaweza kulipa kima cha chini cha mshahara cha Sh315,000 kama shirikisho hilo na kwamba "kama ni hizo kura za wafanyakazi niko tayari kuzikosa". Tucta ilisema kuwa jana ingetoa tamko lake kuhusu mgombea ambaye atawafaa wafanyakazi.

Lakini jana hakuna kiongozi aliyekuwa tayari kutoa tamko la wafanyakazi na habari zinasema kuwa kusita huko kunatokana na ongezeko la kuridhisha la mishahara ya wafanyakazi wa sekta ya umma.

Mwananchi ilipomuhoji katibu mkuu wa Tucta, Nicolas Mgaya kuhusu tamko la shirikisho hilo, alisema kiwango kilichoongezwa kinakidhi mahitaji ya watumishi wa umma kukabiliana na hali ngumu ya maisha ingawa hakijafikia matakwa ya Tucta.

"Matatizo yetu na serikali yamepungua... kiasi kilichoongezwa kinapunguza makali ya maisha kwa watumishi wa umma. Tunafikiria kumpa pilau yetu kiongozi anayesikiliza matatizo ya watu wake," alisema Mgaya ambaye hata hivyo hakuwa tayari kuweka wazi kiwango cha nyongeza hiyo.

Nyongeza hiyo ya mishahara imeanza kutolewa kinyemela bila wafanyakazi kujulishwa mabadiliko katika mishahara yao na badala yake kushitukia wamewekewa fedha zaidi katika akaunti zao za mishahara. Habari zinasema kuwa tayari waraka umeshapelekwa idara tofauti za serikali kuwaeleza viwango vipya vya mishahara na kwamba mabadiliko hayo ni kwa wafanyakazi wa ngazi zote.

Habari za uhakika ambazo gazeti hili inazo zinasema kuwa hatua ya serikali kuongeza mishahara ya wafanyakazi wake imeanza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi uliopita wa Julai.

Katika hotuba yake ya kuzungumzia mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wa serikali ya awamu ya nne, Rais Kikwete alisema kuwa kima cha chini kiliongezeka kutoka Sh84,000 kwa mwaka 2005 hadi Sh 135,000 kwa mwaka 2010. Kauli yake ilimaanisha kuwa mshahara mpya wa kima cha chini, ambao ulitakiwa utangazwe na waziri husika, ulipanda kutoka Sh105,000 hadi Sh135,000.

Waziri Hawa Ghasia, akisoma hotuba ya bajeti ya 2010/11 ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, alisema kuwa serikali itaongeza mishahara ya wafanyakazi, lakini hata hivyo hakutaja viwango vya nyingeza hiyo.

Tucta iliitisha mgomo Mei 5 ikiwa katikati ya mazungumzo ya utatu kuhusu kima cha chini cha wafanyakazi wa sekta ya umma, kupanua wigo wa kodi ili kumpunguzia mfanyakazi mzigo na kuboresha mafao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Katika vikao hivyo, Tucta ilipendekeza kuwa kima cha chini kiwe Sh315,000 lakini serikali ikagoma kwa maelezo kuwa haina uwezo wa kulipa zaidi ya wafanyakazi takriban 350,000 na ndipo Tucta ilipowasilisha pendekezo la pili la Sh260,000 ambalo pia lilikataliwa. Tucta ilishuka hadi pendekezo la Sh160,000, lakini nalo halikukubaliwa na badala yake kima cha chini kikawa Sh135,000.

Juzi, Tucta ilidokeza sifa ya mgombea anayetakiwa wa urais wa Jamhuri ya Tanzania na kueleza kuwa wafanyakazi wasilazimishe "kumpa pilau mtu asiyetaka, bali wampe yule anayezihitaji". Kaimu katibu mkuu wa Tucta, Nicolas Mgaya alisema: "Kuna ile kauli ya 'kama ni hivyo, na kura zao sizitaki.

Kwani jamani kama una karamu nyumbani kwako; mtu akaja ukampa pilau; akalikataa, utamlazimisha ama utampa yule anayekwambia anaihitaji?" Alikuwa akirejea kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati akizungumza na wazee wa Dar es salaam kuhusu mgomo uliopangwa kufanyika Mei 5 mwaka huu kuishinikiza serikali kuongeza kima cha chini cha wafanyakazi wa sekta ya umma, kupunguza kodi inayokatwa kwenye mishahara na kuboresha mafao ya wastaafu.

Alisema serikali imeanza kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na shirikisho lake kuhusu kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa serikali akisistiza kuwa hatua hiyo itaweza kupunguza ugumu wa maisha pamoja na mgogoro baina yake na serikali.
Source: Gazeti la Mwananchi.
 
Kama wafanyakazi wameongezewa mishahara basi hii ni asante Slaa. Bila Slaa kukubali kuwa mgombea CCM haingeogopa wafanyakazi.

Tuambiwe hizo fedha zilikuwa wapi? Zinatumika kama hongo ya kununulia kura? Wafanyakazi zipokeeni lakini kura yenu mpeni Slaa. Ndiye kawaleta hii nyongeza.
 
ongezo la kimyakimya ni hongo ya uchaguzi tu, litaondoka kimyakimya kama lilivyoingia
 
Takukuru, kama mnavyowakamata wengine.............. hebu kamata serikali nzima............. hizi hela zilikuwa wapi..........???? Mbona mwanzo alikana hadi kura zaooo.....???
 
Takukuru, kama mnavyowakamata wengine.............. hebu kamata serikali nzima............. hizi hela zilikuwa wapi..........???? Mbona mwanzo alikana hadi kura zaooo.....???

Itafika mahali tutawadaka hata akina Obama wanaotoa misaada kwetu!
 
Mwananchi ilipomuhoji katibu mkuu wa Tucta, Nicolas Mgaya kuhusu tamko la shirikisho hilo, alisema kiwango kilichoongezwa kinakidhi mahitaji ya watumishi wa umma kukabiliana na hali ngumu ya maisha ingawa hakijafikia matakwa ya Tucta.

“Matatizo yetu na serikali yamepungua... kiasi kilichoongezwa kinapunguza makali ya maisha kwa watumishi wa umma. Tunafikiria kumpa pilau yetu kiongozi anayesikiliza matatizo ya watu wake,” alisema Mgaya ambaye hata hivyo hakuwa tayari kuweka wazi kiwango cha nyongeza hiyo.

......
Katika vikao hivyo, Tucta ilipendekeza kuwa kima cha chini kiwe Sh315,000 lakini serikali ikagoma kwa maelezo kuwa haina uwezo wa kulipa zaidi ya wafanyakazi takriban 350,000 na ndipo Tucta ilipowasilisha pendekezo la pili la Sh260,000 ambalo pia lilikataliwa. Tucta ilishuka hadi pendekezo la Sh160,000, lakini nalo halikukubaliwa na badala yake kima cha chini kikawa Sh135,000.

Kama hicho kiwango ambacho Bwana Mgaya anasema kinakidhi mahitaji ndio hiyo Sh 135,000 kwa mwezi basi tuna safari ndefu sana katika nchi yetu. Siamini kama kiasi hiki ndio kimemfanya abadili msimamo wake wa awali....labda kuna ya zaidi nyuma ya pazia!
 
Na Patricia Kimelemeta
IKIWA imesalia takriban miezi miwili na nusu kabla ya uchaguzi mkuu, serikali inaonekana kuwaangukia wafanyakazi kwa kuongeza mishahara, huku kima cha chini “kikikaribia mapendekezo ya pili ya Tucta ya Sh260,000″ ambayo awali yalikataliwa na serikali.
Ongezeko hilo limefanyika katika kipindi ambacho kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu kura za wafanyakazi ikianza kutumiwa kama mtaji wa kisiasa na wanasiasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31.
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) ilieleza kukerwa na kauli ya Kikwete kuwa serikali yake haitaweza kulipa kima cha chini cha mshahara cha Sh315,000 kama shirikisho hilo na kwamba “kama ni hizo kura za wafanyakazi niko tayari kuzikosa”.
Tucta ilisema kuwa jana ingetoa tamko lake kuhusu mgombea ambaye atawafaa wafanyakazi. Lakini jana hakuna kiongozi aliyekuwa tayari kutoa tamko la wafanyakazi na habari zinasema kuwa kusita huko kunatokana na ongezeko la kuridhisha la mishahara ya wafanyakazi wa sekta ya umma.
Mwananchi ilipomuhoji katibu mkuu wa Tucta, Nicolas Mgaya kuhusu tamko la shirikisho hilo, alisema kiwango kilichoongezwa kinakidhi mahitaji ya watumishi wa umma kukabiliana na hali ngumu ya maisha ingawa hakijafikia matakwa ya Tucta.
“Matatizo yetu na serikali yamepungua… kiasi kilichoongezwa kinapunguza makali ya maisha kwa watumishi wa umma.
 
"Kidatu;1028016]Hii ni RUSHWA. Kuna kila sababu ya kuipeleka serikali mahakamani."

I totaly agree .... Takukuru !!! Where are You!!!?
 
Rushwa hiyo na hapa wafanyakazi hatudanganyiki labda hao wenye vyeo vya kutuliwa na wanaofanana na hao sisiem mmefulia vibaya kwa kauli za kuropoka
 
Busara ya mtu hupindwa kwa uwiano wa maneno na matendo, hivyo mwenye macho haambiwi tazama! Rais wetu hana washauri makini.
 
Back
Top Bottom