Serikali yavumbua jina jipya la semina elekezi, Sasa kuitwa "MTIHANI"

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,896
1,862
Wadau kuanzia sasa hamtasikia neno semina elekezi tena maana serikali yetu sikivu imebadilisha jina

Akizungumza na waandishi wakati wa kutajwa majina ya wakuu wa mikoa Pinda alisema,

“Tumetoa wiki moja, wakuu hawa wajiandae kwenda kwenye vituo vyao vya kazi, watatakiwa kuapa mbele ya mkuu wa mkoa halafu tutawapatia mafunzo kwa wiki mbili pale Dodoma tena nimewaambia watu wa Tamisemi wawape mtihani kabisa,”

Alisema mafunzo hayo yatawahusisha pia wakuu wote wa mikoa na makatibu tawala wote. Alisema: “Sitaki iitwe semina. Ndio maana nimesema wapewe mitihani
.

Sosi: ippmedia.com
 
Yaani kugeuza geuza maneno ndio umekuwa umahiri wetu toka tupate uhuru...imagine kilimo cha kufa na kupona, kilimo uti wa mgongo wa mtanzania, kilimo kwanza na maneno mengine yanayofanana na hayo.
 
Wadau kuanzia sasa hamtasikia neno semina elekezi tena maana serikali yetu sikivu imebadilisha jina

Akizungumza na waandishi wakati wa kutajwa majina ya wakuu wa mikoa Pinda alisema,

"Tumetoa wiki moja, wakuu hawa wajiandae kwenda kwenye vituo vyao vya kazi, watatakiwa kuapa mbele ya mkuu wa mkoa halafu tutawapatia mafunzo kwa wiki mbili pale Dodoma tena nimewaambia watu wa Tamisemi wawape mtihani kabisa,"

Alisema mafunzo hayo yatawahusisha pia wakuu wote wa mikoa na makatibu tawala wote. Alisema: "Sitaki iitwe semina. Ndio maana nimesema wapewe mitihani
.

Sosi: ippmedia.com

Dah! Wakivurunda tutasema kuwa WAMEFELI MITIHANI
 
Back
Top Bottom