Serikali yatunishia misuli wabunge

MrFroasty

JF-Expert Member
Jun 23, 2009
1,195
590
Sasa kusema serekali inapuuza maagizo ya Bunge si ndio kusema kama unapuuza matakwa ya wananchi.Ikiwa Bunge ndio linawakilisha wananchi, na wanapigia kelele wabunge ndio kilio cha wanyonge na wananchi waliowengi.
Sasa hii nchi inafuata sheria za utawala bora au basi ni wizi mtupu?


Serikali yatunishia misuli wabunge

Serikali imeshikilia masimamo wake wa kutokuchukua hatua zaidi dhidi ya watumishi wake waliohusika katika kashfa ya mkataba tata wa Richmond kama ilivyotakuwa na Bunge, na badala yake imesema yaliyotekelezwa yanatiosha.

Ukweli huo umedhihirika jana baada ya Serikali kuwasilisha kwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini taarifa ya utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge kuhusu kashfa ya mkataba wa Kampuni ya Richmond.

Mbali na taarifa ya utekelezaji wa maazimo hayo, pia iliwasilisha inayohusu hatma ya wamiliki wa mgodi wa makaa ya mawe Kiwira.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walizungumza na Nipashe jana kwa sharti la kutotajwa majina walisema kuwa ripoti hiyo haina maelezo ya kuridhisha kujibu hoja za wabunge.

Habari zinaeleza kuwa taarifa ya serikali iliyowasilishwa jana haielezi chochote kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge.

Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam jana, zinaeleza kuwa taarifa hizo ziliwasilishwa kwa kamati hiyo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo.

Baada ya wajumbe wa kamati hiyo kuzisoma, baadhi waliamua kuondoka kimya kimya bila kusubiri kuzijadili

kwa kueleza kuwa Serikali imeonyesha jeuri na dharau kwa Bunge kwa kitendo chake cha kutofanyia kazi mapendekezo ya Bunge.

“Wapo baadhi ya watu wanaodhani maagizo ya Bunge ni lazima yatekelezwe na Serikali, kazi ya Bunge ni kuishauri Serikali kwa hiyo Serikali imeridhishwa na hatua ambazo imekwishachukua kwa watumishi wake waliohusika kwenye sakata la Richmond,” mjumbe mmoja wa Kamati ya Nishati na Madini alinukuu taarifa ya Serikali kwa wabunge.

Alisema taarifa ya Serikali imeeleza kuridhika na maelezo ya awali ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na pia adhabu ya onyo aliyopewa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Dk. Edward Hoseah, baada ya kubainika kufumbia macho madudu ya Richmond.

“Majibu haya yamewakera sana wabunge, tutajadiliana na kuwasilisha mapendekezo yetu kwenye mkutano wa Bunge Dodoma, lakini tumepanga kuishtaki Serikali kwa wananchi ambao ndiye mwajiri wa Bunge na Serikali,” alisema mbunge mmoja.

Vigogo waliotuhumiwa katika kashfa ya Richmond pamoja na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi ambao tayari wamekwisha kustaafu utumishi serikalini.

Ripoti ya Richmond inatarajiwa kuwasilishwa bungeni baada ya makundi katika jamii, wakiongozwa na wabunge kutoridhishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali katika kutekeleza maazimio hayo.

Taarifa ya jana inaonyesha kuwasafisha Mwanyika Dk. Hoseah.

Hata hivyo, Dk. Hoseah, alionywa kwa kutokuwa makini wakati akifanya uchunguzi wa mchakato uliofanikisha kuipa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura Kampuni ya Richmond Development (LLC).

Mbali na Dk. Hoseah, mwingine aliyeonywa, ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya majadiliano ya wataalamu, Singi Madata.

Taarifa ya jana inaeleza kuwa Serikali imeridhishwa na hatua iliyozichukua dhidi ya vigogo hao.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, William Shellukindo (CCM), alithibitisha jana kamati yake kupokea taarifa hizo kutoka serikalini.

Hata hivyo, habari zilizopatikana baadaye zimeeleza kuwa wajumbe hao walifikia uamuzi huo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutoridhishwa na yaliyomo ndani ya taarifa hizo za serikali.

“Baada ya kuondoka kikaoni, sijui wenzetu tuliowaacha walifikia maamuzi gani. Lakini hakuna cha kuridhisha katika taarifa hizo na zitazua malumbano makubwa bungeni. Suala hili CCM wanajimaliza wenyewe. Kwa ufupi ni matatizo matupu,” alisema mjumbe mwingine ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Alisema katika maazimio 23 ya Bunge Serikali imeeleza kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na kamati za nidhamu kwa kuwaonya baadhi ya vigogo waliofumbia macho mkataba huo tata ambao uliliingizia taifa hasara ya mabilioni ya fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mapumziko ya kikao cha kamati yake jana, Shellukindo alisema taarifa kuhusu kashfa ya Richmond, waliipokea na jana asubuhi walianza kuipitia na kuijadili kazi hiyo walitarajia kuifanya hadi usiku.

Alisema mara baada ya kuijadili na kutafakari, wataiwasilisha sambamba na maoni ya kamati katika Mkutano wa 18 wa Bunge, unaotarajiwa kuanza mjini Dodoma, wiki ijayo.

“Tumepokea taarifa ya serikali kuhusu hoja ya Kampuni ya Richmond Development LLC. Tunaendelea na kikao nadhani hadi usiku. Tunajadili na kutafakari ili baadaye tukatoe taarifa bungeni, huko ndiko mtapata taarifa,” alisema Shellukindo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam.

Kuhusu taarifa ya Kiwira, Shellukindo alisema waliipokea na wamekwisha kuishughulikia na kusema: “Serikali imechukua hatua nzuri kuurejesha mgodi huo na kuwalipa waliokuwa wafanyakazi wake”.

Sakata la Richmond na Kiwira ni masuala, ambayo yamezua msuguano baina ya serikali na Bunge kutokana na serikali kusuasua katika kuwasilisha taarifa ya kuridhisha wabunge juu ya utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge kuhusu kampuni hiyo.

Pia, wabunge walitaka kujua kama waliokuwa wamiliki wa Kiwira, akiwamo Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri wake wa Nishati na Madini, Daniel Yona, baada ya serikali kutangaza kuurejesha mgodi huo kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Shirika la Madini la Taifa (Stamico), watalipwa fidia au serikali ndiyo italipwa.

CHANZO: NIPASHE
 
Bunge linawakilisha wananchi lakini wabunge wanawakilisha familia zao,chunguza sana hizo tensi mkuu!
 
Huu ni utawala wa namna gani? Kama maamuzi ni yangu serikali ivunjwe hata kama zimebaki miezi michache kufanya hivyo
 
Bunge linawakilisha wananchi lakini wabunge wanawakilisha familia zao,chunguza sana hizo tensi mkuu!
Aaagh....sasa hao wabunge hawatufai na bakora ya wananchi inajulikana hapo Octoba :rolleyes:

Hii serekali chini ya JK imezidi vituko, wizi na ufisadi kazi kwenu kwenu wadanganyika :D
 
Huu ni utawala wa namna gani? Kama maamuzi ni yangu serikali ivunjwe hata kama zimebaki miezi michache kufanya hivyo

Labda ndiyo nia ya JK, Bunge liikomalie serikali ili alivunje kabla ya Julai na kukipiga bao CCJ!
 
Kamati ya Nishati na Madini imechemsha inapoyachukulia maazimio 23 ya Bunge kama "maagizo" kwa Serikali badala ya "mapendekezo" kwa Serikali! Wakiondoa hiyo notion wataeleweka! Na huko "kuishtaki Serikali kwa wananchi" maana yake nini? Wanajipa kazi unnecessarily, huku wakijua hawataweza kuilazimisha Serikali!
 
Matatizo ya Bunge ni kuingia kwenye mtihani na majibu. Walijua hatua stahili ni kuwafukuza kazi akina Oseah wa Takukuru kumbe ipo namna nyingine! Bunge limechemsha!!!!

Dr. Mwakyembe huna sera kabisa kwa hilo na kamati nzima maana mliacha mwanya wazi kwa serikali kuwachezea katika pendekezo hilo. Inabidi nawe (mwakyembe) uchunguzwe kwa ufisadi wa kushindwa kugundua hilo mapema!!
 
Matatizo ya Bunge ni kuingia kwenye mtihani na majibu. Walijua hatua stahili ni kuwafukuza kazi akina Oseah wa Takukuru kumbe ipo namna nyingine! Bunge limechemsha!!!!

Dr. Mwakyembe huna sera kabisa kwa hilo na kamati nzima maana mliacha mwanya wazi kwa serikali kuwachezea katika pendekezo hilo. Inabidi nawe (mwakyembe) uchunguzwe kwa ufisadi wa kushindwa kugundua hilo mapema!!

Kaazi kweli kweli!
 
Mbunge Yesu tu na Serikali ni Mungu, hapa Tanzania uhuni mtupu, labda lipite bomu tani hamsini juu ya jengo ambalo wana sisi emu wanajadili vikao vya neki, na kutaifisha roho zao zote Maana hao ndiyo wanao tuilia baraka zetu toka kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwa 95% ya wabunge wa sisi emu ni vibaraka wa shetani, na majini
 
Tanzania inanipa raha sana.yaani hii kamati ya bunge ndio utumbo mtupu..na majibu aliyowapa Marmo ndo size yao maana wanapayuka tu hawaelewi wanaongea nini ..Kutwa kukomaa na Richmond kwani hakuna mambo mengine ya kufanya?
 
Back
Top Bottom