Serikali yatoa Tumaini Mahakama ya Kadhi

Na hivi kodi zinazolipwa na waislamu zinaenda wapi? Bakhressa No 1 Taxpayer kodi yake inaenda wapi? Zakhem, SSB, Abood, Zakaria Companies hawa kodi zao zote zinaenda wapi? Mie ninakatwa kodi ya milioni moja kila mwezi inaenda wapi? Msitake kutuzingua hapa!!!

Una uhakika na hicho kilichokuwa na rangi? MTU BINAFSI au KAMPUNI? Kama ni kampuni yawezaje kampuni kuwa "Muislamu?
 
Muslimu for muslimu not for all TAnzanian. Hivi Kodi zitokanazo na kuuza nguruwe, Pombe nazo zaweza endesha mahakama ya kadhia.

Swali zuri sana mwana JF!! Fedha haramu zitatumika kuendeshea mahakama ya kadhi. Misikiti haina hela ya kuianzisha na kuiendesha huko huko misikitini?
 
CIA World Fact Book itakupa jibu lako. Pia sensa ya mwaka 2002 ijapokuwa majibu sijui yako wapi?

CIA WORLD FACT BOOK SI MTOA MAJIBU-SENSA YA 2002 INA MAJIBU SAFI TU-KAMA HUJUI YALIPO NAWEZA KUSAIDIA-KWA KUANZA-ANZA NA HII LINK YA SERIKALI ITAKUPA JIBU LAKO-http://www.tanzaniatouristboard.com/about_tanzania/religion
NAPINGA CIA WORLD FACT BOOK-MAANA KAMA UNATEGEMEA SOURCE ZA DATA ZA NJE-BASI UNGEANGALIA HII KWANZA-http://www.state.gov/r/pa/ei/bgn/2843.htm
 
Kwa hivyo kama hunufaiki na kodi unayolipa serikalini ndio na kodi inayolipwa NA WENGINE igharamie mahakama ya kadhi? Nani na wapi kasema walipakodi ni wakristo peke yao?

Umethibitisha kuwa WEWE NDIE MWENYE FIKRA MGANDO kwa kuona kisichoandikwa - meaning You have a fixation about your own ideas believe it is truth!!!

Nikiuliza kodi yangu kama muislamu mnaripuka lakini nyie kodi zenu ni sahihi kuuliza. Kwahiyo basi kama nyie hamtaki kodi yenu isihudumie mahakama ya kadhi basi pawepo na memorandum of understanding kama UK kwamba kila kiasi fulani cha kodi kinaenda kwa malkia (2%) kwa waislamu pia ifanyike hivyo je na hilo tatizo?
 
Hizo scaremongering machafuko hayawezi kuja kwasababu ya mahakama ya kadhi. Ndio maana sasa napata picha kwanini baadhi ya wapinzani wameshindwa kumbe ubaguzi wa kidini unawasumbua. Tanzania yetu sote mkuu!!!

Naomba kiti moto kiruhusiwe kuwa chakula mashuleni kwani ni haki ya wote
 
Kwani hivi ndugu zangu waislamu, kwani kuna tatizo gani la mahakama ya kawaida? na mtafaidika na nini au taifa lote litafaidikaje na hii mahakama mnayoililia? Mkumbuke kuwa hii ni nchi isiyo na dini na pia kuna ndugu zene wa kikristo nao wanaishi humuhumu na sio ninyi peke yenu na faida ni ingekuwa ni vizuri tuipate wote as a nation! mmefanya research na kuona kuwa hizo nchi ambazi zinapractise hii zimefaidikaje! maana tusiwe tunapiga makelele tu ya kufuata mkumbo bila hata kujua faida wala hasara zake!
 
nikiuliza kodi yangu kama muislamu mnaripuka lakini nyie kodi zenu ni sahihi kuuliza. Kwahiyo basi kama nyie hamtaki kodi yenu isihudumie mahakama ya kadhi basi pawepo na memorandum of understanding kama uk kwamba kila kiasi fulani cha kodi kinaenda kwa malkia (2%) kwa waislamu pia ifanyike hivyo je na hilo tatizo?
kodi yako inaleta elimu, afya, miundombinu, (mafisadi wanakula) kwani wewe uugui au ndugu zako hawasomi
 
Una uhakika na hicho kilichokuwa na rangi? MTU BINAFSI au KAMPUNI? Kama ni kampuni yawezaje kampuni kuwa "Muislamu?

Kwani mwenye kampuni nani au Bakhressa ni PLC mbona unazungumza vitu vya ajabu sio lazima kila kitu ucomment please. Na nina uhakika na hilo labda mwaka huu ibadilike maana wanashindana na TBL nafasi hiyo ya juu.
 
mbona sioni source mkuu hata mie naweza kuweka site nikaandika upupu ninaotaka (i mean hiyo website yako ya tanzania tourist board) tena wakipata wakili makini anaweza kuwasue for misleading information na gross negligence.
Hiyo website sijui umeitoa wapi click link hiyo hapo chini utaona:
https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/geos/tz.html

niko makini mzee

huoni source?kivipi-fuata link hizo then utapata jibu-mawakili wapo-but nao hawawez kufwata mkumbo wakati data ndo zipo hivyo-kama si hivyo serikali ingeshaondoa hizo data mapema sana-thats all mkuu
 
Nikiuliza kodi yangu kama muislamu mnaripuka lakini nyie kodi zenu ni sahihi kuuliza. Kwahiyo basi kama nyie hamtaki kodi yenu isihudumie mahakama ya kadhi basi pawepo na memorandum of understanding kama UK kwamba kila kiasi fulani cha kodi kinaenda kwa malkia (2%) kwa waislamu pia ifanyike hivyo je na hilo tatizo?

Ndugu, you are missing the whole point. Tukianza kufikiria kwa misingi ya vikundi hatutafika popote. The issue ni kuwa public fund ifanye kazi ya kunufaisha kila mtu kwenye jamii - regardless who or what he happens to be. Assuming wewe ni Muislamu, uliamua kuwa hivyo au ni "social accident"? Hata kama uliamua, wote walio waislamu waliamua kuwa waislamu au walijikuta wakiwa waislamu (kwa kuzaliwa katika familia ya waislamu)?

Wazo lako in zuri japo nadhani kwa mazingira ya sasa ya nchi yetu si practical. Kuna ngumi kila kukicha kwenye vikundi vya kijamii (makanisa, misikiti, klabu za michezo n.k) kugombea rasilimali kidogo zilizopo. Tukianza kuwapa fungu toka serikalini unadhani itakuwaje? Kanisa gani lipewe hiyo ruzuku, Wakatoliki? Walutheri, Waanglikana, Wapentekoste n.k. watakaa kimya?

Hiyo ruzuku wapewe BAKWATA au jumuiya gani ya Kiislamu? Taasisi za kidini hupewa misaada na serikali tangu zamani (Chuo cha TANESCO Morogoro kwa mfano), hakujawahi kuwa na malalamiko. Ila hili la ku-formalize matumizi ya kodi kwa ajili ya kundi moja kwenye jamii litatupeleka pabaya.

Nadhani umeelewa hoja yangu.
 
kodi yako inaleta elimu, afya, miundombinu, (mafisadi wanakula) kwani wewe uugui au ndugu zako hawasomi

Hahaha usinichekeshe, nikiumwa nalipa na kuhonga kwa pesa yangu. Miundo mbinu tunatozwa pia ushuru zaidi ya kodi zinazolipwa. Labda wanakula mafisadi. Ndugu zangu yes wamesomeshwa na serikali ila ni mkopo wanaohangaika kuulipa kwa kuhenya. Ijapokuwa wengine walisomeshwa bure I have to admit lakini sawa tuzikokotea hesabu je zinaendana na kiwango ninachotoa?
 
Mbona sioni source mkuu hata mie naweza kuweka site nikaandika upupu ninaotaka (I mean hiyo website yako ya Tanzania Tourist Board) tena wakipata wakili makini anaweza kuwasue for misleading information na gross negligence.
Hiyo website sijui umeitoa wapi click link hiyo hapo chini utaona:
https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/geos/tz.html

Niko makini mzee

KWANI HII INASHIDA GANI CLICK HAPA Tanzania unajua hizi source za sensa nyingi ni misleading my brain tells me kuna wakristu wengi sana bara kuliko waisalmu Zanzibar 99 percent might be muslims maybe sababu wamebadilisha katiba yao na mahakama hiyo wanaweza wakajipa and then I think bye bye muugano
 
Mdondoaji;1277136]

HUONI SOURCE?KIVIPI-FUATA LINK HIZO THEN UTAPATA JIBU-MAWAKILI WAPO-BUT NAO HAWAWEZ KUFWATA MKUMBO WAKATI DATA NDO ZIPO HIVYO-KAMA SI HIVYO SERIKALI INGESHAONDOA HIZO DATA MAPEMA SANA-THATS ALL MKUU

Click link kabla hujacomment
 
Hapo ndipo ninapoona Waislamu mna matatizo kwani huko msikitini hamwezi kuamua mambo yenu mnayoyataka?? Mahakama ya kadhi inatuhusuje sisi Wakristo?? Sisi wakristo tunafanya mashauri yetu makanisani na kumalizana na sadaka zetu hutumika kuendesha mambo iweje ninyi tuwaendeshee mambo yenu kwa kodi zetu??. Msituletee mambo yenu ya Somalia hapa.
 
Ndugu, you are missing the whole point. Tukianza kufikiria kwa misingi ya vikundi hatutafika popote. The issue ni kuwa public fund ifanye kazi ya kunufaisha kila mtu kwenye jamii - regardless who or what he happens to be. Assuming wewe ni Muislamu, uliamua kuwa hivyo au ni "social accident"? Hata kama uliamua, wote walio waislamu waliamua kuwa waislamu au walijikuta wakiwa waislamu (kwa kuzaliwa katika familia ya waislamu)?

Wazo lako in zuri japo nadhani kwa mazingira ya sasa ya nchi yetu si practical. Kuna ngumi kila kukicha kwenye vikundi vya kijamii (makanisa, misikiti, klabu za michezo n.k) kugombea rasilimali kidogo zilizopo. Tukianza kuwapa fungu toka serikalini unadhani itakuwaje? Kanisa gani lipewe hiyo ruzuku, Wakatoliki? Walutheri, Waanglikana, Wapentekoste n.k. watakaa kimya?

Hiyo ruzuku wapewe BAKWATA au jumuiya gani ya Kiislamu? Taasisi za kidini hupewa misaada na serikali tangu zamani (Chuo cha TANESCO Morogoro kwa mfano), hakujawahi kuwa na malalamiko. Ila hili la ku-formalize matumizi ya kodi kwa ajili ya kundi moja kwenye jamii litatupeleka pabaya.

Nadhani umeelewa hoja yangu.

So problem ni utekelezaji sio uamuzi au vp?
 
Hapo ndipo ninapoona Waislamu mna matatizo kwani huko msikitini hamwezi kuamua mambo yenu mnayoyataka?? Mahakama ya kadhi inatuhusuje sisi Wakristo?? Sisi wakristo tunafanya mashauri yetu makanisani na kumalizana na sadaka zetu hutumika kuendesha mambo iweje ninyi tuwaendeshee mambo yenu kwa kodi zetu??. Msituletee mambo yenu ya Somalia hapa.

Absolutely crap je wewe umeambiwa mahakama ya kadhi itawahusu wakristo!!!
 
ubaguzi wa kidini huo na kama ni hivyo wakristo nao wadai mahakama yao kwani tz ina dini siku hizi?

waislamu waliichagua ccm na wakristo chadema, sasa mahakama ya kadhi ni sera waliouziwa waislamu hivyo ni haki yao kuipata na wakristo kama nao wanataka mahakama ya kikristo ambayo naamini haipo kiuhalisia basi nao wanahaki kuwa nayo lakini ni kichekesho kwa wakristo kudai hiyo mahakama mara tu waislamu watakapoipata!!!

hii ni sawa na tabia ya watoto wadogo ambao huoneana wivu ikiwa mmoja kamuomba baba ake amnunulie chupi nyeupe na mwingine atadai nayeye pia anataka anunuliwe chupi kama hiyo!!!!
 
.
Nchi za kiarabu zina misaada ipi kwa taifa la tanzania zaidi ya tende na nyama za kafara kwa mungu wao?. Hata hivyo ni nani aliyewanyima waislamu ruhusa ya kumteua kadhi wao kupitia taasisi zao za kidini. Hapa kinachotafutwa sii kadhi kwa maana ya kadhi bali mamlaka ya kidola yanayotambulika kikatiba na kugaramiwa na serikali kuu. Huu ni uvunjifu wa katiba na kamwe hautavumiliwa.

waislamu inabidi tuwe waangalifu, kuwa endapo waisraeli nao watatoa msaada fedha katika serikali ya tanzania na hela hiyo hiyo ikatumika ktk ujenzi wa mahakama ya kadhi je waislau tutaitenganishaje na kodi nyingine?

Wito kwa ndugu zangu waislamu tuanzishe mahakama yetu kama ibada nyingine bila kutegemea serikali.mbona tuaenda kuhiji makka na hatuombi ruksa wala msaada kutoka serikalini,mbona tunafanya ibada nyingi bila kuhusisha serikali.

Hivi ndivyo wenzetu wanatuona hatuwezi kufanya lolote bila kusimamiwa na serikali, tunajiaibisha ndugu zangu

Back
Top Bottom