Serikali yatoa dhamana bil. 293/- kwa mashirika binafsi:MMMH

OkSIR

Senior Member
Jun 3, 2009
108
1
Serikali yatoa dhamana bil. 293/- kwa mashirika binafsi
JIBU LA SWALI LA MBUNGE Viti maalum

na Mwandishi Wetu, Dodoma



BUNGE limeelezwa jana kuwa serikali imetoa dhamana ya mkopo wa zaidi ya bilioni 293 kwa mashirika binafsi yanayochukua mkopo kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuanzia mwaka 2003.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Fedha na Uchumi Jeremia Sumari aliliambia bunge jana, fedha hizo zimetolewa katika jumla ya kampuni 93.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Maulidah Komu (CHADEMA) aliyetaka kuelezwa, na serikali juu ya idadi ya mashirika ambayo yalidhaminiwa na BoT na dhamana yake ilikuwa ni kiasi gani.
Alisema tangu katika kipindi cha mwaka 2003/2004 hadi 2008/2009 mfuko wa mauzo ya nje ya nchi ulitoa dhamana kwa vyama vya ushirika na kampuni 45 ambazo ilienda kwenye sekta za kilimo, viwanda na biashara.
“Dhamana hii ya mkopo kwa makampuni 45 ilikuwa na thamani ya bilioni 290 milioni 682,” alisema Sumari. Aidha alisema katika mfuko wa mpango wa miradi midogo na ya kati ulishatoa dhamana kwenye sekta ya elimu, hoteli, viwanda, kilimo, ujenzi, afya na biashara kwa mashirika 48 ambao thamani yake ni Sh bilioni 3 na milioni 54,” alisema Malima. Malima alisema Mashirika yanayodhaminiwa na serikali mengi hurejesha mikopo hiyo na inapotokea yakashindwa kurejesha hunyang’anywa dhamana waliyowekewa na serikali hulipa deni.
 
Back
Top Bottom