Serikali yatimua wanafunzi UDSM

Hapa tuna vijana wa UDSM, tunaomba mtwambie.
  • Nini msimamo wa wanafunzi waliofukuzwa mpaka sasa, au wamechukua hatua gani?
  • Nini msimamo wa wanafunzi waliobakia, wanatoa kafara wenzao au inakuwaje
  • Tunaomba maoni yenu kuhusiana na hali ya baadae chuoni hapo kwa kukubali, kuondoka kwa wale waliofukuzwa na kukubali kuendelea na masomo kwa waliobakia, effect yake kwa wanafunzi wanaokuja si wataonewa sana wakijaribu kugoma watafukuzwa kwani wataona ili linawezekana.

Serikali nao tunaomba watuambie imeingia hasara kiasi gani kwa kukopesha watu ambao baadae inawafukuza bila kujali kuwa inawadai kwa mambo ambayo wangekaa meza moja na kuongea, Prof. Mkandara hacha ubabe, kutana na vijana muongee haya mambo yanamalizwa kwa mazungumzo.

Hivi ile taasisi yako ya Democrasia ndo mnatumia nguvu kusolve matatizo ya kisiasa, maana hata ukijaribu kulivika hili tatizo mambo ya kipolisi linarudi kuwa la kisiasa.
 
Kitila,

Haya unayosema ni kweli na ninaamini kina mtatiro na wenzao wanasoma hapa. Migomo sio lazima itumike hata kwenye mambo ambayo yanaweza kuwa solved kwa mawasiliano mazuri. Kama nimeleewa story yako, angalau wewe serikali ilikuheshimu na kuahidi kukopa pesa toka NBC. Katika hii case sioni kama uongozi wa chuo ulikuwa na nia ya kupata suluhu na wanafunzi na msimamo ulikuwa ni kuwa chuo lazima kiamue nani awe kiongozi.

swali dogo kwako,

Je kipindi chenu uongozi wa chuo ulikuwa unaingilia chaguzi za wanafunzi kama Mkandara anavyotaka kufanya hapa?

Hili la uchaguzi nimeshasema tangu jana kwamba hapa utawala umechemsha sana. Enzi zetu mambo ya DARUSO elections yalikuwa ya kwetu na utawala ulikuwa haugusi zaidi ya kumtuma Dean of Students kama observer tu. Ndio nasema wanafunzi sio watoto wadogo, waachwe wafanye mambo yao na wawajibike nayo. Ndio wanajifunza kujitegemea hivyo. Katika hili mbona tupo page moja kabisa.

Tatizo lingine kubwa hapa ni lack of clarity juu ya sababu hasa za mgomo. Sasa wote tuna-struggle kutafuta sababu, lakini ni jukumu la wagomaji: (i) kueleza kwa uwazi kabisa sababu za kugoma (ii) kushawishi jamii kwamba mgomo wao ni muhimu na kwamba wametumia njia zote imeshindikana na imebidi wagome (iii) mgomo wao sio kwa ajili ya maslahi yao leo tu bali pia ni katika kudai mambo ya msingi yatakayosaidia hata kizazi kijacho.

Principle moja tuliokuwa tunatumia sisi ni kwamba tulikuwa hatupo tayari kufanya mgomo (i) bila kueleza sababu vizuri za kugoma na zikaeleweka (ii) tulikuwa tunahakikisha kwamba katika kila mgomo tunakuwa na agenda inayogusa jamii ili tupate sympathy ya kutosha ndio maana utakuta kwamba tuliweza kwenda kupeleka msaada wa unga kwa wale wananchi waliobomolewa nyumba kule Kwamzungwi-Pugu. Na kuna kipindi tuligoma kwa ajili ya pesa za chakula lakini ndani yake tukaweka agenda kwamba tunadai nyongeza ya bajeti katika waizara ya elimu na kila mtu akatuunga mkono. Lengo ilikuwa ni kuonyesha kwamba DARUSO ni chombo cha kuwasemea wasio na sauti (voice of the voiceless)na wala sio chombo cha kutetea mambo ya mkate na bluebend za wanafunzi tu.

Tatizo la wanafunzi wetu leo sababu za migomo (i) hazieleweki kwa hiyo kila mtu anabaki kubuni (ii) hazigusi jamii na hivyo inakuwa rahisi kwa serikali kushinda maana wanaishia kuzomewa na wananchi walio wengi.

Nakuhakikishia serikali haiwezi kufunga chuo kwa sababu ya mgomo ikijua wanafunzi wana sympathy ya wananchi katika mgomo wao. Kila mara serikali kabla haijafunga chuo huwa inasoma kwanza maoni ya wananchi; wakiona wananchi wengi hawaungi mkono mgomo wanafunga, wakigundua wanafunzi wana sympathy ya wananchi hawafungi. Hili ni jambo ambalo viongozi wa wanafunzi ni muhimu wakilijua. Always make sure your agenda is relevant to the people's problems, otherwise mtabaki peke yenu na wananchi wa Manzese watawazomea!
 
Maghembe mnamuonea bure tu. Hata ingekuwa wewe tatizo hili lingekuwepo. Kuweni fair kidogo ktk ukosoaji wenu

sidhani kama unajua unachoongea, we want leaders who can stand on their own feets, kama bado hawezi kusimama mwenyewe na anategemea miguu ya wa juu yake,kwa kifupi HATUFAI KABISA NA AONDOKE,waziri mwingine huyu ashambuliwe ili aondoke
 
Unajua wanafunzi wameshazoeshwa kwamba matatizo yao hayawezi kutatuliwa hadi wagome. Na ni kweli mara nyingi wakigoma hupata walichokuwa wakikitaka. So, it is the question of attitudes. Ndio yale yale tunayoongelea hapa kila siku: respect to the rule of law na ustaarabu. Ongeza na cha tatu sasa: ustahimilivu.

Nakubaliana na wewe kwa asilimia 101!

Jamii yetu imekuwa jamii isiyo na ustahimilivu. Hakuna patience kabisa. Wanafunzi wetu hawawezi kusibiri hata kidogo.

Kimsingi nakubaliana na wewe; lakini ningeweza kusema hivi: mtu huru anayo haki ya kukataa uovu na kutouvumilia hata kwa dakika moja ya ziada. Uovu ukivumiliwa huzaa uovu mkubwa. Ni jukumu la mtu huru kuupinga uovu (evil) na dhulma (injustice) wakati wowote utakapoonekana.

Lakini katika kupinga uovu huo, njia za kufanya hivyo ndizo zinaamua ni kwa mwendo gani uovu hupingwa. Uzito wa uovu pia huamua kama ni hatua gani zichukuliwe kwanza kupambana naye. Hivyo mtu anayekutukana akiwa ndani ya gari na wewe uko unatembea amekutendea uovu. Lakini kulikimbiza gari ili umchape vibao siyo njia sahihi. Hivyo unavuta subira. Lakini mtu akija nyumbani kwako na galoni la mafuta na kiberiti mkononi na anataka kuilipua nyumba yako, huyo anahitaji kupingwa mara moja na kuzuiliwa na siyo kuvutiwa subira.

Na kuna udhaifu mkubwa sana katika uongozi wa wanafunzi. Kuna faslafa ya kijinga kwamba ukiwa kiongozi wa wanafunzi unafuata wanachosema wanafunzi. Hii ni weakness kubwa na sio maana ya uongozi. Ukiwa kiongozi unakuwa na taarifa nyingi zaidi kuliko unaowaongoza kwa hiyo lazima uonyeshe njia.

Mzee huu ni ukweli mkubwa sana ambao siyo tu kwenye serikali ya wanafunzi lakini unaweza kutolewa kwenye semina yoyote ya uongozi. Ndio maana mojawapo ya zile kanuni zangu za uongo inasema viongozi huongoza hawafuati.

Mimi nikakataa, nikawaambia sipo tayari kuongoza mgomo kwa sababu hatuwezi kuvumilia siku tatu wakati kuna watanzania wanashinda njaa kila siku. Nikawaambia wakati sisi tukisema hatuwezi kusubiri siku tatu, kuna watanzania walikuwa wamekufa na njaa kule Gairo. Nikawaambia wanafunzi wenzangu kuwa watanzania wangetudharau kwa kushindwa kuvumilia siku tatu tena tukisubiri utaratibu wa kawaida wa kibenki. Tukalumbana sana na mwisho nikwaambia kama mnaona ni lazima tuandame twende wizarani saa hiyohiyo, basi sikuwa tayari kuongoza huo mgomo na kwamba ningejiuzulu ili wachague kiongozi mwingine.

Hongera kwa hili, kwani ulifanya kitu kinachoitwa kuchukua msimamo badala ya kukubali kuyumbishwa na sauti mbalimbali na ulikuwa tayari ulipie gharama ya msimamo huo.

Baada ya hapo wanafunzi wakapoa, wakatawanyika wakabaki wachache kama 20. Nikawaambia wanafunzi walio wengi wameshanielewa. Ilipofika Jumanne wanafunzi wakapapata pesa zao na mambo yakaendelea kama mdundo. Ndio walinidharau sana siku hiyo Nkrumah na kuniona mimi ni traitor, lakini wengi walinishukuru baada ya siku tatu baada ya kutulia na ku-reflect.

veri veri gud!

Katika pointi zako za mwisho naweza kusema hivi; ni lazima tuwe na utaratibu wa kuwasaidia hawa vijana wanaoingia katika uongozi katika ngazi hizi. Wengine wana kipaji ya kuongoza lakini kipaji hicho hakijanolewa vizuri. Sijui ni lini mara ya mwisho kwa hawa vijana kupata semina ya viongozi au hata kupelekwa "ngurdoto" ya viongozi wa chuo.

Kuchaguliwa tu kwa sababu mtu anaweza kusema na anajenga hoja au kuahidi kutetea wanafunzi hakumfanyi awe kiongozi mzuri. Kujifunza tu mbele ya safari pia ni hatari na ndio maana unaoenekana huo udhaifu. Sijafuatilia profile yako, lakini naweza kusema (nisahihishe) kuwa uongozi wako pale Chuo Kikuu haikuwa mara ya kwanza watu kukudhamini nafasi ya uongozi. Na siwezi kushangaa uamuzi wako ule haikuwa mara ya kwanza kujikuta unalazimika kufanya maamuzi magumu lakini kwa watu wengi lakini ukatumia principles ulizokwisha jifunza kwenye uongozi mdogo au katika mambo yako binafsi.

Ndio maana naamini njia mojawapo ya kuwasaidia hawa vijana ni kuwaandalia vitu kama "semina ya uongozi" au semina ya "utatuzi wa migogoro" n.k Kuwaacha waende hivi na upofu kwa hakika watafanya makosa yasiyo ya lazima.
 
Tunafahamu ya kuwa wap ambao wana sifa ulizotaja hapo juu lakini kushabikia vijana wetu kupigwa, kuwekwa rumande na kutolewa mimba, si sahihi! Pia naomba nikuulize ni kwa nini wanafunzi wa Chuo kikuu ni Vialza kama unavyodai? Who are they and how did they become like that? They were NOT born like that. Ni mazingira. Sasa kama mfano wanaoona ni kwamba viongozi wetu wa nchi wanaiba na kutufilisi, na ni vihiyo na wababe, unafikiri what type of role models do they have to look up to? Acha kumwaga propaganda hapa!

hawezi kukujibu haya maswali kwa sababu anataka kukirudisha chuo kwenye zama za mawe. Tangu lini serikali ikachagulia wanafunzi viongozi wa chama cha serikali yao?

Wakikataa huo upuuzi basi watetezi wa ufisadi wanakuja na matusi na propanda kibao za kupondea wanafunzi bila kujiuliza kabisa kama hoja zao zina msingi au la.
 
Hili la uchaguzi nimeshasema tangu jana kwamba hapa utawala umechemsha sana. Enzi zetu mambo ya DARUSO elections yalikuwa ya kwetu na utawala ulikuwa haugusi zaidi ya kumtuma Dean of Students kama observer tu. Ndio nasema wanafunzi sio watoto wadogo, waachwe wafanye mambo yao na wawajibike nayo. Ndio wanajifunza kujitegemea hivyo. Katika hili mbona tupo page moja kabisa.

Tatizo lingine kubwa hapa ni lack of clarity juu ya sababu hasa za mgomo. Sasa wote tuna-struggle kutafuta sababu, lakini ni jukumu la wagomaji: (i) kueleza kwa uwazi kabisa sababu za kugoma (ii) kushawishi jamii kwamba mgomo wao ni muhimu na kwamba wametumia njia zote imeshindikana na imebidi wagome (iii) mgomo wao sio kwa ajili ya maslahi yao leo tu bali pia ni katika kudai mambo ya msingi yatakayosaidia hata kizazi kijacho.

Principle moja tuliokuwa tunatumia sisi ni kwamba tulikuwa hatupo tayari kufanya mgomo (i) bila kueleza sababu vizuri za kugoma na zikaeleweka (ii) tulikuwa tunahakikisha kwamba katika kila mgomo tunakuwa na agenda inayogusa jamii ili tupate sympathy ya kutosha ndio maana utakuta kwamba tuliweza kwenda kupeleka msaada wa unga kwa wale wananchi waliobomolewa nyumba kule Kwamzungwi-Pugu. Na kuna kipindi tuligoma kwa ajili ya pesa za chakula lakini ndani yake tukaweka agenda kwamba tunadai nyongeza ya bajeti katika waizara ya elimu na kila mtu akatuunga mkono. Lengo ilikuwa ni kuonyesha kwamba DARUSO ni chombo cha kuwasemea wasio na sauti (voice of the voiceless)na wala sio chombo cha kutetea mambo ya mkate na bluebend za wanafunzi tu.

Tatizo la wanafunzi wetu leo sababu za migomo (i) hazieleweki kwa hiyo kila mtu anabaki kubuni (ii) hazigusi jamii na hivyo inakuwa rahisi kwa serikali kushinda maana wanaishia kuzomewa na wananchi walio wengi.

Nakuhakikishia serikali haiwezi kufunga chuo kwa sababu ya mgomo ikijua wanafunzi wana sympathy ya wananchi katika mgomo wao. Kila mara serikali kabla haijafunga chuo huwa inasoma kwanza maoni ya wananchi; wakiona wananchi wengi hawaungi mkono mgomo wanafunga, wakigundua wanafunzi wana sympathy ya wananchi hawafungi. Hili ni jambo ambalo viongozi wa wanafunzi ni muhimu wakilijua. Always make sure your agenda is relevant to the people's problems, otherwise mtabaki peke yenu na wananchi wa Manzese watawazomea!

Kitila

Hebu tafuta mwanausalama yoyote akauleze kwa kina yanayofanyika mlango wa nyuma hapo UDSM. Una bahati katika kipindi chako hukukuwa na matukio makubwa ya kitaifa ambayo yangepelekea serikali kufanya propaganda dhidi ya wanafunzi kama ilivyokuwa wakati wa Nyerere na yale matukio ya wakati wa Mwinyi. Unafahamu jinsi ambavyo wanausalama walisuka ule mpango mzima wa kinachoitwa "kisa cha kubakwa kwa Levina Mukasa?". Ukweli ni kuwa hawa wanafunzi wameingia mtego wa propaganda za serikali. Walikuwa na madai ya msingi ya ufisadi, sasa wameshatolewa kabisa katika mstari- sasa wanaonekana kuwa wanagomea uchaguzi, na wametolewa zaidi kwenye mstari, sasa wanaonekana wanagombea wenzao waliosimamishwa warudi. Kila kukicha wanazidi kuondolewa katika mstari. Kesho utakuta chuo chote kinafungwa na sababu zinazotolewa zitafanya wanafunzi waonekani wajinga kabisa. Ukweli ni kuwa chini ya ufisadi wa EPA, RICHMOND nk- serikali imeiona kuna vuguvugu linafukuta UDSM kama lile la mageuzi ya 1990. Vijana wameamua kuunga mkono upinzani. Na ukitaka ushahidi wa haya ninayoyasema soma Ripoti ya Kamati ya Ulinzi na Usalama iliyowasilishwa kikao cha NEC ya CCM Butiama. Ripoti hiyo imesema wazi kwamba wanafunzi wa UDSM wamekuwa upinzani haswa CHADEMA na kwamba hali hiyo ni tishio kwa serikali. Maelekezo yalitolewa kwamba wote wenye mwelekeo wa upinzani watafutiwe sababu na kwa ujumla UDSM ichonganishwe kwa wananchi ili wanafunzi na jumuia yote ya wasomi pale ionekane hamnazo. Yale maelezo yaliyoandikwa ukweli ni huu niliyoyaweka hapa ni maelezo ambayo nimeyapata toka kwa mwanausalama mmoja. Ni sehemu tu ya maelezo ya wanafunzi ambayo inaelekea waliyaandika kwa kambi ya upinzani bungeni kueleza tukio zima lilivyo. Binafsi siwapendi CHADEMA wanavyofanya siasa yao, lakini hili limenigusa kwa sababu najua chuo kikifungwa waathirika ni pamoja na mwanangu aliyeko pale UDSM mwaka wa mwisho. Hivyo, watanzania tuungane pamoja kuhakikisha chuo hakifungwi. Na hatua ya kwanza ni kujua ukweli wa yote yanayoendelea pale UDSM

The propaganda machinery of the state is now full at play, angalia trick ndogo tu kwa mfano- Mukandala ametumia muda mrefu kueleza jinsi ambavyo wanafunzi ni wavuta bangi, lakini ukiangalia katika ile orodha ya kina mtatatiro na wenzake wanaotajwa kuwa vinara wa mgomo- yale majina ya wanaoitwa wavuta bangi watano si sehemu ya majina yao kabisa. This are pure propagandas and distortions!

PM
 
Hili la uchaguzi nimeshasema tangu jana kwamba hapa utawala umechemsha sana. Enzi zetu mambo ya DARUSO elections yalikuwa ya kwetu na utawala ulikuwa haugusi zaidi ya kumtuma Dean of Students kama observer tu. Ndio nasema wanafunzi sio watoto wadogo, waachwe wafanye mambo yao na wawajibike nayo. Ndio wanajifunza kujitegemea hivyo. Katika hili mbona tupo page moja kabisa.

Asante kwa hili Kitila,

Tatizo lingine kubwa hapa ni lack of clarity juu ya sababu hasa za mgomo. Sasa wote tuna-struggle kutafuta sababu, lakini ni jukumu la wagomaji: (i) kueleza kwa uwazi kabisa sababu za kugoma (ii) kushawishi jamii kwamba mgomo wao ni muhimu na kwamba wametumia njia zote imeshindikana na imebidi wagome (iii) mgomo wao sio kwa ajili ya maslahi yao leo tu bali pia ni katika kudai mambo ya msingi yatakayosaidia hata kizazi kijacho.

Kitila,

Siku zilizopita iliwekwa thread hapa kuwa uongozi wa chuo ulikuwa unaingilia uchaguzi wa wanaDaruso. Wengi hapa JF tukatoa ushauri kuwa uongozi wa chuo usiingilie masuala ya chaguzi za wanachuo. Kilichofuatia ni viongozi wa chuo kuamua kusimamisha mgombea aliyekuwa anapendwa na wanafunzi na kusitisha uchaguzi.

Pamoja na vilio vyote ambavyo serikali ya Daruso na watu wa nje kama sisi tulivyotoa kuwa uongozi wa chuo umwachilie huyo mganda na wanafunzi wengine wafanye uchaguzi wao kwa haki, kilichofuatia ni uongozi wa kidikiteta wa chuo kuwafukuza wanachuo watano na viongozi wengine kwa sababu zisizoelekea.

Siku ya uchaguzi ilipita na ikaonekana kwa serikali imepania kuingilia kabisa huu uchaguzi wa wanafunzi.

Principle moja tuliokuwa tunatumia sisi ni kwamba tulikuwa hatupo tayari kufanya mgomo (i) bila kueleza sababu vizuri za kugoma na zikaeleweka (ii) tulikuwa tunahakikisha kwamba katika kila mgomo tunakuwa na agenda inayogusa jamii ili tupate sympathy ya kutosha ndio maana utakuta kwamba tuliweza kwenda kupeleka msaada wa unga kwa wale wananchi waliobomolewa nyumba kule Kwamzungwi-Pugu. Na kuna kipindi tuligoma kwa ajili ya pesa za chakula lakini ndani yake tukaweka agenda kwamba tunadai nyongeza ya bajeti katika waizara ya elimu na kila mtu akatuunga mkono. Lengo ilikuwa ni kuonyesha kwamba DARUSO ni chombo cha kuwasemea wasio na sauti (voice of the voiceless)na wala sio chombo cha kutetea mambo ya mkate na bluebend za wanafunzi tu.

Kitila,

Hii ni kweli lakini ujue kuwa vijana wana wiki mbili kabla ya mitihani, sidhani kama kulikuwa na uwezekano wa kukuza huu mgomo ili kujumuisha mengine haya.

Tatizo la wanafunzi wetu leo sababu za migomo (i) hazieleweki kwa hiyo kila mtu anabaki kubuni (ii) hazigusi jamii na hivyo inakuwa rahisi kwa serikali kushinda maana wanaishia kuzomewa na wananchi walio wengi.

Kitila,

kama ni swala la kugomea, mbona wazee wa Dar es salaam walizomea wanafunzi wa chuo kikuu wa mwaka 1992 au 1993 kama sikosei ambao walikuwa wanapinga mpango wa serikali wa kuanzisha cost sharing bila kujua kuwa wazazi na watoto wao ndio watakaokumbana na huu mchango wa asilimia 40 wanaoambiwa kuchangia leo hii kwenye elimu ya juu.

Nadhani wakazi wengi wa Dar wamekuwa hawaungi mkono migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu no matter what they do.

Nakuhakikishia serikali haiwezi kufunga chuo kwa sababu ya mgomo ikijua wanafunzi wana sympathy ya wananchi katika mgomo wao. Kila mara serikali kabla haijafunga chuo huwa inasoma kwanza maoni ya wananchi; wakiona wananchi wengi hawaungi mkono mgomo wanafunga, wakigundua wanafunzi wana sympathy ya wananchi hawafungi. Hili ni jambo ambalo viongozi wa wanafunzi ni muhimu wakilijua. Always make sure your agenda is relevant to the people's problems, otherwise mtabaki peke yenu na wananchi wa Manzese watawazomea!

Mkuu Kitila,

Hawa wakazi wa Manzese ndio wanafungua matawi ya ccm day in day out no matter what they hear in the news. Katika hili wape vijana bureki kidogo.

Hata hivyo nakubaliana nawe kuwa inabidi vijana wajipange vizuri na ninaamini wale waliopewa dhamana watasoma hapa. So far wengi wako jela na wengine hawajulikani waliko.
 
samhani nahisi yote mliongea ni sahihi lakini hayana lakini hayazingatii ukweli na wakati. kuwalaumu wanafunzi hawa ambao wanajua nini wanadai huku maisha yanazidi kuwa magumu kwao kusoma kwa tabu huku milioni zaidi ya mia zinalipwa Richmond na nyingine zaidi ya 140 zinalipwa mkapa na wenzake kila siku na mafisadi hapo huru wanatesa tunawaonea. tuwe wakweli tusikurupuke tujadili mambo ya maana sio kupiga porojo eti kwa vile una nafasi ya kutuma ujumbe. ni muhimu tuwe realistic ili ukweli upatikane. kufurahia wanafunzi kupigwa na kupelekwa mahakamani wakati Balali, Mkapa Lowasa na kina Visenti (Chenge) wamefisadi nchi kiasi hiki na bado wanatesa na mashangingi barabaraniwakati hatudai nao wapigwe wala hawapelekwi mahakani ni ujauzito wa mawazo
 
ni yale yale ya utawala wa Msolla! hivi kweli Tanzania hatuna watu wenye akili timamu ambao wanaweza kukaa chini na kutatua matatizo ya Mlimani? Tuombe wawekezaji waje kutuonesha jinsi ya kuendesha Chuo Kikuu cha Taifa...?

Kikulacho ki nguoni mwako. Iweje kila waziri anayekuja anafanya madudu yale yale? kitalu cha virusi hivi inaonekana kiko palepale UDSM. response ya serikali inategemea sana pale UDSM wameihandle vipi hiyo ishu. Prof. Mmari was the last sensible VC there. hao wengine waliofuata wote ni homa tupu. angalia kwa mfano origin ya hii saga ya sasa hivi. hakuna wisdom yoyote, wala the slightest use of basic intellingence, iliyoonekana kutumika.

lakini kuna ukweli pia kuna factors zingine ndani ya serikali. Ni serikali hii ambayo haijali hasara kwa taifa, long term losses kwa taifa kwa ku entertain migogoro uchwara hapo UDSM, in pursuit of short term political shenanigans.
 
kulaumu wanafunzi na kuseherekea kupigwa kwao na kupelekwa mahakamani wakati kina Balali, Mkapa, Lowasa, Vijisenti(Chenge ) na wenzao wanatesa mitaani japo wamefisadi kiasi kikubwa cha mali zetu ni kuwa na ujauzito wa mawazo au utindio wa ubongo
 
Kitila

Hebu tafuta mwanausalama yoyote akauleze kwa kina yanayofanyika mlango wa nyuma hapo UDSM. Una bahati katika kipindi chako hukukuwa na matukio makubwa ya kitaifa ambayo yangepelekea serikali kufanya propaganda dhidi ya wanafunzi kama ilivyokuwa wakati wa Nyerere na yale matukio ya wakati wa Mwinyi. Unafahamu jinsi ambavyo wanausalama walisuka ule mpango mzima wa kinachoitwa "kisa cha kubakwa kwa Levina Mukasa?".

Kweli kabisa PM,

Habari za kiusalama kwenye suala la wanafunzi hawa zinatisha. Kwanza alianza Magembe kwa kuwaonya wanafunzi wasiteue viongozi wenye msimamo, na kisha ni juhudi ya serikali ya kudhibiti kazi na utendaji kazi wa viongozi wa wanafunzi.

Ukweli ni kuwa hawa wanafunzi wameingia mtego wa propaganda za serikali. Walikuwa na madai ya msingi ya ufisadi, sasa wameshatolewa kabisa katika mstari- sasa wanaonekana kuwa wanagomea uchaguzi, na wametolewa zaidi kwenye mstari, sasa wanaonekana wanagombea wenzao waliosimamishwa warudi. Kila kukicha wanazidi kuondolewa katika mstari. Kesho utakuta chuo chote kinafungwa na sababu zinazotolewa zitafanya wanafunzi waonekani wajinga kabisa.

Kuanzia ile siku ambayo Mtatiro na wenzake walitoa tamko la kukemea ufisadi, Mukandala amekuwa anamfuatilia sana huyu Mtatiro na wenzake. Huu ni udikiteta, ufisadi na uuaji wa hali ya juu kabisa unaonyeshwa hapa na Mukandala (ambaye ni mshauri wa Kikwete)

Ukweli ni kuwa chini ya ufisadi wa EPA, RICHMOND nk- serikali imeiona kuna vuguvugu linafukuta UDSM kama lile la mageuzi ya 1990. Vijana wameamua kuunga mkono upinzani. Na ukitaka ushahidi wa haya ninayoyasema soma Ripoti ya Kamati ya Ulinzi na Usalama iliyowasilishwa kikao cha NEC ya CCM Butiama. Ripoti hiyo imesema wazi kwamba wanafunzi wa UDSM wamekuwa upinzani haswa CHADEMA na kwamba hali hiyo ni tishio kwa serikali. Maelekezo yalitolewa kwamba wote wenye mwelekeo wa upinzani watafutiwe sababu na kwa ujumla UDSM ichonganishwe kwa wananchi ili wanafunzi na jumuia yote ya wasomi pale ionekane hamnazo. Yale maelezo yaliyoandikwa ukweli ni huu niliyoyaweka hapa ni maelezo ambayo nimeyapata toka kwa mwanausalama mmoja. Ni sehemu tu ya maelezo ya wanafunzi ambayo inaelekea waliyaandika kwa kambi ya upinzani bungeni kueleza tukio zima lilivyo.

Naona wanataka kuingilia siasa za vyuoni kama vile ambavyo Republicans hapa Marekani wameanza mikakati ya kuingilia vyuo vikuu ili kupunguza influence ya Demokrats vyuoni.

Binafsi siwapendi CHADEMA wanavyofanya siasa yao, lakini hili limenigusa kwa sababu najua chuo kikifungwa waathirika ni pamoja na mwanangu aliyeko pale UDSM mwaka wa mwisho. Hivyo, watanzania tuungane pamoja kuhakikisha chuo hakifungwi. Na hatua ya kwanza ni kujua ukweli wa yote yanayoendelea pale UDSM

CCM wanaweza kudhani kuwa wanawakomoa CHADEMA kwenye hii issue lakini nina hakika kabisa kuwa wanacreate radicals ambao siku moja watajuta kwanini waliingilia uendeshaji wa serikali za wanafunzi vyuo vikuu

The propaganda machinery of the state is now full at play, angalia trick ndogo tu kwa mfano- Mukandala ametumia muda mrefu kueleza jinsi ambavyo wanafunzi ni wavuta bangi, lakini ukiangalia katika ile orodha ya kina mtatatiro na wenzake wanaotajwa kuwa vinara wa mgomo- yale majina ya wanaoitwa wavuta bangi watano si sehemu ya majina yao kabisa. This are pure propagandas and distortions!

PM

Rwekaza Mukandala ni fisadi, dikiteta na muuaji. Nimemweka kwenye notice hapa JF. Nitamfuatilia kama Chenge na sitampa breki kama mkoloni na mwizi mwenye uraia wa utata ROstam Azizi
 
kulaumu wanafunzi na kuseherekea kupigwa kwao na kupelekwa mahakamani wakati kina Balali, Mkapa, Lowasa, Vijisenti(Chenge ) na wenzao wanatesa mitaani japo wamefisadi kiasi kikubwa cha mali zetu ni kuwa na ujauzito wa mawazo au utindio wa ubongo

Kity22,

Wenzako hawajali maisha ya watanzania.
Hebu angalia issue ya wanafunzi chuo kikuu au ile ya waandamanaji wa Buzwagi walivyochukua hatua haraka na kuleta polisi kupiga na kuua watu wakati mafisadi wakitanua tu hapo Dar kama vile hakuna vyombo vya usalama.
 
Rwekaza Mukandala ni fisadi, dikiteta na muuaji. Nimemweka kwenye notice hapa JF. Nitamfuatilia kama Chenge na sitampa breki kama mkoloni na mwizi mwenye uraia wa utata ROstam Azizi

kama kawaida yako... maumivu ya kichwa huanza polepole....
 
Wameingilia uchaguzi, wamefukuza viongozi, wamepiga mabomu wanafunzi bila sababu yoyote, kuna habari kuwa wameua mwanafunzi mjamzito, wamekamata wanafunzi usiku wa manane, hii ni hitimisho la udikiteta, ufisadi na "uuaji" wa Mkandara (ambaye ni mshauri wa Kikwete wa masuala ya siasa).

Mwizraeli ameshindwa kufaulu kwa kutumia mabavu ya kila aina kule Palestina: mauaji, mateso, kila mbinu, lakini binadamu anaonekana hawezi kufugika kama kuku. mabavu hayatatua matatizo ya msingi
 
Mwizraeli ameshindwa kufaulu kwa kutumia mabavu ya kila aina kule Palestina: mauaji, mateso, kila mbinu, lakini binadamu anaonekana hawezi kufugika kama kuku. mabavu hayatatua matatizo ya msingi

Sidhani kama wanakumbuka hili.
Kwa vile wana jeshi na polisi basi wanaona wanaweza kufanya chochote kile wanachopenda.
 
In the early eighties nilipokuwa nawatembelea wenzangu waliobahatika kuingia UDSM niliwakuta wakihangaikia maji. Kama sijakosea ni wakati huo wakajengewa vyoo vya shimo ambapo mtu ukitoka unanuka dawa ya choo. Sasa watoto wao wameingia hapo hapo na matatizo waliyoyakuta baba na mama zao bado yapo. Wamekaa miaka zaidi ya miaka 20 bila kutatuliwa matatizo ya msingi na bado mnataka wawe wastahimilivu? Ustahimilivu una mwisho na mwisho wake mara nyingi si mzuri!

P.S. Karibu tena Bin Maryam!
 
Kweli kabisa PM,

Habari za kiusalama kwenye suala la wanafunzi hawa zinatisha. Kwanza alianza Magembe kwa kuwaonya wanafunzi wasiteue viongozi wenye msimamo, na kisha ni juhudi ya serikali ya kudhibiti kazi na utendaji kazi wa viongozi wa wanafunzi.

Kuanzia ile siku ambayo Mtatiro na wenzake walitoa tamko la kukemea ufisadi, Mukandala amekuwa anamfuatilia sana huyu Mtatiro na wenzake. Huu ni udikiteta, ufisadi na uuaji wa hali ya juu kabisa unaonyeshwa hapa na Mukandala (ambaye ni mshauri wa Kikwete)

Naona wanataka kuingilia siasa za vyuoni kama vile ambavyo Republicans hapa Marekani wameanza mikakati ya kuingilia vyuo vikuu ili kupunguza influence ya Demokrats vyuoni.

CCM wanaweza kudhani kuwa wanawakomoa CHADEMA kwenye hii issue lakini nina hakika kabisa kuwa wanacreate radicals ambao siku moja watajuta kwanini waliingilia uendeshaji wa serikali za wanafunzi vyuo vikuu

Rwekaza Mukandala ni fisadi, dikiteta na muuaji. Nimemweka kwenye notice hapa JF. Nitamfuatilia kama Chenge na sitampa breki kama mkoloni na mwizi mwenye uraia wa utata ROstam Azizi

Kwa mujibu wa Ripoti ya Ulinzi na Usalama iliyowasilishwa kwenye kikao cha NEC Butiama, uamuzi huu umetokana pia na yaliyojiri siku ya wanafunzi duniani Novemba 17 mwaka 2007 ambapo wakati ambapo CHADEMA ilifanya Kongamano ambalo wanafunzi walikwenda kwa gharama zao wenyewe maelfu wakati lile la CCM pamoja na kuwalipa fedha walikwenda wachache tu na waliokwenda bado waliisema serikali ya CCM kutokana na ufisadi. Hivyo, ripoti ya Ulinzi na Usalama kuhusu Hali ya Siasa Tanzania iliyowasilishwa kwenye kikao cha NEC Butiama ikaeleza hatua za kuchukua. Itafuteni tu hiyo ripoti mtaelewa nasema nini. Baadaye sekretariati ya CCM ilakaa na kutoa maelekezo yafuatayo:
1. Mikoa yote yenye vyuo vikuu nchini uongozi wa CCM mkoa ihakikishe wanaoshinda nafasi za uongozi wa wanafunzi wawe wanaCCM kwa gharama yoyote ile. Tayari barua za maelekezo zimashatolewa kwa ajili ya chaguzi za SUA na Mzumbe zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
2. Viongozi wenye msimamo mkali na wale wanaolekea kuunga mkono CHADEMA pale UDSM ama wananunuliwa kwa gharama yoyote au wanatishwa na kunyamazishwa. Rais wa wanafunzi Daudi Deo ameshanunuliwa na sasa yuko kwenye payroll. Tabu ilikuwa kwa Mtatiro na kigenge chake cha vijana wengine kama wakiongozwa na kijana mmoja anayeitwa Owawa
3. Wanafunzi wa UDSM wachonganishwe na umma kwa kuhusushwa na kashfa za ngono, bangi na kuonyeshwa kuwa wanasimamia maslahi yao madogo madogo. Kwa ujumla ni mkakati wa kufunika mijadala ya ufisadi pale chuoni.

Kumbuka haya yalifanyika baada ya Zitto kuzuiwa kutoa mhadhara pale na wanafunzi kuandamana. Mara baada ya Kongamano la Nov 17 yalifuata pia maandamano ya TAHLISO kuhusu ufisadi yaliyokwenda mpaka Jangwani.

PM
 
Back
Top Bottom