Serikali yatimua wanafunzi UDSM

Huu ubeberu ungekuwapo pia katika kufuta mikataba mibovu..........mbona pangekuwa hapakaliki??

Prof Maghembe.........hatua uliyochukua ni ya Kipumbavu........kumbuka mzee wa VIJSENTI amesema.........wewe hukuzaliwa kuwa Waziri........na huu ndio ulikuwa mtihani wako mzuri kuonyesha kwamba wewe ni tofauti na majuza waliopita ku-approach masuala kama haya.

Chuo Kikuu sio shule ya msingi kusema watu wote wanaingia madarasani masaa yanayofanana........kuna watu wanafanya research....kuna wengine siku hiyo hawana darasa.......in short masaa ya wanfunzi chuoni hutofautiana.........wewe unatoa amri kufikia saa fulani wote muwe darasani.....kwani imekuwa shule ya msingi Rufiji ile.......damn!

Wanafunzi wana matatizo yao...hatukatai.....vile vile wana haki zao..........yaani NYIE MIJITU MLIO NA MIWAZO ISIYOBADILIKA BADO MNAFIKIRIA ENZI ZA CHAMA KIMOJA..........amri amri..........ni hatari na wa kuogopwa kama UKOMA

Shame on You......Maghembe
 
Haya pia bado si sababu ya udikiteta na ufisadi uliofanywa na Mkandara kwenye hii issue ya wanafunzi.

Si kweli kwamba haya yanatokea kila siku. Mambo ya ngono yapo hata Harvard na sio sababu tu ya kudiscrediti wanafunzi nakisha kuwapiga mabomu.

tusiwe na majibu rahisi kama Kikwete alipokuwa anajaribu kuiponda filamu ya Hauper maarufu kama "mapanki" aliposema ukahaba uko dunina nzima. Mimi sihalalishi wanafunzi kupigwa marungu wala mkandara kuwa fisadi, hoja yangu hapa tupunguze ushabiki kwenye mambo yanayogusa uhai wa taifa letu.

kama hata Havard kuna digrii za "chupi" jee sababu zake zinafanana vyanzo vyake na za hapa kwetu? wanafunzi wetu naamini kabisa wana mambo yanayofanana hata na vyuo vingine vikuu duniani,lakini vyanzo vyake ni vilevile?
 
Ngabu hapa inabidi kweli usemi wako utumike tena.

Yaani huuyu Mkandara na wenzake hapo wamefanya kitu ambacho wanajua kuwa wanafunzi hawatakubali hata kidogo na inakuwa kama vile wamefanya makusudi au kwenye usemi wako - ndivyo walivyo.

Utashangaa kusikia kuwa huyu Mkandara ni rafiki ya karibu wa Kikwete na mshauri wake wa kisiasa. No wonder nchi inakwenda kuzimu.

Yaani wanakimbilia kupiga wanafunzi, kuwafukuza chuo, na kuwaweka ndani wakati richmonduli bado wanalipwa mabilioni ya pesa na kina Chenge na Karamagi wakidunda mtaani kama hawana akili nzuri vile.

Haya matatizo ya wanafunzi UDSM nimeanza kuyasikia tokea Kuhanga alipokuwa VC (at least as far as I can remember)....conventional wisdom would tell you that for something that happens over and over...given the passage of time...they would have already found a curative solution for the problem. But no....same thing keeps on happening again....and again...and again...
 
Wanafunzi wa UDSM simamieni haki yenu bila woga. Na labda hamjui tu, lakini nguvu yenu na ushawishi wenu katika jamii ni mkubwa ajabu. Wanafunzi wa vyuo vikuu huko Indonesia waliweza kuuondoa madarakani utawala wa kifisadi miaka ya 80/90.
Ni wakati mwingine tena na pia fursa nyingine tena ambayo wana UDSM hawatakiwi kuichezea!Sasa mwendo ni mbele na hakuna kurudi nyuma! Nyie ndio chachu ya mabadiliko nchini mwetu! Historia ya dunia inaonyesha hivyo!
Mwaka 1990 ulitokea mgomo pale Same Sekondari!Maji lilikuwa ni tatizo sugu..wananfunzi wakipitisha miezi na miezi bila kuoga..huku wakikatisha muda wa masomo ili kuweza kwenda zaidi ya umbali wa km 3 kuchota maji kwa ajili ya chakula na walimu!
Ndiyo wasomi wetu tunavyowaandaa!?Kuanzia utawala wa mwl Nyerere shule zimekuwa zikiendeshwa kama kambi za ki hitler Hitler! Kuwapa vijana elimu lakini for just manipulation na si kuwa andaa kuja kuwa viongozi ama kuwa na taaluma pamoja na mazingira mazuri ya kuitumia taaluma yao kwa manufaa ya jamii!

Waziri wa maji Kisanji wakati huo alifanya ziara shuleni hapo..na wanafunzi wakampokea kwa furaha kubwa huku nyimbo za CCM zikiimbwa kwa furaha ambapo hata baadhi ya vijana kutokwa na machozi ya furaha kutokana na ukweli kuwa karaha ya maji ilikuwa ya kutisha!Jirani na shule kuna jela na wanafunzi ni kugombea maji na wafungwa kila kukicha!Vyoo vipo vya kisasa kabisa..na inaelekea vilijengwa wakati wa ukoloni,ila maji yalikuwa adimu hivyo vyoo na mabafu kupigwa kufuli..
watu kujipangusa tu kwa maji..na vyoo vya mashimo ambapo ukiingia humo inabidi uende uchi!..wakati huo almaarufu "uchizi"..choo kilikuwa uchizi kikweli kwani pamoja na kupata shida kubwa ya kupumua wakati wa haja..still ngozi yako inanuka kama vile ni marashi..na kuitoa huwezi since maji hakuna!Na darasani uvumile kidogo hadi harufu iishe!Kisanji alianza hotuba yake kwa kusema hivi"Naona mnafurahia sana kuja kwangu..lakini sijabeba maji mgongoni"
Alitoa hotuba ya kukatisha tamaa na propaganda..akaishia zake na huo ukawa mwisho..nadhani mambo bado ni yale yale pale Same..Mgomo ulitokea kwa sababu ya ufisadi wa viongozi wa kuwalisha wanafunzi madudu na wao na familia zao kuweka pesa mfukoni kwa manufaa yao.Na kutokuwajali wanafunzi na kuwaona kama ni wahuni tu!
Vijana wa mlimani wote mnayajua hayo!Ni wakati wa kufanya mabadilko na hakuna wengine wa kuyasimamia zaidi yenu!Nchi iko gizani na UFISADI UMESHAMIRI!Hofu kubwa ya mafisadi ni UDSM!Mkandala maybe anadhaniwa kuwa anakisomo kizuri cha kuwa neutrelize vijana!Inashangaza kuona kuwa serikali yetu inashinda kuwaenzi vijana wetu ili kuweza kujenga taifa lenye mafanikio..badala yake wanaweka vizuizi ili waendelee kutawala na kunyonya milele!Tunataka vijana wakigraduate waende kwenye shughuli za ujenzi wa taifa na wajengewe mazingira hayo na si kuwaacha watange tange mitaani!Na pia kuwaandaa kisaikolojia kuanzia mashuleni hadi vyuoni!Kuwapa heshma...Kwamba wao ni watu muhimu kwa maendeleo ya taifa!
Mpaka hapo viongozi watakapowachukulia vijana kwa heshima..migogoro bado itaendelea kuwepo!
Mpaka hapo viongozi watakapoamua kuacha kujilimbikizia mali badala yake wawajengee vijana wetu mazingira bora ya elimu,vitendea kazi pamoja na mishahara mizuri kwa maprofessa wetu!Mpaka hapo serikali itakapogundua huduma muhimu za kijamii kwenye institution zetu za elimu...bado migomo itakuwepo tu!
Hadi hapo vijana watakapoachiwa wajiamulie mambo yao na ku think independently na kuachana na sera mbovu tulizozirithi wakati wa ujamaa!
Nilitembelea Blogu ya Michuzi nikaona watu wanatuma picha za sekondari mbali mbali nchini ziko vile vile miaka nenda miaka rudi..kukame kuchafu..no body cares..and then kuna watu wanasema "vijisenti"..kuna watu wanafuja mamia ya mabilioni!Hawa vijana wana elimu ya kutosha kuona nini kinaendelea..they know their rights and they want change!Sio kwa manufaa yao tu..bali ya vizazi vijavyo na taifa kwa ujumla!Mpaka hayo na mengine mengi tu yatakapozingatiwa..bado kutakuwa na migomo tu..nafikiri this time kitaeleweka!
 
Hivi ni wakati gani ulikua bora
wakati wa mkoloni mwuepe ama wakati huu wa mkoloni mweusi??

Nimegundua tz sio tu kunahitajika kuondoa serikali ya CCM bali kunahitajika kujikomboa kwa kuondoa serikali ya mkoloni mweusi.
 
Huu ubeberu ungekuwapo pia katika kufuta mikataba mibovu..........mbona pangekuwa hapakaliki??

Prof Maghembe.........hatua uliyochukua ni ya Kipumbavu........kumbuka mzee wa VIJSENTI amesema.........wewe hukuzaliwa kuwa Waziri........na huu ndio ulikuwa mtihani wako mzuri kuonyesha kwamba wewe ni tofauti na majuza waliopita ku-approach masuala kama haya.

Chuo Kikuu sio shule ya msingi kusema watu wote wanaingia madarasani masaa yanayofanana........kuna watu wanafanya research....kuna wengine siku hiyo hawana darasa.......in short masaa ya wanfunzi chuoni hutofautiana.........wewe unatoa amri kufikia saa fulani wote muwe darasani.....kwani imekuwa shule ya msingi Rufiji ile.......damn!

Wanafunzi wana matatizo yao...hatukatai.....vile vile wana haki zao..........yaani NYIE MIJITU MLIO NA MIWAZO ISIYOBADILIKA BADO MNAFIKIRIA ENZI ZA CHAMA KIMOJA..........amri amri..........ni hatari na wa kuogopwa kama UKOMA

Shame on You......Maghembe

Maghembe mnamuonea bure tu. Hata ingekuwa wewe tatizo hili lingekuwepo. Kuweni fair kidogo ktk ukosoaji wenu
 
Nyani, alipoteuliwa kuwa Waziri wa Elimu ya Juu miongoni mwa mambo ya kwanza ambayo angetakiwa kushughulikia ni suala la Mlimani. Ni rahisi kutumia nguvu kuliko kutumia akili!
 
Nyani, alipoteuliwa kuwa Waziri wa Elimu ya Juu miongoni mwa mambo ya kwanza ambayo angetakiwa kushughulikia ni suala la Mlimani. Ni rahisi kutumia nguvu kuliko kutumia akili!

Nadhani wakati mwingine sisi tulioko kwenye sidelines ni rahisi kukosoa na kusema mtu afanye hivi au vile au angefanya hivi au vile. It may no be that easy. Put your self in his shoes and walk a mile....then probably you'll see how difficult it is. Kila mtu anaweza kukosoa....kutenda ni jambo jingine...
 
Nadhani wakati mwingine sisi tulioko kwenye sidelines ni rahisi kukosoa na kusema mtu afanye hivi au vile au angefanya hivi au vile. It may no be that easy. Put your self in his shoes and walk a mile....then probably you'll see how difficult it is. Kila mtu anaweza kukosoa....kutenda ni jambo jingine...

Ngabu kumbuka kuwa huyu Maghembe ndiye alikaririwa kwenye media akisema kuwa matatizo ya wanafunzi ni kuwa wanachagua viongozi ambao ni wenye msimamo mkali. Na akawa anataka wanafunzi wasiwe wanachagua viongozi wenye kutetea masilahi yao bali wale "wapole na wenye kusmile" kama Kikwete.

katika hili, alionyesha kabisa kuwa anataka kuingilia uchaguzi wa wanafunzi vyuo vikuu. baada ya haya kutokea sishangai amefunga chuo haraka namna hii.
 
tusiwe na majibu rahisi kama Kikwete alipokuwa anajaribu kuiponda filamu ya Hauper maarufu kama "mapanki" aliposema ukahaba uko dunina nzima. Mimi sihalalishi wanafunzi kupigwa marungu wala mkandara kuwa fisadi, hoja yangu hapa tupunguze ushabiki kwenye mambo yanayogusa uhai wa taifa letu.

Hakuna ushabiki hapa zaidi ya kushika bango kama kawaida ya JF kwenye mambo muhimu ya taifa. Hili swali la kuingilia uhuru wa wanafunzi wa chuo kikuu kuchagua viongozi wao ni muhimu kama lile la ccm kupiga viongozi wa chadema wakati wa uchaguzi wa kiteto

kama hata Havard kuna digrii za "chupi" jee sababu zake zinafanana vyanzo vyake na za hapa kwetu? wanafunzi wetu naamini kabisa wana mambo yanayofanana hata na vyuo vingine vikuu duniani,lakini vyanzo vyake ni vilevile?

Hili swali unaweza kumuuliza yule prezidaa wa havard aliyefukuzwa kuwa very sexist na mambo mengine mengi ambayo hayajatajwa.
 
Na Watashitakiwa Kama Watu Huru Na Sio Kama Wanafunzi Wa Udsm

Kwani wewe ndio muendesha mashitaka? mbona hukomi kujikombakomba kwa polisi na uendeshaji wao. Au unataka kugeuza hii issue ya wanafunzi kama ulivyofanya kwenye issue ya wanajamboforums?
 
Maghembe mnamuonea bure tu. Hata ingekuwa wewe tatizo hili lingekuwepo. Kuweni fair kidogo ktk ukosoaji wenu

tatizo la maghebe ni kukurupuka kufukuza wanafunzi na kuondoa udhamini.
wakati mafisadi wanaosababisha matatizo hayo yote hawatiwi hata kiboko.

kiongozi msomi unatakiwa kua na msimamo na kusimamia haki na kufuata kanuni.

Hata mkubwa wako akikulazimisha kufanya kitu ambacho unaamini sio ,unamkatalia akukulazimisha unabwaga manyanga achukue maamuzi yeye,ni kitu ambacho wanaojiita wasomi hawakifuati.

Maghebe hajafuata kanuni zozote wala taratibu zozote Maana pamoja na kua bodi ya mkopo ipo chini yao Lakini ikubukwe ule ni mkopo ambao una TERMS na Conditions Na pia anaposema wamewafutia udhamini ana maana Gani ??Jamani ule ni mkopo.

Huyu Maghembe naye ni kama Mkandala hakuna chochote hapo darasani wamepita Elimu zero
 
Fair iko wapi......kuwafukuza hata wasiohusika hiyo ndio fair..........kutumia nguvu kwa watu walio cafeteria (mwanafunzi mjamzito) hii ndio fair.......kuingilia uchaguzi wa wanafunzi hiyo ndio fair........hivi jamani tuko ktk era gani........hizi speculation za Mars kugonga Earth tutaziacha lini

........Yes hata ningekwa mimi tatizo lingekuwepo.......lakini hiyo ndio njia fair ya kutatua tatizo??......kupiga watu!!!!

......Wanafunzi wanaoleta fujo (kuvunja milango na vioo) si wanajulikana.......kwa nini hao wasichukuliwe hatua.....hii mambo ya ku-generalise mambo............ndio Upumbavu wa Maghembe.

"Ni rahisi kutumia nguvu kuliko kutumia akili"......na huu ndio upumbavu alioufanya Maghembe
 
If Mukandara can't stand the heat of good governance he should probably step out of the kitchen of leadership.

When shall they learn a lesson that police brutality wont solve any thing?.
 
Katika maelezo yake, Prof Maghembe alisema kuwa wanafunzi hao wametimuliwa baada ya kukaidi amri ya uongozi wa chuo iliyowataka warejee madarasani.

Tangu lini mwanafunzi wa Chuo Kikuu anaamuriwa kuingia darasani? Halafu unamfukuza kwa kutokuingia darasani? Kama uprofesa ni huu, nashukuru mungu sikuzigusa hizo anga tukufu nikabakia fundi mchundo.

Chuo Kikuu gani ambacho hakina wavuta bangi? Clinton alivuta, Obama alitumia mpaka cocaine inasema george W naye haukwa nyuma kwenye haya masuala! Wangapi tumewaona wakitumia hayo majani wakati wa ujana wao na sasa ni viongozi wa kuaminika dunia nzima? Chuo Kikuu kinazuia kubusiana wanafunzi! Hiki ni Chuo Kikuu au shule ya msingi? Ni lazima tuanze kuwa'treat' wanafunzi wa Chuo kikuu kama watu wazima na kuwapa heshima wanayozstahili. Ni lazima tuanze kuheshimu sacrifice na gharama ambayo jamii imeingia kumfikisha huyo mwanafunzi mahali pale. Ni lazima tuanze kutambua kuwa pale na sehemu nyingine kama zile ndiyo font ya vichwa vyetu vya baadae na ni lazima tuwape uhuru wa kutafakhari na kudadisi mambo bila kuwaingilia. Wakitoka hapo, dunia itawaweka sawa lakini wakati wako pale waachiwe waweze kufikia their full potential.
 
Nadhani wakati mwingine sisi tulioko kwenye sidelines ni rahisi kukosoa na kusema mtu afanye hivi au vile au angefanya hivi au vile. It may no be that easy. Put your self in his shoes and walk a mile....then probably you'll see how difficult it is. Kila mtu anaweza kukosoa....kutenda ni jambo jingine...

Lakini Nyani kuna kauli ambazo angetoa ingawa ni za kisiasa , lakini zingekuwa na Positive effect, one kumuita Prof Mkandara na watu wake, pili kuongea na Viongozi wa Wanafunzi, tatu kupata taarifa toka kwa Usalama wa taifa na hata facts zingine angezipata toka kwa indepent side of the issue, maana hata magazeti wameandika, mfano suala la Maji kule mabibo kuwa Mradi wa Mtu kwa kusingizia Pump mbovu, suala la Lift kama ni ya kutengenezwa au kubadilishwa, na muda muaafaka wa kubadili ni upi.
Then basing on those ciorcumstance angewasiliana na Pinda na ikiwezekana Raisi, kabla ya kutoa hiyo taarifa ya serekali, kama ni kuunda tume ya kufuatilia madai ya pande zote, hiyo inge-create a cooling off period for both sides , wakati serekali inaufuatilia kwa undani zaidi huo mgogoro.na Muafaka wake uwe vipi.
Leo hii tusingekuwa tuna zungumzia Chuo kufungwa, bali situation ya kufuatilia matatizo ya hizo pande mbili.
Sasa hivi tuna lalamika tanzania kielimu tupo nyuma vis a vis majirani zetu, lakini bado tunaona majibu ya matatizo ya chuo ni kufunga chuo? Kwa mtindo huo tutafika kweli? Kuna Cost ya kifedha, adha za manyanyaso ya hao wanafunzi, hasa wa kike, kifedha etc etc
Unajua mtu ukiwa Msomi ulio bobea kama Prof Magembe analysis yako na maamuzi yako yanatakiwa yasiwe ya kukurupuka na ya muda mfupi, na madhara makubwa.na Hizi ni opportunity chache ambapo Msomi anaweza kuonyesha alivyo tofauti na mwana siasa asiye msomi au asiye na busara.
 
wakienda uholazi si ndio basi kabisa
prof wakati wa mapumuziko anajisogeza pembeni analikamua jani.

tukirudi tz
uzinzi
hao maprof na mawaziri mbona ma magari yao hua hayaishi pale Ohio au nawo tuwavizie tukiwakamata tuwafukuze kazi na tuwapeleke rumende

maadili
mbona hao ma prof hua wanakata ulabu hadi wanajikojolea.
 
Tangu lini mwanafunzi wa Chuo Kikuu anaamuriwa kuingia darasani? Halafu unamfukuza kwa kutokuingia darasani? Kama uprofesa ni huu, nashukuru mungu sikuzigusa hizo anga tukufu nikabakia fundi mchundo.

Chuo Kikuu gani ambacho hakina wavuta bangi? Clinton alivuta, Obama alitumia mpaka cocaine inasema george W naye haukwa nyuma kwenye haya masuala! Wangapi tumewaona wakitumia hayo majani wakati wa ujana wao na sasa ni viongozi wa kuaminika dunia nzima? Chuo Kikuu kinazuia kubusiana wanafunzi! Hiki ni Chuo Kikuu au shule ya msingi? Ni lazima tuanze kuwa'treat' wanafunzi wa Chuo kikuu kama watu wazima na kuwapa heshima wanayozstahili. Ni lazima tuanze kuheshimu sacrifice na gharama ambayo jamii imeingia kumfikisha huyo mwanafunzi mahali pale. Ni lazima tuanze kutambua kuwa pale na sehemu nyingine kama zile ndiyo font ya vichwa vyetu vya baadae na ni lazima tuwape uhuru wa kutafakhari na kudadisi mambo bila kuwaingilia. Wakitoka hapo, dunia itawaweka sawa lakini wakati wako pale waachiwe waweze kufikia their full potential
.

Fundi nimeongezea font size kwenye maandishi yako hapa.

Yaani huyu Mkandara ndiye ana taasisi ya demokrasia na whatever the name anaita lakini bado ana mawazo yale yale ya zamani ya kuingilia chaguzi na masomo ya wanafunzi!

Mengine uliyosema ni kweli tupu na sina cha kuongeza mkuu!
 
Back
Top Bottom